Thursday 9 February 2017

UFAFANUZI JUU YA UVAAJI WA SARE ZA JWTZ NA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa sare hizo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika maeneo yao.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
source: Fullshangweblog
Share:

MZAZI ATAKAYEMRUHUSU MTOTO WAKE KUSHIRIKI KAMARI KUSHTAKIWA


Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha (kamari) anahesabiwa kufanya kosa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Asha Abdullah Juma juu ya kuongezeka kwa maduka ya kucheza Kamari yanayojulikana kama Jack Pot katika miji mingi hapa nchini hivyo kusababisha uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya vijana.
“Michezo yote ya kubahatisha ikiwemo kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha namba 4 ya mwaka 2003, sura 41 pamoja na Kanuni zake,” alifafanua Dkt. Kijaji.
Aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendesha biashara ya michezo ya kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka nyingine za biashara.
Vile vile sheria hiyo inakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.
Aidha mtu yoyote ambaye atamruhusu mtoto chini ya miaka 18, kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha anahesabika kufanya kosa na anastahili kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
Dkt. Kijaji amesema kuwa ikiwa kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa kubahatisha, Bodi inamamlaka ya kumfutia leseni.
Hivyo basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha.
Pia, Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia vijana wao kucheza michezo ya kubahatisha pale wanapoona kuwa uchezaji wao unakuwa na matokeo hasi.
Hata hivyo amesema kuwa, michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu na sheria kama shughuli nyingine. Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa, wanaoendesha michezo hiyo wanazingatia sheria na kanuni zilizowekwa pamoja na wazazi, walezi na jamii kuhakikisha vijana wanazingatiia mila na desturi zinazolinda maadili ya Kitanzania wanapokuwa wanajishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.
Share:

Vita dhidi ya dawa za kulevya DSM Watu maarufu wakiwemo wanasiasa waguswa


Sakata la dawa za kulevya katika jiji la dsm limeendelea kutikisa watu maarufu,wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa Pamoja na Kiongozi maarufu wa dini ambao wametakiwa kwenda kituo cha polisi cha kati siku ya ijumaa kwa ajili ya mahojiano.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza na vyombo vya habari ametangaza Orodha mpya ya watu 65 ambao wanadaiwa kujihusisha kwa namna moja au nyingine katika kuuza au kusaidia kuingiza dawa za kulevya hapa nchini au nje ya nchi.
Baadhi ya watu maarufu wanaotakiwa kuripoti kituo cha polisi cha kati Siku ya Ijumaa ni pamoja na Mbunge mstaafu wa kinondoni Iddi Azzan,Mfanyabiashara Yusuph manji,Mbunge wa hai Freeman Mbowe,mchungaji Josephat Gwajima,huku wafanyabiashara maarufu akiwemo Hussein pamba kali ,mwinyi machapta pamoja na boss Chizenga wakazi wa kinondoni.
Aidha makonda amewataka wamiliki wa hotel wakiwemo Cassino sea cliff,Parm beach casino,Sleep way ,Yatch Club pamoja na Viongozi wa makampuni ya mafuta yakiwemo GBP,Tanga Petrolium,na Nas Hauleg nao kujisalimisha Polisi siku ya ijumaa.
Share:

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA KUTEMBELEA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE (TERMINAL III) DAR ES SALAAM LEO



Share:

Monday 6 February 2017

HIZI HAPA HABARI KALI SIKU YA LEO JUMATATU FEB 6 2017

HIZI HAPA HABARI KALI SIKU YA LEO JUMATATU FEB 6 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI TAREHE 6.2.2017,SOMA HAPO>>>>>>>>https://goo.gl/870nRt

Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/dXaecr

 

VIDEO | MAdada Sita-TMK-MKUBWA NA WANAWE - Matobo | Watch/Download,DOWNLOAD HAPO>>>>>>>> https://goo.gl/tjX7pO

 

Watoto wote wanaweza kupatiwa vyeti vya kuzaliwa -Mwakyembe,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>https://goo.gl/EBMoQV

 

Mbowe awakutanisha mameya sakata la UDA,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>https://goo.gl/au0m8z

Vyakula Muhimu Kwa Waja Wazito,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/f1uG5D

Cameroon yatawazwa mabingwa wa Afcon 2017,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/hj3H8A

Serikali yashauriwa kupiga marufuku viroba,SOMA ZAIDI HAPO IMEKUAJE>>>>>>>>https://goo.gl/43vERh

Uporaji kwenye maduka, bodaboda wazua hofu,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>>>https://goo.gl/G25KvW

Ukata kuchelewesha utoaji wa haki,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>https://goo.gl/7tsesX

Kulala chali kwa mjazito ni hatari kwa mtoto,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>>>>https://goo.gl/HtPDQ0

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>>>>https://goo.gl/jxdi2d

 TAFADHALI WATUMIE WENZAKO TAARIFA HIZI

MASWAYETU BLOG TEAM

 

 

 

 

 

 

 

Share:

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo

Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo na leo tunaendelea kuangalia chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.
Mtu mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za majani. Anahitaji zaidi ukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali.

Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10.

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI
Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.
Hapa chini nimekuwekea jedwali la jumla la vyakula na vinywaji vyenye asidi sana, asidi ya kati na alkalini sana, vile vya kuviepuka ni vile vyenye asidi sana, orodha itaendelea kuboreshwa;

Mayai na bidhaa za maziwa

  • Alkaline: mtindi
  • Neutral: mtindi mtupu (plain Yogurt ),
  • Acid: siagi, krimu, mayai, jibini ngumu (Hard Cheese), Ice Cream, jibini ya kiwandani (Processed Cheese), maziwa

Vyakula jamii ya maharage

  • Alkaline: Lima, njegere, Snap, String
  • Neutral: Soya
  • Acid: Black, Garbanzo, Kidney, dengu

Vyakula jamii ya karanga

  • Alkaline: lozi, Nazi freshi (fresh)
  • Neutral:
  • Acid: Brazil, korosho, Nazi kavu (dried coconut), Macadamia, karanga, Pecan, Pistachio, Walnut

Mboga za majani

  • Alkaline: asparaga (Asparagus), kiazisukari (Beets), brokoli (broccoli), kabeji, karoti, Koliflawa (aina ya kabichi – Cauliflower), figili (Celery), tango, mwani (Kelp), saladi (Lettuce), uyoga, vitunguu, kotimiri (Parsley), Bell Peppers, viazi ambavyo havijamenywa (with skin), boga (Squash), nyanya
  • Neutral: Horseradish, Rhubarb, Sauerkraut
  • Acid: Spinachi iliyopikwa, viazi ambavyo vimemenywa (no skin Potato), achali

Matunda

  • Alkaline: tufaa (Apple), parachichi, tende, mtini, zabibu, balungi, Kiwi, Limau, ndimu, embe, tikiti maji, chungwa, mpichi, Pears, Stroberi
  • Neutral:
  • Acid: Blueberry, Cranberry, plamu (Plum), plamu kavu (Prune)

Vinywaji

  • Alkaline: Maji ya limau, Chai ya tangawizi
  • Neutral: Maji
  • Acid: Chai ya rangi, Bia, kahawa, vinywaji vyenye kafeina, juisi za viwandani (processed), Liquor, Soda, Wine

Viongeza utamu

  • Alkaline: Asali mbichi (Raw Honey), sukari mbichi (Raw Sugar), Stevia
  • Neutral:
  • Acid: Viongeza utamu vyote vya kutengenezwa (Artificial Sweeteners)

Nyama

  • Alkaline:
  • Neutral:
  • Acid: Nyama ya ng’ombe, kuku, Samaki, mbuzi, batamzinga, nyama ya nguruwe, Sungura

Mafuta

  • Alkaline: mafuta ya mbegu za katani
  • Neutral: mafuta ya lozi, Canola, mafuta ya nazi, mafuta ya mahindi, Margarine, mafuta ya zeituni, Safflower, mafuta ya ufuta, mafuta ya Soya, mafuta ya alizeti
  • Acid:

Vitafunwa & nafaka

  • Alkaline: Amaranth, Millet, Quinoa
  • Neutral:
  • Acid: Barley, Buckwheat, Oats, mchele, Rye, Spelt, ngano, Pasta (vyakula jamii ya tambi), biskuti

Mbegu

  • Alkaline: Alfalfa (sprouted), chia (sprouted), Sesame (sprouted)
  • Neutral:
  • Acid: boga, alizeti, ngano
Share:

Kulala chali kwa mjazito ni hatari kwa mtoto


Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali  wapo kwenye hatari  ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.

Katika utafiti  uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito  walikuwa  kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na  kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.

Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya  watoto wafu wanaozaliwa  katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Mkuu wa utafiti huu,Louise O'Brien  kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na gharama yoyote ile.

Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri  kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.

Utafiti huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney Stillbirth Study ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito wako kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto wafu.Utafiti huu wa Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha wanawake wajawazito 295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia.

Naye mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka Sydney's Royal Prince Alfred Hospital amesema “Tafiti za awali zilionyesha ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito, hupunguza mzunguko wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.Lakini  pia ni vizuri kwa wanawake ambao ni wajawazito  kutotaharuki kama wakati mwingine watalala chali.’’Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito waliohusishwa kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya kwamba ni vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya  namna ya kulala kwa wanawake wajawazito.

Pia kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa chali (mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti kama hizi katika mazingira ya kwetu.
Share:

Ukata kuchelewesha utoaji wa haki

Bukoba.  Ukata katika Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba umesababisha majaji kutoendeleza vikao vya kusikiliza mashauri 24 ya kesi za mauaji, hali itakayosababisha haki kutokutolewa kwa wakati.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salvatory Bongole akizungumza wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini, alisema hadi Desemba mwaka jana hakuna kesi iliyokuwa imezidi miezi sita katika mahakama zote za mwanzo.

Alisema wamejitahidi kumaliza mashauri mengi kwa wakati pamoja na kupunguza malalamiko,  huku kesi 81 zikizidi mwaka mmoja katika mahakama za wilaya kwa kuwa korti hizo hazikuwa na uwezo nazo.

Oktoba 27 mwaka jana katika kesi ya jinai namba 67/2015, Mahakama Kuu chini ya Jaji Firmini Matogolo ilitoa uamuzi baada ya  miaka minane kwa  kuwatia hatiani wanandoa Lameck Bazil na Pancras Minago kwa mauaji ya mlemavu wa ngozi, Magdalena  Andrea yaliyotokea mwaka 2008 wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Share:

Uporaji kwenye maduka, bodaboda wazua hofu

Mbeya. Wamiliki wa maduka, bodaboda na glosari jijini hapa wameingiwa hofu baada ya kuibuka kundi la watu wanaodaiwa kuwa majambazi wanaopora fedha na pikipiki tangu mwishoni mwa Januari.

Mitaa iliyoonja adha ya wavamizi hao ni ya Mafiati, Mwanjelwa, Mabatini, Soweto na Mabanzini ambako vikundi hicho vilivunja maduka matano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema  wanawashikilia watu watatu wakituhumiwa kuhusika na matukio hayo.

Kidavashari alisema upelelezi wa awali unaonyesha kundi hilo la watu hutoka Tunduma mkoani Songwe na hupokewa na wenyeji ambao huwaongoza katika uporaji.

 Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Kanda ya Soweto, Joseph Patrick alisema hivi karibuni kuna watu waliofika eneo hilo saa 3:00 usiku waliowavamia madereva na kuwapora fedha na baadaye walivamia Mtaa wa Block Q walikopora pikipiki mbili.
Share:

Serikali yashauriwa kupiga marufuku viroba


Mbulu. Serikali imetakiwa kupiga marufuku pombe kali zinazofungwa kwenye pakiti maarufu viroba, ili kuwanusuru vijana na ulevi unaosababisha Taifa kupoteza nguvu kazi.

Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara, Padri James Amnaay alitoa rai hiyo juzi alipopokea msaada wa vyakula, nguo na sabuni kutoka  Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wilayani hapa.

Padri Amnaay alisema iwapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo, itasaidia vijana kutojiingiza kwenye ulevi ambao umekithiri na kusababisha baadhi yao kuwa vichaa.

Alisema kutokana na urahisi wa kubeba na bei nafuu, pombe hizo zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa hatimaye kujiingiza kwenye dawa za kulevya.
Share:

Vyakula Muhimu Kwa Waja Wazito

Wiki iliyopita tuliona orodha ya vyakula hatari kwa wajawazito. Orodha hiyo imekatazwa kuliwa na wajawazito kwa sababu ina madhara kwa afya ya mtoto. Darasa hili ni muhimu kama mama anahitaji kuzaa mtoto mwenye afya na akili timamu.

Baada ya kujua orodha ya vyakula visivyofaa kwa wajawazito, wiki hii tujifunze vyakula vinavyofaa kuliwa zaidi na wajawazito.

Kumbuka kwamba vyakula vyote vinaweza kuwa ni muhimu mwilini lakini huzidiana kulingana na mahitaji na hali ya mtu kwa wakati maalumu.

Mahitaji ya madini na vitamini mwilini wakati wa ujauzito huwa ni makubwa, hususani madini ya kashiamu, chuma na Vitamin B9 (folic acid).

MADINI YA KALISI (Calcium)
Wakati wa ujauzito, madini mengi ya kalisi husafirishwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo, mama huhifadhi madini hayo mwilini mwake. Kiumbe kinapokamilisha umbo lake katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho, hifadhi hiyo huanza kutumiwa na kiumbe hicho, hivyo mahitaji yake kuongezeka.

Katika kipindi hiki, mjamzito anatakiwa kula kwa wingi vyakula vinavyoongeza madini ya kalisi kama vile maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa. Kukiwa na upungufu wa madini hayo, meno ya mama na mifupa huathirika pia.

MADINI YA CHUMA (Iron)
Mahitaji ya madini ya chuma nayo huwa makubwa kwa wajawazito. Madini hayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu ambayo huhitajika kwa wingi na mama pamoja na mtoto.

Madini joto hupatikana kwa kula kwa wingi vyakula kama vile nyama, samaki, mayai, vyakula vilivyopikwa kwa nafaka zisizokobolewa (ugali wa dona, mkate mweusi, n.k) na mboga za majani kama vile spinachi na brokoli. Ili kupata madini hayo ya kutosha kutokana na vyakula hivyo, inashauriwa mjamzito kutumia pia vidonge vya Vitamin C (Vitamin C food supplements).

VITAMIN B9 (Folic Acid)
Vitamini hii ni muhimu sana kwa mjamzito, ni kosa kubwa sana la kiafya kwa mjamzito kuwa na upungufu wa vitamin hii. Vitamin B9 ndiyo inayohusika na ukuzaji na uimarishaji wa mfumo wa fahamu wa kiumbe tumboni.

Aidha, Vitamin hii ndiyo inayotoa kinga ili viungo vya mtoto visiathirike na kuepusha uzaaji wa watoto walemavu au wenye kasoro za viungo kama ‘midomo ya sungura’ na kadhalika.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin B9 ni pamoja na mboga za majani, juisi ya machungwa, mapeasi, vyakula vilivyopikwa kwa ngano na mchele (hasa brown rice) na mayai.

Hata hivyo, kutokana na hali ya vyakula vyetu, mjamzito hawezi kupata kiwango kinachotakiwa cha vitamin hiyo kwa kula vyakula peke yake.

Ili kupata kiwango cha vitamin hiyo kinachotakiwa, mjamzito atatakiwa kutumia pamoja na vidonge vya lishe vya Vitamin B9 ili kuepuka upungufu huo. Inashauriwa kutumia vidonge hivyo miezi michache kabla ya kushika mimba na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, kipindi ambacho vitamin hiyo huhitajika kwa wingi.

Kwa ujumla, lishe bora ni muhimu kwa mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito wake. Matatizo mengi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali, hutokana na upungufu wa madini na vitamin muhimu mwilini katika kipindi cha ujauzito.
Share:

Cameroon yatawazwa mabingwa wa Afcon 2017

Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon imetawazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2017 baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Misri kwa mabao 2-1,  yaliyofungwa na Nicolas N'Koulou na Vincent Aboubakar.
Share:

Mbowe awakutanisha mameya sakata la UDA


MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amekutana kwa dharura na mameya, manaibu meya na viongozi waandamizi kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili suala la Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Hivi karibuni, Rais John Magufuli wakati akizindua Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (DART) alitoa siku tano kwa uongozi wa Jiji kuhakikisha Sh bilioni 5.8 zilizolipwa na Kampuni ya Simon Group zinapangiwa matumizi baada ya kuuzwa hisa asilimia 51 kati ya 100 kwa kampuni hiyo.
Jiji la Dar es Salaam kwa sasa linaongozwa na Ukawa chini ya Meya kutoka Chadema, Isaya Mwita. Katika kikao cha baraza Halmashauri ya Jiji hilo chini ya Meya Mwita kilichofanyika wiki iliyopita, kilishindwa kufikia mwafaka wa kuzipangia matumizi fedha hizo kutokana na madai ya wajumbe wa baraza hilo kuwa kitendo hicho ni kubariki ufisadi wa kuuza hisa kwa Simon Group.
Kikao hicho cha Baraza kilifanyika ili kuitikia agizo hilo la Rais Magufuli alilolitoa wakati wa uzinduzi wa mradi wa Dart.
Hata hivyo, pamoja na siku tano alizotoa kuisha bado halijapatiwa ufumbuzi. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipozungumzia suala hilo nje ya ukumbi wa Bunge, alikiri kuwaita viongozi hao wa jiji la Dar es Salaam ili kuzungumzia suala hilo la UDA.
“Nimewaita ili tuzungumze sintofahamu ya suala hili ili tupate msimamo wa pamoja.Tunahitaji kupata suluhisho la suala hili ili wakazi wa Dar es Salaam wanufaike na Uda,” alisisitiza.
Katika jiji la Dar es Salaam lenye halmashauri sita, Ukawa ilishinda halmashauri tatu ikiwemo halmashauri ya jiji hilo inayoongozwa na Mwita, Ubungo ikiongozwa na Boniface Jacob na Ilala chini ya Charles Kuyeko.
Baadhi ya viongozi hao wa Ukawa wa Dar es Salaam walionekana wakirandaranda katika viwanja vya Bunge jana na baadhi yao walikiri kuitwa na mwenyekiti huyo wa Chadema huku wakidai kuwa hawafahamu wameitiwa nini.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene akizungumzia kushindwa kugawanywa kwa fedha hizo alitaka watendaji wa jiji hilo wapewe muda ili waweze kuja na suluhisho la suala hilo.
Alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia maagizo ya Rais Magufuli kuhusu matumizi ya fedha hizo, lakini endapo atapewa maelekezo kuhusu fedha atayatekeleza.
Share:

Watoto wote wanaweza kupatiwa vyeti vya kuzaliwa -Mwakyembe

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema inawezekana kuwasajili watoto wote nchini na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.
Mwakyembe aliyasema hayo katika hafla ya kukabidhi tuzo zilizotolewa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa viongozi wa mikoa ya Iringa na Njombe.
Ilikuwa ni hatua ya kuwapongeza na kutambua mchango wao katika kufanikisha utekelezaji wa mpango wa kuwasajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika mikoa yao.
“Iringa na Njombe wameweza kusajili watoto kwa asilimia 100 kwa kipindi cha miezi minne, hivyo kama mikoa mingine itaiga mfano kwa mikoa hii basi serikali itaweza kukamilisha, ndani ya muda mfupi, kuwasajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano,” alisema.
Alieleza kwamba mikoa ya Mwanza, Mbeya na Songwe imekuwa ikitekeleza mpango huu kwa zaidi miaka mitatu lakini mpaka sasa hawajafikia kusajili watoto kwa asilimia 80, hivyo akakasisitiza viongozi wahakikishe suala hilo linafanikiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya awali yaliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson, hali ya usajili katika mikoa ya Iringa na Njombe ilikuwa sio ya kuridhisha kwani ni watoto asilimia 11.7 katika mkoa wa Iringa na asilimia 8.5 katika mkoa wa Njombe ndio walikuwa wamesajiliwa.
“Hivi karibuni tutaanza utekelezaji wa mpango huu katika mikoa ya Shinyanga na Geita na tutatumia uzoefu tulioupata katika mikoa ya Iringa na Njombe ili kuhakikisha na huko tunapata mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi” alissema Hudson.
Katika hafla hiyo Mwakyembe alikabidhi tuzo na hati za pongezi kwa halmashauri 11, Ofisi zote za wakuu wa wilaya za mikoa ya Njombe na Iringa na kwa ofisi za za wakuu wa mikoa hiyo.
Share:

VIDEO | MAdada Sita - Matobo | Watch/Download


Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI TAREHE 6.2.2017

Share:

Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger