Thursday 4 March 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 4, 2021



Magazetini leo Alhamis March 4 2021






















 

Share:

Wednesday 3 March 2021

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHAKI SHINYANGA MJINI..ATOA PONGEZI KWA VIONGOZI


Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akiwa ameshikilia boksi la chaki alipotembelea Kiwanda cha  Chaki 'Shinyanga Standard Chalk' na kujionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifuatiwa na mwenyekiti wa kiwanda hicho, Hashim Issa
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akisaini kitabu cha wageni ndani ya stoo ya Kiwanda cha  Chaki 'Shinyanga Standard Chalk'  wakati akijionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akiangalia chaki zilizotolewa kwenye mtambo muda mfupi baada ya kutengenezwa katika Kiwanda cha  Chaki 'Shinyanga Standard Chalk'
Muonekano wa maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba ametembelea Kiwanda cha  Chaki 'Shinyanga Standard Chalk' na kujionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho kinachoendeshwa na vijana kilichopo katika Mtaa wa Miti Mirefu Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kiwanda hicho Machi 2,2021, Mhe. Kirumba
aliwapongeza viongozi wa serikali wilaya ya Shinyanga kwa kuendelea kuwapigania vijana katika kupata fursa mbalimbali za  kiuchumi ikiwemo uanzishwaji wa  kiwanda hicho cha kwanza cha kutengeneza chaki katika mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Kirumba aliwapongeza vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kiwanda hicho, Hashim Issa kwa uthubutu wao kuanzisha kiwanda pamoja na changamoto zote wanazopitia ikiwemo ya kukosa soko la uhakika waendelee kutengeneza chaki nzuri na zenye kiwango.

Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na vijana hao, mbunge Santiel Kirumba aliwachangia kiasi cha shilingi 250,000/=  kama mchango wake katika  kuchochea shughuli za kiwanda.

Soma pia:
Share:

RAIS MWINYI ATEUA WANACHAMA WA ACT WAZALENDO KUWA MAWAZIRI


Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, amewateua wanachama wawili wa Chama cha ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban na Nassor Ahmed Mazrui kuwa mawaziri.

Kushoto ni Omar Said Shaaban, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda na kulia ni Nassor Mazrui, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Afya.

Uteuzi huo umeanza hii leo Machi 3, 2021, ambapo Omar Shaaban, ameteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda huku Nassor Mazrui, ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

Mwingine aliyeteuliwa leo ni Dkt. Saada Mkuya Salum, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na wote kwa pamoja wataapishwa kesho Machi 4.
Share:

KAKA WAWILI WAUANA BAADA YA WAKE ZAKE ZAO KUCHAPANA MAKONDE

Wananchi wakiwa eneo la tukio
**
Wenyeji wa Kaniga Makome eneo bunge la Muhoroni, kaunti ya Kisumu nchini Kenya wameachwa midomo wazi kufuatia kisa kilichoplekea kaka wawili kupoteza uhai wao. 

Wakazi waliomboleza kaka hao Joseph Othoro na Kennedy Otieno ila ndani yao maswali mengi yalibaki bila majibu kuhusu tukio hilo la kuogofya.

Otoro mwenye umri wa miaka 37 aliaga dunia usiku wa Jumatatu, Machi 1,2021 huku mdogo wake Otieno (36) akifuata mapema asubuhi siku iliyofuata. 

Kulingana na ripoti ya polisi , ndugu hao wawili walishambuliana kwa saa kadhaa usiku wa Machi 1,2021 na walipata majeraha ambayo yalisababisha vifo vyao.

 Mzozo baina yao uliibuka wakati wake zao walitandikana Jumapili, Februari 28,2021 hatua ambayo ilizidisha hasira kati ya Othoro na Otieno usiku huo.

Kaka hao walishambuliana bila huruma na kutokana na majeraha waliyokuwa nayo walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu.

 Otieno aliaga dunia wakati akikimbizwa hospitalini usiku naye Othoro alithibitishwa kufuata baadaye asubuhi ya Jumanne, Machi 2,2021.

Chanzo - Tuko News


Share:

MWALIMU AMKATA PANGA MWALIMU MWENZAKE OFISINI WAKIGOMBANIA PENZI LA MWANAFUNZI WA 'FIELD'

Picha haihusiani na habari hapa chini
*
Polisi katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata mwalimu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Karoti baada ya kudaiwa kumshambulia mwenzake kwa panga wakiwa afisini. 

Kamanda wa polisi Mwea Mashariki Daniel Katavi alisema mshukiwa huyo anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Wang’uru.

"Pia tumepata silaha ambayo inasemekana alitumia kumshambulia mwenzake katika eneo la shule," Kitavi aliiambia Citizen Digital.

 Kulingana na mkuu huyo wa polisi, mtuhumiwa alimshambulia mwenzake wa kiume kuhusu madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mwenzao wa kike ambaye yuko katika mazoezi ya kufunza shuleni humo. 

"Walimu hao wawili wa kiume wako kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mmoja wa kike ambaye yuko Field shuleni hapo, ”Kitavu alisema.

Mkuu huyo wa Mwea Mashariki alisema mtuhumiwa alidhani alikuwa amemuua mwenzake.

 "Alikuwa bado angali shuleni baada ya tukio hilo wakati wenzake walikuwa wakihangaika kumsaidia mwathiriwa na wengine wakiwaita maafisa wa polisi. 

Atashtakiwa kwa jaribio la mauaji, ” Kitavi aliongeza. Mhasiriwa, Alfose Orina anasemekana kuwa katika hali mbaya katika hospitali ya kibinafsi huko Mwea baada ya kukatwakatwa kichwani. 

Tukio hilo linajiri wakati Wizara ya Elimu inakabiliana na kuongezeka kwa visa vya utundu katika taasisi za elimu.

Waziri wa Elimu George Magoha alisema kuwa visa vya wanafunzi kuwashambulia walimu na utumiaji wa dawa za kulevya viliongezeka baada ya shule kufunguliwa Jumatatu, Januari 4.

 Wanafunzi katika taasisi mbali mbali kote nchini waliripotiwa kuchoma mabweni, kuwashambulia walimu na wanafunzi wenzao wakitumia silaha hatari.

Kuhusiana na kisa cha hivi punde kuwahusu walimu hao haijabainika iwapo Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) itachukua hatua dhidi ya mwalimu huyo.

Chanzo- Tuko News

Share:

Majaliwa: Tpa Imarisheni Usimamizi Wa ‘flow Meter’


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ihakikishe inaendelea kuimarisha usimamizi wa mitambo ya mita za upimaji wa mafuta (Flow Meter) ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona makusanyo yote ya mapato kutoka katika bandari zote nchini yanayokusanywa na TPA yanaingia katika mfuko mkuu wa Serikali na kwamba haitakubali kubaki na mtu yeyote anayejihusisha na upotevu wake.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hay leo (Jumatano, Machi 3, 2021) baada ya kukagua mitambo ya mita ya mafuta Kigamboni na Kurasini Oil Jety (KOJ) kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na utekelezwaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali aliyoyatoa katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 2016 alipofanya ziara katika eneo la mitambo ya mita ya mafuta (Flow Meter) ya Kigamboni na KOJ.

Amesema kipindi hicho teknolojia iliyokuwa inatumika haikuwa nzuri sana na ilikuwa inaifanya Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha mafuta na kusababisha mapato yaliyokuwa yakipatikana kuwa madogo, hivyo Serikali iliyopita ilifanya maamuzi ya kununua flow meter ya Kigamboni.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuimarisha ununuzi wa mitambo hiyo kwa lengo la kuboresha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara hasa kwenye sekta ya mafuta. ”Leo nimekuja kuona hatua sahihi tuliyofikia na nimeridhishwa na utekelezaji wake.”

Amesema baada ya kuona mifumo ya upimaji si sahihi sana Serikali ilipendekeza vinunuliwe viwanja Kigamboni ili kujenga matenki ambayo yatapokea mafuta kutoka bandarini, licha kupimwa katika ‘flow meter’ yanapopelekwa kwa mteja yatapimwa tena kuhakikisha mteja anapata kiwango sahihi cha mafuta anachokihitaji.

”Nimefurahi kupata taarifa kwamba viwanja vimenunuliwa na sasa zabuni ya ujenzi wa matenki mapya inafanywa, tukishafika hapo Taifa litanufaika sana kuwa na mafuta mengi yaliyopo kwenye akiba yetu. Pia hata wateja wanaotaka mafuta watakuwa wanaagiza wakati wowote kulingana na mauzo waliyoyafanya na kiwango wanachokihitaji kwa wakati huo.”

Waziri Mkuu amesema matanki hayo yatatoa fursa kwa nchi jirani ambazo zinatumia bandari hiyo kuagiza mafuta kwani wataweza kuhifadhi mafuta yao na kuiwezesha bandari hiyo kufanya biashara ya mafuta ndani na nje ya nchi. Ameagiza zabuni ya ujenzi wa matanki hayo iharakishwe ili ujenzi uanze mara moja.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Bandari iimarishe usimamizi wa ‘flow meter’ na pia inatakiwa ianzishe idara maalumu ya kuzisimamia katika bandari zote. Amesema watendaji wa idara hiyo ndio watakaowajibika kwenye utunzaji na utoaji wa huduma katika eneo hilo.

Awali, Mhandisi wa Idara ya Mafuta wa TPA, Mhandisi Yona Malago alimueleza Waziri Mkuu hatua zilizochukuliwa na TPA ili kuhakikisha ufanisi wa kushusha mafuta kupitia mita ya Kigamboni unafikiwa. ”Hatua ya awali ni ile iliyowezesha mita kufanyakazi bila kusimama na hatua ya pili ni kufanya ukarabati mkubwa wa mita ikiwemo kurekebisha machujio.”

Alitaja hatua nyingine zilizochukuliwa  kuwa ni pamoja na kuweka wafanyakazi wenye sifa, vigezo na uwezo wa kusimamia mita hizo ikiwa ni pamoja na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa umeme, mitambo na tehama na kufanya mafunzo kwa wafanyakazi wa TPA ambao wanasimamia utendaji wa mita hiyo.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Burundi Yaiomba Tanzania Kuisemea Kimataifa


Burundi imeiomba Tanzania kuendelea kuisemea nchi hiyo katika majukwaa ya Kimataifa ili iweze kuondolewa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Jumuiya ya Ulaya jambo linalozorotesha  maendeleo ya kiuchumi kwa nchi hiyo.

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Burundi, Mhe. Isidore Ntirampeba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi unaofanyika kwa ngazi ya wataalam mjini Kigoma tarehe 3 na 4 Machi 2021.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge amesema Tanzania itaendelea kuisemea Burundi katika majukwaa ya Kimataifa ili Burundi iondolewe vikwazo vyote vya kiuchumi ilivyowekewa ili kuipa nafasi nchi hiyo kuendelea na jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Pamoja na hilo Balozi Ibuge ameihakikishia Burundi kuwa, Tanzania itaendelea na jitihada zake za kuisadia nchi hiyo kuingia katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili iweze kuungana na nchi za ukanda huo katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

“Tanzania na Burundi zimeendelea kushirikiana kwenye Nyanja za Kimataifa na Kikanda kupitia Jumuiya za EAC, ICGLR, AU na Umoja wa Mataifa (UN). Ni kupitia ushirikiano huu, Tanzania itaendelea kuisemea Burundi katika majukwaa ya kimataifa ili iondolewe vikwazo vyote vya kiuchumi ilivyowekewa. Na kwa mara nyingine na uhakikishia ujumbe wa Burundi kwamba Tanzania itaendelea kuunga mkono ombi la nchi hiyo la kuwa mwanachama wa SADC” alisema Balozi Ibuge.

Katika hatua nyingine, Balozi Ibuge alieleza kwamba Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ni fursa nzuri ya kujadili masuala mbalimbali yenye manufaa kwa nchi zote mbili na kuwataka wajumbe wa mkutano huo kujipanga kutekeleza kikamilifu yale yote yatakayokubalika katika mkutano huo.

Mkutano huu umeanza kwa ngazi ya wataalam na utamalizika kwa ngazi ya Mawaziri tarehe 5 Machi 2021 ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AFrika Mashariki ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.


Share:

Ujumbe Kutoka U.A.E Kukagua Viwanda Vya Nyama Nchini


Na. Edward Kondela
Balozi wa Falme za Nchi za Kiarabu (U.A.E) hapa nchini Mhe. Khalifa Almarzooqi Abdulrahman amesema ataandaa wajumbe kutoka U.A.E kuja hapa nchini kutembelea viwanda vya kuchakata nyama ili kujiridhisha na ubora wa nyama kwa ajili ya kupeleka katika nchi zao.

Akizungumza leo (03.03.2021) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, mara baada ya kumtembelea katika ofisi ndogo za wizara hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam, balozi huyo amesema ni muhimu kwa viwanda vya kuchakata nyama vilivyopo hapa nchini kupata soko la uhakika katika nchi za Falme za Kiarabu kwa kuzingatia Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo.

Aidha, amewaasa wamiliki wa viwanda hivyo kuketi pamoja na kuwa na umoja wao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amemweleza balozi huyo kuwa viwanda vingi vya kuchakata nyama vinakabiliwa na changamoto ya masoko kupeleka bidhaa zao nchi za nje kutokana na kudaiwa kukosa sifa kulingana na baadhi ya sheria na kanuni zilizopo katika nchi hizo za kuingiza nyama kutoka nchi za nje.  

“Viwanda vyetu vya kuchakata nyama licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuchinja idadi kubwa ya ng’ombe, mbuzi na kondoo lakini bado vinakabiliwa na changamoto ya kukosa masoko ya kupeleka bidhaa zao mara baada ya kuchakata nyama.” Amesema Mhe. Ndaki

Kuhusu ujumbe kutoka Falme za Nchi za Kiarabu (U.A.E) kuja nchini kutembelea viwanda vya kuchakata nyama na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa kama alivyoahidi balozi wa U.A.E hapa nchini Mhe. Khalifa Almarzooqi Abdulrahman, Waziri Ndaki amesema ujumbe huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa viwanda hivyo kupata masoko ya bidhaa zao nchi za nje.

Pia, Waziri Ndaki kuhusu sekta ya uvuvi amemwambia balozi huyo kuwa serikali iko katika hatua mbalimbali za kuhakikisha uvuvi wa bahari kuu unaanza katika ukanda wa Bahari ya Hindi kwa kujenga bandari ya uvuvi pamoja na ununuzi wa meli za uvuvi.


Share:

WAZALISHAJI WA MAFUTA YA KULA NYANDA ZA JUU KUSINI WAPIGWA MSASA


Wadau wa mafuta ya kula Nyanda za Juu Kusini wakifuatilia kwa karibu mafunzo yaliyotolewa na TBS kwa kushirikiana na BRELA, SIDO na Wakala wa Vipimo.


Wazalishaji wa mafuta ya kula wametakiwa kufuata kanuni bora za kilimo, usindikaji na zile za afya ili kuongeza uzalishaji nanubora wa bidhaa hiyo nchini.

Wito huo ulitolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wauzaji, wasambazaji na wenye maduka yanayouza mafuta wapatao 972 yaliyofanyika katika mikoa minne ya nyanda za juu kusini kuanzia February 19 hadi 29 mwaka huu.

Mafunzo hayo yalihusisha wadau hao kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kutaka wazalishaji wa mafuta nchini kusaidiwa ili waweze kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyi.

Kwa sasa mafuta ya kula yanayozalishwa nchini ni tani 200, 000 kwa mwaka, wakati mahitaji halisi ni kati ya 400,000 hadi 600,000.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na BRELA, SIDO na Wakala wa Vipimo (WMA), ambapo kila mmoja alieleza wadau hao nafasi yake katika kufanikisha uzalishaji na ukuzaji biashara ya mafuta.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Udhibiti Ubora wa Bidhaa TBS, Baraka Mbajije, aliwataka wazalishaji wa mafuta kufuata kanuni bora za kilimo, usindikaji pamoja na za afya.

Mbajije alisema kanuni bora za kilimo zinahusiha mbegu bora, kuvuna kwa wakati na mazao yanayovunwa kwa ajili ya uzalishaji mafuta yanatakiwa yawe yamekomaa.

Kwa upande wa kanuni bora za usindikaji kwa mujibu wa Mbajije ni pamoja na kuzingatia usafi hasa kwenye mazingira ya viwandani.Alisema mazingira ya uzalishaji viwandani yanatakiwa kuwa safi pamoja na mashine zinazotumika.

Akizungumzia kanuni bora za afya, Mbajije alisema wazalishaji wanatakiwa kuhakikisha vifaa vya kuhifadhi mafuta ni safi ikiwa ni pamoja na madumu yanayotumika kuhifashi mafuta hayo yawe yamesafishwa vizuri.

" Madumu wanayoweka mafuta wahakikishe wameyasafisha vizuri na waweke lebo zinazoeleza bidhaa hizo ni za aina gani," alisema na kuongeza kwamba haikubaliki kwenye vifungashio ambavyo wazalishaji wanaweka mafuta iwe lebo inayohusu bidhaa nyingine.

Aidha, alisema mafuta ya kula hayatakiwi kuwekwa juani, kwani yanapokuwa juani kuna kemikali zinazozalishwa na zinaweza kusababisha magonjwa ikiweno kansa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Abel Mwakasonda, alitoa mwito kwa wadau hao kusajili TBS majengi ya bidhaa za vyakula na vipodozi.

Alisema kwa kufanya hivyo Shirika hilo litaweza kuwafikia kwa urahisi.

" Tunatoa mwito kwa wadau kufika TBS, wasiogope kama kuna makosa tutawasaidia kuyarekebisha," alisema Mwakasonda.

Alisema ni muhimu kwa wafanyabishara kusajili bidhaa na majengo ya vyakula na vipodozi kwa mujibu wa sheria ambayo imetokana na mabadiliko ya Sheria ya fedha ya mwaka 2019.

Sheria hiyo ilirudisha majukumu ya usimamizi wa usalama na ubora wa vyakula na vipodozi kwa TBS kutoka kwa iliyokua Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA).

Alisema usajili wa bidhaa majengo ya vyakula na vipodozi ni takwa la kisheria ili kuwawezesha kufanya biashara zao urahisi.

Usajili majengi ya biashara unawapa wafanyabiashara uhakika wa kutunza bidhaa na wanasajili jengo kulingana na bidhaa zinazoenda kuhifadhiwa humo.

Kwa upande wa usajili wa bidhaa, eneo linalohusika ni bidhaa za chakula na vipodozi.Usajili wa vipodozi vilivyopigwa marufuku kwenye soko la Tanzania haviingizwi nchini kutokana na kuwa na viambata sumu.

Mafunzo hayo kwa wazalishaji wa mafuta ni mwendelezo wa mafunzo yaliyokwisha kutolewa katika mikoa Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma.

Share:

UKARABATI WA MTO LUKOSI RUAHA MBUYUNI WAKAMILIKA

Mhandisi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daniel Manase akizungumzia kuhusu kazi ya kurejesha Mto Lukosi katika njia yake asili, Ruaha Mbuyuni Mkoani Iringa.


 

Mtambo aina ya Excavator ukifanya kazi ya kuiinua tuta kwa kupanga mawe katika mto Lukosi, ili kuurejesha katika njia yake ya asili.

Picha ni Banio linalotumika kupitisha maji kutoka katika chanzo na  kupeleka katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Ruaha Mbuyuni
Picha inaonesha Muonekano wa Tuta, likiendelea kufanyiwa kazi katika mto Lukosi, Ruaha Mbuyuni

 

Na Mwandishi  Wetu,Ruaha Mbuyuni–Iringa

Ukarabati wa kingo za Mto Lukosi uliyopo katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, unayopeleka Maji yake katika mto Ruaha mkuu na kutumika katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni, umekamilika baada yakusombwa na mafuriko makubwa yalitokea mwaka jana, yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika ukanda wa nyada za nyanda za juukusini.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo Mhandishi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Daniel Manase alisema mafuriko hayo yaliyoharibu kingo yenye urefu wa takribani mita 180, yalisababisha kingo za mto kubomoka n ahivyo mto kuacha njia ya asili nakuanza kupita kwenye mkondo mpya uliojitokeza.


Aliongeza kwakusema kuwa Kuhama kwa mto kulipelekea banio la skimu ya Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni kukosa maji na mazao yaliyokuwa shambani yalikauka, Mhandisi Manase Alisema, baada ya kufika katika eneo hilo nakuona hali halisi kazi kubwa ilikuwa nikutengeneza barabara ya muda kwanza ili kuweza kufika katika eneo liliko haribika kutokana na mazingira kutokuwa rafiki.

Alisema, Kazi ya ujenzi iliendelea kwa kujaza mawe na vifusi katika ujenzi wa tuta ili kulimmarisha.

“Pamoja na kwamba tulikuwa na vifaa vyetu, tulipata msaada wanyongeza ya eskaveta, kutoka kwa muwekezaji Kilimanjaro express anayefanya uwekezaji katika maeneo hayo, nakufanya kazi usiku na mchana karibia masaa 29, ili kuweza kuzunguka na kuziba gema maana maji yalikuwa yanakula gema.”Alibainisha.

“Tulizunguka kwa umbali wa kilometa 25 ili kuweza kubeba mawe na vifusi kuhakikisha kazi inakamilika, mwanzoni tulikuwa tunazunguka umbali wa kilomita tano kutokana na kwamba hali haikuwa nzuri ikabidi tuzunguke hizo kilomita 25.”Alisisitiza Mhandisi Manase.

Mhandisi Manase alisema, Kazi ya kupandisha tuta ilikuwa na changamoto ya mvua kutokana na kwamba vifaa vilikuwepo, magari yaliyokuwa yakikwama yalikwamuliwa.

Aliendelea kusema kuwa kwasasa kazi hiyo imekamilika na wananchi katika maeneo hayo wanaweza kuendelea na shughuli za kilimo katika skimu ya Ruaha mbuyuni kama kawaida kwani hali ya mazingira sasa imesharudi katika hali yake ya kawaida.





Share:

MWENDESHA BODABODA AKATWA SHINGO KWA WAYA WA UMEME BARABARANI



Mfano wa nyaya za umeme
**
Na Yeremia Ngerangera - Namtumbo

Dereva wa pikipiki katika kijiji cha Mgombasi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma Kaimu Kinokwite (28) amekufa kwa kukatwa shingo na waya wa umeme baada ya kunaswa na waya uliokuwa umekatisha barabara.

Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mgombasi Hance Mwailima alisema kuwa walimwona kijana huyo akirushwa kutoka katika pikipiki na kutupwa mbali baada ya kunaswa na waya huo.

Mwailima alidai marehemu alimbeba abiria wakitokea mgombasi madukani (kijiweni) wakielekea kijiji cha Mtumbatimaji katika harakati za kununua mahindi na walipofika katika kitongoji cha Dodoma jirani na shule ya msingi Mgombasi walipatwa na mkasa huo na mwenzake alikimbia .

Aidha mwailima alidai katika eneo hilo la tukio hapakuwa na alama yoyote iliyowekwa kuashiria kuwa kuna kazi ya kuweka nyaya za umeme katika nguzo za umeme hali iliyomfanya dereva wa bodaboda huyo kukumbana na mkasa akiwa katika mwendo kasi .

Kaimu mtendaji wa kijiji cha Mgombasi bwana Saidina Assedi Sandali alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa marehemu alifikishwa kituo cha afya Namtumbo licha ya kuwa alishafariki katika eneo la tukio .

Mtendaji wa kata ya Mgombasi bwana David Julius Kitalika pamoja na kukiri kutokea kwa kifo hicho aliwataka madereva wa pikipiki kuwa waangalifu muda wote wakiwa barabarani hasa katika kipindi hiki cha utengenezaji na uwekaji nyaya za umeme unaendelea katika vijiji vya kata ya mgombasi.

Marehemu karimu alizikwa katika makaburi ya minazini kata ya Rwinga katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo wanakoishi wazazi wake.

Via Michuzi blog

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 3,2021

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger