Monday, 29 December 2025
Sunday, 28 December 2025
VIJANA WASHAURIWA KUKUZA BIASHARA KWA HATUA STAHIKI
Saturday, 27 December 2025
MAPACHA WA ARUSHA: KUTOKA MAADUI WAKUBWA HADI MARAFIKI WA DAMU

Huu ni ushuhuda wa kweli kutoka jijini Arusha, kuhusu familia ya Mzee Abdulah na mkewe. Maisha yao yalianza kwa furaha tele walipowapata watoto wao mapacha, Baraka na Faraji. Tangu utotoni, walikuwa kama pete na kidole; walivaa sare, walisoma shule moja, na hata mmoja akiumwa, basi mwingine naye aliishiwa nguvu.
Matatizo yalianza baada ya kumaliza elimu ya msingi. Baraka alichaguliwa kujiunga na shule ya kutwa ya kawaida, huku Faraji akifanikiwa kwenda Shule ya Kitaifa (National School). Tangu siku hiyo, ule uzi uliowaunganisha ulikatika. Chuki ilitanda, dharau ikaingia, na mapacha hawa wakawa kama paka na panya. Nyumba ya Mzee Abdulah ilijaa huzuni na simanzi.Baada ya jitihada za kifamilia kushindikana, Mzee Abdulah alimshirikisha rafiki yake wa karibu ambaye alimuelekeza kwa mtaalamu mashuhuri, Dr. Magongo. Ingawa Mzee Abdulah alikuwa na kusitasita awali, upendo kwa wanawe ulimfanya apige hatua hiyo ya kishujaa kutafuta suluhu kwa Dr. Magongo.
Baada ya Mzee Abdulah kufuata maelekezo yote ya Dr. Magongo, anga la nyumba yake lilianza kubadilika. Siku ya kwanza ya kukutana kwao ilikuwa ya kipekee na haitasahaulika.Baraka alikuwa ameketi nje, kwenye kile kiti cha mbao ambacho mapacha hao walipenda kukaa zamani kabla ya chuki kuingia. Faraji alitoka ndani, na badala ya kupita kwa dharau kama ilivyokuwa desturi yake, alisimama ghafla na kumtazama ndugu yake. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, macho yao hayakujawa na hasira, bali yalijawa na shauku na majonzi ya kupotezana.
Faraji alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya. Alimsogelea Baraka na kumuwekea mkono begani, ishara ambayo ilimfanya Mzee Abdulah, aliyekuwa akichungulia dirishani, kutokwa na machozi ya furaha.”Ndugu yangu Baraka, nimekukumbuka. Shule na madaraja vilitutenganisha, lakini damu yetu ni moja.”Fariji alisema (Akisimama na kumkumbatia ndugu yake kwa nguvu) Baraka alinena na kusema “Nilidhani umenisahau kwa sababu ya mafanikio yako, lakini moyo wangu ulikuwa unakuita kila siku.”
Walikaa hapo kwa saa kadhaa, wakisimuliana mambo ya shuleni na kucheka kama walivyofanya walipokuwa watoto wadogo. Ile hali ya mmoja kuhisi maumivu ya mwingine ilirejea papo hapo; Baraka alipokuwa akisimulia changamoto za shule yake, Faraji aliahidi kumsaidia kwa vifaa na maarifa aliyopata kwenye shule ya kitaifa.Tangu siku hiyo, ile kuta ya chuki ilibomoka kabisa.
Friday, 26 December 2025
DKT HOMERA AKABIDHI MABOMBA YA SHILINGI MILIONI 30 KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAJI NAMTUMBO
Mwalimu Saidi Homera akikabidhi mabomba kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt Juma Zuberi Homera na Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania Na Mwandishi Wetu Malunde 1-Blog
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amekabidhi mabomba yenye thamani ya shilingi milioni 30 kama hatua za dharura za kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo hilo.
Msaada huo umetolewa kabla ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji ya Serikali, ukiwa na lengo la kupunguza kero ya maji kwa wananchi wa Namtumbo.
Akikabidhi mabomba hayo kwa niaba ya Mbunge, Mwalimu Saidi Homera amesema msaada huo umetokana na juhudi binafsi za Dkt. Homera, kama sehemu ya dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Ameeleza kuwa hatua hiyo inaonesha uwajibikaji na ukaribu wa mbunge kwa wananchi wake.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo, David Mkondya, amesema mabomba hayo yatatumika kukamilisha uchimbaji wa visima 10 katika vijiji 10.
Baada ya uchimbaji, visima hivyo vitawekewa mifumo ya pampu za umeme na matenki ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 20,000 hadi 50,000 kulingana na idadi ya watu, hatua itakayoongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 74 hadi kufikia asilimia 76.
Baadhi ya wakazi wa Namtumbo, akiwemo Diwani wa Kata ya Namtumbo Rajab Uhonde, wamempongeza na kumshukuru Dkt. Juma Homera kwa jitihada zake za kutatua changamoto za wananchi.
Wamesema msaada huo unaonesha mbunge yupo karibu na wananchi na anashughulikia kero zao, huku wakimpongeza pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za Serikali katika ujenzi wa miradi mikubwa ya maji katika mji wa Namtumbo.















