Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia uadilifu wa viongozi walioko chini yake.
Askofu Machimu amesema hayo leo Jumapili Machi 20,2022 wakati ibada iliyofanyika katika Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT).
Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Rais Samia amekuwa madarakani amekuwa akihimiza uadilifu kwa viongozi walioko chini yake hali inayosababisha nchi kuendelea kupiga hatua kimaendeleo.
Akihimiza waumini kuendelea kusali na kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake Askofu Machimu amesema ni wajibu wa waumini wa kanisa hilo kuedelea kusali na kuomba katika familia zao wakiliombea Taifa na viongozi wake maana pasipo amani na utulivu waumini hawawezi kupata nafasi ya kufanya shughuli zao.
Pia Machimu, amewashukuru waumini wa kanisa hilo kwa kudumisha umoja na mshikamano kwa wachungaji na viongozi hilo hali inayowapa moyo wa kuendelea kuhubiri na kulitangaza neno la Mungu.
Kwa upnde wao badhi ya waumini walio walio hudhuria ibada hiyo waliahidi kuyezingai maagizo naUshauri ulio tolewa na Asofu kwa kuwa waminifu katika familia najamii ikiwemo kuendelea kuomba na kusali wakiliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake.
0 comments:
Post a Comment