Sunday 16 May 2021

Rais Hussein Mwinyi Mgeni Rasmi Uzinduzi Wa Mbio Za Mwenge Wa Uhuru 2021


Na: Mwandishi Wetu – Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo kitaifa zitazinduliwa Uwanja wa Mwehe – Makunduchi, Mkoani Kusini Unguja, Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokutana na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021..

Mheshimiwa Mhagama alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2021 ni Mbio maalum, umaalum wake pia unatokana na Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika Wilaya 150 za kiutawa tu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Halimashauri za Wilaya 195 kama ilivyozoeleka.

“Chombo hiki sasa ni budi kikimbizwe tena nchini kote baada ya kutofanya kazi toka mwaka 2020 kutokana changamoto za Ugonjwa wa Corona, hivyo ili kiweze kurejesha matumaini kwa watanzania na kuwahimiza kuchapa kazi chini uongozi shupavu wa Serikali ya awamu ya sita inayoongwa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mhagama

Alifafanua kuwa, Falsafa ya Mwenge Mwenge wa Uhuru ndio chimbuko la Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964 na Azmio la Arusha la mwaka 1967.

Akinukuhu maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa mwaka 1958 wakati akihutubia kikao cha 35 cha Umoja wa Mataifa na kuyarudia tarehe 22 Oktoba, 1959 wakati akihutubia Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (LEGCO) “Sisi watu wa Tanganyika, tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pamejaa chuki na heshima palipo na dharau”

“Ni mwaka wa 29 sasa toka Mbio za Mwenge wa Uhuru zilivyoanzishwa na waasisi wetu na umeendelea kuwa chombo muhimu kwa Taifa kwa kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu.” alieleza

Aliongeza kuwa Mwenge wa uhuru na mbio zake zimekuwa na faida kwa taifa ikiwemo kuendelea kuhamasisha Wananchi kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi.

Pia Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidhi ya Rushwa na matumizi ya Dawa za kulevya na sasa zitaichukua dhana ya Lishe bora kwa afya Imara ya Watanzania. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto zinazowakabili watanzania wote.

Aidha, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wote wa Zanzibar, kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwehe   Zanzibar na kuungana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kufanikisha shughuli muhimu kitaifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Leila Mohamed Mussa alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamefanikiwa kukamilisha maandalizi kwa asilimia 100.

“Watendaji wa Serikali zote mbili wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ufanisi wa uzinduzi hu una hivyo Mwenge huo kuanza kukimbizwa rasmi” alisema Mheshimiwa Leila

Alitumia pia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa Makunduchi na maeneo mengine mbalimbali kujitokeza kwa wingi.

Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2021, unahusu matumizi sahisi ya TEHAMA, chini ya Kauli mbiu isemayo: “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu .Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”. Pamoja na Ujumbe huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi na Viongozi kote nchini, kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, ugonjwa Malaria, mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya, Mapambano dhidi ya Rushwa na kuhamasisha Wananchi juu ya Lishe bora kwa afya imara.

MWISHO


Share:

Majaji Walioteuliwa na Rais Samia kuapishwa kesho, wakuu wa mikoa keshokutwa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho anatarajia kuwaapisha Majaji 28 wa Mahakama ya Rufani  na Majaji wa Mahakama Kuu aliowateua siku chache zilizopita.

Taarifa iliyotolewa leo na kusambazwa kwenye vyombo vya habari na , Mkurugenzi wa kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa imebainishwa kuwa hafla ya kuwaapisha majaji hayo itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kikwete.

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa keshokutwa Rais Samia atawapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi aliyowateua Mei 15, 2021.


Share:

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.


Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.


Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.


Share:

Mpyaa : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILIYOBORESHWA ZAIDI 2021...HABARI BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Share:

WAZIRI LUKUVI AVALIA NJUGA FIDIA KWA WANANCHI


 Na Munir Shemweta
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amejitwisha mzigo wa wananchi waliowasilisha kwake malalamiko ya fidia kwenye maeneo mbalimnbali nchini kupitia Program ya Funguka kwa Waziri kwa kuamua kuchukua hatua ya kuandika barua za madai kwa taasisi na idara zinazodaiwa fidia.

Hatua hiyo inafuatia wananchi wanaodai fidia kuzingushwa kupatiwa fidia ya maeneo yao yaliyotwaliwa kwa shughuli mbalimbali za maendeleo na kuamua kuwasilisha malamiko kwa Waziri wa Ardhi kupitia fomu maalum za Funguka kwa Waziri.

Akizungumza katika kipindi Maalum cha Funguka kwa Waziri kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC ONE tarehe 15 Mei 2021 saa tatu usiku, Lukuvi alisema, uchambuzi wa malalmiko/ migogoro ya matumizi ya ardhi iliyowasilishwa kwake kupitia Fomu za Funguka ulionesha malamiko mengi yapo kwenye masuala ya fidia.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, katika uchambuzi huo asilimia 39.4 ya malalamiko inaonesha yako katika masuala ya fidia huku uvamizi wa maeneo ukiwa na asilimia 29.4, migogoro ya kifamilia asilimia 22.9 na ile iliyopo mahakamni asilimia 5.5 na malalamiko ya milki  na upimaji pandikizi ikiwa ni asilimia 2.8.

‘’Rais alishatoa maelekezo wote waliochukua ardhi ya wananchi lazima walipe fidi, wote waliorudisha fomu za Funguka kwa Waziri kwangu mimi nimechukua uwakili na nitaandika barua kwa kila anayedaiwa fidia iwe Mkurugenzi, Katibu Mkuu au Mkurugenzi wa TANROADS’’ alisema Lukuvi.

Waziri Lukuvi ambaye alikuwa akimjibu mwananchi kutoka mkoani Arusha Hassan Othman Shao aliyelalamikia serikali ya kijiji cha Ngabodo kuchukua eneo lake bila kufuata utaratibu wa kulipa fidia alisema, suala la fidia kwa wananchi wanaochukuliwa maeneo yao siyo la hiari bali ni matakwa ya kisheria na limetamkwa pia katika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na linatakiwa kutekelezwa kwa wakati.

‘’ Napenda niwaambie  wote wanaofikiri kulipa fidia ni hiari, hakuna mali itakayochukuliwa bila fidia na ipo sheria ya utwaaji ardhi na ardhi inapotwaliwa, mtwaaji anatakiwa kulipa fidia kwa mmiliki wa asili na fidia lazima iwe kamilifu na kulipwa kwa wakati, iwe kwenye migodi,  barabara au uendelezaji wowote lazima walipe fidia’’ aliongeza Waziri Lukuvi

Akielezea Programu Maalum ya Funguka kwa Waziri, alifafanua kuwa ofisi yake tayari imeanza program hiyo awamu ya pili baada ya ile ya kwanza kuonesha mafanikio makubwa na kueleza kuwa katika awamu ya pili ya zoezi hilo, fomu zilisambazwa kwa wananchi kupitia ofisi za Kata, Vijiji na Mitaa na kufanyika chini ya uratibu wa Ofisi za Ardhi za Mikoa na Halmashauri zake.

Alisema, hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2021 jumla ya fomu zilizochukuliwa na wananchi zilikuwa 24,442 ambapo fomu zilizojazwa ni 3,171 na hadi sasa malalamiko yaliyokwisha fanyiwa kazi ni 1,144 ikiwemo wananchi husika kupatiwa barua za namna lalamiko/mgogoro  ulivyomalizika na hiyo ni katika mikoam mbalimbali.

Katika majibu yake kwa wananchi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo Fidia, Ufutaji Miliki za ardhi, Uvamizi wa Maeneo,Mdalali wa ufuatiliaji malalamiko, Utapeli katika masuala ya ardhi, Mauziano ya Ardhi yanayofanyika kienyeji, Makubaliano binafsi yanayozusha migogoroo ya ardhi, Mipango Miji pamoja na Urasimishaji.


Share:

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO APIGA KURA KUCHAGUA MBUNGE BUHIGWE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisubiria kukabidhiwa karatasi ya kupiga kura kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupiga kura Polling Station Wilayani Buhigwe MKoani  Kigoma Anania Emily leo Mei 16,2021 kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Buhigwe


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipiga Kura ya katika Kituo cha kupiga kura Polling Station Wilayani Buhigwe MKoani  Kigoma leo Mei 16,2021 kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Buhigwe.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Share:

Sales Representative – Geita at StarTimes

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB DESCRIPTION POSITIONS Sales Representative – Geita (1) DUTIES AND RESPONSIBILITIES Set the sales targets, and elaborate specific programs Develop and maintain the market agents Implement the channel sale policy, and formulate promotion plan Enlarge channel sales market and achieve expected sales targets Keep good relationship with dealers, and resolve the problem customers faced, dealing with […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Sales Representative – Mwanza (2) at StarTimes

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB DESCRIPTION POSITIONS Sales Representative – Mwanza (2)   DUTIES AND RESPONSIBILITIES Set the sales targets, and elaborate specific programs Develop and maintain the market agents Implement the channel sale policy, and formulate promotion plan Enlarge channel sales market and achieve expected sales targets Keep good relationship with dealers, and resolve the problem customers faced, dealing […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Sales Representative – Tabora at StarTimes

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB DESCRIPTION POSITIONS Sales Representative – Tabora (1) DUTIES AND RESPONSIBILITIES Set the sales targets, and elaborate specific programs Develop and maintain the market agents Implement the channel sale policy, and formulate promotion plan Enlarge channel sales market and achieve expected sales targets Keep good relationship with dealers, and resolve the problem customers faced, dealing with […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Regional Sales Manager – SIMIYU at StarTimes

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB DESCRIPTION POSITIONS Regional Sales Manager – SIMIYU (1) DUTIES AND RESPONSIBILITIES Set the sales targets, and elaborate specific programs Develop and maintain the market agents Implement the channel sale policy, and formulate promotion plan Enlarge channel sales market and achieve expected sales targets Keep good relationship with dealers, and resolve the problem customers faced, dealing […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

NURSES at Tindwa medical and health service

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Tindwa medical and health service is local registered company dealing with providing Emergency Medical Services, Waste and Environmental Management, Occupation Health and safety both local and international and Medical Supplies Services. Currently, it is looking for a position below… NURSES Duties and Responsibilities. Appropriately triage patients and initiate orders from approved protocols. Manages mechanically ventilated […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MEDICAL DOCTORS at Tindwa medical and health service

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Tindwa medical and health service is local registered company dealing with providing Emergency Medical Services, Waste and Environmental Management, Occupation Health and safety both local and international and Medical Supplies Services. Currently, it is looking for a position below… MEDICAL DOCTORS Duties and Responsibilities. Engage in direct clinical practice as the principal component of his/her […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 16,2021















Share:

SIMBA SC YAAMBULIA KICHAPO CHA MAGOLI 4 - 0 AFRIKA KUSINI


Klabu ya Simba imepokea kichapo cha mabao 4-0 na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa FNB Jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 

Mabao ya Kaizer Chiefs yamefungwa na Eric Molomowanadou Mathoho dakika ya sita, Samir Nurkovic dakika ya 34 na 57 na David Leonardo Castro Cortés dakika ya 63.

Sasa Simba SC watatakiwa kushinda 5-0 katika mchezo wa marudiano Jumamosi ya wiki ijayo ili kwenda Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1975.
Share:

Saturday 15 May 2021

JINSI NILIVYORUDISHA MCHUMBA WANGU KWANGU

 Kwa majina naitwa Aisha Hamisi,nina umri wa miaka 24.Ninafanya biashara ndogo ndogo katika mkoa wa Dar es salaam mtaa wa Kariakoo.

Biashara yangu ni kuuza nguo za kike na kiume hapa Kariakoo. Kazi yangu inanisaidia kuendesha maisha yangu ya kila siku hapa Dar es salaam. 

Siku moja nikiwa kazini kwangu nilikutana na kijana mmoja anaitwa Yusufu,Yusufu alianza tabia ya kuja kunitembelea kazini kwangu mara kwa mara na mwisho wake tukapeana namba za simu na kuanza kuwasiliana.

Siku zilivyokuwa zinasonga ndiyo jinsi mawasiliano yangu na Yusufu yalizidi hatimaye tukawa wapenzi na baada ya miezi 3 kuisha tukiwa kwenye mahusiano,Yusufu aliniomba tuwe wachumba bila kusita nilikubali kwa haraka maana nilimpenda sana Yusufu.

 Mahusiano yangu na Mchumba wangu Yusufu yalizidi kupamba moto,hatua hiyo ilisababisha ndugu na Jamaa kuweza kumfahamu Yusufu. Kulingana na mipango yetu tulikubaliana kuwa mwezi wa tano 2019 tuweze kuoana. Kwa Upande wangu niliona kuwa siku hazisogei kulingana na mawasiliano yangu na mchumba wangu Yusufu yalivyokuwa na mipango tuliliyokuwa tunapanga juu ya maisha yetu baada ya ndoa.

 Mwezi mmoja kabla ya ndoa kufika,Mchumba wangu alianza kubadilika bila sababu,ilifikia hatua nampigia simu hapokei na muda mwingine natuma message asubuhi ananijibu jioni au kutojibu kabisa. Kulingana na mazoea niliyokuwa nayo ya kuongea na Mchumba wangu nilishindwa kuvumilia tabia hiyo.

Kwa wakati huo nisingeweza kukutana na Yusufu kwa sababu muda huo alikuwa amerudi kwao mkoa wa Mwanza na mimi nipo Dar es salaam, NiLijikuta natoa machozi na kuongea pekee yangu mara kwa mara nikijiuLiza kwa nini Yusuyu kabadilika kiasi hicho na sikuweza kupata majibu kwa muda huo.

Mawasiliano yetu yalizidi kuwa mabaya zaidi kila kukicha,ikanibidi nimwambie Best yangu Fatuma juu ya hali niliyonayo na ninavyojisikia.Best yangu alishtuka sana na kuniuliza sababu gani Yusufu kabadilika hata sikuwa na jibu la kumwambia,Fatuma akaniomba namba ya Yusufu na kumpigia alipokea simu vizuri na kuongea na Fatuma.

Fatuma alipomuuriza juu ya mahusiano yangu na yeye na wapi nimemkosea au kumkwaza hapo hapo alikata simu hata bila kumjibu chochote Moyo wangu uliniuma sana na kuanza kutoa machozi ndiyo Fatuma akaniambia kuwa kuna doctor Kiwanga yupo nchi jirani ya Kenya.

Hapo hapo akampigia Best yake anaishi Manzese na kumuomba namba ya Doctor Kiwanga. Baada ya dakika 5 best yake Fatuma akatutumia namba hii +254 769404965 nikaweka kwa simu yangu na kupiga,Simu yangu ilipokelewa kisha nikajitambulisha doctor akaniuliza naitaji kusaidiwa nini,bila kusita nikaeleza mahusiano yangu na Yusufu na alivyonibadilikia na kumuomba Doctor anisaidie maana tarehe na mwezi tuliyokuwa tumekubaliana kufunga ndiyo ilikuwa karibu.

Hapo hapo kwa simu doctor akaniambia nisubiri dakika 35 nimpigie simu tena. Baada ya dakika 35 kuisha nilipiga simu na Doctor akaniambia kuwa kazi yangu itafanyika kwa siku mbili na ndani ya hizo siku akaniomba nisimpigie simu Yusufu wala kutuma text.

 Nakumbuka ilikuwa siku ya pili saa tano asubui nikaona simu yangu inaita nilivyopokea nikasikia sauti ya Yusufu,Moyo wangu ulishtuka sana pia kuwa na furaha muda huo. Ndiyo Yusufu akaniomba msamaha kwa kila jambo lililotokea hapo nyuma pia akaniambia yupo njiani anarudi Dar es salaam.

Bila kupoteza hata dakika 5 nilimpigia doctor na kumwambia hali halisi ilivyo na jinsi Mchumba wangu alivyopiga simu na kuomba msamaha.

Baada ya nusu saa Yusufu akanipigia simu tena na kuniambia kuwa kanitumia 500,000 kwa namba yangu ya vodacom kwa ajiri ya maandalizi ya baadhi ya vitu niliyokuwa nimemwambia hapo mwanzo.moyo wangu ulijaa furaha na kumpigia tena doctor kiwanga juu ya pesa niliyopewa kwa ajili ya maandalizi ya Harusi.

katika maongezi doctor akanambia ana uwezo wa kusaidia mtu popote alipo hata bila kufika ofisini kwake pia akasema anatatua shida kama kurudisha mpenzi ,kupata cheo kazini,kushinda kesi makamani,kusaidia watu ambao wana visirani na mikosi katika maisha yao pia kutatua changamoto zirizopo ndani ya familia.

 Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kiwanga doctors kunisaidia Kumrudisha mchumba wangu pia furaha ya moyo wangu bila kusahau kutoa shukrani zangu kwa best yangu Fatuma kwa kusimama na mimi kwa shida na karaha.

 Natoa wito kwa mwenye shida na matatizo mbalimbali tembelea website ya kiwanga doctors ambayo ni www.kiwangadoctors.com , Unaweza wapata pia kwa kupiga namba Au WhatsApp +254 769404965
Share:

NAMUNGO FC WAITUNISHIA MISULI YANGA SC ...MASHABIKI WAONDOKA KWA HASIRA BAO KUKATALIWA

Vigogo Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Hata hivyo mashabiki wa Yanga waliondoka na hasira uwanjani kufuatia refa Hance Mabena wa Tanga kukataa bao lao lililofungwa na mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne kwa kichwa akimalizia mpira wa kona kipindi cha pili.

Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 28 na inabaki nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wa mechi tatu mkononi, wakati Namungo FC yenyewe inafikisha pointi 36 baada ya mechi 26 nayo pia inabaki nafasi ya 10.

Via Binzubeiry blog
Share:

AZAM, SIMBA NA YANGA ZOTE ZATINGA ROBO FAINALI LIGI KUU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 20


TIMU za Simba, Yanga na Azam FC zimefuzu Robo Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kumaliza katika nafasi mbili za mwanzo katika makundi yao.

Pamoja na Simba walioshika nafasi ya pili Kundi B, Yanga walioongoza Kundi A na Azam FC waliomaliza nafasi ya pili Kundi A, timu nyingine ni Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Mwadui, Tanzania Prisons na JKT Tanzania.

Prisons na JKT wamefuzu kama ‘best losers’ baada ya kukusanya pointi nyingi kwenye nafasi ya tatu katika makundi yao ikilinganishwa na Ruvu Shooting.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger