Friday, 19 February 2016
Thursday, 18 February 2016
Mwanamke kakutwa Hostel za wanachuo Dar akiwa kang’olewa meno, jamaa wakataka kumbaka…(Hekaheka+Audio)
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
http://cdn12.hulkshare.com/dev12/0/009/752/0009752381.fid/hekaheka_february_18.mp3?key=59f5ac62e592ef7ac71e7450fe8c7f6c&dl=1
Kwenye Hekaheka ya Clouds Fm
Feb 18 2016 inamuhusu Mwanamke mjamzito na watoto wake wawili kukutwa
katika hostel za Wanafunzi Dar, kaamua kuondoka nyumbani baada ya kuwa
akipokea kipigo mara kwa mara kutoka kwa mume wake kwa madai kuwa
kamsababishia maambukizi ya UKIMWI.
Geah Habib alipata time ya kuhoji imekuwaje hadi akawa hapo? ‘Ugomvi wetu ni wa muda mrefu, baada ya kupata mwanamke mwingine mume wangu akaanza kuninyanyasa hadi tumefikishana kwa mabalozi‘
‘Madai yake eti mimi nimeuleta
UKIMWI ndani ya nyumba, mimi nikaamua kuondoka hadi muda huu nipo hapa
kwasababu pia amekuwa akininyanyasa‘
Full stori nimekurekodia kwenye hii sauti hapa chini…http://cdn12.hulkshare.com/dev12/0/009/752/0009752381.fid/hekaheka_february_18.mp3?key=59f5ac62e592ef7ac71e7450fe8c7f6c&dl=1
Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 Matokeo Kidato cha nne 2015
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1. Pande ya mkoani Lindi,
2. Igawa ya Morogoro,
3.Korona ya Arusha,
4. Sofi ya
Morogoro,
5. Kurui ya mkoani Pwani
6. Patema ya Tanga
7. Saviak ya Dar es
salaam,
8. Gubali ya Dodoma,
9. Kichangani ya Morogoro
10. Malinyi ya Morogoro.
KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015
KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE QT 2015
<<<< BONYEZA HAPA>>>>>>
HIZI NDIZO SHULE ZILIZOONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.Kazirege –Kagera

1.Kazirege –Kagera
2.Alliance Girls-Mwanza
3. St
Francis Girls-Mbeya
4. Alliance Boys-Mwanza
5. Canossa-DSM
6. Marian Boys-Pwani
7. Alliance Army Rock-Mwanza
8. Feza Girls-DSM
9. Feza Boys-DSM
10. Uru
Seminary-Kilimanjaro
KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015
KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015
KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE QT 2015
<<<< BONYEZA HAPA>>>>>>
AUDIO:Alichokiandika Wema Sepetu baada ya mimba yake kuharibika
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Moja ya
stori kubwa zilizokamata kwenye mitandao ya kijamii feb 17 2016 ilikuwa
ni post ya mrembo wa bongo, Wema Sepetu. Wema aliandika maelezo kuhusu
kuharikika kwa mimba yake.
Full stori nimekuwekea pia kwenye hii sauti ikiwa ni pamoja na interview niliyowahi kufanya na Idris Sultan…
NECTA:UFAULU ,MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015 WASHUKA WANAFUNZI 113,489 WAPATA ZERO
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema
kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka
2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.
==>> Bofya <<Hapa Kuona Matokeo >>
Mpekuzi blog

AU
Kasi Ya Rais Magufuli Yawagonganisha Waziri Wa Afya na Mkuu wa Wilaya Temeke
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Siku mbili baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema Wilaya ya Temeke
inaongoza mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wagonjwa sita wa
kipindupindu, Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Sophia Mjema amesema hadi jana
hakukuwa na mgonjwa hata mmoja.
Baada ya DC huyo kukanusha, jana wizara hiyo ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na ugonjwa huo.
Kipindupindu
ni moja ya vigezo vinne vilivyowekwa na Rais John Magufuli kupima
utendaji kazi wa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri
kabla ya kufanya uteuzi mpya.
Jumatatu iliyopita akiwa Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Waziri Ummy alitoa takwimu za ugonjwa huo na
kuitaja Temeke kuwa kinara lakini juzi, Mjema alisema kulikuwa na
wagonjwa ambao hawakuwa wamethibitika kama wanaugua kipindupindu.
Jana,
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema juzi
kulikuwa na mgonjwa mmoja wa kipindupindu lakini aliruhusiwa baada ya
kupona.
“Kwa hiyo leo (jana) Manispaa ya Temeke haina hata mgonjwa mmoja na kambi ni nyeupe haina mtu,” alisema.
Alisema
manispaa hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni za afya
ili kujikinga na ugonjwa huo baada ya kufanikiwa kuutokomeza.
“Hatutapumzika tutaendelea kuwakumbusha wananchi kutunza mazingira yao kuwa safi kwa sababu kipindupindu ni hatari,” alisema.
Wakati
ofisa hiyo akisema hayo, Waziri Ummy alitoa taarifa akisema Mkoa wa Dar
es Salaam kwa siku 10 zilizopita kuanzia Februari 7 hadi 16 kulikuwa na
wagonjwa 16; Temeke 12 na Ilala wanne.
Alisema wizara yake
ndiyo yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa jamii, hivyo
wagonjwa hao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu
katika kambi ya kipindupindu kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya
Amana kwa wagonjwa wa Ilala hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu
wa mwongozo.
Afukuzwa CCM Kwa Kumfanyia Kampeni Edward Lowassa
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Halmashauri
ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga
baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
Licha
ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama
hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana
viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.
Akizungumza
baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa,
Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea
malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe
huo kutokana na kupungukiwa na sifa.
Kalidushi
alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia
kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa
ni kosa.
Katibu
wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga
kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa
chama hicho kuwafukuza wasaliti.
Wednesday, 17 February 2016
Walimu Watatu Wakatwakatwa Mapanga Huko Musoma, Mara
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Walimu
watatu wa shule ya Secondary Mara iliyopo katika manispaa ya mji wa
Musoma Mkoani Mara,Vedastus Rwechungula ,Juma Amos Na Maccelo Ndege,
Wamekatwa Mapanga sehemu mbali mbali ya miili yao walipokuwa wakirejea
shuleni hapo Usiku wa Saa Nne toka matembezini.
Wakizungumza
wakiwa wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Musoma,Walimu hao wamesema
kuwa Vitendo vya Uhalifu jirani na Shule hiyo vimekuwa vikijitokeza
mara kwa mara kutokana na vibaka waliopo katika eneo hilo kuwakata watu
kwa mapanga.