Sunday, 1 December 2024

SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE

 
Utendaji kazi wa kiwango cha juu wa Rais Samia Suluhu Hassan, umewezesha eneo kubwa la nchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa mijini na vijijini hali iliyoifanya Serikali kutaka mafanikio hayo yalindwe.

Ikumbukwe kuwa  hadi kufikia Februari 2024, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ilifikia asilimia 79.6 ikilinganishwa na asilimia 77 Februari, 2023.

Kwa upande wa mijini upatikanaji wa maji umefikia asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 88 Februari 2023.

Mafanikio hayo ni makubwa na ndio yamempa nguvu Kaibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuwataka watumishi wa Sekta ya Maji kuhakikisha wanalinda mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.

Mhandisi Mwajuma ametoa agizo hilo katika kikao chake na watumishi wa Wizara hiyo jijini  Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Rais Samia, kupitia Wizara ya Maji, imeweka malengo makubwa ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa uhakika wa maji safi na salama kwa wananchi wote nchini. 

Malengo haya ni sehemu ya juhudi za kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kwa mujibu wa mpango wa serikali ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafikiwa asilimia 95% ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wa wananchi wa Vijijini asilimia 85 wawe wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.

Malengo hayo yanategemewa kufanikishwa na miradi mbalimbali kama Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), ambayo inalenga kuboresha miundombinu ya maji na kuongeza upatikanaji wa maji vijijini na mijini. 

Serikali pia inashirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa ili kufanikisha malengo haya.

Share:

Saturday, 30 November 2024

TRA YAENDELEZA REKODI YAKE UANDAAJI WA MAHESABU TUZO ZA NBAA


Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA) yaibuka mshindi wa jumla kwenye uandaaji wa hesabu za kifedha zinazozingatia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) na Sekta za Kibiashara (IFRS). Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) jana 29/11/2024.

Vilevile, TRA imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories)kwenye tuzo hizo.

Akizungumza baada ya kupata tuzo hizo Naimbu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha amesema tuzo hizo ni uthibitisho wa dhamira ya TRA ya kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na weledi katika matumizi sahihi ya viwango vya juu vya kitaalamu katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa zake za kifedha.

Bw. Mcha ameongeza kuwa TRA inao watumishi wenye weledi wa kutosha katika usimamizi bora wa kifedha na uandaaji wa taarifa zinazozingatia viwango vya kimataifa. “Tuzo hizi ni uthibitisho kuwa TRA tunao watumishi wenye weledi katika kusimamia, kuandaa na kuwasilisha taarifa za fedha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa”.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imekuwa ikiandaa tuzo kila mwaka kwa waandaaji wa taarifa za kifedha zinazozingatia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) na Sekta za Kibiashara (IFRS) ambapo tuzo za uwasilishaji wa taarifa za kifedha kwa mwaka 2023 zimetolewa jana tarehe 29.11.2024 APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Share:

NAIBU WAZIRI SAGINI- MSIKATISHWE TAMAA KATIKA KUPAMBANIA HAKI ZA BINADAMU


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu umetakiwa kutokukata tamaa licha ya kupitia kadhia ya vitisho,kutukanwa na kupewa majina mabaya wakiwa katika jukumu lao la mapambano yao dhidi ya udhalimu na dhuluma dhidi ya haki za binadamu.

Hayo yamesemwa leo Novemba 29,2024 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Jumanne Sagini katika maadhimisho ya kusherekea  siku ya wanawake watetezi wa haki za binadamu ambayo hufanyika Novemba 29 kila mwaka.

Amesema Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na masuala ya haki za binadamu,wanajukumu la pamoja la  kuweka mifumo ambayo itawezesha wanawake hao wanaohusika na utetezi wa haki za binadamu,kufanya kazi yao katika mazingira salama.

"Mmeweza kushawishi serikali kuwa na Sheria zinazotoa usawa wa kijinsia  na kukemea sheria kandamizi dhidi ya wanawake na wasichana,mmechangia pia ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za maamuzi" Amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu,Wakili Maria Matui amesema kuwa bado hakuna mfumo rafiki ambao unamwezesha mwanamke mtetezi kufanya kazi yake bila hofu

"Tumeona bado hakuna mfumo wa kumtetea mwanamke huyu anayewasemea walio wengi ambao hawawezi kujiongelea haki zao"Amesema.

Sambamba na hayo,Wakili Matui ametoa ombi kwa serikali kuunda mifumo itakayomsaidia  mwanamke mtetezi wa haki za binadamu ili kumuweka katika mazingira salama katika utekelezaji wa jukumu hilo.

Nae Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Suzan Namondo amesema Muongozo huo wanao utarajia wanategemea usaidie kuanzia ngazi ya chini ya Kijiji hadi kitaifa ili kutetea haki za binadamu wakiwa wanajiamini kulingana na sheria na taratibu za nchi.

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kumbukizi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Mtandao huo.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 30,2024

Share:

Friday, 29 November 2024

BUTONDO ASHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo,ameshiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye kituo cha kitongoji cha Nzugimtogwe Lagana.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umefanyika leo Novemba 27,2024 ambapo wananchi  wamechagua Mwenyekiti wa kijiji,kitongoji, Mtaa na wajumbe ambao wataongoza ndani ya miaka mitano hadi 2029.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger