Friday, 21 March 2025

EWURA YAPOKEA MAONI YA WADAU KUHUSU UBORA WA HUDUMA

Mhandisi Mwandamizi wa Maji na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Amani Nyekele akiwapitisha washiriki wa mkutano katika vipengele vya Kanuni vinavyopendekezwa kuboreshwa, wakati wa mkutano wa EWURA na Watendaji wa Mamlaka za Maji nchini jijjni Dar es Salaam leo 20 Machi 2025

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam:

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo, 21 Machi 2015, imekutana na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kwa lengo la kupokea na kujadili maoni kuhusu maboresho ya Kanuni za Ubora wa Huduma ya Maji ili kuongeza ufanisi kwa Mamlaka hizo katika kuwahudumia wateja wake.

Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Maro, alibainisha kuwa baadhi ya maboresho ya Kanuni hizo ni pamoja na mapendekezo ya kuongezeka muda wa kutumika bei za maji kutoka miaka mitatu ya sasa hadi mitano, kuboresha muda wa kuwasilisha taarifa za utendaji, na kuweka ukomo wa mipango ya kibiashara ya mamlaka za maji.

Sabina Faya, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mha. Mwajuma Waziri, aliwasisitiza washiriki kutoa maoni yenye tija ili yawe na matokeo chanya katika kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa huduma ya maji kwa wateja nchini.


Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Exaudi Maro,akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa Mamlaka za Maji uliondaliwa na EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025 jijini Dar es Salaam.


Sehemua ya washiriki kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia mkutano wa wadau uliondaliwa na EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025 jijini Dar es Salaam.


Sehemua ya washiriki kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia mkutano wa wadau uliondaliwa na EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025 jijini Dar es Salaam.
Share:

Thursday, 20 March 2025

WANANCHI NJOMBE WAOMBWA KUSHIRIKI MDAHALO KUHUSU SEKTA YA MISITU

Na Elizabeth John, NJOMBE.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi, Dk. Pindi Chana ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa mingine wanaoshiriki  kwenye maadhimisho ya kilele cha Siku ya Misitu Duniani kushiriki kwenye mdahalo kuhusu Sekta ya Misitu unaoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba mjini Njombe ili kupata elimu ya uhifadhi kutoka kwa wataalam waliobobea katika sekta hiyo.

Dk. Chana ametoa kauli hiyo  leo wakati akikagua maandalizi ya Siku ya Misitu Duniani na hatimaye kuongea na washiriki wa mdahalo unaoendelea kwa siku ya tatu sasa katika viwanja hivyo mjini Njombe ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea.

"Ndugu zangu nawasihi kupokea heshima hii tuliyopewa na Rais wetu kipenzi,  Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutuletea  maadhimisho haya ili yafanyike katika mkoa wa Njombe" ,amefafanua Dk. Chana.

Share:

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAINGIA MAKUBALIANO NA BAHATI NASIBU YA TAIFA KUPANUA UPATIKANAJI WA MICHEZO YA KUBAHATISHA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Posta Tanzania limeingia makubaliano ya ushiriano na Bahati Nasibu ya Tanzania ili kuongeza upatikanaji wa michezo ya kubahatisha nchini.

Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya Shirika la Posta Tanzania, Jukwaa la Bahati Nasibu ya Taifa linalenga kutoa michezo iliyo rafiki, rahisi na yenye uwazi kwa washiriki wote, ikiimarisha dhamira yake ya kuboresha maisha ya watanzania kote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo leo Machi 20, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara za Kielektroniki na Huduma za Kifedha wa Shirika la Posta Tanzania, Constantine Kasese amesema kupitia upatikanaji wa majukwaa ya bahati nasibu katika ofisi zao, itasaidia kuleta urahisi wa upatikanaji wa tiketi za michezo ya kubahatisha na kuchangia juhudi za taifa za kuwainua wananchi.

" Tumejikita katika kuwaunganisha watu na huduma muhimu kote nchini. Ushirikiano huu unawiana na maono yetu ya kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ithuba Tanzania, Kelvin Koka amesema dhamira yao ni kuhakikisha kila mtanzania anaweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha.

Amesema kupitia mtandao wa Shirika la Posta Tanzania watafanikiwa kuwafikia watu wote nchini na kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kushiriki katika michezo ya kubahatisha.


Share:

"HAIWEZEKANI ANIFANYIE HIVI HALAFU ANIACHE", MDADA ASIMULIA



Jina langu ni Aisha kutoka Tanga nchini Kenya, kipindi cha nyuma nilikuwa kwenye uhusiano na kijana mtanashati kweli kweli, kila mwanamke mwenye afya njema, basi ni lazima angevutiwa naye kimahaba. 

Kijana huyu aitwaye, Abdallah alikuwa akifanya kazi ya kuongoza watalii katika maeneo mbalimbali hapa Tanga, aliwahi kuniambia kuwa utanashati wake ndio uliofanikisha kupata kazi hiyo yenye fedha nyingi. 

Kijana huyo katika mchezo wa kitanda hakuwa mchovu hata kidogo kwani alikuwa bingwa kila wakati tulipokuwa na mchuano, alijua kunichanganya sana kwa penzi lake tamu ajabu, alijua kunipa raha kusema kweli hadi nikawa sijielewi kwake. 

Hata hivyo, siku zilipozidi kwenda mambo yalianza kubadilika kwani Abdallah hata alianza kutorudi nyumbani kama iliyokuwa kawaida yake kila wikendi kitu ambacho kilininyima raha kabisa. 

Suala hili lilianza kunitia wasiwasi kwani sikuamini pendo langu kwake lingeelekezwa kwingine, nilikumbwa na msongo wa mawazo kwani alikuwa ndiye mpenzi wangu wa kwanza kuwahi kumpata katika ujana wangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu. 

Kuna siku alinitembelea na nilipomuliza mbona tabia zake zilikuwa zimeanza kubadilika alisema kuwa kila kitu kilikuwa shwari, hivyo niendelee kumwambini kama mpenzi wake, basi nilikubaliana naye kishingo upande. 

Ila akilini nilijua kwamba alikuwa akinificha ukweli wa mambo, pia nilifahamu kuwa alikuwa keshapata mpango wa kando jambo lililonikasirisha kwani urembo wangu huu ulikuwa kwa ajili yake. 

Jinsi muda ulivyokuwa ukisonga ndivyo mambo yalikuwa yanakuwa hata mabaya zaidi kwani wakati mwingine hata alisusia kunipa mapenzi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma. 

Nilifahamu kwamba alikuwa amepata mpenzi mwingine na hapo uhusiano wetu yakaisha kwa wakati ule huku nikiachwa mpweke bila kujua nini cha kufanya maishani, tayari kashanitoa bikira halafu ananiacha. 

Basi nilibaki nimesononeka tu, baada ya siku kadhaa nilikumbana na tovuti ya Kiwanga Doctors nilipokuwa katika hali ya kusoma vitu mtandaoni. 

Nilifuatilia kila kitu kilichoendelea kwenye tovuti ile na hapo nikaona kuwa Kiwanga Doctors alikuwa na uwezo wa kunisaidia kumrudisha mpenzi wangu.  

Nilifunga safari hadi kwenye ofisi za Kiwanga Doctors huko Migori, Kenya kwa ajili ya usaidizi, alinishughulikia kupitia utaalam wake wa miaka mingi (get back your ex lover) na kunihakikishia kuwa mambo yatakuwa sawa. 

Kisha nikarejea nyumbani, baada ya siku chache Abdallah alinipigia simu kwamba alitaka tukutane. Siku iliyofuata nilienda kwake, nilipofika alinipokea vizuri na kuniomba msamaha pamoja na kunipa zawadi. 

Tangu siku hiyo uhusiano wetu umekuwa imara kwani mwishowe tulifunga ndoa ya kifahari na kuwa mke na mume na sasa tuna familia ya watoto wawili wa kiume. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

INEC YATOA UFAFANUZI WANAOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA DAR

 


Share:

WANANCHI WAASWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA MKOANI RUVUMA

Muonekano wa miundombinu ya barabara inayoendelea kutekelezwa na TANROADS Mkoani Ruvuma

Na Regina Ndumbaro Ruvuma. 

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Ruvuma, Saleh Juma, amewataka wananchi wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla kutunza na kulinda miundombinu ya barabara, ikiwemo taa na alama mbalimbali. 

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga barabara, hivyo wananchi wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu kwa muda mrefu.

Aidha, Saleh ameeleza kuwa TANROADS imebaini ongezeko la wizi wa alama za barabarani, ambazo zinauzwa kama chuma chakavu, hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. 

Amesema kuwa kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Barabarani, wameweka mikakati ya kuwadhibiti wahalifu wanaoharibu miundombinu hiyo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Pia, ametaja changamoto ya magari mazito yanayosafirisha makaa ya mawe kupitia barabara zisizo na uwezo wa kubeba uzito mkubwa, jambo linalosababisha uharibifu wa barabara na madaraja. 

Ametoa mfano wa barabara ya Nangombo–Chiwindi, ambapo daraja la Nangombo limeanza kuchakaa kutokana na mzigo mkubwa wa magari yanayopita eneo hilo.

Wananchi wa Ruvuma wametoa wito kwa Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaojihusisha na wizi wa alama za barabarani. 

Ali Mselem, mfanyabiashara wa soko la Bombambili, amesema wizi huo unaweza kusababisha ajali, huku Baraka Komba akisema kuwa wahusika wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kudhibiti uhalifu huo.

Share:

TASAF KUBORESHA ZAIDI AJIRA ZA MUDA MFUPI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Shadrack Mziray amesema ziara ya mafunzo nchini, Afrika Kusini kuhusu utekelezaji wa ajira za muda mfupi itawasaidia kuimarisha utendaji.

Viongozi na TASAF  kutoka Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), akiwemo Waziri wa Wizara hiyo George Simbachawene wapo nchini Afrika Kusini kwa mualiko wa serikali hiyo, kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO), ambapo wanajengewa uwezo kuhusu mchakato wa ajira za muda mfupi.

“Kwetu sisi ziara hii, itatusaidia kwa sababu hivi sasa tunakwenda kukamilisha awamu ya pili ya mpango wa kunusuru kaya maskini hapo Septemba,”amesema Mziray katika ziara hiyo iliyoanza Machi 17 hadi 23.

Nakuongeza kuwa, “Lakini tupo katika utaratibu mzima wa kutengeneza programu mpya, hivyo yale tutakayojifunza hapa tutayachukua ili kuboresha kwenye programu mpya ya TASAF inayokuja” .

Amesema Serikali ya Afrika Kusini imewahamasisha kwa namna inavyotekeleza na kutengeneza mradi huo unaotoa fursa nyingi za ajira na ujuzi hasa kwa vijana wanaomaliza vyuo, lakini wanapata changamoto ya kupata ajira.

Mziray amefafanua kuwa vijana pia wanakuwa wamesoma nadharia, sasa wanapata nafasi ya kushiriki kwa vitendo kupitia shughuli mbalimbali zinazotekelezwa.

Kwa upande wake, Waziri Simbachawene amesema wameshiriki mkutano unaohusu ajira zisizo rasmi ambazo Serikali ya Afrika Kusini wameziwekea utaratibu mzuri tangu miaka 20 iliyopita.

Simbachawene amesema kwa sababu ajira hizo, zimeongezewa wigo na hadi kufikia kuwajengea vijana ujuzi, ujasiriamali na kuziba pengo la ukosefu wa ajira.

Katika mafunzo hayo, Simbachawene amesema mbali na kumaliza masomo yao, wahitimu wakiwemo na vyeti vyao, wanashiriki ajira katika kampuni za umma.

“Wenzetu (Afrika Kusini) wana hii programu ambayo inawasaidia sana vijana waliomaliza vyuo, ni kama vile tu Tanzania tulivyotengeneza mtaala ambao tunataka kuutekeleza sasa,”amesema   Simbachawene.

Meneja wa Masijala ya Kumbukumbu za Walengwa Tasaf, Philipine Mmari wa TASAF, amesema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza umasikini na imekuwa na utekelezaji kwa awamu tofauti.

Kwa mujibu wa Mmari, TASAF awamu ya tatu imekuwa na vipengele viwili kikiwemo cha kunusuru kaya za walengwa kilichokwisha mwaka 2019, na sehemu ya pili ilianza mwaka 2019 hadi Septemba 2025.
 
“Katika utekelezaji mpango huu, afua tatu muhimu ikiwemo uahulishaji wa fedha kwa kaya zenye uhitaji, na zile zenye watu wenye ulemavu, afua nyingine ni ajira za muda kwa kaya zenye watu kuanzia umri wa miaka 18 hadi 65,”amesema.

Mmari amesema afua ya mwisho ni kuunda vikundi visivyopungua watu 15 na kuweka akiba kwa ajili kukopeshana.   

Share:

SOUWASA YAPITA NYUMBA KWA NYUMBA KUHAMASISHA WATEJA KUREJESHA HUDUMA ZA MAJI


Wafanyakazi wa SOUWASA wakitoa elimu kwa mwananchi na mkazi wa Ruhuwiko Shuleni kuhusu umuhimu wa matumizi ya maji na kutumia fursa iliyotolewa bure ya kurejeshewa maji.
Wafanyakazi wa SOUWASA Songea wakizungumza na wananchi kuhusu huduma hiyo ya maji kwa kurejeshewa bila fidia yoyote

Na Regina Ndumbaro, Ruvuma

Katika kuelekea kilele cha Wiki ya Maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imezindua kampeni maalumu ya kuhamasisha wateja waliositishiwa huduma kurejesha maji yao kwa kulipa nusu ya deni lao. 

Kampeni hii inalenga kuwapa fursa wakazi wa Manispaa ya Songea kurejesha huduma zao kwa urahisi, huku ikihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa maji safi na salama.

Timu maalumu ya SOUWASA, ikiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Bi Baby Biko, imetembelea maeneo ya Ruhuwiko Kanisani na Ruhuwiko Shuleni ili kutoa elimu na kuwaeleza wananchi kuhusu ofa hii maalumu. 

Timu hiyo imepita nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila mkazi anayehitaji kurejesha huduma za maji anapata taarifa sahihi na fursa ya kufanikisha hilo kwa urahisi.

Ofa hii maalumu inatoa nafasi kwa wateja waliositishiwa huduma kurejeshewa maji bila fidia yoyote, endapo watalipa nusu ya deni lao ndani ya muda uliopangwa. 

Kampeni hii itadumu kwa wiki moja, kuanzia tarehe 16 hadi 22 Machi 2025, na imelenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Songea wanaokabiliwa na deni la maji.

SOUWASA inawataka wakazi wa Manispaa ya Songea kuchangamkia fursa hii kwa haraka ili kuepuka usumbufu wa ukosefu wa maji katika makazi yao. 

Huduma ya maji ni hitaji la msingi kwa kila kaya, hivyo mamlaka hiyo imeamua kuweka mazingira wezeshi kwa wateja wake ili waendelee kupata huduma bora kwa gharama nafuu.

Kampeni hii ni sehemu ya juhudi za SOUWASA kuhakikisha kila mkazi wa Songea anapata maji safi na salama kwa matumizi ya kila siku. 

Mamlaka hiyo inaendelea kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa bili zao kwa wakati ili kuepusha usitishaji wa huduma na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji kwa wote.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger