Thursday 17 October 2024

UZUSHI WA WANAHARAKATI DHIDI YA RAIS SAMIA WAFICHUKA



Katika mazingira ya kisiasa yanayozidi kujaa maneno ya uzushi na habari za kughushi, kundi moja la wanaharakati wanaojificha jijini Nairobi limejikuta katika fedheha kubwa baada ya kujaribu kumchafulia jina Rais Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutumia taarifa za uongo.

Kundi hili linadai kuwa CCM imenunua magari aina ya Toyota Land Cruiser kwa bei ya dola za Kimarekani 200,000 (sawa na shilingi milioni 540 za Kitanzania). Hata hivyo, taarifa hizo zilihusishwa na picha zinazodaiwa kuonyesha magari hayo yakipakiwa katika eneo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Lumumba, Dar es Salaam.

UKWELI ULIVYO

Baada ya uchunguzi wa haraka kupitia mtandao wa Google, ukweli ulibainika kuwa picha zilizotumiwa na wanaharakati hao si za magari yaliyonunuliwa na CCM, wala hayakuhusiana na Tanzania. Picha hizo zinatokana na makala ya BBC Top Gear yenye kichwa cha habari “This Secret Dealer Is Selling New Old Toyota Land Cruisers That Are Supposed To Save The World.” Magari hayo yameonekana yakiwa yamepakiwa kwenye stoo moja nchini Uholanzi, yakisubiria wateja.

Tukio hili linaonyesha wazi jinsi wanaharakati hao walivyojaribu kutumia mbinu za udanganyifu kueneza habari potofu kwa lengo la kuipaka matope serikali ya Rais Samia. Picha hizo zilikuwa ni za magari ya Toyota 650 ambayo hayahusiani kabisa na Tanzania, achilia mbali UVCCM.

MBINU ZA KUPOTOSHA NA AJENDA BINAFSI

Wanaharakati hawa wamekuwa wakijaribu kwa muda mrefu kumchafua Rais Samia na uongozi wake kwa kueneza taarifa za kughushi. Inaonekana wameishiwa hoja za msingi, na sasa wanatumia mbinu za kutunga hadithi za uongo, huku wakilenga kuendeleza ajenda zao zisizokuwa na msingi wa kweli.

Kile kinachowasukuma wanaharakati hawa ni uhitaji wa fedha kutoka kwa wafadhili wa nje, ambao wanasubiri kuona ajenda inayoendeshwa dhidi ya serikali ya Tanzania. Katika jitihada za kujihakikishia fedha hizi, wanaharakati hawa wamekuwa wakiwalipa vijana wa mitandao ya kijamii ili kusambaza uzushi unaolenga kupotosha umma kuhusu uongozi wa Rais Samia.

KIPAJI CHA UONGO KIMEFIKIA KIWANGO CHA JUU

Mbali na kuwa na ajenda za kisiasa, wanaharakati hawa wanaonekana kuwa na kipaji cha hali ya juu cha kuunda hadithi za uongo. Walakini, badala ya kutumia kipaji hicho kwa manufaa ya jamii, wanakitumia kutunga simulizi za kupotosha ili kuwadanganya wananchi na ulimwengu mzima.

Pengine sasa ni wakati mwafaka kwa wanaharakati hawa kufikiria njia nyingine ya kutumia kipaji chao cha kutunga hadithi. Badala ya kuzusha na kueneza uongo kwa lengo la kupata fedha, wanaweza kutumia uwezo wao huo wa ubunifu kutunga script za tamthilia au filamu, ambazo zinaweza kupata nafasi kwenye runinga au majukwaa ya burudani. Bila shaka, wanaharakati hawa wana uwezo wa kuwa "director" wa uongo, na "Mariawood" inaweza kuwa kiwanda sahihi cha kuzalisha hadithi zao za kufikirika.

HITIMISHO

Kisa hiki cha udanganyifu kinathibitisha jinsi baadhi ya wanaharakati wamepoteza uhalali wa hoja zao na kuamua kuingia kwenye njia ya uongo na uzushi. Taarifa zisizo na msingi kama hizi zinaharibu hadhi ya siasa za Afrika na kuchochea migogoro isiyo na sababu. Ni muhimu kwa jamii kuwa na uwezo wa kuchuja na kuhoji taarifa zinazotolewa na vyanzo visivyo na uhakika, kwani ukweli hauwezi kusimama na uzushi.

Katika nyakati hizi ambapo ukweli na uongo vimechanganyika, tukio hili linatufundisha kwamba uchunguzi wa kina na uhakiki wa taarifa ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote. Wananchi wanapaswa kuwa macho dhidi ya propaganda zinazolenga kupotosha ukweli, ili kulinda amani na utulivu wa taifa.

Share:

MRADI WA MAJI NGARA KUNUFAISHA MAELFU YA WANANCHI, HISTORIA NYINGINE KUANDIKWA

 

 Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog.

Changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama inatajwa kuwa historia kwa siku za usoni kwa wananchi wa Kijiji cha Katerere Kata ya kanazi Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Ruhoro kukabidhi mradi wenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kwa Mkandarasi unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 16, 2024 ambapo Mkandarasi anatarajiwa kuanza utekelezaji huo ndani ya siku saba ambao utatekelezwa kwa kipindi kisichozidi miezi nane ukiwa na lengo la Kumtua mama ndoo kichwani ambapo mara baada ya kukamilika wanatarajia kuingiza maji kwa kaya 100.


Mradi huo ambao ni neema kwa wananchi hao ni baada ya Serikali kufanya juhudi za muda mrefu za kuchimba visima ambavyo juhudi ziligonga mwamba kwa kukosa maji na hatimaye suluhisho limepatikana.


Ndaisaba amewataka wananchi kutunza mradi huo ili uweze kuwahudumia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kumtaka mkandarasi huyo kufanya kazi nzuri ili kutimiza mkakati wa Serikali ya kuhakikisha mwananchi anapata huduma zote muhimu kwa wakati.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa kufanikisha mpango wa wananchi kupata maji safi.














Share:

KAWAIDA AMJIBU LEMA, HIZI HAPA SABABU ZILIZOWAFANYA VIONGOZI WA CHADEMA KUTIMKIA CCM

Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida akihutubia wananchi wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Oktoba 17, 2024.

Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog.

Kufuatia Kauli za kiongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godless Lema zilizozua taharuki katika mitandao ya kijamii kuwakashfu baadhi ya viongozi na wasimamizi wa uandikishaji daftari la mkazi akilalamikia kutokufuata taratibu rasmi Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida ameonyesha kustaajabishwa na jambo hilo.


Hayo yamejiri leo Oktoba 16, 2024 Wilayani Ngara Mkoani Kagera wakati alipokuwa kwenye ziara ya kawaida ya kukijenga Chama ambapo pamoja na mambo mengine ametolea ufafanuzi wa mada hiyo na kwamba haina uhalisia bali analenga kuvuruga uchaguzi kwa kupotosha umma.


"Leo Asubuhi wakati naangalia mitandaobya kijamii nikamuona kiongozi mmoja wa upinzani Godless Lema akilalamika na kuaminisha umma eti Kuna mambo ya ovyo yanafanyika, kuwa wakurugenzi wa uchaguzi na mawakala wanaosajili watubkwenye madaftari ya makazi kwamba wanawasajili wanafunzi wa shule katika lile Daftari". Amesema Kawaida


“Tunalaani kitendo hichi, wanataka tuwapore watu haki zao za msingi?, tunawataka waendelee kusajili muhimu wawe wametimiza umri wa kupiga kura hata kama bado anasoma, wangetumia muda mwingi wa malalamiko kuwahamasisha watu waende kujiandikisha na waweze kupigiwa kura” Kawaida.


Ikumbukwe kuwa kauli hiyo imekuja mara baada ya Godbless Lema kudai kuwa baadhi ya vituo vya uandikishaji havifanyi kazi kwa uadilifu na kwamba baadhi ya maafisa wa uandikishaji wanakwepa taratibu rasmi hivyo haridhishwi na mwenendo wa zoezi hilo linaloendelea Nchini.


Aidha katika Mkutano huo Kawaida akiambatana na viongozi wengine wamepokea wanachama wapya waliokuwa viongozi watatu kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM huku chanzo wakieleza ni kuridhishwa na maendeleo wanayoyapata nchini yatokanayo na Utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala CCM.


Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida amempongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa jitihada anazozifanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kuanzia ngazi ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwainua kiuchumi.


Mamia ya Wananchi wakifurahia jambo katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.


Sehemu ya wananchi walioshiriki katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.



Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro akihutubia mamia ya wananchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.


Wananchi wakifurahia jambo katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.


Picha za Matukio Mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.


Picha ya pamoja: Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida, Viongozi wa Chama, Mbunge wa Jimbo La Ngara Ndaisaba Ruhoro katika picha ya pamoja na wanachama wapya waliokuwa Viongozi wa CHADEMA ambao wamekaribishwa rasmi kwasasa ni wanachama wa CCM  Oktoba 17, 2024  Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida akimkaribisha mwanachama mpya kutoka CHADEMA Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
















Share:

Tuesday 15 October 2024

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA VETA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewahamasisha vijana kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA, ili waweze kuajiriwa au kujiajiri kwa urahisi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo juzi, tarehe 11 Oktoba 2024 alipokuwa akizindua Wiki ya Vijana Kitaifa katika uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza.

Amesema Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa vijana kupitia ujenzi wa vyuo vya VETA ambapo vyuo vipya 25 vimekamilika na vingine 65 vinajengwa katika kila wilaya na kwamba jukumu lililobaki ni la vijana kujiunga na mafunzo katika vyuo hivyo ili kujipatia ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas P. Katambi (MB) ameipongeza VETA kwa juhudi za kusaidia kukuza na kuendeleza ubunifu wa vijana.

Katambi ameyasema hayo alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho hayo, tarehe 10 Oktoba 2024 na kujionea ubunifu mbalimbali wa wahitimu kutoka vyuo vya VETA nchini.

Kipekee, Mhe. Katambi amevutiwa zaidi na ubunifu wa mhitimu wa chuo cha VETA Mwanza, Benjamin Samweli ambaye ametengeneza gari linalotumia injini ya pikipiki lenye uwezo wa kubeba nusu tani, kutembea Kilometa 80 kwa saa, kutumia lita moja kwa Kilometa zaidi ya 20.

“Serikali katika Sera yake ya maendeleo ya vijana imeongelea kuwezesha vijana wenye uwezo na vipaji kuhusiana na ubunifu na uvumbuzi. VETA fuatilieni COSTECH kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kumsaidia mhitimu huyu kukuza na kuendeleza kipaji chake kwa kupatiwa mkopo nafuu ili aweze kuendeleza kipaji chake,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na Mafunzo na Elimu ya Ufundi Stadi ili kukuza uchumi wao kupitia ajira rasmi na zisizo rasmi.
Share:

SERIKALI KUANZA MAHOJIANO RASMI NA WAKIMBIZI


Serikali ya Tanzania inatarajia kuanza mahojiano ya kina na wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini ifikapo 2025. Mahojiano haya yatashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Lengo kuu ni kubaini changamoto wanazokabiliana nazo wakimbizi na kutafuta suluhisho la kudumu kulingana na maoni yatakayokusanywa katika mahojiano.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo, alipowasilisha ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 75 wa Kamati Tendaji ya UNHCR nchini Uswisi, tarehe 15 Oktoba 2024.

Mhe. Sillo alibainisha kwamba Tanzania inahifadhi wakimbizi zaidi ya 240,000, wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alisema serikali imefanikiwa kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi 17,283 kwa mwaka huu, ambapo wakimbizi 12,717 walirudi kwa hiari katika nchi zao za asili, na 4,566 walipatiwa makazi mapya katika mataifa mengine.
Aidha Mhe. Sillo katika Ujumbe wake alieleza kuwa licha ya Mafanikio hayo, Operesheni za Kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, hasa katika sekta za afya na elimu katika kutoa huduma bora kwa Wakimbizi

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake katika kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi na sasa kujikitika katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa Wakimbizi hao. Aidha alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana ili kusaidia wahanga wa migogoro na kuhakikisha wanapata misaada inayohitajika.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger