Wednesday, 16 December 2020

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MSANII MAARUFU WA FILAMU MOHAMED FUNGA FUNGA 'MZEE JENGUA'

...

Jeneza lililobeba mwili wa Mzee Jengua
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Mohamed Fungafunga, maarufu kama Jengua enzi za uhai wake


Mamia ya wakazi wa Dar es salaa na nje ya Dar es salaam leo wameungana kuuzika mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Mohamed Fungafunga, maarufu kama Jengua  kwenye makaburi ya Mburahati Jijini Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika leo Jumatano Desemba 16,2020 mchana walifurika wasanii wa tasnia mbalimbali kama vile wanamuziki, waigizaji, wanasoka, mabondia na wengineo.

Wachekeshaji na mastaa wa filamu kama Steve Nyerere, Miss Lucy Charles, Mzee Jumbo, Kingwendu, JB, Mama Kanumba, Patrick Kanumba, Bi Staa, Tito, Ringo, Tin White, Kivurande na Hashim Kambi ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye mazishi ya Mzee Jengua.

Enzi za uhai wake marehemu alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuigiza vizuri uhusika wa ukatili na kupenda kutamani kutoka kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo.

Jengua alifariki dunia jana Disemba 15 nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwigizaji mkongwe, Muhogo Mchungu (kushoto), akishiriki tukio la maziko.
Sehemu ya waombolezaji waliofurika msibani hapo.
Mwili wa marehemu ukiswaliwa.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger