Wednesday, 30 August 2023

MHANDISI MARYPRISCA AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA BODI YA WAKURUGENZI RUWASA



Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maji , Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso amefungua mafunzo elekezi kwa bodi ya wakurugenzi RUWASA ambapo yanafanyika Mkoani Iringa.

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Mahundi amesema kuwa kama Wizara wana amini kuwa maadili ya viongozi ni msingi muhimu wa uongozi bora na wenye tija kwa maendeleo endelevu.

"Hivyo, kwa kusimamia maadili, wajumbe wa bodi mnatakiwa kutekeleza majukumu ya kuiongoza RUWASA. Ni matarajio yangu kwamba mafunzo haya yatawapa mwanga na kuwaimarisha katika kuongoza kwa mfano na kuendeleza maadili ". Amesema

Pia,Mhe.Mahundi amesisitiza kwa Wajumbe wa Bodi kuwa wanahitaji kufahama na kusimamia viashiria hatarishi ili kuhakikisha ustawi na uendelevu wa taasisi. Wajumbe wa Bodi mnahitaji kuwa na ufahamu wa viashiria hatarishi.

Hivyo na kusema kuwa mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutambua, kusimamia, na kupunguza viashiria hatarishi kwa ustawi wa RUWASA.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Bi. Ruth Koya amempongeze Mhe. Rais kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi ya pili ya RUWASA.

Vilevile ameishukuru Wizara ya Maji kwa ushirikiano mzuri wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.
Share:

RAIS SAMIA AZINDUA MAABARA YA TEHAMA SKULI YA SEKONDARI YA KIZIMKAZI MKUNGUNI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akivuta kitambaa kuzindua Maabara ya TEHAMA katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni chini ya Ufadhili wa Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) tarehe 29 Agosti, 2023 katika Shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua chumba cha TEHAMA katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni chini ya Ufadhili wa Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) tarehe 29 Agosti, 2023 katika Shamra shamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

Share:

Tuesday, 29 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 30,2023
































Share:

WAZIRI NDALICHAKO NA KATAMBI WAPONGEZWA KWA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA WASTAAFU

 

 WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi wakiwa bungeni wakisikiliza maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu masuala ya wastaafu leo  Agosti 29, 2023 bungeni Dodoma.

.............

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi kwa kushughulikia kwa karibu masuala ya wastaafu.

Dkt.Tulia ametoa pongezi hizo Agosti 29, 2023 bungeni baada ya Naibu Waziri Katambi kujibu maswali ya wabunge kuhusu masuala ya wastaafu.

Amesema “Naibu Waziri ameonesha utayari kama Mbunge ana changamoto apelekewe, mimi ni shahidi wanafanya kazi nzuri Waziri Ndalichako na Naibu Waziri Katambi, wanasikiliza hoja ukiwapelekea na wanafuatilia kuhakikisha mtumishi au mstaafu anasaidiwa.”

Amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii huku akipongeza maboresho yanayoendelea kufanywa kwenye utoaji huduma kwa wastaafu.

Awali, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imekuwa ikishughulikia masuala ya wastaafu kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.

Share:

TBS YAPONGEZWA KUONA UMUHIMU WA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE


*************

Na Mwandishi wetu

UONGOZI wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi, umejenga kiwanja cha mchezo wa Pete chenye ubora wa hali ya juu.

Kiwanja hicho kimezinduli jana Makao Makuu ya Shirika, Ubungo, jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Lazaro Msasalaga, hafla iliyoenda sambamba na ufunguzi wa Bonanza 2023.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Msasalaga, aliupongeza uongozi wa TBS kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi.

"Kwa kutambua hilo, uongozi uliona ni vema kujenga kiwanja cha michezo chenye ubora wa hali ya juu, kiwanja hiki ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata sehemu nzuri ya kufanya mazoezi na kucheza mechi zao badala ya kwenda kucheza kwenye viwanja vya taasisi nyingine," alisema Msasalaga na kuongeza;

"Na hii itaokoa muda na kurahisisha ufanyaji wa mazoezi kila jioni." Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wafanyakazi kushiriki kwenye Bonanza hiyo.

Alisema katika Bonanza hiyo ya nne kufanyika tangu kuanzishwa rasmi kwa Viwango Sports Bonanza mwaka 2020, itakuwa ni ya kipekee ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Alisema Bonanza hiyo, ambayo ilianza Agosti 28 likitarajiwa kuhitimishwa Septemba 2, mwaka huu itashirikisha timu sita kutoka kurugenzi zifuatazo;

Kurugenzi ya Udhibiti Ubora (DOM), Kurugenzi ya Raslimali Watu na Utawala (DHRA), Kurugenzi ya Upimaji Ugezi (DTM), Kurugenzi ya Uandaaji Viwango (DSD), Timu ya watoa huduma TBS, ikihusisha wanaotoa huduma ya hakula, ulinzi na usafi.

Timu hiyo ya watoa huduma inashiriki Bonanza hiyo kwa mara ya kwanza ili kudumisha ushirikiano, kwani na wao ni wanajamii ya TBS.

Kwa mujibu wa Msasalaga, Bonanza hiyo itashirikisha michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu, kuvuta kamba, rede na michezo ya jadi.

Share:

WAZIRI NDALICHAKO ARIDHISHWA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa kwanza kushoto) akikagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.

Na. Mwandishi wetu Manyara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema ameridhishwa na maandalizi ya shughuli za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.

Prof. Ndalichako amesema hayo Mkoani humo alipofanya ziara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za kilele hicho zitakazofanyika Oktoba 14, 2023.

Aidha ameutaka uongozi wa mkoa huo kukamilisha ujenzi wa uwanja wa kwaraa kabla ama ifikapo Septemba 30, 2023.

Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha zaidi ya shilingi Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo na miundombinu nyingine.

Prof. Ndalichako ametoa wito kwa watanzania hususan mikoa ya Jirani kujitokeza kushiriki katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, amekagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho hayo, Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki.

Waziri Ndalichako katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) akikagua uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana Mkoani Manyara.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) akikagua Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa Mkoani Manyara



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa kwanza kushoto) akikagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akikagua miundombinu ya uwanja wa kwaraa patakapo fanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara, kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.


Vijana wa halaiki watakao shiriki katika siku ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.


Muonekano wa uwanja wa Kwaraa ambao unatarajiwa kukamilika Septemba 30, 2023 kwa ajili shughuli za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Manyara.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 29,2023



 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger