Wednesday, 9 December 2020

RAIS MAGUFULI : MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI MKACHAPE KAZI KWELI KWELI...BORA UFANYE MAAMUZI BADALA YA KUTOFANYA KABISA

...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewataka Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwenda kuchapa kazi huku akiwasisitiza kufanya maamuzi yanayohusu maslahi ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Disemba 9,2020 Ikulu Chamwino Dodoma wakati akiwaapisha Mawaziri 21  na Manaibu Mawaziri 22 aliowateua Disemba 5,2020.

"Mkachape kazi kweli kweli. Ni nafuuu ukafanye uamuzi mbaya kuliko kutofanya uamuzi kabisa. Kafanyeni uamuzi unaohusu maslahi ya Watanzania, uamuzi utakaosaidia watu wanyonge.Sisi tunataka speed kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo",amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewataka watendaji wa serikali kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kuepuka kutuma nyaraka za serikali kwenye magroup 'Whatsapp' 

"Fanyeni kazi kwa uadilifu na mkazingatie maadili. Hii teknolojia mpya mkaitumie vizuri,muache kutumia nyaraka za serikali kwenye magroup",amesema.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger