Friday 11 October 2024

ALIIBA NG'OMBE WANGU ILI AKALIPE MAHARI

Jina langu ni Simon kutoka kaunti ya Vihiga, nilikuwa mfanyabishara haswa wa kilimo, nilikuwa na ng’ombe wawili wa maziwa ambao walikuwa wananipa faida kubwa sana kutokana na uuzaji wa maziwa.

Nilifanya pia ukulima wa nyanya lakini uuzaji maziwa ulikuwa na faida sana kulinganisha na kilimo cha nyanya, kazi hii iliniwezesha kulipia wanangu karo ya shuleni, kuwezesha wanangu kupata lishe bora na hata kufanya maendelea mengi pale nyumbani.

Ng’ombe wangu walikuwa wenye afya kutokana na mimi kujua ni kipi haswa walihitaji ili kuleta faida, ila siku moja niliamka na kukuta zizi la ng’ombe langu lilikuwa wazi.

Kufumba na kufungua macho hapakuwa na mifugo wangu niliowategemea, nilikumbwa na mshutuko wa moyo na hata nilidhani kwamba walikuwa tu karibu, kumbe walikuwa tayari wameshaibiwa.

Niliripoti kituo cha Polisi mjini Luanda, niliamini kwamba Polisi wangenisaidia kupata haki lakini kila mara walisema kwamba walikuwa wakifanya uchunguzi kubaini ni wapi walikuwa mifugo wangu.

Ama kwa hakika sikuridhishwa na majibu yale ya polisi kwani nilikuwa nikitaka mifugo wangu, mara Eunice akanielekeza kwa Dr Bokko, aliniambia ni mtaalamu wa mitishamba ambaye anaweza kunisaidia kupata suhisho.

Nilifika kwa Dr Bokko na akanishugulika na kunipa ukakika kwamba baada ya siku mbile wezi wa mifugo yangu yatapatika wala nisiwe na wasiwasi.

Siku tatu baada ya kurejea nyumbani, niliitwa kwenye familia moja kwa uharaka, nilipofika nilipata umati mkubwa wa watu nje ya nyumba ya mtumishi mmoja.

La kushangaza ni kwamba alikuwa ni Pasta wa dhehebu letu, yeye ndiye alikuwa ameiba mifugo yangu, alisema kwamba alifanya vile kwa kuwa alitaka kuwatumia kulipa mahari yake.

Niliwarejesha mifugo wangu nyumbani, tangu siku ile hakuna yeyote anayethubutu kushika mali yangu.

Pia Dr Bokko hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa, husuluhisha shida za kifamilia kama kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba na mwenza wako wa maisha nk. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Dr Bokko kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

WADAU WA SEKTA YA MADINI WATEMBELEA BANDA LA TBS MAONESHO YA SABA YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA


Na Mwandishi Wetu, Geita

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekutana na wadau wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla na kuwapata elimu kuhusu masuala ya madini.

Shirika hilo limekutana na wadau pamoja na wananchi hao kuwapatia elimu hiyo kwenye Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita kuanzia Oktoba 02 ambapo yatafungwa Oktoba 13.

Maonesho hayo yalifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo jana, Afisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, alisema shirika hilo linaandaa viwango vya sekta ya madini, hivyo alisema kupitia maonesho hayo wanakutana na wadau wa sekta hiyo na kuwapa elimu.

Aidha, Mtemvu alisema mbali na kukutana na wadau wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla, kupitia maonesho hao wanakutana na wajasiriamali na kusikiliza na kutatua changamoto zao na kuwaelimisha na kuwahamasisha kuhusishana na umuhimu wa kuzalisha bidhaa zilizothibitishwa ubora na shirika hilo.

Mtemvu alisema shirika hilo litaendelea kutimiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wajasiriamali wanashiriki katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.

Alisema Serikali inatumia sh. milioni 250 kwa mwaka kugharamia gharama zote za wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha, hivyo wanapofika TBS wanapata huduma hiyo bure.

"Ndiyo maana tumetumia fursa hii na Maonesho ya Madini kuelimisha taratibu za kufuata ili kuwezakuthibitisha bidhaa zao bure," alisema Mtemvu.

Akifungua maonesho hayo ,Dkt. Biteko alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha, kuvutia na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya madini ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.
Share:

Thursday 10 October 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 11, 2024

Share:

NJIA TULIYOTUMIA KUSHINDA KESI BAADA YA KUDHULUMIWA SHAMBA LETU

Jina langu ni Juma, siku moja mtu mmoja tajari alivamia shamba letu na kukatakata kila kitu kilichokuwa humo kama mazao na hata kubomoa nyumba yetu na kudai kuwa shamba hilo lilikuwa lake na hakutaka kuona mtu yeyote shambani humo.

Alimuonya mama yangu hasiaribu kumshtaki kortini kwani atakuwa anapoteza muda wake kama yeye ana fadha nyingi na kuweza kuwapa Majaji wa Mahakama rushwa hivyo ni lazima kuwa atashinda.

Hivyo kwa uwoga mama yangu alinyamaza kama maji mtungini, aliweza kunipigia simu na kuniarifu yote hayo na kuniomba niende nyumbani kumsaidia jambo hilo.

Niliweza kurudi nyumbani kwetu kutoka Nairobi na kuenda kwa tajiri yule na kumuuliza mbona alifanya kitu kama hicho, cha kushangaza mwanaume huyo aliwaita Polisi na kuwaarifu kuwa nimemtishia kumtoa uhai.

Nilifikishwa kwenye kituo cha Polisi na kutozwa faini, siku iliyofuatia maafisa wa Polisi walikuja tulikokuwa tumehamia na kutupa onyo kali kama tutaendelea kumsumbua tajiri yule aliyepokonya shamba letu.

Baada ya wiki moja hivi mke wangu aliniomba nifike kortini kutafuta haki, aliniambia kuwa atanionyesha njia rahisi ya kuweza kuishinda kesi hiyo, basi nilifanya hima na kufika mahakamani na kumshtaki tajiri yule. 

Niliporejea nyumbani mke wangu alinipeleka kwa Dr Bokko, niliweza kuwaeleza kila kitu, walifanya ganga ganga zao na kunipa ahadi za kuishinda kesi ile.

Siku iliyofuatia tuliweza kufika kortini na Jaji aliagiza tajiri yule kuturejeshea shamba alilotupokonya, pia alitozwa faini ya Ksh100,000, Mama yangu alirejeshewa shamba lake na kwa sasa anaishi maisha yake mazuri.

Pia Dr Bokko wanatibu magonjwa kama saratani ya mapafu, kifua kikuu na mengine mengi, pia wanatatua mizozo ya ndoa, mashamba na mapenzi. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

Wednesday 9 October 2024

NJIA TULIYOTUMIA KUSHINDA KESI BAADA YA KUDHULUMIWA SHAMBA LETU

Jina langu ni Juma, siku moja mtu mmoja tajari alivamia shamba letu na kukatakata kila kitu kilichokuwa humo kama mazao na hata kubomoa nyumba yetu na kudai kuwa shamba hilo lilikuwa lake na hakutaka kuona mtu yeyote shambani humo.

Alimuonya mama yangu hasiaribu kumshtaki kortini kwani atakuwa anapoteza muda wake kama yeye ana fadha nyingi na kuweza kuwapa Majaji wa Mahakama rushwa hivyo ni lazima kuwa atashinda.

Hivyo kwa uwoga mama yangu alinyamaza kama maji mtungini, aliweza kunipigia simu na kuniarifu yote hayo na kuniomba niende nyumbani kumsaidia jambo hilo.

Niliweza kurudi nyumbani kwetu kutoka Nairobi na kuenda kwa tajiri yule na kumuuliza mbona alifanya kitu kama hicho, cha kushangaza mwanaume huyo aliwaita Polisi na kuwaarifu kuwa nimemtishia kumtoa uhai.

Nilifikishwa kwenye kituo cha Polisi na kutozwa faini, siku iliyofuatia maafisa wa Polisi walikuja tulikokuwa tumehamia na kutupa onyo kali kama tutaendelea kumsumbua tajiri yule aliyepokonya shamba letu.

Baada ya wiki moja hivi mke wangu aliniomba nifike kortini kutafuta haki, aliniambia kuwa atanionyesha njia rahisi ya kuweza kuishinda kesi hiyo, basi nilifanya hima na kufika mahakamani na kumshtaki tajiri yule. 

Niliporejea nyumbani mke wangu alinipeleka kwa Dr Bokko, niliweza kuwaeleza kila kitu, walifanya ganga ganga zao na kunipa ahadi za kuishinda kesi ile.

Siku iliyofuatia tuliweza kufika kortini na Jaji aliagiza tajiri yule kuturejeshea shamba alilotupokonya, pia alitozwa faini ya Ksh100,000, Mama yangu alirejeshewa shamba lake na kwa sasa anaishi maisha yake mazuri.

Pia Dr Bokko wanatibu magonjwa kama saratani ya mapafu, kifua kikuu na mengine mengi, pia wanatatua mizozo ya ndoa, mashamba na mapenzi. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

LSF NA NORTH – SOUTH COOPERATION ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO LONGIDO.



Longido, Arusha 08 Oktoba 2024.

LSF, kwa kushirikiana na wadau wake NORTH-SOUTH COOPERATION kutoka Luxembourg, imekamilisha mradi wa miaka miwili unaojulikana kama ‘Wanawake Tunaweza,’ ambao umeleta mafanikio makubwa katika kuwawezesha wanawake na watoto wa kike kutoka jamii ya Kimasai wilayani Longido.

Mradi huu, ulioanza kutekelezwa mwaka 2022, umelenga kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi kwa kuwajengea uwezo kupitia vikundi vya wanawake 11 na kuwaanzishia miradi mbalimbali ya ujasiriamali kama vile ufugaji wa mifugo, uuzaji wa nafaka, utengenezaji wa urembo wa Kimasai, kilimo cha bustani, pamoja na shughuli za VICOBA.

Kupitia mradi huu, akinamama wameweza kuanzisha kikundi cha pamoja kijulikanacho kama ‘Osiligi’ na wamepatiwa vyerehani 11 kwa ajili ya kushona taulo za kike zinazotumika tena (Reusable Sanitary Pads). Taulo hizi zimesaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa kike katika shule za Lekule na Namanga, ambao ni miongoni mwa wanufaika wakuu.

Mbali na hayo, mradi umeweza kuwasaidia watoto wa kike kupata mazingira bora ya kusomea kwa kujenga mabweni mapya, huku zaidi ya wasichana 1,214 wakiwa wamefaidika kupitia shughuli mbalimbali za elimu, usawa wa kijinsia, na haki zao za msingi.

Aidha, zaidi ya wanawake 209 wamenufaika moja kwa moja katika eneo la ujasiriamali, huku jumla ya watu 2,500 wakiwemo wanaume na wanawake wa Longido wakielimishwa juu ya masuala ya kijinsia na haki ya mwanamke kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huu.

Mradi pia umeweza kuwajengea uwezo viongozi wa kimila takribani 20, huku wakishirikiana na wanaume shupavu (Male Champions) 7 waliopatiwa mafunzo maalum kupitia shirika la WASHEWILO, ambalo pia linapata ufadhili kutoka LSF, ili kuleta mabadiliko chanya katika mtazamo wa jamii kuhusu haki za wanawake.

Mafanikio mengine makubwa ni kuboresha chumba cha Tehama (ICT room) katika shule ya Namanga, kwa kuweka kompyuta, viti, na vifaa vya kisasa vinavyowezesha wanafunzi 40 kupata elimu ya Tehama kwa wakati mmoja.

Pamoja na maboresho haya, kampeni ya upandaji miti katika mashule na jamii imewezesha miche 1,420 kupandwa na kuhudumiwa licha ya changamoto ya ukame kwenye eneo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huu, Meneja Mawasiliano wa LSF alitoa wito kwa serikali ya wilaya na wadau wengine kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanadumishwa na kuendelezwa.

Alisisitiza kuwa, licha ya hatua kubwa iliyofikiwa, bado kuna maeneo ya kuboresha hasa katika kupanua masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa vikundi hivyo na kuhakikisha kuwa mipango ya kuwasaidia kinamama hao inafuatiliwa na kutekelezwa kikamilifu.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Lekule iliyopo Longido Mkoani Arusha, akiwafundisha wanafunzi wa Shule hiyo somo la Kompyuta katika Chumba kilichokarabitiwa kwa Ufadhili wa LSF kwa Kushirikiana na North - South Cooperation ya nchini Luxembourg.
Share:

Tuesday 8 October 2024

RC MWASSA : WAGOMBEA FANYENI KAMPENI ZA KISTAARABU NA ZENYE STAHA



Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa mkoa wa Kagera hajat Fatma Mwassa amewataka wagombea wote na vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na zenye staha katika uchaguzi wa serikali za mtaa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 8,2024 amesema kuwa novemba mosi hadi saba wagombea watachukua fomu na kurudisha huku Novemba 20 hadi 26 itakuwa zoezi la kampeni kwa wagombea.

Aidha amesema kuwa mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na watu wenye umri wa miaka18 na kuendelea wapatao 1,566,530 ambapo amewataka watu wote hao kujitokeza katika zoezi la kupiga kura ili kutumia haki yao ya kimsingi na kikatiba ya kupiga kura na kusema kuwa mkoa wa kagera una vituo vya uandikishaji wa wapiga kura vipatavyo 3,833.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewakaribisha wananchi wote, makampuni ya uzalishaji wa vyakula, wakulima, wafugaji na wavuvi kushiriki kwa pamoja katika maadhimisho ya chakula duniani.


Amesema kuwa maadhimisho ya siku ya chakula duniani mwaka huu yanaadhimishwa kitaifa katika Mkoa wa Kagera.


Aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya ccm manispaa ya Bukoba kuanzia tarehe 10 -16 octoba 2024 na kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 13, na kufungwa na waziri wa kilimo Mh. Hussein Bashe tarehe 16 Oktoba mwaka huu.


Maadhimisho hayo yatakuwa na shughuli mbalimbali ambazo ni mashindano ya mitumbwi ya uvuvi wa samaki, mashindano ya upishi wa asili, ushirikishwaji wa watoto katika unywaji wa maziwa, maonesho ya chakula, burudani,elimu ya uhifadhi wa chakula salama,na udhibiti wa sumu kuvu, Huku yakiambatana na kauli mbiu ya mwaka huu "haki ya chakula kwa wote kwa maisha bora ya sasa na yajao".







Share:

DAWASA YAGONGA HODI KWA WANANCHI KINONDONI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Wiki ya huduma kwa mteja ikiwa inaendelea, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetembelea wateja wake katika maeneo ya Msasani, Masaki, Mwananyamala wilayani Kinondoni kwa lengo la kubadilishana nao mawazo juu ya uboreshaji huduma za maji.


Akizungumza na wateja mbalimbali, Meneja wa DAWASA Kinondoni, Ndugu Tumain Muhondwa ameahidi kuendeleza mashirikiano mazuri yaliyopo baina ya Mamlaka na wateja ili kuhakikisha huduma bora inawafikia wote kwa wakati.

"Leo tumetembelea wateja mbalimbali ambao ni Slipway Hotel, Seacliff Hotel, Ada estate na Ubalozi wa Marekani na pia wateja wa kawaida katika kata ya Mwananyamala na Kinondoni. Tumeahidi kuboresha huduma ya maji katika maeneo yao," ameeleza ndugu Muhondwa.

Muhondwa ameongeza kuwa Mamlaka imejipanga kuongeza maunganisho ya huduma ya maji na kufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa huduma ifikapo mwaka 2025.

"Tumeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutembelea wateja wakubwa na wadogo, tunafahamu kuna maeneo ambayo huduma haijafika, nipende kuwahakikishia wananchi kuwa Mamlaka inafanya kazi kubwa kusogeza huduma maeneo yote kwa kuongeza vyanzo vya maji na kufanya miradi ili kila mwananchi apate huduma ya maji," ameeleza ndugu Muhondwa.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwananyamala na Meya wa manispaa Wilaya ya Kinondoni, ndugu Songoro Mnyonge ameishukuru DAWASA kwa huduma bora zinazotolewa na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwa Mamlaka ili huduma izidi kuimarika.

"Nikiri kwamba DAWASA wanatoa huduma hapa kwetu, huduma ya maji tunaipata kama inavyostahiki na imechangia utulivu mkubwa kwa wananchi, tutaendelea kutoa ushirikiano kwao ili huduma iwe bora na endelevu," ameeleza ndugu Mnyonge.

Josephine Wange mkazi wa Kinondoni ameishukuru DAWASA kwa kuwafikia katika wiki ya huduma kwa mteja na kueleza kuridhishwa na huduma.

Wiki ya huduma kwa wateja inaakisi usimamizi bora na wa viwango wa huduma zitolewazo na Mamlaka kwa wateja na kaulimbiu ya mwaka huu inasema "Ni zaidi ya Matarajio."
Share:

DAWASA YANOGESHA WIKI YA HUDUMA KISARAWE

 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imeanza kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kisarawe kwa zoezi la kutembelea wateja mtaa kwa mtaa katika Kata ya Kisarawe hususan maeneo ya Bomani na Matumbini.


Zoezi hilo la kutembelea wateja Mtaa kwa Mtaa limelenga kuwafikia wateja kwenye maeneo yao na kuwahudumia kwa kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitatua.

Maadhisho ya wiki ya huduma kwa wateja hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema "Ni Zaidi ya Matarajio".
Share:

NSSF KUFIKISHA HUDUMA KWA WATEJA KIDIJITALI ZAIDI



*Mkurugenzi Mkuu asema kila mwanachama atafungua madai ‘online’

*Aahidi kuifikia sekta isiyo rasmi ili Watanzania wengi waweze kunufaika na huduma za NSSF 

Na MWANDISHI WETU
MBEYA. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) amesema Mfuko unaendelea kuboresha na kutoa huduma bora kwa wateja kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA, ambapo kwa sasa wanachama wanaweza kufungua madai kidijitali ‘online’ bila ya kulazimika kufika katika Ofisi za NSSF.

Amesema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuwaondolea kero wananchi, ambapo kwa upande wa NSSF wanachama wanapata taarifa zao mbalimbali huko huko waliko jambo ambalo linawaondolea usumbufu wa kufuata huduma umbali mrefu.  

Bw. Mshomba amesema hayo tarehe 7 Oktoba 2024 jijini Mbeya wakati akifungua Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyobeba kauli mbiu isemayo ‘Huduma Bora Popote Ulipo’.

Aidha, amesema NSSF inaendelea kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi ambayo imebeba kundi kubwa la Watanzania kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wa madini na wajasiriamali wengine ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha bora ya sasa na ya baadaye.

Bw. Mshomba amewahakikishia wateja kuwa NSSF iko imara na endelevu katika kutoa huduma za hifadhi ya jamii hususan kupitia majukumu ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao. Hivi sasa thamani ya Mfuko imefikia trilioni 8.5.

“Natumia fursa hii kuwashukuru wateja, watumishi wenzangu, Bodi ya Wadhamini, Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Waziri Mkuu hawa wote wamekuwa wadau muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma zetu,” amesema Bw. Mshomba.

Amesema mafanikio makubwa ambayo NSSF imeyapata yamechangiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye katika uongozi wake amefungua nchi na kumekuwa na ongezeko kubwa la waajiri kutokana na mazingira mazuri aliyoweka.
Naye, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya, amesema wanaendelea kuboresha huduma za wateja siku hadi siku kwa kuwa umuhimu wa wateja ni mkubwa na ndio sababu za kuwepo kwa NSSF.

Amesema wanachama wachangiaji wa NSSF wameongezeka kutoka 1,189,000 mwezi Juni 2023 na kufikia 1,342,654 mwezi Juni 2024. Idadi ya wanufaika wa Pensheni nao wameongezeka ambapo mpaka kufikia mwezi Juni 2024 wamefikia wastaafu 31,914.

Bw. Mziya amesema wanufaika wa mafao mengine wakiwemo wa Matibabu wamefikia 207,229 mpaka kufikia Juni 2024 na kuwa idadi ya waajiri imeongezeka na kufikia 41,616.

Amesema wanufaika wa Mafao ya Uzazi mpaka kufikia Juni 2024 walikuwa 10,809, wanufaika wa Mafao ya Kupoteza Ajira mpaka kufikia Juni 2024 walikuwa ni 109,286. “Hivyo utaona idadi ya wateja wetu imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na sisi kipaumbele chetu ni kuendelea kutoa huduma bora na kuongeza idadi ya wanachama wengi zaidi,” amesema Bw. Mziya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Ekwabi Mujungu ameahidi kuwa wafanyakazi wataendelea kusikiliza wateja, kutoa huduma za kipekee, kuwasiliana kwa uwazi, kujitolea kwa wateja kwa maana ya kuvaa viatu vyao, kujifunza na kuboresha huduma kila siku, lengo ni kupunguza malalamiko.

Naye Robert Kadege, Meneja wa Huduma kwa Wateja, amesema Wiki ya Huduma kwa Wateja ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1987 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja pamoja na wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wanachama.

Amesema NSSF inatumia wiki hii kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa huduma bora kwa wateja na kuwashukuru kwa namna ambavyo wanaunga mkono juhudi mbalimbali za NSSF ambapo kwa sasa imejikita katika kuboresha huduma zake kupitia mifumo ya kidijitali.

Awali, Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Bw. Deus Jandwa amewahakikishia wateja kuwa wanaendelea kutoa huduma bora za hifadhi ya jamii, kutatua kero mbalimbali pamoja na kufikisha elimu ya hifadhi kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.












 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger