Friday, 16 September 2016

HIZI HAPA KURASA ZA NDANI MAGAZETINI LEO SEP 16 2016

...

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10

Magazeti ya Leo Ijumaa

Published in Jamii

MIAKA KUMI YA MJENGWABLOG: ' Njiani Kwenda Kwa Rais' -5

Published in Jamii


- Ziara Mbili Za Nje Zilizowatenganisha Kambona Na Nyerere..
Ndugu zangu,
Mama yangu mzazi enzi za usichana wake alisoma Middle School ya pale Mtaa Kichwele ( Sasa Uhuru Street). Shule hiyo ikaja kujulikana kama ‘ Uhuru Girls’.
Ni mmoja wa waliobahatika kuimba nyimbo mbili tofauti za taifa; moja ya mkoloni, na nyingine ya Tanganyika Huru.
Ananisimulia walivyokuwa wakijipanga mstari asubuhi na kuimba; “ God Save The Queen!’ Na baada ya Desemba 9, 1961, katika mstari huo huo, wakaimba kwa furaha na kwa kujivunia; “ Mungu Ibariki Afrika”.
Ndio, Tanganyika ikazaliwa, na ikawa kweli ‘ Young Nation’- Taifa Changa. Na Julius na wenzake akina Oscar na Rashid walikuwa vijana kweli. . Wakati ule wa uhuru hakuna mmoja wao aliyeivuka umri wa miaka 40. Julius Nyerere alikuwa kijana wa miaka 39 tu.
Hao walikuwa marafiki watatu. Ndio, Julius Nyerere, Oscar Kambona na Rashid Kawawa. Katika uchanga ule kama taifa, Julius na Oscar wakafarakana. Urafiki ukaisha na Oscar akakimbilia ’ Kwa Mama’- London.
Jana nilimalizia kwa kuandika, kuwa makala haya ni jaribio la kuvunja ukimya wa juu ya nini kilitokea takribani miaka hamsini iliyopita. Ni mmoja tu wa mfano , wa jinsi umma ulivyofichwa ukweli wa juu ya nini hasa kilitokea kikasababisha mfarakano wa waliopata kuwa viongozi wa mstari wa mbele kwenye harakati za kuanzishwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika; Julius Kambarage Nyerere na Oscar Salathiel Kambona.
Niseme tu, haya ni moja ya maandiko yangu muhimu tangu nianze kushika kalamu na kuandika. Na naandika nikiwa sina hata chembe ya hofu. Ni kwa sababu moja kuu; kuwa yanahusu historia yetu na mustakabali wa nchi yetu. Sote tuna wajibu wa kuandika historia yetu.
Hii ni nchi yetu. Hatuna sababu za kuionea aibu historia yetu, badala yake, tujivunie, kuwa tuna historia. Na ni unyonge na utumwa kusubiri wasomi kutoka Marekani na Ulaya waje kutafiti na kutuandikia historia yetu. Historia yako isimulie mwenyewe. Hivyo basi, tuna wajibu wa kuifanya kazi hiyo.

Historia itusaidie kutukumbusha machungu na furaha ya tuliyoyapitia kama taifa. Si kwa kuandika tu, hata kwa kusimulia machache tuliyoyashuhudia.
Naam, tumeona, kuwa Julius Nyerere na Oscar Kambona walikuwa viongozi vijana sana katika Tanganyika huru ya wakati huo. Ikumbukwe, wakati tukipata uhuru, Nyerere alikuwa na miaka 39 na Oscar alikuwa na miaka 36.
Hawa walikuwa ni vijana waliokabidhiwa dhamana kubwa ya kuingoza nchi kubwa ya Tanganyika. Naamini, walikuwa ni wenye dhamira njema kwa taifa hili; Julius, Oscar, Rashid na wenzao wengine katika TANU.
Ukweli unabaki, kuwa Oscar Kambona hakuikimbia nchi yake kwa kashfa ya kuiba fedha ya Serikali au ufisadi mwingine. Maana, haiyumkini Kambona aliyeaminiwa na Nyerere akaja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU, akawa Waziri wa kwanza wa Elimu wa Tanganyika huru, akaja kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na hata kwa wakati mmoja kushika wizara mbili; Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Nje. Kwamba, aje tena baadae kutuhumiwa uhaini na hata kushukiwa uraia wake.
Ukweli ni kuwa marafiki hawa wawili; Oscar Kambona na Julius Nyerere walikuwa na mgongano wa tofauti ya kimaono ya kisiasa yaliyoathiri hata urafiki wao. Wawili hawa walikuwa kama Ghandi na Nehru katika India. Julius Nyerere alitaka kuifuata njia Ghandi na ambayo kwa kweli ndio iliyotufikisha hapa leo, kama taifa moja, lenye utulivu , amani na mshikamano wa watu wake.
Njia ya Ghandi ikoje?
'Village Swaraj'. Kwa maana ya kuimarisha vijiji vya Ujamaa na kujenga misingi ya Ujamaa na Kujitegemea. Kwamba vijiji vijitegemee kwa chakula. Uzalishaji uwe wa ushirika na mengineyo yenye kutofautiana na njia ya ubepari kama ya Nehru.
Taifa kwa kuifuata njia ya Ghandi ni taifa lililojengwa katika misingi ya Ujamaa. Sina hakika hata leo, kama njia ya Nehru aliyotaka kuifuata Oscar Kambona ingeliacha taifa letu likabaki salama. Maana, nchi yetu ilikuwa changa na yenye watu wengi masikini. Mfumo wa kibepari, kama ilivyo njia ya Nehru, ungejenga zaidi matabaka ya kijamii na kutanua pengo la walionacho na wasio nacho.
Hivyo, tunaona, kuwa migongano ya kifikra kati ya Oscar Kambona na Julius Nyerere ilianza kuonekana dhahiri katika ziara mbili walizozifanya kwa pamoja katika mataifa mawili tofauti. Ziara ya Marekani mwaka 1963 na ziara ya Uchina mwaka 1965.
Na hapo katikati kuna jambo lililoopelekea uwepo wa mahusiano ya mashaka kati ya Julius Nyerere na Oscar Kambona. Ni uasi wa jeshi ( Army mutiny) wa Janauri 20, 1964. Ni nini kilitokea Januari 20?
Itaendelea kesho..
Maggid Mjengwa,
0754 678 252

Ripoti Imewasuta Madalali Sekta Ya Utalii...!

Published in Jamii



- Tulisema, VAT Ya Utalii Ni Vita Ya Madalali Dhidi Ya Wazalendo..
Ndugu zangu,
Ukweli huu nilipata kuuandika huko nyuma..http://mjengwablog.com/.../26835-vat-ya-utalii-ni-vita-ya-mad...
Tanzania: Tourism Industry Booms Despite New Tax
By Bernard Lugongo
Tourism prospectus looks brighter even after recent introduction of the Value Added Tax (VAT) on tourism services, with an increased revenue and tourist arrivals, according to a new report.
Safaris in TanzaniaThe report by .. Read More..http://allafrica.com/stories/201609150139.html
Ndugu zangu,
Zama hizi za Magufuli ni zama za kodi. Mwenyekiti wenu na risiti nahifadhi.
Msije mkashangaa ikifika Desemba kila mwajiriwa akaambiwa awasilishe wastani wa kodi wa sahani moja ya chakula alichokula akiwa kazini kwa siku zote 365 za mwaka.
La sivyo, awasilishe vielelezo vya risiti ya sahani alizolipia kodi. Mwenyekiti wenu nitawasilisha lundo la risiti!
Mchana mwema.
Maggid,
Iringa.(P.T)
719a2166
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari. Katika mkutano huo aliwaeleza kuhusu Matembezi ya Hisani yanayoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuchangia waathirika wa  Tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni. Matembezi hayo yatafanyika tarehe 17 Septemba, 2016 Jijini Dar es Salaam. Pia aliwajulisha kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kutekwa kwa madereva wa malori huko DRC.
719a21811
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na  Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa matembezi ya hisani ili kusaidia wahanga waliokumbwa na maafa ya  tetemeko  la ardhi  lilitotokea  Septemba 10 mwaka huu, huko mkoani  Kagera.
Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga amesema kuwa, matembezi hayo ya hisani ya kilomita tano yataongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
   Aliongeza kuwa Matembezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi Septemba17 mwaka huu, ambapo yataanzia Bwalo la Polisi Osterbay (Polisi Officer’s Mess) kuanzia saa 12 asubuhi.
Aidha amesema kuwa, matembezi hayo yana lengo la kuhamasisha wafanyabiashara, taasisi za fedha, kampuni mbalimbali pamoja na  jamii ya watanzania, wanadiplomasia waliopo nchini kuchangia kwa kutoa misaada mbalimbali ili kusaidia wahanga maafa ya tetemeko la ardhi la mkoani  Kagera.
“Tunafanya kampeni hii ya tembea kwa ajili ya Kagera, kwa lengo la kuwahamasisha watanzania, wafanyabashara na jumuiya ya wanadiplomasia waliopo nchini ili kila mtu aweze kushiriki kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kitakachosaidia wenzetu waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Kagera” alisema Kasiga
Hivyo basi, Wizara hiyo imeeandaa daftari maalumu la michango kwa jumuiya ya mabalozi  katika nchi zote zenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, ili kuunga mkono zoezi la kuwasaidia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba.
Pia Serikali imefungua akaunti rasmi kwa jina la Kamati Maafa Kagera katika benki ya CRDB ya  mkoani Kagera yenye namba 0152225617300 ambayo itakayotumika kupokea  michango kutoka kwa watu mbalimbali. (P.T)

SERIKALI KUFUTA UJINGA IFIKAPO MWAKA 2030

Published in Jamii
1
 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (katikati), akisoma hutuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kusoma Vitabu chini ya Hema Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale, iliyoratibu maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki Elimu, John Kalaghe.

 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kulia), akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Mradi wa Usomaji Room to Read, Mkurugenzi wa Mradi, Room to Read, Juvenalius Kurulatera na Mkurugenzi Mkuu, Haki Elimu, John Kalaghe.
 wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

 Wanafunzi wakishiriki maadhimisho hayo.

 Maadhimisho yakiendelea.
 Wadau wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
 Mkutano ukiendelea.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbaruku kutoka wilayani Bagamoyo wakiigiza Igizo la Almas na Jitu kwenye maadhimisho hayo.

 Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza mada.
 Wanafunzi kutoka kituo cha kujisomea cha Early Lead Club wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wadau na raia wakigeni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Ofisa wa Room to Read kutoka Mikocheni, Veronica Mahenge (kulia), akitoa zawadi ya vitabu kwa wanafunzi waliosoma vizuri vitabu mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.
Na Dotto Mwaibale
OFISA Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawe, amesema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wamefuta ujinga nchini.

Mapunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu kwenye hema yanayoadhimishwa duniani kote. 

Alisema moja ya shabaha iliyopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kila mtoto nchini anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.

“Nafahamu shirika lenu la Room to Read limekuwa likitumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa kuweza kujenga maabara katika shule zetu, kutoa vitabu na mambo mbalimballi katika kupambana na elimu,” alisema.
Alisema takwimu za kitaifa za sensa ya makazi na watu katika mwaka 2012 zinaoonesha kuwa asilimia  22 ya watanzania hawezi kusoma na kuandika kwa ufasa, 81.7 ni wenye ya msingi 14.4 ndio wenye elimu ya sekondari na asiimia 2.3 elimu ya  chuo. 

Alisema kiwango hicho kidogo kinasababisha watoto kutokuwa na msingi imara katika kipindi cha mwazoanapoanza shule.

“Kwa mfumo unaofanywa na Room to Read katika kuhakisha wanafunzi wanajua kusomma na kuandika afikapo darasa la tatu ni wazi kuwa serikali tunapaswa kujifunza ili kuhakisha hadi ifikapo 2030 tunakuwa tumefanikiwa kufuta ujinga,” alisema Mapunda.


Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inayosema ‘Kuandika yaliyoita, Kusoma yajayo’ itumike kutafakari kufuta ujinga.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale alisema siku ya usomaji duniani ni siku muhimu kwa wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio ya kiserikali na serikali.
Alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka  ifakapo Sepemba 9, ikiwa ni kutimiza azimio la Tehrani lilipitishwa mwaka 1965 ambapo kwa mwaka huu wanaadhimisha miaka 50 tangu kuazshwa kwake mwaka 1966.
“Kutokana na kuwepo kwa mitiani ya Taifa ya darasa la saba, sisi Room to Read  na washiriki wezetu tuliona ni vyema kuadhimisha siku hio leo ili kupisha tukio muhimu la wadau wetu,” alisema.

Mwakabwale alisema takwimu za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka 2015 zinaonesha hali ya usomaji duniani katika nchi saba Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ni ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watazania wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.

Alisema Nchi ya Burundi inaongoza katika nchi za ukanda huo kwa asilimia 85.6 ya wananchi wake wanajua  kusoma na kuandika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na nchi nyingine.

Maadhimisho hayo yalinogeshwa na Taasisi ya Room to Read kwa kufanya maonesho ya vitabu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kupata fursa ya kusoma vitabu na kuulizwa maswali pamoja na kupata zawadi za vitabu

mkuu wa wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi

Mkuu wa wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji

Mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.


Mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.
Na fredy mgunda,iringa. 
MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.
Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri Wiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Wiliamu
Aidha Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
 “ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Wiliamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.
“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la mufindi kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema nyimbo
Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya mufindi.
“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema kaguo.
Mashindano ya mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.  (P.T)

Dr. Stephen Nindi(katikati) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe walipotembelea eneo la upimaji.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe akipongeza hatua ya upimaji wa ardhi na kuahidi kuendelea kutembelea kuona maendeleo

Bw. Ally Amri(kushoto) ambaye ni  Land Surveyor akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe namna zoezi la upimaji linavyofanyika

 Christian Thomas(aliyevaa shati la blue) ambaye ni mwenyekiti wa kijiji akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe namna zoezi la upimaji wa Ardhi lilivyo wasaidia

 Viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wakiwa katika eneo la moja ya kijiji kuona jinsi shughuli za upimaji zinavyokwenda 

 Hiki ni  kifaa kiitwacho Real Time Kinematic (RTK) ni moja ya kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji wa ardhi.

Bw. Charles Charokiwa Msumari(katikati) Afisa Mifugo Msaidizi Mkuu wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe alipotembelea kituo chao ambacho wanakitumia kukusanyia taarifa mbalimbali na shughuli zao

Baadhi ya wadau mbalimbali wakiendelea kufuatilia kwa makini maelezo 

Mtaalam wa GIS Theonest Mlolewe akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe (hayupo pichani) namna wanavyofanya kazi. Picha zote na Fredy  Njeje/ Blogs za Mikoa
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Stephen Kebwe amesema  kazi ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi kwa kiasi kikubwa itapunguza na  kuondoa migogoro mbalimbali ya ardhi inayotokea katika kijiji kwa kijiji,kata kwa kata au kitongoji kwa kitongoji  na kusisitiza kuwa Serikali haitashindwa kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakaekwamisha kazi ya  upimaji wa ardhi yenye lengo la upangaji wa matumizi bora ya ardhi.
Akizungumza  na wanakijiji wa kijiji cha Dihombo,Dkt.Kebwe alisema kazi hiyo itasimamiwa kikamilifu na kamati husika za ulinzi na usalama kutoka Wilayani,Kata hadi Mkoa kuhakikisha inafanikiwa. Alisema kazi hiyo inayofanywa ya upimaji wa ardhi itakuwa ndio muarobaini wa kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara ikiwemo ya Wakulima na Wafugaji katika mkoa huo.
Alisema kwa sasa wapimaji wa ardhi wanatumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo kwa kiasi kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila mtu kumiliki kipande cha eneo lake.
"Nakumbuka wakati wa kampeni mwaka jana,Rais Dkt.John Magufuli alihaidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa,kwa miaka mitano hii vijiji takribani 7500  vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo kwa kila mwaka vitapimwa vijiji 1500,"alisema. Alisema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza.
"Kazi hii ya upimaji wa maeneo katika kuhakikisha kunampango bora wa matumizi ya ardhi ni mpango wa nchi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa Morogoro kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi ambapo utahusisha nchi nzima,"alisema Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi(NLUPC),Dkt.Stephen Nindi alisema ofisi yake inafanya kazi na wadau mbalimbali wa masuala ya ardhi zikiwepo wizara pamoja na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali ikiwemo Shirika la Kimataifa la Care,Shirika la Oxfam,Chama cha Wafugaji Tanzania,Chuo kikuu cha Ardhi pamoja na Tamisemi.
Dkt.Nindi alisema kwa sasa kazi ya ya upimaji inafanywa na vifaa maalum vya kisasa vijulikanavyo kwa jina la Real Time Kinematic ambavyo vinafanya kazi kwa urahisi zaidi,licha ya vifaa hivyo kwa sasa vipo viwili nanvyakukodisha. "Tunahitaji kuwa na vifaa hivi walau vitano ambavyo vitatuwezesha kupima kwa wakati na kukaimilisha zoezi hili kwa haraka na kifaa kimoja kinagharimu kiasi cha sh.milioni 80,"alisema Dkt Nindi
Naye Mratibu wa Programu ya Ufugaji Asili kutoka Shirika la Kimataifa la Care,Marcely Madubi alisema suala la ardhi ni moja ya masuala muhimu yanayozingatiwa na shirika lao katika mikakati yao ya kimataifa. Alisema wadau mbalimbali nchini wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia suala hili la kuhakikisha upimaji wa ardhi unafanikiwa hususani katika kuchangia ununuzi wa vifaa vya teknolojia mpya ya upimaji(Real Time Kinematic)ili kuwezesha upimaji wa ardhi kwenda kwa haraka zaidi na kupunguza migogoro inayoendelea kujitokeza.  (P.T)

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mghamila 'Super D' kushoto akisaini mkataba wa bondia Iddi Mkwela wa pili kushoto ambaye atazipiga october 23 na Issa Nampepecha kulia katika ukumbi wa CCM mwijuma Mwananamala katikati ni Ibrahimu Kamwe 'Bigryth' ambaye ni mlatibu wa mpambano uho Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Mkwela kushoto akitambiana na Issa Nampepeche mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Octobe 23 katika ukumbi wa CCM MWIJUMA Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na mabondia Iddi Mkwela wa Pili kushoto Issa Nampepeche pamoja na Ibrahimu Kamwe mabondia hao wamesaini kuzipiga october 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA IDDI MKWELA AKISAINI MKATABA

ISSA NAMPEPECHE AKISAINI MKATABA

Bondia Iddi Mkwela kushoto akitambiana na Issa Nampepeche mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Octobe 23 katika ukumbi wa CCM MWIJUMA Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA IDDI Mkwela amesaini mkataba wa kuzipiga na Issa Nampepecha mpambano wa raundi kumi siku ya October 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma mpambambano wa raundi kumi uzito wa KG 61
Mpambano uho ulio ratibiwa na Ibrahimu Kamwe utawakutanisha mabondia vijana ambao ni wadogo sana katika mchezo wa masumbwi nchini na watazipiga raundi kumi siku hiyo
pia kutakuwepo na mapambano mbalimbali ya utangulizi siku hiyo
akiongea wakati wa utiaji saini mkataba uho bondia Mkwela amesema amejipanga vizuri kumpiga Nampepeche kwani atojali kuwa na bifu na watu mbalimbali ili mradi aeze kuibuka na ushindi wa nguvu siku hiyo
nae Nampepeche amesema kuwa anaendelea na mazoezi kama kawaida ivyo mashabiki wake wategemee ushindi tu kwani siku hiyo atakuwa uwanja wa nyumbani na atokuwa na msalia mtume
Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi (P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...
Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...
Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...
Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...
Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...
Soma zaidi
mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.
bshyera11_ba222.jpg

Smartads



Maoni ya Wanakijiji

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger