Tuesday 20 April 2021
RAIS SAMIA AKUTANA NA SPIKA NDUGAI IKULU DODOMA
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI
WAZIRI UMMY AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI HALMASHAURI YA SENGEREMA
NAIBU WAZIRI KATAMBI: SERIKALI KUENDELEA KUWAPATIA VIJANA WA KITANZANIA MAFUNZO YA STADI ZA KAZI
RAIS WA CHAD AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA WAASI
Jeshi la Chad limetangaza kuwa Rais wa nchi hiyo Idriss Deby amefariki baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya waasi.
Deby alienda mwishoni mwa wiki kuvitembelea vikosi vya nchi hiyo ambavyo vinapambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo. Waasi hao wamevuka mpaka wakitokea Libya.
Kifo chake kimetokea ikiwa ni saa chache tu tangu matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Aprili 11 kuonesha kuwa anaongoza kwa asilimia 80. Kwa ushindi huo, Deby angeiongoza nchi hiyo kwa awamu ya sita mfululizo.
Serikali na bunge vimevunjwa na sasa baraza la kijeshi ndilo litakaloiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi 18 ijayo.
TBS YAFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KANDA YA MAGHARIBI KWENYE MADUKA YA VYAKULA NA VIPODOZI
Tanzia : MKURUGENZI WA SHUWASA FLAVIANA KIFIZI AFARIKI DUNIA
Monday 19 April 2021
WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA FEDHA WA WAKALA WA MABASI YA MWENDO KASI 'DART'
KOCHA JOSE MOURINHO AFUKUZWA KAZI
TIC YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA TANGA CEMENT JIJINI TANGA
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo |
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda
TANGA
MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda leo ametembelea na kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kiwanda cha Saruji cha Tanga Cement kilichopo Jijini Tanga huku akieleza kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na kampuni hiyo kwa kuchangia kiasi kibwa katika maendeleo ya nchi.
Meneja huyo wa TIC,Daudi Riganda amefanya ziara leo Jumatatu Aprili 19,2021 akiwa ameambatana na Nestory Kissima.
Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho, Bw. Riganda alisema mwekezaji wa Kampuni ya Tanga Cement ni miongoni mwa wawekezaji mahiri waliosajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania na kupewa hadhi ya wawekezaji mahiri.
Bw. Riganda alisema wamefika kiwandani hapo kuangalia uwekezaji uliofanyika na kuangalia mkataba “Performance Contract” uliosainiwa baina ya Serikali na Wawekezaji hawa ni namna gani ulivyotekelezwa na kila upande.
Katika ziara hii, TIC wamejionea uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 147.65 uliofanywa na kampuni hii, huku ajira zipatazo 330 za moja kwa moja na 677 zisizo za moja kwa moja zikitengenezwa kupitia uwekezaji huu. Kampuni ya Tanga Cement ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika kulipa kodi katika Kanda ya Kaskazini.
Aidha Alisema imeonekana kwamba kuna matokeo makubwa yaliyopatikana upande wa teknolojia ambazo zimeingizwa nchini kupitia mradi huo huku akieleza kufurahishwa zaidi na namna kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuajiri idadi ndogo ya wafanyakazi wa kigeni huku idadi kubwa ikiwa ni wafanyakazi wa Kitanzania, wengi wao wakiwa ni vijana wa kitanzania.
“Wapo wafanyakazi wa kigeni hawazidi watano na idadi kubwa walioajiriwa kwenye mradi huu wakiwa ni vijana wa Kitanzania kwa hakika hili limetufurahisha sana “Alisema
Meneja huyo alisema suala lingine ambalo limewafurahisha ni jinsi suala la mazingira na usalama kazini yalivyozingatiwa tokea unapoingia getini mpaka unapotoka kiwandani.
Hata hivyo, imebainika kuwa Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kupitia mkataba walioingia na wawekezaji hawa hasa katika kipengere cha msamaha wa kodi ya zuio “withholding tax” kwenye mkopo wa kigeni ulioingizwa na kampuni hii kutoka nchini Afrika ya Kusini kwa vile serikali ilipaswa kutoa notisi kwenye Gazeti la Serikali kuruhusu msamaha huo kitu ambacho hadi hii leo hakijafanyika.
Kutokana na dosari hii maafisa wa TRA waliwaandikia kuwataka kulipa kodi yote kama inavyopaswa na pale walipotoa maelezo walijikuta wakifungiwa akaunti zao za benki, kitu kilichowafanya kuanza kulipia kodi hiyo.
Bw. Riganda aliahidi kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha mamlaka za serikali zenye dhamana ya kuhakikisha mikataba inayoingiwa baina ya Serikali na wawekezaji inasimamiwa kama ilivyosainiwa.
Meneja huyo alisema wao kama Kituo cha Uwekezaji watawasilisha malalamiko hayo kwa mamlaka za serikali kupitia Mkurugenzi wao wa kituo cha Uwekezaji ambaye atazungumza na Waziri wa Uwekezaji ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia namna gani mikataba hiyo baina ya wawekezaji mahiri na serikali inaheshimika ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza kuwapata wawekezaji nchini.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema alisema huo ni mradi mpya wa laini ya kuzalisha Clinka uliogharamu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 147 na walisaini mkataba huo na TIC.
“ Lakini mpaka sasa haijatangazwa na Gazeti la Serikali na hivyo kuifanya Serikali kuonekana haijatimiza wajibu wake kulingana na mkataba ulioingiwa na pande hizo mbili, kitu kilichosababisha usumbufu kwa wawekezaji hasa kwenye masuala ya kodi ambazo TRA inawadai”, alisema.
Kampuni ya Tanga Cement ilikuwa na mpango wa kufungua kiwanda kingine cha saruji mkoani Arusha jirani na eneo la uwanja wa ndege wa KIA, mradi ambao ulikadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 50,hata hivyo wawekezaji hao wamesitisha mpango huo ambao ungetengeneza ajira na mapato zaidi kwa serikali, hadi hapo suala hili la kimkataba “performance contract” litakapopata suluhisho na kodi hiyo kusamehewa kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.
RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI JIONI HII
MPINA AMVAA CAG HASARA ATCL
WAKAMATWA WAKIIBA SIMU MECHI KATI YA SIMBA SC NA MWADUI FC IKIENDELEA...RPC ATAKA WALIOIBIWA WAKAZICHUKUE
WANAUME WAWILI WAANGUKA NA KUZIMIA BAADA YA KUIBA NGURUWE WA BIBI
Afisa Mkuu msaidizi wa polisi eneo la Shisembe Mike Shivanda amethibitisha kisa hicho kulingana na ripoti ya OB iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Shinyalu kwamba nguruwe hao waliibiwa Aprili 17,2021 majira ya saa nne asubuhi.
"Iliripotiwa na Mike Shivanda, chifu msaidizi, eneo dogo la Shisembe, kwamba wanaume wawili walianguka na kupoteza fahamu ndani ya kijiji cha Munyolo katika eneo la Murhanda takriban kilomita sita kaskazini mwa kituo hicho.
"Maafisa walitembelea eneo la tukio na kupata wanaume wawili, ambao ni; Nicholas Abung'ana, mwanaume wa Luhya mwenye umri wa miaka 50, na Alexander Savala, wa kiume wa Luhya mwenye umri wa miaka 50 wakiwa wamelala katika nyumba zao, hawawezi kuongea au kuamka," ripoti ilisema.
Mwanamke mzee ambaye nguruwe wake waliibwa alitambuliwa kwa jina Doris Achitsa, 65, ambaye anadaiwa kuwa mwajiri wa Abung'ana.
Achitsa ni binamuye Savala, ambaye ni mmoja wa washukiwa ambaye alipatikana amepoteza fahamu.
Kulingana na ripoti ya polisi kwenye kitabu cha matukio (OB), mwanamke huyo ambaye alionekana mwenye masikitiko makubwa alitafuta huduma za mganga mmoja Kaunti ya Bungoma ambaye alimtembelea nyumbani kwake majira ya saa 12 jioni na kufanya ibada zake kabla ya kuondoka ambapo ilipotimia saa 1 usiku, wanaume hao wawili walianguka na kupoteza fahamu.
Mfuasi huyo alikuwa ameacha maagizo kwamba mtu yeyote atakayeathiriwa asichukuliwe hospitalini bali aachwe katika hali yoyote aliyokuwa nayo hadi asubuhi atakaporudi.
Ndugu zao walisisitiza kwamba maagizo ya mfuasi wa ibada yazingatiwe.
Ripoti ya maendeleo ya kesi ya PUI ifuatwe," iliongeza.