Saturday, 28 February 2026

BARRICK YAPONGEZWA KWA KUWEKA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA MICHEZO BUZWAGI

 
Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi akitoa maelezo kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake walipotembelea kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia na Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi.

**


Mgodi wa Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa kwa kushirikiana na Serikali umepongezwa kwa kuweka miundombinu ya kituo cha michezo ambacho kitasaidia kukuza mchezo wa soka na michezo mingineyo nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, alipoongoza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa wa shirikisho hilo kutembelea eneo hilo ambapo amesema miundombinu iliyopo inaridhisha.

Amesema miundombinu hiyo kuanzia nyumba za malazi kwa wanamichezo, viwanja vya michezo, usalama, pamoja na mazingira yake kwa ujumla ipo katika hali nzuri na inakidhi mahitaji ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

“Natoa shukrani kwa kampuni ya Barrick na Serikali kwa kukubali ombi la kuanzishwa kituo cha michezo katika eneo la mgodi uliofungwa, tunafurahi kuona kituo kiko katika hali nzuri na kina viwango vikubwa kwa ajili ya kuhudumia wanamichezo, hii ni fursa muhimu kwa maendeleo ya michezo yetu”, amesema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Taifa ya TFF, Azan Mufti, amesema kutengwa kwa eneo hilo kwa ajili ya wanamichezo kunadhihirisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya sekta binafsi na wadau wa sekta ya michezo katika kufanikisha ajenda ya Serikali ya kukuza vipaji na kuendeleza michezo nchini.

Naye Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi, amesema kutengwa kwa eneo la kujengwa kituo cha michezo katika eneo hilo la mgodi uliofungwa kumezingatia dhamira ya kampuni ya kusaidia jamii sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza vipaji na kuchochea maendeleo ya michezo nchini.
Share:

ROCK BLOCK YACHOCHEA MAPINDUZI YA UJENZI KILIMANJARO



- Ajira 122 zatengenezwa, Serikali yavuna Shilingi Milioni 400/-

πŸ“Rombo, Februari 28, 2026

MGODI wa Rock Block uliopo Wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, umeendelea kuwa kichocheo cha mageuzi katika Sekta ya Madini ya Ujenzi kwa kuzalisha ajira 122 na kuiingizia Serikali zaidi ya Shilingi milioni 400 katika kipindi cha miaka mitatu ya uendeshaji wake.

Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Abel Madaha, amesema hayo kupitia mahojiano maalum Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa uchimbaji na uchongaji wa miamba kwa ajili ya kutengeneza matofali na bidhaa nyingine za ujenzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kusimamia na kuendeleza madini ya ujenzi ili kuongeza thamani na mapato ya taifa.

Amesema mgodi huo umeendelea kuchangia mapato ya Serikali kupitia ada, mrabaha na kodi mbalimbali zinazolipwa kwa taasisi ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Halmashauri ya Wilaya, hali inayochochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Rombo na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

Mhandisi Madaha amefafanua kuwa miamba inayochimbwa katika eneo la Holili ilitokana na milipuko ya lava kutoka Mlima Kilimanjaro, jambo linalolifanya eneo hilo kuwa na malighafi adimu na ya kipekee inayopatikana Rombo pekee nchini.

Amesema bidhaa zinazozalishwa na mgodi huo ni pamoja na matofali ya miamba, paving blocks, vigae, coblestone, wall cladding, kerbstone zinazotumika katika utengenezaji wa kingo za barabara, pozolana — mchanga maalum mweusi unaotumika katika uzalishaji wa Saruji na kazi nyingine za ujenzi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Madaha, matofali ya miamba yana uimara mara tatu zaidi ya matofali ya kawaida, hayaathiriwi na fangasi wala ukungu na hudumu kwa muda mrefu, jambo linaloyafanya kuwa chaguo sahihi kwa miradi ya kisasa ya ujenzi. 

Amewahimiza wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika Sekta ya Madini ya ujenzi kwa kuwa ina fursa kubwa ya kukuza uchumi na ajira.

Naye Mkurugenzi wa Rock Block Limited, Fabian Woisso, amesema kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi 72 wa kudumu na vibarua 50, hatua inayochangia kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana katika eneo hilo.

Amesema soko la bidhaa zao ni la ndani ya nchi, hususan katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo mahitaji ya vifaa vya ujenzi yamekuwa yakiongezeka kufuatia kukua kwa miradi ya miundombinu na makazi.

Aidha, Woisso amesema kampuni imewekeza katika miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR), ikiwemo ujenzi wa barabara ya kilomita tisa kutoka Holili hadi Kidondoni, ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Kidondoni na uchangiaji wa matofali kwa shule na vituo vya polisi.

Amehitimisha kwa kuwataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini ya Ujenzi, akisisitiza kuwa sekta hiyo ina uwezo wa kuongeza ajira, mapato ya taifa na kuimarisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.












Share:

SERIKALI YADHAMIRIA KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI DAR ES SALAAM




NA MWANDISHI WETU ,DAR

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa DART amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inamaliza changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, ili wananchi waweze kupata huduma bora, ya haraka na yenye uhakika.

Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya usafirishaji jijini humo, Dkt. Yonazi amesema Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha sekta ya usafiri wa umma.

Alisema katika ziara hiyo, kamati ilitembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) pamoja na Kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kujionea maendeleo ya uwekezaji uliofanywa.

“Ni dhamira ya Serikali kuhakikisha usafiri wa Dar es Salaam unakuwa bora, wa kisasa na unaokidhi mahitaji ya wananchi. Tumejionea miundombinu iliyowekwa na jitihada zinazoendelea kuboresha huduma,” alisema.

Dkt. Yonazi alibainisha kuwa tayari kampuni zimeanza kuleta mabasi mapya, hatua itakayoliwezesha jiji hilo kuwa miongoni mwa majiji yenye usafiri wa kisasa barani Afrika. Aliongeza kuwa mabasi mengi yatatumia gesi asilia, huku Serikali ikiwa imejenga miundombinu ya vituo vya gesi ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi.

Aidha, alisema Serikali imewekeza katika mifumo ya TEHAMA itakayomwezesha mwananchi kutumia kadi maalumu kulipia nauli bila kulazimika kupanga foleni, jambo litakaloongeza ufanisi na kupunguza usumbufu.

Katika hatua nyingine, aliwahakikishia wananchi kuwa mabasi yote yaliyoharibika yatafanyiwa ukarabati na kurejea barabarani ili kuimarisha upatikanaji wa huduma.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Bw. Said Tunda alisema lengo kuu ni kurejesha furaha kwa wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwapatia usafiri wa uhakika.

Pia aliwataka waendesha daladala kuendelea kutoa huduma huku Serikali ikiendelea kufanya mazungumzo nao ili kupata utaratibu bora wa ushirikiano, hususan kwa zile zilizopewa kibali cha kutumia barabara ya mwendokasi.

Hatua hizo zinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia miundombinu imara na huduma bora za kijamii.




Share:

Friday, 27 February 2026

KAMATI YA UONGOZI WA MRADI WA JNHPP YAKAGUA MAENDELEO YA BWAWA LA JULIUS NYERERE



Na mwandishi wetu

Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), tarehe 26 Februari 2026, imekagua maendeleo ya uzalishaji wa umeme katika mradi huo na kueleza kuridhishwa na usimamizi pamoja na utekelezaji wake, uliokidhi viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyowekezwa na Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi , amesema kamati imefurahishwa na namna bwawa hilo linavyochochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji wa umeme unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, hatua inayochangia kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umeme.

“Tumeridhishwa na jinsi mradi huu ulivyosimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Ukilinganisha na miradi mingine barani Afrika, mradi huu umejengwa kwa ubora wa hali ya juu na umeleta unafuu katika huduma ya umeme nchini. Haya ni mafanikio makubwa kwa Taifa,” ameeleza Dkt. Yonazi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bw. Petro Lyatuu, amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na mchango wake tayari umeanza kuonekana.

Amefafanua kuwa mwaka 2021, gridi ya taifa ilikuwa na jumla ya megawati 1,600, lakini kwa sasa uwezo wa uzalishaji umefikia zaidi ya megawati 4,000, zaidi ya mara mbili ya kiwango cha awali.

“Kwa sasa bwawa linazalisha umeme na tija yake imeonekana wazi. Kuongezeka kwa uzalishaji kumeimarisha gridi ya taifa na tunaendelea kuongeza nguvu katika sekta ya nishati kwa ajili ya maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi,” alisisitiza  Lyatuu.

Aidha kwa hatua nyingine Kamati hiyo ilitembelea kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Chalinze, kinachopokea umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere na kusambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji, Mhandisi Antony Mbushi, amesema kituo hicho kimekamilika na tayari kinafanya kazi.

Ameongeza kuwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma umefikia asilimia 71.58, huku mradi wa kusafirisha umeme kutoka Chalinze kupitia Kinyerezi hadi Mkuranga umefikia asilimia 59.76.

‘’Kamati imeridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo na kusisitiza kuwa mpango uliopo ni kuendelea kuongeza uzalishaji ili kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa ya uhakika na endelevu’,’Aliongeza Mha. Mbushi

Katika hitimisho la ziara hiyo, Kamati imeeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya umeme unaifanya Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji na kitovu cha usambazaji wa umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.








Share:

Thursday, 26 February 2026

JINSI NILISHINDA MITA NA FOOTBALL BET MOJA SAFI


Nilikuwa nikijaribu bahati yangu kwenye betting kwa muda mrefu, kila wiki nikipoteza pesa bila kuonekana na hakuna sababu dhahiri. Kila mara nilijikuta nikihisi nimechoka, kuchanganyikiwa, na wakati mwingine kushuka moyo.

Rafiki zangu walinipa ushauri, lakini kila mbinu waliyojaribu ilikuwa ile ile—kupoteza tena. Nilihisi labda betting si kwaajili yangu, na mara nyingi nilijiuliza kama nilikuwa nikifanya kitu kisicho na maana.

Hali hiyo ilinifanya nisahau sababu niliyoanza betting furaha na ndoto ya kupata faida ya haraka. Nilijaribu kuongeza dau, kuchanganya mbinu, hata kubashiri kwa kutumia hisia zangu, lakini matokeo hayakuwa tofauti.

Share:

SERIKALI YATOA TAHADHARI MLIPUKO WA MAFUA MAKALI YA INFULUENZA, UVIKO 19, HOMA YA DENGUE NA KIPINDUPINDU






Share:

Wednesday, 25 February 2026

PROF. SHEMDOE AONGOZA UJUMBE KUMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA KILIMO, ARDHI NA MAENDELEO VIJIJINI, COLOMBIA


Na OWM - TAMISEMI, Colombia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa nchi zinazoshughulika  na masuala Kilimo, Ardhi na Maendeleo vijijini,  ulioanza  Februari 24, 2026 nchini Colombia kwenye jiji la Cartegina.

Prof. Shemdoe amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo, baada ya Mhe. Rais kupokea mwaliko wa kuudhuria mkutano huo kutoka kwa Rais Gustavo Petro Urrego wa Colombia. 

Lengo kuu la mkutano huo uliohudhuriwa na nchi zaidi 100 duniani, ni kutoka na mwafaka wa namna gani matumizi bora ya ardhi katika kilimo yanaweza kupunguza migogoro ya ardhi na kuharakisha maendeleo vijijini.

Aidha nchi hizo zaidi ya 100 zilizoshiriki mkutano huo, ambazo zinashughulika na masuala ya Kilimo, Ardhi na Maendeleo ya Vijijini, zimepata fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya kilimo, Ardhi na Maendeleo Vijijini pamoja na matumizi ya teknolojia katika shughuli hizo, ambapo wananchi katika mataifa hayo watanufaika.

Katika Mkutano huo wa siku tano unaotarajiwa kufikia tamati Februari 28, 2026 Prof. Shemdoe ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde, wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na  Wizara ya Kilimo, lengo likiwa ni kutimiza ndoto za  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuleta mapinduzi ya kilimo nchini ili kuwanufaisha watanzania na kuwapatia tabasamu la kudumu.

Share:

WANANCHI PERAMIHO , SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI



Na Mwandishi wetu, Ruvuma

Wapiga Kura 127,632 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa kuchagua Mbunge katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma na Kata ya Shiwinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Februari 25, 2026 mjini Songea Mkoani Ruvuma wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Februari 26, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika.

“Kati yao wapiga kura 120,780 ni wa Jimbo la Peramiho na wapiga kura 6,852 wapo katika kata ya shiwinga na jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika, ambapo vituo 354 vipo Jimbo la Peramiho na vituo 19 vipo katika Kata ya Shiwinga Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,”amesema Jaji Mwambegele.

Aidha, amesema kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Peramiho vyama vya siasa 15 vimesimamisha wagombea na kwa upande wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Shiwinga vyama vya siasa nane (08) vimesimamisha wagombea.

“Natumia fursa hii kuvikumbusha Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kesho Februari 26, 2026 kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumlishia kura. Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo na Kata husika, wamekamilisha taratibu zinazoweka mazingira yanayowawezesha mawakala wa vyama vya siasa kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi,”alisema Jaji Mwambegele.

Amesema, mawakala hao, wanawajibika katika kulinda maslahi ya vyama na wagombea wao. Hivyo, wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu za Uchaguzi na maelekezo ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao vituoni.

Jaji Mwambegele amesema vituo vitafunguliwa saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na kwamba ifikapo muda wa kufunga kituo saa 10:00 kamili jioni, kama wapiga kura bado wapo kwenye mistari, mlinzi wa kituo atasimama nyuma ya mtu wa mwisho na zoezi la upigaji kura litaendelea hadi wapiga kura walio kwenye mstari watakapomalizika.

“Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kuondoka eneo la kituo cha kupigia kura; na Mpiga kura awapo kituoni, anatakiwa kufuata maelekezo yote atakayopewa na karani mwongozaji wapiga kura,”amesema Jaji Mwambegele.

Kwa mpiga kura ambaye ameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na taarifa zake zipo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililopo katika kituo husika, lakini amepoteza kadi yake au kadi yake imeharibika, ataruhusiwa kupiga Kura kwa kutumia moja wapo ya vitambulisho cha Taifa NIDA, Leseni ya udereva au Pasi ya kusafiria (Passport).




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 25,2026



Magazeti




















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger