Tuesday, 7 April 2026

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 7,2026

Magazeti



 













Share:

Monday, 6 April 2026

TUME YA UCHUNGUZI YAONGEZEWA MUDA TENA HADI APRILI 24,2026


Na Mwandishi Wetu Dodoma

MAMLAKA ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.

Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.
Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.

Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.

Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.

Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
Share:

POLISI TANGA WAOKOA VIJANA 87 WALIOINGIZWA KWENYE MTEGO WA UTAJIRI WA HARAKA MTANDAONI


Na Hadija Bagasha - Tanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia Kikosi cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), limefanikiwa kuwaokoa vijana wapatao 87 waliokuwa wametapeliwa fedha zao kupitia mtandao  baada ya kushawishiwa kujiunga na kampuni inayojinasibisha kufanya biashara ya mtandao inayofahamika kwa jina la Champions E-Commerce Education ambapo katika tukio hilo vijana hao walihamasishwa kujiunga na kampuni hiyo kwa ahadi ya kupata utajiri wa haraka kupitia biashara za mtandaoni. 

Kwa mujibu wa Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana hao ni kutokea Mikoay a Mtwara, Iringa, Daresalaa na Morogoro ambao walishawishiwa kujiunga na Kampuni hiyo kwa ahadi ya kupata utajiri wa haraka kupitia biashara za mtandaoni, ambapo walielezwa kuwa wangeanza kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi mara baada ya kukamilisha mafunzo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa Tanga Almachius Mchunguzi ameeleza kuwa kila kijana alitakiwa kuchangia kiasi cha fedha kuanzia shilingi laki sita (600,000) hadi kufikia shilingi milioni nne (4,000,000) kama mtaji wa awali pamoja na gharama za mafunzo, fedha ambazo walidaiwa kuambiwa ndizo zingewapa fursa ya kuanza biashara na kupata faida  kwa haraka.

Hata hivyo, baada ya kujiunga na mfumo huo, vijana hao walikutwa wakiishi katika mazingira yasiyoridhisha huku wakiendelea kupatiwa mafunzo yanayodaiwa kuwajengea uwezo, wakisubiri kupata utajiri waliokuwa wameahidiwa.

Katika operesheni hiyo, Jeshi la Polisi limekamata na kuwashikilia kwa mahojiano zaidi watu wawili waliokuwa wakisimamia kundi hilo ambao ni Mohammed Hamis Idrisa (24) mkazi wa Masiwani Jijini Tanga, na Fidolini Hamisi Rashidi (21) mkazi wa Mbugani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa wito kwa wananchi kuwa makini na aina ya uwekezaji unaohusisha ahadi za kupata faida kubwa kwa muda mfupi bila kuwa na taarifa sahihi, pamoja na kufanya uhakiki kama kampuni husika imesajiliwa na mamlaka halali.

Polisi imewataka wananchi kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kujiunga na taasisi au kampuni yoyote inayojihusisha na uwekezaji hususan kupitia mitandao, ili kuepuka kuingia kwenye mitego ya utapeli.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea huku Jeshi la Polisi likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na utapeli wa aina hiyo.




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 6,2026

         
 Magazeti
   


Share:

Sunday, 5 April 2026

UKOMAVU WA KISIASA: RAIS SAMIA AZIBA MAKOVU YA UCHAGUZI, AKUTANA NA WAGOMBEA URAIS 16 IKULU

 

Katika hatua inayotajwa kama kielelezo cha juu cha ukomavu wa demokrasia na uongozi wenye busara, Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na waliokuwa wagombea urais 16 alioteuliwa nao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 0755844215 

Mkutano huo wa kihistoria uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi 2026, umelenga kuimarisha maridhiano ya kitaifa na mshikamano baada ya kipindi cha ushindani wa kisiasa.

Wadau mbalimbali wa siasa, wasomi, na wachambuzi wamemwagia sifa Rais Samia kwa hatua hiyo, wakibainisha kuwa imesaidia "kuziba makovu" yaliyotokana na joto la uchaguzi. 

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ally Khatib, amepongeza kitendo hicho akisema kinaleta tafsiri njema ya demokrasia na kukuza siasa za staha. 

Amesema kuwa washindani kukaa meza moja na mshindi ni ishara kuwa maslahi ya Tanzania ni makubwa kuliko itikadi za vyama.

Mwanasiasa mkongwe, Hamad Rashid, amebainisha kuwa mkutano huo ni utekelezaji wa vitendo wa falsafa ya Rais Samia ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya). 

Rashid ameshauri utaratibu huu uwe wa kudumu na hata kuingizwa kwenye mfumo wa maandishi kama kanuni ya nchi, huku akitoa mwito kwa upande wa Zanzibar kuiga mfano huo ili kuunganisha wananchi.

Uchambuzi wa wasomi, akiwemo Dk. Paul Loisulie wa UDOM na Goodluck Ng’ingo, unaonesha kuwa Rais amefanya jambo la msingi kwani amani na utulivu ndivyo vinavyotoa nafasi kwa serikali kutekeleza majukumu ya maendeleo kwa wananchi.

 Wamesisitiza kuwa siasa za kuheshimiana hupunguza taharuki, hasa katika zama hizi ambapo mitandao ya kijamii hutumika vibaya kuchochea migogoro.

Kwa upande wake, Rais Samia kwa kuitikia wito huo wa wagombea wenzake, amethibitisha kuwa milango yake iko wazi kwa majadiliano yenye tija. 

Viongozi hao wa vyama 16 walipata fursa ya kuwasilisha maoni yao kuhusu hali ya nchi, amani, na mshikamano, jambo linalotuma ujumbe mzito kwa ulimwengu kuwa Tanzania ni taifa linalotatua tofauti zake kupitia mazungumzo ya kistaarabu badala ya mivutano. 

Share:

MALUNDE 1 BLOG INAKUTAKIA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA!

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 5,2026

magazeti






Share:

Saturday, 4 April 2026

MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA SHINGO SHINYANGA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi akizungumza na vyombo vya habari mjini Shinyanga Jumamosi Aprili 4, 2026.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi akizungumza na vyombo vya habari mjini Shinyanga Jumamosi Aprili 4, 2026.

Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kuhusiana na mauaji ya kikatili ya mwanamke Hollo Ruchanganya (60), mkazi wa kijiji cha Bunambiyu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, huku uchunguzi wa awali ukihusisha imani za kishirikina.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Shinyanga leo Jumamosi Aprili 4, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watuhumiwa hao wanahojiwa ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

Katika tukio hilo, marehemu Hollo Ruchanganya aliuawa kikatili kwa kukatwa shingoni na mtu asiyejulikana, kabla ya mwili wake kutupwa katika shamba la mahindi jirani na makazi yake.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, mtuhumiwa wa mauaji hayo anadaiwa kuwa mgeni aliyefika nyumbani kwa marehemu majira ya saa 3:00 usiku wa Aprili 3, 2026, ambapo alikula chakula pamoja na marehemu na wajukuu wake.

 Baadaye marehemu alimsindikiza mtuhumiwa huyo kwa lengo la kumpeleka kwa mtalaamu wa tambiko linalodaiwa kuzuia kupata watoto pacha.

Inaelezwa kuwa muda mfupi baada ya kutoka, mtu huyo alirejea nyumbani na kurejesha tochi, akiwataarifu wajukuu wa marehemu kuwa bibi yao angerudi asubuhi kutoka kwa mganga anayeelezwa kuwa ni ndugu yake.

Mwili wa marehemu uligunduliwa asubuhi na mjukuu wake aliyekuwa akielekea shambani, baada ya kuona damu nyingi na nguo za marehemu njiani. Baada ya kutoa taarifa kwa ndugu, walifanikiwa kuufuatilia mwili huo uliokuwa umetupwa shambani ukiwa na jeraha kubwa la kukatwa shingoni.

Kamanda Magomi amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger