Ameeleza kuwa baadhi ya vinywaji vya kampuni hiyo vitahifadhiwa kwenye benki ya damu ya Kituo hicho cha afya, na kwamba wananchi watakaohudhuria kutoa damu watapewa vinywaji hivyo kama sehemu ya mchango wao katika kuokoa uhai.
Amesisitiza kuwa vinywaji vya Jambo, ambavyo vimebeba ladha ya Sikukuu, vitakuwa na manufaa kwa watu wote, hasa wale watakaoshiriki katika michango ya damu, kwani vina sukari rafiki kwa afya na vinasaidia kuongeza nguvu.
Amefafanua kuwa, Kampeni ya Selebretika Kijamukaya inalenga kuhamasisha jamii kufurahia bidhaa za Jambo na kusaidia kuokoa maisha kwa kuchangia damu wakati wa msimu wa sikukuu.