Tuesday, 18 November 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 19,2025




Magazeti ya leo







Share:

TIRDO YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA MKA MBADALA, YALENGA UBORA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA


DAR ES SALAAM, Novemba 17, 2025 — Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) limetoa mafunzo maalum kwa wajasiriamali wanaojihusisha na utengenezaji wa mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya misitu, yakiwa na lengo la kuongeza ujuzi na kuboresha ubora wa bidhaa hiyo kufikia viwango vinavyotakiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, Mhandisi Ramson Mwilangali, amesema mafunzo hayo yanajumuisha nadharia, vitendo na elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na namna sahihi ya kuhifadhi bidhaa za nishati mbadala.
Wajasiriamali Kujengewa Mtandao na Kupimwa Bidhaa Bure

Mhandisi Mwilangali amesema kupitia mkutano na mafunzo hayo, TIRDO imelenga kujenga mtandao wa wajasiriamali utakaowawezesha kubadilishana ujuzi kati yao na wataalamu wa shirika hilo.

Aidha, alibainisha kuwa mara baada ya mafunzo, wajasiriamali watakaonza uzalishaji wa bidhaa hizo watapatiwa huduma ya kupimwa bure sampuli za mkaa kupitia maabara za TIRDO ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia sokoni zina ubora unaohitajika.

“Pale tutakapobaini kuna upungufu, kama taasisi tutatoa maelekezo ya nini kifanyike ili kufikia kiwango kinachotakiwa. Baada ya marekebisho, sampuli inaweza kupimwa tena na kuingia sokoni ikiwa safi na kwa gharama nafuu kwa watumiaji,” amesema.

Wadau Wapongeza Mafunzo

Kwa upande wake, mwakilishi wa kikundi cha Fahari Kijani Group kutoka Tabora, Bw. Amiri Kassanga, amesema walipoanza kutengeneza mkaa mbadala hawakuzingatia matakwa ya viwango, lakini sasa wana matumaini makubwa ya kukuza uzalishaji kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Blamo Tech Engineering Limited, Bi. Modesta Lukosya, alisema taasisi yake imejikita katika uzalishaji wa nishati safi ili kuwaokoa wanawake na watoto ambao wamekuwa wahanga wa nishati chafu inayozalisha gesi ukaa.

“Tumejikita kwenye kuzalisha nishati safi ili kuokoa wanawake na watoto wanaoathirika na matumizi ya nishati chafu,” amesema.

Wito Kwa Serikali na Wadau

Mkazi wa Mbagala, Bi. Hadija Said, ameishukuru TIRDO kwa mafunzo hayo akisema yatamsaidia kujikimu kiuchumi kama mwanamke mjasiriamali. Ameomba serikali na wadau kujitokeza kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwawezesha wahitimu kuanzisha viwanda na kuendeleza uzalishaji wa mkaa mbadala.
Share:

WATATU MBARONI TABORA KWA KUJITEKA ILI KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU



Na mwandishi wetu, Tabora

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora limetangaza kuwashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutoa Taarifa za Uongo kuwa wametekwa ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa ndugu na wana familia wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, CP Richard Abwao amewaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa wanaoshikiliwa ni Khadija Jimmy Murijo (39), Kabila Mpare ambaye pia ni mke wa Bw. Emmanuel Peter Mchali, Ashura Swalehe (48) na Vitus Joseph (34) ambapo wote wanadaiwa kushirikiana kutengeneza taarifa ya uongo kwamba Khadija Jimmy ametekwa na watu wasiojulikana.

Watuhumiwa hao inaelezwa kuwa walitengeneza uongo huo ili kujipatia fedha kwa mume wa Khadija Murijo, ambapo walijipatia kiasi cha shilingi 1, 385, 800 kati ya Shilingi Milioni 2 walizoziamrisha kuzipata kutoka kwa Bw. Emmanuel.

Awali walieleza kuwa Khadija alikuwa ametekwa huko Ulyankulu na katika uchunguzi uliofanyika ulibaini kuwa Mtuhumiwa huyu alikuwa ameenda Wilaya ya Urambo, Kijiji cha Vumilia na baada ya uchunguzi inaonekana fedha hizi zote walizitolea kwenye Wilaya ya Kaliua. Uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani." Amesema Kamanda Abwao.

Kwa upande wake Mume wa Khadija, Bwana Emmanuel Peter Mchali amesema siku hiyo alipigiwa simu na Mke wake na kumueleza kuwa ametekwa na kupata vitisho kutoka kwa mwanaume mmoja kupitia simu ya mkewe, wakimtaka atoe Milioni mbili ili kuweza kuachiwa kwa mkewe, suala ambalo lilimlazimu kukopa fedha ili kwenda kulipa kwa watuhumiwa hao.

Aidha kwa Upande wake Mtuhumiwa mwingine Ashura Swalehe ameeleza namna ambavyo alirubuniwa na Wifi yake ili kudanganya na kubeba fedha kwa mumewe akidai kuwa Mume wake ambaye ni mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, amekuwa amuhudumii yeye na mtoto wake licha ya kuwa na kipato kikubwa, suala ambalo limekuwa likimfanya kukosa huduma muhimu za kila siku.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 18,2025

Magazeti

 
Share:

Monday, 17 November 2025

BONANZA LA IRINGA MOTOR SHOW LAKUSANYA WANA IRINGA PAMOJA... DC SITTA APONGEZA


NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, amepongeza hatua kubwa iliyochukuliwa na waandaaji wa Iringa Motor Show, akisema kuwa bonanza hilo limeanza kuwa kichocheo muhimu cha kukuza utalii ndani ya Wilaya ya Iringa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla.

 Akizungumza katika viwanja vya Kihesa Kilolo wakati wa tamasha hilo la michezo, DC Sitta alisema kuwa uamuzi wa vijana na wadau kuandaa bonanza hilo umefungua ukurasa mpya katika jitihada za kutangaza vivutio vya utalii kupitia michezo ya mbio za magari.

Akitoa pongezi zake mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo, DC Sitta alisema bonanza hilo limeifanya Iringa kuwa kitovu cha kukusanya wapenda michezo ya magari kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. 

Alisema kuwa kuwaleta pamoja wadau wa michezo hayo si tu kunachochea burudani, bali pia kunatoa fursa kwa wageni na wenyeji kuona maeneo mbalimbali ya vivutio ndani ya wilaya.

Kwa mujibu wa Sitta, michezo ya mbio za magari ni sehemu ya vivutio vinavyoweza kuongeza idadi ya watalii ikiwa itaendelezwa kikamilifu.

 “Waandaaji wa Iringa Motor Show mmefanya jambo kubwa sana. Mnawavuta watu wengi, mnaibua vipaji, lakini muhimu zaidi, mnachochea utalii,” alisema DC Sitta.

 Aliongeza kuwa Serikali inaona umuhimu wa mabonanza kama hayo na itaendelea kuyapa kipaumbele kwa kuwa yanachangia uchumi wa eneo husika na taifa kwa ujumla.

Akitaja hatua zinazochukuliwa na serikali, DC Sitta alisema kuwa eneo la Kihesa Kilolo tayari limeshatengwa kirasmi kuwa sehemu ya shughuli za kitalii kupitia mradi wa kuendeleza utalii kusini (Southern Tourism Circuit Development). 

Alisema eneo hilo litaendelea kuboreshwa ili liwe na mvuto wa kudumu na kuwa kivutio kikubwa kwa wageni na wawekezaji katika sekta ya utalii na michezo.

“Tutaendelea kuhakikisha eneo hili linaboreshwa, linapimwa, na linakidhi vigezo vya kuwa moja ya maeneo ya kimkakati kwa ajili ya shughuli za burudani na utalii. Hii ni fursa kwa vijana na wote wanaojikita katika sekta ya utalii kuungana nasi kubadilisha sura ya Iringa,” alisema.

Aidha, DC Sitta aliwataka wadau wa utalii, wafanyabiashara, na makampuni binafsi kuendelea kujitokeza kudhamini mabonanza kama haya ili yawe na kasi na mvuto mkubwa zaidi. 

Alisema udhamini wa kutosha utawezesha matukio hayo kufanyika mara kwa mara na kwa kiwango kikubwa zaidi, hali itakayoongeza mapato na ajira katika mji wa Iringa.

DC Sitta pia aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema imeweka misingi thabiti ya kuimarisha utalii nchini kupitia programu mbalimbali, ikiwemo kuzindua filamu na makala za kimataifa zinazotangaza Tanzania.

 Alisema mwelekeo huo umetia chachu katika maeneo yote ya nchi, na Iringa ni miongoni mwa wanufaika wakubwa kutokana na rasilimali na vivutio ilivyonavyo.

Kwa upande mwingine, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa mstaafu, Richard Kasesela, hakuficha hisia zake kuhusu bonanza hilo. Kasesela alisema kuwa amevutiwa na ubunifu na juhudi zilizowekwa na waandaaji wa Iringa Motor Show. Aliwashauri vijana na wadau wasichoke bali waendelee kuandaa matukio hayo mara kwa mara, kwani yana mchango mkubwa sio tu katika kukuza utalii bali pia kuinua uchumi wa watu wa Iringa.

“Mimi ni mdau wa michezo, nimefurahi sana kuona vijana wa Iringa wanafanya jambo kubwa kama hili. Naahidi kushirikiana nanyi kadri ninavyoweza ili bonanza hili liwe kubwa zaidi ya hapa lilipoanza,” alisema Kasesela.

Akitoa taarifa za maandalizi na malengo ya bonanza hilo, Mratibu wa Iringa Motor Show, Amjad Khan, alisema kuwa hafla hiyo imebeba kaulimbiu “Iringa Yetu, Michezo Yetu.”

 Alisema kaulimbiu hiyo inabeba dhamira ya kuunganisha wakazi wa Iringa kupitia michezo, burudani, ubunifu na utalii. Alifafanua kuwa lengo la bonanza ni kuibua vipaji vipya, kuimarisha michezo ya mbio za magari na mingineyo, pamoja na kuongeza mwamko wa vijana kujikita katika shughuli zenye tija.

Amjad Khan alisema kuwa Iringa Motor Show haitakuwa tukio la mara moja, bali ni mpango endelevu utakaofanyika mara kwa mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Alisema wanatarajia kuongeza idadi ya washiriki kutoka mikoa mingine na hata nchi jirani, ili kulifanya bonanza hilo kuwa la kitaifa na baadaye kimataifa.

Bonanza la mwaka huu lilikusanya washiriki kutoka Iringa na nje ya Mkoa wa Iringa  huku watu wengi wakifurika kushuhudia magari mbalimbali yaliyoshindanishwa katika mbio hizo. Tukio hilo lilipambwa na burudani za wasanii wa ndani, maonesho ya bidhaa, chakula, michezo ya watoto na fursa za kibiashara.

Tukio la Iringa Motor Show limeonesha kuwa Iringa ina nafasi kubwa katika kukuza utalii kupitia michezo, ubunifu na ushirikiano wa wadau. Matumaini yameongezeka kwamba mabonanza yajayo yatakuwa makubwa zaidi, yakichochea uchumi na kuongeza pato kwa wananchi wa Iringa na taifa kwa ujumla.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger