Wednesday, 9 December 2020

KIKUNDI CHA WANAWAKE 'ITAMBUE THAMANI YAKO' LATOA MSAADA KWA WAFUNGWA WANAWAKE GEREZA LA KAHAMA

...
Na Kijukuu cha Bibi K - Kahama
Jamii wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuwakumbuka wafungwa na mahabusu waliopo Gerezani kwa kuwatembelea na kuwapa misaada na vitu na maneno ya faraja.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kikundi Wanawake cha Itambue Thamani Yako (I.T.Y) Minael Donald wakati wakikabidhi misaada ya chakula, mavazi, sabuni na taulo za kike kwa wafungwa wanawake katika Gereza la Kahama.

Bi. Minael amesema kuwa katika jamii kuna watu wengi ambao wanauwezo wa kuwasaidia wafungwa waliopo Kwenye magereza mbalimbali nchini na kwamba kuwatembelea na kuwapa misaada inawafariji na kuwatia moyo dhidi ya kesi zao zinazowakabili.

Katika hatua nyingine amewakaribisha wanawake wengine wilayani Kahama kujiunga na kikundi hicho ili waweze kujitambua,Kujipenda na kujitunza.

Akiongea kwa niaba ya Uongozi wa mkuu wa Gereza na Gereza la wanawake Kahama Staff Sajenti wa Gereza hilo Anastazia Martine amekishukuru kikundi hicho kwa misaada waliotoa na kutoa wito kwa vikundi vingine kuwatembelea wafungwa na kuwafariji dhidi ya mashauri yao.

Kikundi cha wanawake cha Itambue Thamani Yako (I.T.Y) kipo nchi nzima na kimeanzia kwenye mtandao wa Kijamii wa Facebook mbapo kwa Wilaya ya Kahama Kina wanachama zaidi ya 90 na wengine wakiendelea kujiunga na kikundi hicho.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger