Monday, 17 March 2025

VIJANA WA UVCCM MKOA WA SHINYANGA WATAKIWA KUIMARISHA UMOJA NA USHIRIKIANO ILI KUJENGA CHAMA IMARA



NA NEEMA NKUMBI  -  KAHAMA


Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wametakiwa kuwa wamoja na kushirikiana kwa karibu pia kusajili wanachama wapya na kuimarisha jumuiya yao kwa lengo la kujenga chama imara.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, katika baraza la vijana Mkoa wa Shinyanga lililofanyika Machi 15, 2025, katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.


Mlolwa amesema kuwa, huu sio muda wa kufukuzana au kutoa watu katika nyadhifa mbalimbali walizonazo, bali vijana wanapaswa kuvumiliana wakati wa changamoto na kuzungumza kwa pamoja ili kuzitatua.


“Vijana mna nafasi kubwa ya kulitumikia taifa. Huu sio muda wa kumfukuza kiongozi kutoka wadhifa alionao, bali ni wakati wa kukaa mezani tuongee na kama kuna kiongozi mwenye changamoto, ajadiliwe kwanza katika jumuiya yake na si kutolewa bila kujua kutoka kwa jumuiya,” alisema Mlolwa.


Pia, amewataka vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huu, na iwapo watashindwa, wawe na kifua kipana na kuweza kustahimili changamoto zote.


Akisoma taarifa ya umoja wa vijana CCM, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Naibu Katalambula, amesema hadi sasa Mkoa wa Shinyanga una wanachama wa UVCCM 169,426, waliosajiliwa kielektroniki na kulipa ada, na mkakati wao ni kuendelea kusajili wanachama zaidi.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benard Werema, amesema kuwa kulikuwa na changamoto ya baadhi ya vijana kutolewa katika nyadhifa zao, lakini anashukuru kuwa uongozi wa CCM umesikiliza na kutatua changamoto hiyo, na sasa vijana wamerudishwa na chama kiko salama.


Werema pia ameeleza kuwa azimio la jumuiya ya vijana ni kuunga mkono Azimio la Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025 jijini Dodoma, ambalo lilipitisha wagombea wa Chama kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025.


Vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga wamesema wapo tayari kuhakikisha ushindi mkubwa wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa kuhamasisha ushiriki wa vijana katika uchaguzi na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki kupiga kura.


“Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga tunathibitisha kwa kauli moja kuwa tutahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025. CCM Daima – Vijana ni Nguvu ya Ushindi!”





 Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Shinyanga Arnold Bweichum akizungumza katika baraza la vijana Mkoa wa shinyanga lililofanyika machi 15, 2025.
Vijana wa skauti wakiwa katika hali ya ukakamavu
Share:

Sunday, 16 March 2025

ASKOFU MTEULE WA KKKT DAYOSISI YA MWANGA DKT. MONO APOKELEWA KWA SHANGWE KUBWA SHINYANGA


Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry

Na Isaac Masengwa
*******************
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Daktari Daniel Henry Mono amepewa mapokezi makubwa na waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayofanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Mapokezi hayo makubwa yakiongozwa na Askofu wa dayosisi hiyo Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu, yamekuwa mapokezi ya kwanza tangu ateuliwe kuwa askofu wa dayosisi ya Mwanga na yamefanyika leo Machi 15, 2025.

Akizungumza katika sala fupi ya mapokezi hayo iliyofanyika katika usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga, Askofu mteule Daktari Daniel Henry Mono amesema kuwa hakutegemea kukutana na mapokezi makubwa kama haya.


"Kwa kweli leo nimetekewa kwa sababu ukweli kabisa sikujua kama kuna jambo la namna hii. Nimekutana na jambo ambalo sikulitegemea kabisa, nimeona magari, watu na tarumbeta ambapo nilijikuta nikitekewa"

"Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa yote aliyotenda, ninamshukuru kwa jinsi alivyonipitisha katika utumishi wake na mpaka sasa ameniita tena kutumika katika nafasi hii kubwa."

"Pia nikushukuru sana baba Askofu Yohana Ernest Nzelu, umekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu, nimeishi na wewe kama rafiki na kama ndugu. Hata ulipofika wakati wa kufanya kazi na wewe nimefurahi sana kufanya kazi na mimi. Pia nikushukuru hata kwa jinsi umenishauri katika kuliendea jambo hili."

"Lakini pia nikushukuru sana baba Askofu mstaafu Makala, umekuwa mwalimu wetu mwema katika utumishi huu. Umenipa malezi mazuri ya kiutumishi, umetuntengeneza hadi kuwa hivi nilivyo. Kupata nafasi kama hii wewe umekuwa sehemu ya kufikia hatua hii."

Naye Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Yohana Ernest Nzelu, amemshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii ya utumishi aliyoipata askofu mteule Daktari Mono.

"Ni haki yetu kama dayosisi kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii aliyoipata

"Nimshukuru sana Baba Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala kwa kuwa yeye ndio amekuwa lango la wengine kupata nafasi kama hizi. Katika utumishi wako umekuwa chanzo cha sisi wengine kupata nafasi hizi."

"Nimepokea barua kutoka dayosisi ya Mwanga wakiniomba Daktari Mono uende ukatumike katika dayosisi ya Mwanga".

"Nami nimewajibu majibu ya awali kuwa Daktari Mono atakuja kutumika katika dayosisi ya Mwanga tukiwa tunasubiri maamuzi ya mwajiri wake"

Naye kwa upande wake askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo Askofu Makala amempongeza Askofu mteule Daniel Mono na kumtaka kuwa kiongozi atakayeandaa viongozi wajao.

"Ukipewa nafasi ya kuongoza andaa wengine ili kanisa liweze kusonga mbele. Baba askofu mteule hongera sana, wewe nenda kafanye kazi ya Mungu kwa kadri Mungu atakavyokutumia."

Daktari Daniel Henry Mono ni msaidizi wa Askofu wa dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria. Na alichaguliwa na mkutano mkuu wa dayosisi ya Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro kuwa askofu wa pili wa dayosisi hiyo yeye akiwa katika majukumu yake Nchini Burundi.

Hii inakuja baada ya aliyekuwa Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo Chediel Sendoro kufariki dunia mwaka jana Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akitoa neno la shukrani kwa waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakati wa mapokezi

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akitoa maelekezo wakati wa mapokezi yaAskofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono


Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akiwasili usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakati wa mapokezi hayo
Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel Mono akifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo

Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono.
Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala (katikati), Mama Askofu mstaafu Mdiakonia Lilian Makala (kushoto) na Chaplain wa Kanisa Kuu Mchungaji Zinyangwa Silas Mkiramweni wakifuatili kwa makini tukio la kumpokea Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Henry Mono

Akofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (kulia) na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi (kushoto) wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu wakati wa mapokezi hayo


Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono




Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akifauatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi yake mkoani Shinyanga
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akifuatilia kwa umakini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono (kulia), Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (katikati) Mama Askofu Lilian Yohana Ernest Nzelu (katikati) na Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel Mono (kulia) wakiwa wanafuatilia kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo

Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Waumini na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga wakati wa mapokezi
Waumini na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga wakati wa mapokezi
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono

Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 16,2025










Share:

Saturday, 15 March 2025

JUMBE ATOA TIKETI 100 MASHABIKI WA STAND UNITED FC KUSHUHUDIA MECHI DHIDI YA MTIBWA SUGAR, MILIONI 2 WAKISHINDA, LAKI 2 KILA GOLI IKO PALE PALE

 

Mhandisi James Jumbe Wiswa, mdau mkubwa wa michezo na mpenzi wa timu ya Stand United FC, ameahidi kutoa motisha ya kipekee kwa timu hiyo endapo itaifunga Mtibwa Sugar FC katika mchezo wa Ligi ya Championship utakaochezwa Machi 17, 2025, katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga. Ahadi hiyo ya milioni mbili ni sehemu ya juhudi za kuboresha michezo na kuhamasisha wachezaji wa Stand United FC kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Machi 14, 2025, mjini Shinyanga, mdau wa michezo Jackline Isaro, amesema Mhandisi Jumbe ametoa ahadi hiyo ya shilingi milioni mbili kama sehemu ya kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kuhakikisha timu ya Stand United inafanikiwa kuingia Ligi Kuu ya Tanzania.

 Isaro amesisitiza kuwa motisha hiyo ni muhimu kwa timu hiyo, kwani inatoka katika mdau ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kuona timu hiyo inaendelea kufanya vizuri.

Mhandisi James Jumbe, ambaye pia ni mkazi wa Shinyanga, ameeleza kuwa amehamasika kutoa motisha hii ili kusaidia timu ya Stand United FC, ambayo ni timu muhimu kwa jamii ya Shinyanga. Jumbe aliweka wazi kuwa ikiwa timu itashinda na kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar FC, atatoa zawadi ya shilingi milioni mbili kama ishara ya kutambua na kuenzi juhudi za wachezaji. 

Aidha, amesema kwamba atatoa shilingi 200,000 kwa kila goli litakalofungwa na Stand United katika mchezo huo, ikiwa ni motisha ya ziada kwa wachezaji kuongeza juhudi.



Motisha ya Tiketi Bure kwa Mashabiki

Mbali na motisha kwa wachezaji, Mhandisi Jumbe pia ameahidi kununua tiketi 100 kwa ajili ya mashabiki wa Stand United FC, ili waweze kuingia bure uwanjani. Huu ni msaada mkubwa kwa mashabiki, ambao mara nyingi wanakutana na changamoto za kiuchumi kuweza kumudu gharama za tiketi za uwanja. Jackline Isaro alieleza kuwa hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kwamba mashabiki wanapata nafasi ya kuwa sehemu ya mchezo huo muhimu, huku pia wakionyesha ushirikiano mkubwa kwa timu yao ya Stand United.

“Motisha hii ni sehemu ya kuongeza nguvu na hamasa kwa timu ya Stand United na mashabiki wake. Tunataka kuhakikisha kuwa timu inapata sapoti kubwa kutoka kwa jamii na mashabiki ili iweze kufikia malengo yake ya kurejea kwenye Ligi Kuu,” amesema Isaro.

Wito kwa Wananchi wa Shinyanga

Isaro pia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao ya Stand United FC katika mchezo huo wa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar. Alisema kuwa ni muhimu kwa timu hiyo kupata pointi tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumbani ili kuhakikisha wanarejea kwenye Ligi Kuu ya Tanzania na kurejesha heshima ya mkoa wa Shinyanga katika ulingo wa michezo.

“Tunataka kurudisha heshima ya mkoa wetu wa Shinyanga kwa kuiinua timu ya Stand United FC, ambayo inadhaminiwa na Jambo Group. Mchezo huu ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio ya timu yetu, na tunawaomba wananchi wa Shinyanga wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao,” amesema Jackline.

Stand United FC Yajivunia Motisha

Kwa upande wake, Afisa Habari wa Stand United FC, Ramadhani Zoro, alitoa shukrani kwa Mhandisi James Jumbe na Jambo Group kwa motisha hii ya kipekee. Zoro ameeleza kuwa ahadi ya shilingi milioni mbili na motisha ya tiketi 100 kwa mashabiki, pamoja na shilingi 200,000 kwa kila goli, ni mambo yatakayosaidia kuongeza ari ya wachezaji na kuhakikisha wanashinda mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

“Tunamshukuru Mhandisi Jumbe kwa motisha hii. Kuahidi milioni mbili iwapo tutashinda na tiketi 100 kwa mashabiki ni jambo kubwa na muhimu kwa timu yetu. Timu yetu iko tayari na mazoezi yanaendelea vizuri. Tunaahidi kuleta ushindi katika mchezo huu muhimu,” amesema Zoro.

Stand United FC inatarajia kushuka uwanjani dhidi ya Mtibwa Sugar FC katika mechi ya muhimu ya Ligi ya Championship, huku wakilenga kushinda ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu na kurejesha heshima ya mkoa wa Shinyanga katika michuano ya kitaifa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger