Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Saturday 17 August 2019

Bashe ataka Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kuwa kiungo cha biashara ya mazao Baina ya Kenya na Tanzania

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya mazao hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya  biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara endelevu.

“Biashara tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo inaendelea.” Alifafanua.

Alisema timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa namna gani  wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.

“Sisi Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya biashara.” Alifafanua.

Alisema katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze kusajiliwa Kenya Bureau of Standards ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bila vikwazo vyovyote.

“Tunatengeneza Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara hiyo.” Alibainisha Mhe. Bashe.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Dkt. Slaa Awakemea Watanzania Wanaoikosoa Serikali Mitandaoni

Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbord Slaa amekemea tabia ya baadhi ya watanzania kubeza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano huku akibainisha kuwa vitendo vya kutumia mitandao ya kijamii kukosoa utendaji wa serikali unawapa shida mabalozi kuitetea nchi huko walipo,kwasababu vitendo hivyo vinawakatisha tamaa wahisani wanaotaka kuisaidia Tanzania.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Startv wakati wa ziara ya mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani walitembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR eneo la Soga Mkoani Pwani.

Ametoa mfano kutokana na kauli aliyoitoa kongozi fulani ambaye hakumtaja imesababisha watalii 100 kutoka Sweden kuahirisha safari ya kija Tanzania kwa ajili ya kutalii.

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wapo katika ziara ya kutembelea na kuijonea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano kwa fedha za ndani.

Credit: Startv.


Share:

LIVE: Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Za SADC - Dar Es Salaam Tanzania

LIVE: Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Za SADC - Dar Es Salaam Tanzania


Share:

Jela Miaka 30 Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela mkazi wa kata ya Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji, Isack Balayabala (25)  baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kaulananga.

Akisoma hukumu hiyo jana Ijumaa Agosti 16, 2019  hakimu wa mahakama hiyo, Eliya Baha alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 kwa  kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Katika kesi hiyo ya  jinai namba 46 ya mwaka 2019 mahakama hiyo imesema  imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na hivyo kwa kuzingatia  kifungu cha sheria cha 60A kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 Jela


Share:

Polepole: Rais Magufuli amenituma niwaeleze kwamba hataongeza hata dakika tano Muda wake wa Uongozi Ukiisha

Katibu wa Itikadi na unenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa ametumwa na Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli awaeleze watanzania wote kuwa hayupo tayari kuendelea kuongoza nchi mara baada ya muda wake wa uongozi kufika kikomo kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakitaka iwe hivyo.

Polepole amezungumza hayo  jana akiwa mkoani Dodoma wakati akizungumza na baraza kuu la umoja wa wanawake wa chama hicho (UWT) ambapo amewataka wanachama hao kuacha kuendeleza mjadala huo ambao Mwenyekiti wao amesema unamkwaza.

Kwa mujibu wa Polepole, aliitwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli na kumtaka awatangazie Watanzania kwamba nchi inaongozwa na katiba na sheria.

Alisema Rais alisikia watu wakizungumza kuhusu kuongezewa muda baada ya kumaliza ukomo wa muda wa uongozi wake na kusema ni jambo linalomkwaza.

Alisema muda wake wa kumaliza uongozi ukifika mwisho atang'atuka mara moja na hataongeza hata dakika tano kwa kuwa uongozi ni mgumu.

"Wale wanachama wenzangu ambao mnaendeleza huu mjadala wa kuongezwa muda wa uongozi naomba muuwache maana Mwenyekiti anasema anakwazwa,"alisema Polepole.

Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, aliwataka katika kuteua wagombea wajiepushe na walaghai na wasio kubalika na jamii kwa kuwa inawavunja moyo wanawake ambao ni wapiga kura waaminifu.

"Wapiga kura waaminifu ni wanawake lakini tungesema wanaume wakapige kura tungeshaliwa kitambo. Tusiwavunje moyo wanawake kwa kuwateulia wagombea wasio na uwezo,"alisema.

Sambamba na hilo, Katibu alisisitiza kuendelea kuwatumia wanawake kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa watalisaidia taifa kupiga hatua zaidi kimaendeleo.


Share:

Serikali Yaahidi Kuendelea Kutatua Changamoto Za Utalii Nchini.

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kupunguza adha mbalimbali  zinazowakabili Wadau wa Utalii likiwemo suala la  polisi wa usalama barabarani kusimamisha magari yenye watalii mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alipokuwa akizungumza na Wadau wa Utalii nchini  katika kongamano la Utalii lililofanyika mkoani Arusha.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii nchini imejenga vituo vya ukaguzi wa magari vya utalii ili kupunguza usumbufu kwa watalii barabarani.

Amesema vituo  hivyo vitashughulikia masuala ya msingi likiwemo suala madereva wenye watalii kupimwa kilevi.

Amesema mbali na kilevi, Vituo hivyo vitashughulikia vitendo vyote ya uhalifu watakavyofanyiwa watalii.

Aidha, Mhe.Kanyasu amesema lengo la Serikali ni kupunguza kero kwa watalii ili wafikie milioni mbili mwaka 2019.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mhe.Kanyasu amesema licha ya  kujengwa vituo hivyo  vya ukaguzi lakini  bado kuna kero ambazo  zinafanyiwa  kazi lengo likiwa ni kuboresha sekta ya utalii.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amewataka wadau wa utalii kufuata sheria lakini akataka kupewa taarifa za polisi wanaowakwaza.

"Nipigieni simu hata saa nane za usiku kwa askari wanawaomba rushwa nishughulike nao" Alisisitiza Shana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema lengo la Arusha kuanzisha vituo vya ukaguzi magari ni kupunguza kero.

Amesema uwepo wa vituo hivyo vitafanya  mazingira bora kwa  watalii na wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Watalii (TATO) Wilbard Chambulo amesema ujenzi wa vituo hivyo ni hatua muhimu ya kuwahakikishia watalii usalama wao pindi  wakiwa barabani pamoja na mali zao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda amesema mkoa wa Arusha ni mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine kwa kujenga vituo hivyo ili kupunguza kero kwa watalii.


Share:

Rais Wa Zambia Edgar Lungu Aongoza Kikao Cha Siasa,ulinzi Na Usalama Cha SADC Troika Jijini Dar

Rais wa Zambia Mh. Edgar Changwa Lungu,ambaye ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) pichani kati akiongoza kikao cha ulinzi na usalama kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC (SADC) kilichofanyika  jana jioni  kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika – SADC, Dkt Stergomena Tax.

Rais wa Angola Mh. Joao Lourenco Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) anayemaliza muda wake akiwa katika kikao hicho kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zimbabwe Mh. Emmerson Dambudzo Mnangagwa anayechukua nafasi ya Uenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) akipitia baadhi ya nyaraka za kikao hicho kilichofanyika jana  jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Share:

MENO BANDIA YAKWAMA KOONI KWA WIKI MOJA..ASHINDWA KUMEZA VITU

Mgonjwa mmoja nchini Uingereza amejikuta katika maumivu makali baada ya meno yake ya bandia kunasa kooni kwa wiki moja.

Mgonjwa huyo mwenye miaka 72 alikuwa akilalamika kupata maumivu makali wakati wa kumeza vitu na kukohoa damu katika kipindi chote hicho.

Bwana huyo, alimeza meno hayo wakati akifanyiwa upasuaji wa tumbo.

Undani wa tukio hilo umechapishwa kwenye jarida la kisayansi la BMJ ambapo watunzi wake wamewataka madaktari kuhakikisha wagonjwa wao wanaondoa meno ya bandia kabla ya upasuaji.

Siku sita tu baada ya upasuaji huo uliofanyika mwaka 2018, bwana huyo alienda kwa daktari na kulalamika kuwa anashindwa kumeza vyakula vizito.

Madaktari awali waliamini kuwa hiyo ni athari ya kuwekewa mpira kwenye kinywa wakati wa upasuaji, na kumpatia dawa za kukabiliana na maumivu na maambukizi ya koo.

Lakini baada ya bwana huyo kurudi tena baada ya siku mbili akiwa na malalamiko zaidi, madaktari ikabidi wamfanyie uchunguzi zaidi wa koo.

Vipimo vya miale ya X-Ray vikaonesha kuwa kuna meno ya bandia matatu na chuma chake cha kuyashikilia.

Baada ya hapo, mzee huyo akawaambia madaktari kuwa alipoteza meno yake ya bandia katika kipindi ambacho alilazwa hospitalini kwa upasuaji wa tumbo.

Ikalazimika afanyiwe upasuaji wa haraka wa koo, lakini akarudi hospitali mara nne zaidi ili kuongezewa damu.Hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget imesema imejifunza kutokana na makosa ya upasuaji huo.

Watafiti wameeleza katika ripoti yao kuwa kuna zaidi ya mkasa mmoja wa watu kumeza meno ya bandia wakati wakipigwa dawa za usingizi.

Uwepo wa meno bandia ama kifaa chochote cha bandia kinywani, unatakiwa uripotiwe kabla nda baada ya upasuaji, wamesisitiza kwenye ripoti ya jarida hilo.

Hazel Stuart, ambaye ni mkurugenzi wa matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget ambapo upasuaji huo ulifanyika amesema uchunguzi wa kina ulifanyika juu ya tukio hilo.

"Baada ya tukio hilo, michakato yetu imepitiwa upya, na maboresho yamefanyika katika kila eneo la mahitaji, na tuliyojifunza tumehakikisha yanawafikia wafanyaki wetu wote ili kuepuka makosa," amesema.
Chanzo - BBC
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 17 August

















Share:

Friday 16 August 2019

Kasi Ya Maendeleo Ya Rais Magufuli Kusaidia Kuimarisha SADC

Na Judith Mhina-Maelezo
Kasi ya Maendeleo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliyoionyesha katika kipindi cha miaka minne akiwa madarakani, itaamsha ustawi wa miradi ya kimkakati katika Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC.

Dhahiri, bila kificho kitendo cha kumkabidhi na kuwa Mwenyekiti wa SADC Rais Magufuli kitachochea ongezeko la shughuli za miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo, ambayo haikutegemewa na jamii ya Jumuiya SADC kama inaweza kutekelezwa na Tanzania na kuwa mfano wa kuigwa.

Mafanikio ya Rais Magufuli yameonekana waziwazi katika miradi mikubwa ya maendeleo, matukio kadhaa ya kitaifa na kimataifa, ambayo yamedhihirisha kuwa juhudi na mtazamo wa Rais Magufuli ni faraja na muelekeo mzuri wa kufanikisha maendeleo katika nchi wanachama wa- SADC.

Akitoa hotuba ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa Rais Magufuli amesema”Katika kutekeleza mipango ya maendeleo na dira ya kufikia uchumi wakati ifikapo 2025, Tanzania inawakaribisha wawekezaji mbalimbali na kwa kuwa Afrika ya Kusini imepiga hatua kubwa katika Viwanda nawaaalika wafanyabiashara kuja kuwekeza katika Viwanda mbalimbali hudusan vya dawa na vifaa tiba, kuchakata madini na kwamba serikali iatatoa ushikiano  utakaohitajika”.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa sisi Tanzania tumeamua  kununua bidhaa kutoka Afrika ya Kusini, ambapo, hata pikipiki zinazotumika katika  mapokezi ya wajumbe kutoka nchi za SADC zimetoka Afrika ya Kusini. Amesisitiza Rais Magufuli.

Kama hiyo haitoshi, amemuomba Rais Ramaphosa kuongeza ushirikiano katika utalii hasa kwa kuwa wao wanapokea watalii takriban milioni 10 kwa mwaka ikilinganishwa na Tanzania inapokea watalii milioni 1.5 kwa mwaka. Katika hilo alitoa wito Afrika ya Kusini kuongeza safari za treni ya watalii na wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli  na fukwe za Tanzania, dhamira ambayo si kwa Afrika Kusini tu bali kwa nchi zote za SADC.

 Akiongea mara baada ya kuwasili nchini Zimbabwe mapema mwezi  Mei, Rais Magufuli amesema “Wakati umefika Jumuia ya Kimataifa kuiondolea nchi ya Zimbabwe vikwazo kwa kuwa vikwazo hivi vinaadhiri wananchi wanyonge wa Zimbabwe”

Aidha, Rais Magufuli amewaambia mabalozi wa nchi mbalimbali walioko Zimbabwe kuwa vikwazo hivi pamoja na kuwaadhiri Wazimbabwe pia, vinawaadhiri mabalozi na familia zenu mlioko hapa. Wakati umefika mliangalie hili na kuliondoa. Ili kila raia, aishiye Zimbabwe afurahie maisha mapya  na kuweza kushirikiana katika nyanja za uchumi kuongeza biashara na ushirikiano kati yetu.

Hakika Rais Magufuli amedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo katika SADC, hakuna nchi  yeyote ya Afrika na dunia kwa ujumla iliyowahi kutamka nchi ya Zimbabwe iondolewe vikwazo kutoka kwa bwana wakubwa wa dunia. Hii inadhihirisha Rais Magufuli atachochea  ukuaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo, kuhakikisha ushirikiano na nchi za Kusini mwa Afrika na kuleta ustawi wa hali za maisha za wananchi wanyonge katika jumuiya.

Katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa ziara yake nchini Namibia Rais Magufuli alihakikisha anaelekeza kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara katika nchi za Kusini mwa Afrika ili kukuza zaidi ushirikiano ambao utawaletea maendeleo wananchi wa pande zote mbili

Akifungua msimu wa ununuzi wa tumbaku  nchini Malawi Rais Magufuli amesema “Wananchi walio wengi Barani Afrika wapo katika sekta ya kilimo, hapa Malawi nimeambiwa zao  la Tumbaku linachangia asilimia 80 ya ajira, asilimia 60 ya fedha za kigeni na asilimia 37 ya pato la Taifa”.

Uchumi wa nchi nyingi za Afrika zinategemea kilimo kinachochangia pato kubwa la Taifa  pia, ni sekta inayoajiri watu wengi katika nchi zetu, Tanzania inatoa ajira kwa asilimia 70, mali ghafi asilimia 60 asilimia 30 inachangia pato la Taifa  na huingiza asilimia 20 ya fedha za kigeni. Hii inadhibitisha kilimo ni sekta muhimu Barani Afrika. Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli aliongeza  na kusema “Nimeambiwa katika uzinduzi wa zao la Tumbaku Serikali imeweka njia mbili za ununuzi kwa njia ya mkataba au mnada na Serikali imweka bei elekezi lakini, niwaomba wanunuzi msisite kununua kwa bei ya juu  ili kuwapa motisha wakulima wa zao la tumbaku pia mzingatie ubora na msichafue tumbaku kwa lengo la kuongeza uzito”.

Hotuba hii dhahiri inaonesha nia  hakika unaona dhamira yake ya kuhakikisha wakulima wadogo wa tumbaku wananufaika na kilimo wanachokifanya  badala ya kunufaisha watu wa kati na wenye Viwanda bila kujali uwepo wa bei nzuri kwa wakulima. Rais Magufuli anatambua ukubwa wa kundi hili ambalo likiinuliwa uchumi wake maendeleo kwa nchi za SADC yataonekana.

Akionyesha Afrika ilivyo tegemezi kitu ambacho sio kizuri Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa, mazao ya chakula kwa sasa ni mazao ya biashara, kwa sasa Afrika wastani wa chakula kinachoingizwa kutoka nje kina gharama ya Bilioni 35 za Marekani. Ambapo soko la chakula Barani Afrika  ni Dola za Marekani 300.

Vilevile, dhamani ya soko la mazao ya chakula kwa soko la Afrika itafikia dola Trilioni 1 mwaka 2030. Tanzania mwaka 2019 imevuna mazao ya chakula ya ziada ikilinganishwa na Malawi, hivyo tunawakaribisha Malawi kuja kununua chakula kutoka Tanzania

Akielezea mikakati sita ya kukuza uchumi wa SADC, Rais Magufuli amesema “Ni lazima kuondoa vikwazo visivyo na maana kama ututuri wa kodi, kuondoa utitiri wa Taasisi zinazothibiti biashara, ili kuchochea kasi ya viwanda na maendeleo katika Jumuia ya SADC”.

Pia, Rais Magufuli amependekeza mambo kadhaa katika hotuba yake ya ufunguzi ya wiki ya Viwanda kama vile, tekinolojia ya viwanda, ambapo anahakika hii italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda ndani ya Jumuiya ya SADC.

Akiangalia soko la SADC, Rais Magufuli amesema soko la watu milioni 350 na zaidi ni kubwa, idadi hii ya watu inatupa  jukumu la kujenga uchumi ndani ya Jumuiya husika. Pia, ubunifu ni kitu ambacho Rais amekiona ni muhimu katika Jumuiya, na kuhamasisha matumizi ya tekinolokia rahisi kwa kuwa rasilimali ya vijana wengi ipo, wenye vipaji katika sayansi na tekinolojia.

Aidha, uanzishwaji wa Viwanda vidogo vidogo kwa sababu hivyo ndivyo vinavyogusa watu wengi na kusisitiza viwanda hivi ndivyo vitakavyo inuka na kuwa viwanda vikubwa hapo baadaye. Hivyo ni lazima Jumuia iweke mazingira wezeshi katika kukuza sekta ya Viwanda. Amesisitiza Rais Magufuli.

Hii ikiwa ni pamoja na uwepo wa nishati ya umeme ya uhakika na bei nafuu, sekta ya usafiri na usafirishaji iwe rahisi na ya uhakika mfano reli ya kisasa (SGR), miundombinu ya barabara, usafiri wa anga wa uhakika.  Pia, kuruhusu idadi ya watu ndani ya Jumuia kutumia soko lililopo bila vikwazo kutoka nchi moja kwenda nyingine na kuhakikisha sekta binafsi inashiriki ipasavyo katika kujenga viwanda.

Rais Magufuli amesema”Tuhimize sekta binafsi, iache kulalamikia badala yake ipambane na changamoto zilizopo na kushirikiana na Serikali husika kuzitatua,  ili kutumia fursa zilizopo ipasavyo”.

Rais Magufuli ameonesha dhahiri nia yake ya kuhakikisha nchi za SADC zinafanya biashara, uwekezaji kuboresha miundombinu, kuongeza uzalishaji wa nishati ili kujenga Viwanda zaidi,  kuimarisha ulinzi na usalama na kulinda historia yetu kwa sasa na vizazi vijavyo ili kutambua tulipotoka, tulipo na tuendapo.

Pamoja na yote Rais Magufuli hakuacha ajenda yake ya lugha adhimu ya Kiswahili ambayo kwa hakika binafsi  nasema yeye ni shujaa wa kupigia chepuo lugha hii. Kila mtu ni shahidi hapa Tanzania kuwa tangu aingie madarakani amehakikisha anaitendea haki lugha hii kwa kuitumia katika shughuli  zake zote za Kitaifa na Kimataifa.

Ukiacha hafla zake chache kama pale alipoongea na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Afrika ya Kusini  mwaka 2017 ziara ya Rais Jacob Zuma wakati huo, kwa sasa ni msataafu Ambapo aliomba radhi Watanzania kuwa atatumia lugha ya Kiingereza,  ili wafanyabiashara na wawekezaji waone umuhimu wa kumuelewa na kuwekeza nchini Tanzania.

Pamoja na mambo mengine muhimu, ziara hiyo ilizaa  makubaliano ya pamoja kuwa Afrika ya Kusini itaingiza  mitaala ya lugha a kiswahili katika shule zake za msingi na sekondari, hivyo kuwa na hitaji la  Waalimu kutoka nchini Tanzania. Ambapo Rais Magufuli aliwataka Waalimu kuchangamkia fursa hiyo.

Bila kificho tunajivunia lugha hii yenye  historia ya kujenga umoja na mshikamano, pia ni lugha ambayo inaasili  ya Afrika ambapo haimilikiwi na kabila lolote bali na Jumuia ya Afrika Mashariki na Tanzania ndio nyumbani kwake.

Ziara ya Rais Magufuli nchini Namibia mapema mwezi Mei mwaka huu,  imezaa kusainiwa kwa makubaliano ya pamoja ya kuwa lugha ya kishwahili iwe katika mitaala wa shule za msingi na sekondari  nchini Namibia. Hivyo nchi hiyo inahitaji kupatiwa waalimu wa lugha husika kutoka Tanzania.

Kama alivyoelezea  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Paramagamba Kabudi na ajenda ya kunadi lugha ya kishwahili  iwe moja wapo ya lugha rasmi za SADC . Hakika ni kielelezo kuwa ikitumika katika nchi wananchama wa SADC itafufua ari ya umoja na mshikamano wa kweli katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Ajenda hii ya matumizi ya lugha ya kiswahili iliyoibuliwa na kushikiwa bango na Rais Magufuli wakati alipohudhuria mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Afrika, mapema mwaka 2017. Alihutubia Mkutano huo kwa lugha ya kishwahili wakati wa ufunguzi wa jengo la kihistoria  la Julius Nyerere la Amani na Usalama Jijini Adiss Ababa Ethiopia kama Makao makuu ya Jumuia hiyo.

Juhudi hizo za Rais Magufuli  hatimaye zimeleta ajenda itakayowasilishwa leo katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi za Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika. Hivyo Lugha ya Kiswahili iwe lugha rasmi ya Mawasiliano SADC kama Kiingereza, Kifaransa na Kireno.

Nchi nyingine zilizoridhia kuingiza lugha ya Kiswahili katika mitaala ya shule zake za msingi na sekondari ni pamoja na Sudan Kusini, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa ni pamoja na kuomba kupatiwa waalimu wa lugha hiyo kutoka Tanzania.


Share:

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431


Share:

Mabalozi 42 wa Tanzania Nje ya Nchi Wasifu ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3)

Na Mwandishi Wetu
Mabalozi  42 wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali Duniani wamesifu ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3) kwa kuwa umekuja wakati muafaka, ambapo wawekezaji wengi wanapenda kwenda nchi zenye miundombinu bora nay a kisasa.

Mabalozi hao wametoa kauli hiyo leo walipofanya ziara ya Kikazi ya kutembelea Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3).

Balozi Wilson Masilingi anayeiwakilisha nchi nchini Marekani, amesema jengo hili ni la kisasa na linavifaa bora, ambapo Watanzania wanapaswa kujivunia maendeleo haya, ambapo sasa kuna mpango wa safari za kutoka moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Marekani.

Naye Balozi Abdallah Possi anayeiwakilisha Tanzania nchini Ujerumani, kwa jengo hili sasa kutachagiza uwingi wa watalii kutoka nchi mbalimbali duniani, ambapo ndege nyingi zitatumia JNIA.

“Miradi hii ukiwemo huu wa jengo la tatu la abiria ni muhimu kwa wageni wanaoingia nchini, kwani litarahisisha usafiri kwa watu wa Mataifa mbalimbali wanaoingia nchini na kutoka nchini,” amesema Dkt. Possi.

Balozi Fatma Mohamed Rajabu anayewakilisha nchi nchini Qatar, amesema anatarajia ongezeko la ndege ya Air Qatar kwa safari za Tanzania, pamoja na kuja kila siku mara moja.

“Nitaenda kueleza ubora wa jengo letu hili na ninaimani pamoja na ndege ya Qatar inakuja kila siku lakini wanaweza kuongeza safari kwani tumekuwa na jengo la kisasa zaidi na lenye kupokea abiria wengi,” amesema Balozi Fatma.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wibroad Slaa ametoa wito kwa Mabalozi wenzake kuitangaza zaidi Tanzania Kimataifa kwa kuonesha miradi yote mikubwa na uwekezaji wanaoweza kuwekeza sehemu mbalimbali nchini.

“Msiogope kulitangaza Taifa letu katika maendeleo yanayofanyika sasa chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwekeza kwa ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati,”amesema.

Hatahivyo,  mabalozi hao wamesifu juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano iliyopo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius  Nyerere.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale alisema jengo hilo linauwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka, ambapo linavifaa vya kisasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama amesema jengo hilo pia lina ukumbi wa Wafanyabiashara Mashuhuri.


Share:

Waziri Mkuu: Tupo Tayari Kushirikiana Na Afrika Kusini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini katika kutimiza azma yake ya kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Amesema Tanzania inahitaji uungwaji mkono na Serikali ya Afrika Kusini hususan katika kipindi hiki ambacho imedhamiria kuimarisha shughuli za uzalishaji kupitia viwanda kwa lengo la kufikia uchumi wa kati..

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 16, 2019) wakati wa ziara ya Kiserikali ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro.

Ameyasema kwa kuwa changamoto zinazoikabili Tanzania katika nyanja mbalimbali zinafanana kwa kiasi fulani na zile za Afrika Kusini kwani historia za nchi hiyo na jiografia vinafana na Serikali ya Tanzania.

Akizungumzia kuhusu eneo la Mazimbu, Waziri Mkuu amesema kuwa lina uhusiano mkubwa na historia ya nchi hizo mbili kwa sababu huwezi kuulezea vizuri uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini pasi na kulitaja eneo hilo.

Waziri Mkuu amesema eneo la Mazimbu limebeba historia muhimu ya kumbukumbu ya vuguvugu la ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

“Mheshimiwa Rais, Tanzania ikishirikiana na nchi tano zilizokuwa katika kundi la mstari wa mbele (Angola, Tanzania, Zambia, Botswana na Msumbiji) ilijishughulisha sana katika ukombozi kusini mwa Afrika na katika kukomesha sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa sera za ubaguzi wa rangi zilikoma mwezi Februari 1994 na kufuatiwa na uchaguzi huru na wa haki uliopelekea kupatikana kwa Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo, Hayati Mzee Nelson Mandela mwezi Mei 1994.

“Tunapoongelea kukoma kwa sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, siku zote tutawakumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwal. Julius Nyerere na Hayati Mzee Nelson Mandela kwa utumishi wao uliotukuka kwa kujenga misingi imara ya umoja katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini”.

Amesema misingi imara iliyojengwa na wazee wetu hao, imekuwa chachu ya ushirikiano kwenye majukwaa ya Kimataifa hususani katika kupambana na ubaguzi wa kiuchumi na unyanyasaji wa aina mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema namna pekee ya kuwaenzi viongozi wetu hao ni kuendelea kujenga umoja na kushirikiana katika kuimarisha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

Kwa upande wake, Rais Ramaphosa amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango mkubwa ulioutoa kwa nchi ya Afrika Kusini wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo, hivyo wataendelea kuimarisha ushirikiano.

Rais huyo wa Afrika Kusini amesema Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Serikali Tanzania katika kuboresha masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali na kukuza teknolojia.

Pia amesema watairisha chuo cha SUA kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ili kulifanya eneo hilo kuwa la kisasa. “Tutaboresha na shule katika eneo hili na kuweka utaratibu wa walimu wake kutembeleana na wa Afrika Kusini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.”

Rais Ramaphosa aliwasili katika uwanja wa ndege wa Morogoro saa 4.21 asubuhi na kupokelewa na Waziri Mkuu. Kisha alitembelea campus ya Solomon Mahlangu na kujionea maeneo ambayo wapigania uhuru wa Afrika Kusini walikuwa wakikutana na kupanga mipango mbalimbali.

Pia kiongozi huyo ambaye kwa mara ya kwanza amefika mkoani Morogoro leo alitembelea campus ya Mazimbu na kujionea sehemu ambazo waliishi wapigania uhuru wa nchi yake na kisha aliweka shada la maua kwenye makaburi ya wapigania uhuru. Ameondoka uwanja wa ndege wa Morogoro na kuelekea jijini Dar es Salaam saa 1.59 mchana.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
IJUMAA, AGOSTI 16, 2019.


Share:

Mgogoro Wa Mpaka Na Mapato Ya Madini Halmashauri Mbili Wamalizwa

Na Issa Mtuwa “WM” Nachingwea Mtwara
Mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu  kuhusu mpaka wa uchimbaji madini uliohusisha eneo (leseni) moja kwenye ardhi ya halmashauri za wilaya mbili ya Nachingwea na Liwale  kila upande ukiwa na wachimbaji wadogo umetatuliwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo tarehe 15/08/2019 mara baada ya kufanya ziara katika eneo hilo na kufanya mkutano na wachimbaji wadogo wa pande zote mbili na viongozi wa kuu wa wilaya zote mbili.
 
Mgogoro huo wa mpaka na leseni umedumu kwa muda mrefu ukiwa na vyanzo viwili vikuu vya mgogoro. Moja,  mgogoro wa eneo ambalo wachimbaji wadogo wananchimba hivi sasa wamedai eneo hilo lilikuwa la Omar Said Kojogo ambae kwa mujibu wa wachimbaji wadogo walimlipa fidia ndugu Kojogi ili eneo hilo limilikishwe kwa jumuia ya wachimbajio wadogo lakini bado walikuwa hawajapatiwa leseni hiyo kama wamiliki wapya. 
 
“Mhe. Naibu Waziri tatizo la mgogoro wa leseni hapa bado haujatatuliwa kwa kuwa sisi wenyewe wanaaporo tulichangishana na kumpa Omar Said Kojogo Tsh.  2,852,000/= ili leseni hiyo iwe ya wanaaporo (Wachimbaji wadogo) lakini mpaka leo hatujapatiwa” alisema Machui Bausi.
 
Chanzo cha pili cha mgogoro huo ni mgao wa mapato yanayopatikana katika eneo hilo. Kila halmashauri inataka ichukuwe  mapato kitu ambacho kilikuwa kinaleta mvutano nani anastahili kwa kuwa leseni ya eneo hilo ipo katika halmashauri zote mbili. za Nachingwea na Liwale zote za mkoa wa Lindi.
 
Aidha, changamoto nyingine ambayo wachimbaji wadogo wamemwambia Naibu Waziri ni tatizo la soko la kuuzia madini ambapo wamemuomba Naibu Waziri kuwasongezea soko la madini katika eneo hilo ili kuwaondolea ushawishi wa kutorosha na kwenda kutafuta soko kwingine na ili mapato ya serikali yasipotee.
 
“Mhe. Naibu Waziri sisi hapa kiliochetu ni soko, hapa tulipo hata ukitaka kuuza madini lazima uende Ruangwa au Tunduru umbali uliopo ni mkubwa kufika huko. Na soko kubwa la Madini ya vito ni Tunduru, kwa hiyo ili mapato ya serikali yasipoteee tunaomba soko liwe hapa hapa sisi tuuze madini yetu na watu wa TRA wawepo ili tukiuza tuu serikali inachukuwa chake hapo hapo” alisema Ijumaa Iddi mwenyekiti wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo.
 
Katika kupatia majibu hoja zote zilizo wasilishwa, Naibu Waziri alianza kwa kusema.
 
“Mimi na waziri wangu Biteko iwe mchana iwe usiku, tutafika mahali popote ili kuhakikisha serikali inapata mapato kupitia madini, hivyo uwepo  wangu hapa  ni kwa sababu hiyo na ili pesa hiyo ipatikane lazima migogoro na hizi kero lazima zimalizwe ili mchimbe, muuze na kisha mlipe mapato ya serikali” alisema Nyongo.
 
Katika kujibu hoja, Naibu Waziri alianza kwa msimamisha Kaimu Afisa Madini Mkazi mkoa wa Lindi Mhandisi Iddi atoe ufafanuzi kuhusu  leseni na umiliki wa eneo hilo. 
 
“Mhe. Naibu Waziri, kwanza kabisa niseme eneo hili lina leseni halali inayo milikiiwa na ndugu Omar Said Kojogo anae miliki kihalali kwa leseni Na. PML 36821 Southern Zone ya Tshs. 1,937,000. Na kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 hairuhusu kutoa leseni kwenye eneo moja ambalo teyari ilishatolewa na mahali hapa palishatolewa leseni kama nilivyosema, na kama itakuwa hivyo mlabda kwa kesi maalum, hata hivyo suala hili lilishashugulikiwa na muda si mrefu leseni yao itakuwa teyari” alisema Mhandisi Idd Msikozi. 
 
Kuhusu kilio cha masoko, Naibu waziri alisema kwanza anawashukuru wachimbaji hao kwa kitendo chao cha kulilia soko ili madini yao yakauzwe kwenye masoko rasmi. Amesema serikali imetoa agizo kila mkoa uwe na soko la madini ili serikali ipate fedha za kutosha kupitia madini ili fedha hizo zikatumike kwenye shuguli nyingine za maendeleo.
 
Amesema mpango wa sasa wa wizara ni kuhakikisha kuwa kuna vituo vya kununulia madini kwenye maeneo ya wachimbaji ili wanaporo wasitembee mwendo mrefu kufuata soko.
 
“Ndugu zangu wanaaporo, kiliochenu kuhusu soko kimenigusa sanaa, na sisi kama wizara ndio kitu ambacho tunakisisitiza kila mahali, kwa hiyo hapa hapa naagiza Afisa Madini Mkoa na Uongozi wa Wilaya kaeni chini kwa haraka mjadili ili kituo cha kununulia madini hapa kianzishwe  mara moja na serikali ianze kukusanya mapato yake”. Aliongeza Nyongo.
 
Baada ya kutolea majibu ya hoja za wachimbaji hao, Naibu waziri pia aliwaagiza wachimbaji kuanzisha mfuko wa mahafa na dharula ili uwezo kuwasaidia mara miongoni mwao anapopatwa na tatizo ahudumiwe kwa huduma ya awali huku akisubiri utaratibu binafsi wa kutatua tatizo lake.
 
Kwa upande mwingine Nyongo ameuagiza uongozi wa Wilaya zote mbili ukae pamoja na kuweka utaratibu utakao wezesha kuwa na kituo cha kutolea huduma ya kwanza kwa maana pawe na “Nurse” kwenye eneo hilo kwa utaratibu watakao ukubaliana. Aidha, halmashauri hizo ziweke vyoo maeneo hayo kwa kuwa wachimbaji hao wanalipa fedha serikalini hivyo wanastahili huduma hiyo.
 
Wakati huo huo Naibu Waziri amewapongeza viongozi wa Wilaya zote mbili kwa jitihada zao za kutatua mgogoro huo awali kabla hajafika hasa katika kukubaliana namna kukusanya mapato ya kila upande kwani mapato yote yanakwenda kwenye mfuko mmoja wa serikali. 
 
Kwa upande wao viongozi wa wilaya ya Nachingwea Katibu Tawala Husna Sekibobo na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwamba kwa pamoja walimshukuru Naibu Waziri kwa kufika katika eneo hilo na kujione hali halisi kutoa majibu ya moja kwa moja ya hoja zilizo wasilishwa na waliahidi maelekezo na maagizo yake watayatekelezwa.
 
Ziara ya Naibu Waziri ilikuwa ya kukamilisha ratiba ya ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko aliesitisha ziara yake mkoani humo na kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya majukumu mengine.


Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger