Sunday, 19 April 2026

BARRICK BULYANHULU YAKABIDHI TREKTA WILAYA NYANG’WALE KUFANIKISHA USAFI WA MAZINGIRA


Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kulia) akipeana mkono wa shukrani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack wakati wa hafla ya makabidhiano ya Trekta kwa ajili ya kusomba taka na kufanya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack (kushoto) wakipongezana na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Trekta kwa ajili ya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
  Muonekano wa Trekta iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa ajili ya kusomba taka na kufanya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
Viongozi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale wakipeana vifaa kwa ajili ya usafi kwenye halmashauri hiyo.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena akizungumza kwenye halfa hiyo ya makabidhiano ya trekta kwa halmashauri ya Nyang’wale
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack (Katikati) na kulia kwake ni Senkondo Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena wakiwa kwenye utiaji wa saini katika halfa ya makabidhiano ya trekta kwa ajli ya kusomba taka na ufanyaji wa usafi kwenye halmashauri hiyo
Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale wakiwa kwenye picha ya pamoja
***

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeendelea kutekeleza sera yake ya mkakati endelevu wa kusaidia jamii baada ya kukabidhi trekta ya kusomba taka yenye thamani ya shilingi  milioni 66 pamoja na vifaa vya kufanyia usafi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika juhudi zake za kutunza mazingira nchini.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya trekta hiyo, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nyang'wale , Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, John Isack alisema msaada huo umekuja kwa wakati katika juhudi za kulinda na kutunza mazingira kwa maslahi ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake.

“Tunashukuru Barrick Bulyanhulu kwa msaada huu wa trekta , tunaamini sasa hali ya usafi katika Wilaya yetu itakuwa nzuri kwa kiasi kikubwa kwani hii ni trekta ya pili wametupatia, matarajio yetu ni kuongeza kasi ya kuondoa taka kutoka hapo awali ya kutoa mara mbili kwa wiki, awali tulikuwa tunazoa taka katika siku za Alhamisi na Jumatatu hivyo tutaongeza siku pia tunatarajia kuongeza huduma kwa maeneo ya miji inayokuwa kwa kasi kibiashara kama vile Bosolwa, Nyijundu, Bukwimba na maeneo ya migodini",alisema.

Isack aliongeza kuwa kampuni ya Barrick Bulyanhulu kupitia uwekezaji wake imefanikisha miradi mingi ya kijamii na utunzaji wa mazingira wilayani humo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii ambayo inazidi kuboresha maisha ya wananchi.

“Leo tumepokea Trekta ambalo limenunuliwa na kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa gharama ya Shilingi Milioni 66 , Trekta hili ni maalum kwa kazi ya kuzoa uchafu na kupeleka dampo kwa kweli ni msaada mkubwa kwa wilaya yetu kwani kwa miaka mingi sana tumekuwa na changamoto juu ya uzoaji wa taka katika mitaa yetu ukichukulia kwamba mji wetu unakua kwa kasi na kupelekea uzalishaji wa taka kuongezeka kwa kasi, na ni matarajio yangu sasa mazingira ya Wilaya yetu yatakuwa safi, nichukue fursa hii kuwaomba wananchi kufanya usafi kila siku kwani tayari kwa sasa tunalo trekta ambalo litakuwa linasomba taka mara kwa mara”, alisema.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo alitoa shukrani kwa viongozi wa serikali na wananchi kwa kuwa na uhusiano mzuri na Kampuni hiyo na kuongeza kuwa msaada wa trekta lililokabidhiwa ni kwa ajili ya kufanya usafi na utunzaji wa mazingira.

“Niwaombe ndugu zangu usafi ni jukumu letu sote,trekta hili tulitunze ili liweze kuboresha mazingira yetu ipasavyo ,milioni 66 ni pesa nyingi hivyo naamini tutakuwa tumefungua njia ya kuboresha mazingira ya usafi wilayani Nyang’hwale, haswa ikizingatia kampuni ya Barrick Bulyanhulu ni wadau wakubwa wa utunzaji wa mazingira”, alisisitiza Zuwena.







Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 19,2026




Magazeti
Share:

Saturday, 18 April 2026

WACHIMBAJI WA MADINI MWAKITOLYO WALIA NA TOZO MPYA YA HALMASHAURI,UZALISHAJI WA SUASUA

Share:

RAIS SAMIA AMERIDHIA MILIONI 544 ZILETWE BAHI KUJENGA SHULE YA SEKONDARI CHIFUTUKA - PROF. SHEMDOE



Na OWM - TAMISEMI, Bahi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amemuarifu kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wananchi wa Kata ya Chifutika lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo la kupatiwa shilingi milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Chifutuka ambayo itakidhi uhitaji wa wananchi wa kata hiyo. 

Prof. Shemdoe amesema hayo leo Aprili 17, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne wilayani Bahi, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani humo. 

“Mhe. Mbunge alinifuata kabla sijasimama kuzungumza, akiomba shule ya sekondari ijengwe Kata ya Chifutika, nikawasiliana na Mhe. Waziri Mkuu na kuliwasilisha ombi hilo kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameridhia milioni 544 ziletwe kujenga shule ya sekondari,” amesema Prof. Shemdoe.

Kutokana na kuridhiwa kwa kiasi hicho cha fedha, Prof. Shemdoe kwa niamba ya wananchi wa Kata ya Chifutuka Wilayani Bayi amemshukuru kwa moyo wa dhati Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchema kwa upendo mkubwa waliouonesha kwa wananchi wa Kata hiyo Chifutuka.

Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, fedha hizo zimeridhwa na Mheshimiwa Rais kwasababu lengo la Serikali ni kuendelea kuimarisha elimu nchini,  ikizingatiwa kuwa Bahi imeonesha juhudi kubwa na kuwa Halmashauri ya kwanza kitaifa kwenye ufaulu wa mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2025.






Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 18,2026


Magazeti





Share:

Friday, 17 April 2026

OFISI YA AFISA MADINI MKAZI MKOA WA SINGIDA YATOA MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WADOGO KWA USHIRIKIANO NA UNDP



Na mwandishi wetu,Singida

Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imeendesha mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini yenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu uchimbaji salama, wenye tija na unaozingatia utunzaji wa mazingira.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea wachimbaji uwezo katika matumizi ya teknolojia bora za uchimbaji, usimamizi wa afya na usalama migodini, uongezaji thamani wa madini pamoja na kuimarisha biashara ya madini kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta ya madini.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Mhandisi Sabai Nyansiri, amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha sekta ya madini inachangia kikamilifu maendeleo ya wananchi na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kuongeza tija, kipato na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia misingi ya usalama, uhifadhi wa mazingira na uendelevu wa rasilimali madini.


Share:

MTANDA AAGIZA UKAGUZI MKALI WA MAZINGIRA MWANZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, ametoa wito kwa wananchi kushiriki ipasavyo katika kutunza Mazingira huku akilitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na maafisa mazingira wa Halmashauri kuendelea kufanya kaguzi za mara kwa mara za kimazingira ili kuhakikisha usafi na usalama wa mazingira unaimarishwa.

Akizungumza katika kikao na viongozi wa NEMC pamoja na wanahabari, Mhe. Mtanda alisisitiza umuhimu wa utekelezaji madhubuti wa Sheria za mazingira ili kulinda rasilimali za asili na afya ya jamii.

Alieleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 191, Serikali imeweka marufuku kwa shughuli zote zinazochangia uchafuzi wa mazingira, hususan katika maeneo ya vyanzo vya maji na maeneo tengefu.

Aidha, alifafanua kuwa Kifungu cha 57 cha sheria hiyo kinakataza mtu yeyote kujenga, kufanya shughuli au kutupa taka ndani ya umbali wa mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji au eneo la hifadhi, hatua inayolenga kulinda rasilimali hizo muhimu.

Mhe. Mtanda alibainisha kuwa marufuku hiyo imekuja kufuatia ongezeko la vitendo vya uharibifu wa mazingira vinavyohatarisha vyanzo vya maji, afya za wananchi pamoja na uendelevu wa rasilimali za asili.

Hivyo, serikali imechukua hatua za makusudi kuhakikisha maeneo muhimu ya kimazingira yanahifadhiwa ipasavyo.

Katika kuimarisha utekelezaji huo, serikali kupitia mamlaka za mikoa na halmashauri imeongeza juhudi katika usimamizi wa mazingira, ikiwemo kulinda misitu, kuhifadhi vyanzo vya maji na kuboresha miundombinu ya ukusanyaji na utupaji wa taka.

Sambamba na hilo, ukaguzi wa kimazingira unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali yenye shughuli za kijamii na kiuchumi kama vile baa, kumbi za starehe, viwanda na maeneo ya biashara.

Lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha kuwa shughuli zote zinaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya usafi, usalama na utunzaji wa mazingira.

Alionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kukiuka sheria za mazingira.

Hatua hizo ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa wahusika wa vitendo kama utupaji taka ovyo, ujenzi holela katika vyanzo vya maji na uchomaji wa misitu.

Aidha, serikali inaendelea kushirikiana na wananchi kwa kutoa elimu ya mazingira na kuendesha kampeni za uhamasishaji ili kuongeza uelewa wa umuhimu wa kuhifadhi mazingira.

Ushirikiano huo umetajwa kuwa ni muhimu katika kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger