Thursday, 27 March 2025

EVA: HADITHI YA MATESO YA NDOA NA HATMA YA KIFO


Huzuni kubwa ilitanda miongoni mwa watu tuliokuwepo wakati mwanamke mmoja aliposhuka kwenye gari kwa tabu huku akiwa na magongo.

Binafsi nilikuwa nimevunjika mguu na nilikuwa siko sawa sana kisaikolojia lakini nilipomwona mwenzangu, ghafla nilihisi nimepona. Kwa kweli mtu hakuhitaji kuuliza kujua kuwa mwanamke huyo alikuwa amepata ajali kubwa sana katika maisha yake.

Nilimsaidia kushuka na baadae nikaita waandishi wenzangu na tukaa kumhoji kwani tulijuzwa kwamba alikuwa na madhira makubwa ambayo alikuwa ameyapata. Tukio hili lilitokea miaka 15 iliyopita lakini bado ninakumbuka uso wa mwanamke huyo ambaye baadae nilikuja kujua kuwa anaitwa Eva.

Swali langu la kwanza nililomuuliza Eva ilikuwa kuhusiana na aina ya ajali aliyopata kwani niliamini lazima alipata ajali kubwa sana. Alisita kwanza kuniambia na baadae akanijuza kwamba alikuwa ameolewa na alikuwa na watoto watatu na ndipo akaanza kunisimulia.

“ Ndoa yangu imekuwa na mateso sana. Nimekuwa nikivumilia vipigo ambapo mume wangu alifikia hatua ya kunichoma na pasi hapa kwenye ziwa lakini nimekuwa navumilia kwa ajili ya Watoto lakini kwa sasa nimechoka,” alisema Eva huku akinionyesha kidonda kikubwa kwenye ziwa lake.

Niliendelea kumdodosa zaidi anijuze ajali iliyomsababishia yeye kutembea na magongo na ndipo aliponijuza kwamba kulitokea kutoelewana kati yao na katika mabishano mume wake alimsukuma kutoka ghorofa ya kwanza ya nyumba yao hadi chini ambapo alivunjika uti wa mgongo.

“ Nililazwa hospitalini ambapo madaktari wameniambia kwamba maisha yangu yote itanibidi kutembelea magongo kwani niliumia vibaya,” alisema Eva huku akifuta machozi.

Ukimya mkubwa ulitawala mahali pale na ilituchukua muda kuendelea na mahojiano hayo. Baadae nilimtafuta mume wake ambae alikuwa mkali ambapo pia alitoa vitisho.

Juhudi zilifanyika ambapo mume wake Eva alikamatwa huku wanasheria wakihangaika kumpa msaada wa kisheria.

Niliendelea kufuatilia hali ya Eva kwa karibu lakini wiki mbili baadae nilipatwa na mshtuko mkubwa Eva aliponiambia kwamba ameamua kufuta mashtaka na kurudi kwa mume wake.

Nilitumia muda mrefu sana kumshauri na kumuasa kuwa kama mwandishi nilihisi kwamba simulizi yangu nitakayoandika baada ya hapo huenda isiwe nzuri sana kwani nilihisi kabisa

atakumbwa na jambo baya kwani sikuamini kwamba mume wake atakuwa amebadilika hata kidogo.

Ni miaka 15 imepita toka nifanye mahojiano na Eva. Mapema mwaka huu tulikuwa na kikao kuongelea masuala ya ukatili nikatoa mfano wa Eva namna alivyorudi licha ya kupewa ulemavu huku nikisema natamani kujua anaendeleaje. Mkuu wangu wa kazi ambae tulishirikiana nae kufanya usaidizi kwa Eva aliniita pembeni na kunijuza kuwa Eva alifariki dunia wiki moja tu baada ya kurudi nyumbani kwake kwenye ndoa. Nilipata maumivu makubwa na sijui nini kilimuua.

Zipo simulizi nyingi sana zinazoendana na Eva. Kwa sasa, vitendo vya mauaji ya wenza vimeshika kasi huki vingi vikichangiwa na watu kujaribu kuvumilia kwa matumaini kuwa mwenza huyo atabadilika.

Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP) pamoja na mashirika mengine ya kifeminia yamekuwa yakishauri umuhimu wa kujenga nyumba salama ambapo wahanga wa ukatili watakaa na kupata misaada yote ikiwemo ya kiafya, unasihi na matibabu. Uwepo wa nyumba hizo unaweza kusaidia wahanga wa ukatili lau kuwa na muda wa kutafakari wakati wakipanga kusonga mbele. Upo pia umuhimu wa kuwekeza kwenye afya ya akili kwani ni dhahiri kwamba ni ngumu kwa mtu mwenye akili timamu kumuua mwenza na kuendelea na maisha kama hakuna kitu kinachoendelea.

Ni vema pia wazazi tukawafundisha watoto wetu wote wa kiume na kike kwamba ni afadhari waondoke na hata kurudi nyumbani iwapo mahusiano au ndoa zina vitendo vya ukatili kuliko kuvumilia na kurudi kwenye jeneza. Nyakati zimebadilika sana lakini ipo haja ya viongozi wa dini, wa mila na wadau wote kuendelea kufanya kazi ya kutokomeza ukatili kwani hali inatisha.

Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wahanga wa ukatili kama Eva na wengineo.

Share:

GST YASAINI HATI YA MAKUBALIANO (MoU) NA TAASISI YA JIOSAYANSI NA RASILIMALI MADINI YA KOREA KUSINI KIGAM


• Watanzania kujengewa uwezo kwenye kada ya Jiosayansi na Utafiti wa Madini

📍 Seoul, Korea Kusini.

Wizara ya Madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) na Taasisi ya Jiosayansi na Rasilimali Madini ya Korea Kusini (KIGAM) zimetia saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kufanya tafiti za pamoja za Jiosayansi. 

Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika Machi 26, 2025 Jijini Seoul, Korea Kusini wakati ya ziara ya Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa kushiriki Mkutano wa wadau wa madini mkakati ulioandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Korea Kusini na wadau wa Sekta Binafsi kutoka nchini Tanzania na Korea Kusini.

Hati hiyo pamoja na masula mengine itahusisha mashirikiano kwenye kufanya miradi ya pamoja ya utafiti wa jiolojia, jiokemia na utafiti wa kina wa jiofizikia ili kuibua maeneo mapya yenye madini muhimu na madini mkakati.

Maeneo mengine ya makubaliano hayo ni pamoja na kuendeleza miradi ya pamoja ya utafiti wa majanga ya asili, kujengeana uwezo zaidi wa kitaalam na mafunzo kwenye kada jiosayansi na utafiti wa madini, kufanya tafiti za uchenjuaji madini, kuandaa mifumo ya utunzaji wa taarifa za jiosayansi na kuimarisha maabara ya GST.

Kabla ya hafla ya utiaji saini, Ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ya KIGAM ikiwa ni pamoja na masuala ya maabara, utafiti wa njia mbalimbali za uchenjujai madini hususan madini mkakati, utafiti wa teknolojia za utengenezaji wa vifaa vya teknolojia ya kijani ikiwa ni pamoja na betri za magari ya umeme, utambuzi wa majanga ya asili ikiwa ni pamoja na mitetemo na milipuko na kutembelea Chuo cha Jiosayansi na Rasilimali Madini kinachomilikiwa na KIGAM.

Akielezea Ushrikiano huo ulioafikiwa, Dkt. Kiruswa aliishukuru Serikali ya Korea Kusini kupitia KIGAM kwa kukubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia GST kufanya tafiti za jiosayansi na kuwajengea uwezo watanzania na kuahidi kufuatilia utekelezaji wa Hati hiyo ili iweze kuleta manufaa chanya yalidhamiriwa.

Share:

Wednesday, 26 March 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 26,2025




Magazeti
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger