Sunday 1 September 2024

MATI SUPER BRANDS YASHIRIKI MANYARA DAFTARI DAY JOGGING

 



Na Mwandishi Wetu ,Manyara.


Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imeshiriki na kudhamini Matembezi maalumu ya kuhamasisha Wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura yanayofahamika kama "Manyara Daftari Day " ambapo Mamia ya wakazi wa mkoa wa Manyara wameshiriki matembezi hayo yaliyofanyika katika viwanja ya Tanzanite Kwaraa Stadium.

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi ya Kilomita 4.4 yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wamedhamini matembezi hayo ili kuhamasisha Wananchi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka.

Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo ni sehemu ya Jamii na imekuwa ikiunga mkono shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo matembezi hayo ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbali mbali ili kupata viongozi bora watakaoleta maendeleo kuanzia ngazi ya mtaa,vijiji,kata,jimbo na Taifa.

"Tumeanza kuhamasisha vijana kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapira kura hata kwenye viwanda vyetu kuhakikisha kuwa wanajiandikisha na ikiwapendeza wanaweza kuweka kituo maalumu karibu na kiwanda chetu ili vijana wengi waweze kujiandikisha",ameeleza Mulokozi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura litakaloanza Septemba 4 hadi 10 mwaka huu.





Share:

WMA YAPANGA KUNG'ARA SHIMUTA

Vikosi vya mpira wa miguu  kutoka Wakala wa Vipimo vikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo.

*****************

Ikiwa imebaki miezi miwili kuelekea mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi ( SHIMUTA) ambayo yamepangwa kufanyika katika Viwanja vya CCM Mkwakwani mkoani Tanga kuanzia tarehe 10 hadi 24 Novemba,2024, Wakala wa Vipimo (WMA)imefanya bonanza la michezo leo Agosti 31,2024, katika viwanja vya Tcc Chang'ombe (Gwambina) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mashindano hayo.

Katika kuhakikisha kuwa WMA inapata timu bora na yenye ushindani, Watumishi wa Taasisi hiyo wameshriki michezo katika bonanza hilo ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete, drafti, na kuvuta kamba ili kujiweka tayari na kuwa na utimamu wa mwili kuelekea SHIMUTA.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo, Kaimu Mkurugenzi Huduma za Biashara wa WMA Bw. Karim Mkorehe ameeleza kuwa mazoezi ya kutafuta wachezaji wa kushiriki katika michuano ya SHIMUTA yameanza mapema ili kuhakikisha ushiriki wa taasisi unakuwa na tija.

Aidha, Mkorehe amesisitiza kuwa ufanyaji wa mazoezi ya pamoja huimarisha afya, na huleta umoja na hivyo kuwataka watumishi kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kujenga utimamu wa mwili.

"Michezo ni afya na katika siku hii maalumu ya bonanza licha ya kucheza michezo mbalimbali pia watumishi wamepata nafasi ya kupima afya zao, pia wamepata chanjo ya homa ya ini na upimaji wa VVU " amesema Mkorehe.

"Leo ni siku ya kwanza ya mazoezi yetu, tutakaa na kuandaa mpango mzuri wa mazoezi ya mara, tunatarajia kuongeza michezo mingine kama vile kukimbia mbio ndefu na fupi, lengo letu ni tuwe tayari kwa mashindano ya SHIMUTA na tufanye vizuri" ameongeza Bw.Mkorehe.

Kwa upande wake Mwandishi Mwendesha Ofisi wa WMA Bi. Hamida Salum ameupongeza Uongozi wa WMA kwa kuona umuhimu wa mazoezi kwa watumishi wake na kutoa wito kwa watumishi wote wa WMA kujitokeza kwa wingi na kushiriki mazoezi kwa mujibu wa ratiba husika.

"Leo tumejumuika watumishi wa WMA kutoka ofisi za makao makuu, Ilala,Temeke,Kinondoni na wenzetu wa mkoani Pwani katika bonanza hili, tumecheza tumefurahi na kuweka miili sawa, tukiwa na nia na kufanya vizuri mazoezini tutaiwakilisha vyema WMA katika SHIMUTA ya mwaka huu hapo Tanga" ameongeza Bi Hamida.

Mashindano haya ya SHIMUTA yalianzishwa mnamo mwaka 1967 na kusajiliwa rasmi mwaka 1973. Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na huandaliwa kwa awamu na mikoa tofauti ambayo hupewa dhamana ya kuandaa mashindano kutoka kwa waratibu SHIMUTA. WMA itashiriki mashindano hayo kikamilifu.

Timu za mpira wa pete za Wakala wa Vipimo zikiwa katika mazoezi wakati wa Bonanza la Vipimo katika viwanja vya TCC Chang'ombe

Timu ya Wanawake ya kuvuta kamba ikiwa katika mazoezi ili kujihimarisha kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya SHIMUTA

Watumishi wa Wakala wa Vipimo wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kushiriki katika michezo mbalimbali

Timu ya mchezo wa drafti ikijifua kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali


Share:

Saturday 31 August 2024

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 1, 2024

Share:

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA CHEMCHEMI YA AJABU YA KONDOA MJINI.. "KUNA ULINZI MKALI WA NYOKA WATATU"

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika chemchemi ya ajabu ya maji iliyopo Kondoa Mjini Mkoani Dodoma - Picha na Malunde Media
Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika chemchemi ya ajabu ya maji iliyopo Kondoa Mjini Mkoani Dodoma 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wametembelea chemchemi ya ajabu ya maji iliyopo Kondoa Mjini Mkoani Dodoma ambayo inayozungukwa na madhari nzuri ya misitu na viumbe hai mbalimbali wakiwemo ngedere, nyoka na chui mmoja.

Waandishi wa hao wa habari wameshuhudia maajabu ya Chemchemi hiyo iliyopo msituni yenye maji asili ya chumvi ambayo imejengewa ukuta na kuifanya iwe chanzo kikuu cha maji chenye uwezo wa kusambaza maji kwa wakazi wa eneo hilo.

Mmoja wa walinzi wanaolinda eneo hilo anasema chemchemi hiyo ina ulinzi mkali wa nyoka watatu wakubwa ambao huonekana nyakati za usiku wakizunguka kwenye chemchemi lakini pia endapo katika eneo hilo akaingia mtu mwenye nia ovu/mbaya nyoka hao huonekana hata kama ni mchana ili kuzuia janga.

Waandishi wa habari wameelezwa kuwa wageni kutoka maeneo mbalimbali hufika katika chemchemi hiyo ambayo inalindwa na nyoka nyakati za usiku na kuchukua maji hayo ambayo yanadaiwa huondoa balaa/mikosi na kuponya magonjwa.

Msitu unaozunguka chemchemi hii pia unachangia katika uhifadhi wa mazingira na ni nyumbani kwa mimea na wanyama wa aina mbalimbali.

Chemchemi ya Kondoa Mjini, kama sehemu ya mazingira yenye rasilimali za maji, ina maajabu kadhaa yanayoiweka kuwa ya kipekee, mfano Uwepo wa Maisha ya Wanyama na Mimea: Chemchemi ya Kondoa inatoa maji safi na yenye unyevu kwa mazingira ya karibu, na hivyo kuunda mazingira yenye muktadha mzuri kwa wanyama na mimea. Hii inajumuisha aina mbalimbali za mimea ya msitu, wanyama wa porini na viumbe vidogo vidogo.
Pia Uhifadhi wa Maji, Chemchemi hii ni muhimu kwa uhifadhi wa maji kwa ajili ya wakazi wa Kondoa na maeneo jirani. Inasaidia katika kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kunywa, kilimo, na matumizi mengine ya nyumbani, hasa katika nyakati za ukame.

Kuhusu Mchango wa Mazingira, Chemchemi ya Kondoa ni sehemu ya mfumo wa maji wa chini ya ardhi ambayo ina mchango mkubwa katika kudumisha mazingira ya asili.

Kihistoria na Utamaduni, Chemchemi ya Kondoa pia ina umuhimu wa kihistoria na kitamaduni. Chemchemi hii ina hadithi na imani zinazohusishwa nayo, na hivyo kuwa sehemu ya urithi wa kitamaduni wa jamii katika eneo hilo.

Chemchemi ya Kondoa ina umuhimu katika urithi wa kitamaduni wa eneo hilo. Hadithi, hadithi za kienyeji, na simulizi zinazohusiana na chemchemi hii zinatoa mwangaza kuhusu maisha na imani za watu wa eneo hilo.

Kwa upande wa Utafiti wa Kijiolojia na Hidrolojia, Chemchemi hii ni muhimu kwa tafiti za kijiolojia na hidrolojia kwa sababu inatoa maelezo muhimu kuhusu michakato ya mawe na jinsi maji yanavyotiririka chini ya ardhi.
Pia inasemekana kuwa mzungu (mmoja wa wageni au mtafiti wa kigeni) alitumbukia kwenye chemchemi ya Kondoa wakati alikuwa akichunguza au kutembelea eneo hilo.

Hadithi kuhusu mzungu kutumbukia kwenye chemchemi ya Kondoa ni maarufu kama simulizi ya kihistoria au hadithi inayohusishwa na eneo hilo. Hadithi hii inaeleza tukio la zamani ambalo linaweza kuwa na sehemu ya ukweli, lakini mara nyingi ni sehemu ya urithi wa kitamaduni wa eneo hilo.

Ipo Hadithi kuhusu tembo kutumbukia kwenye chemchemi ya Kondoa ni sehemu ya simulizi za kienyeji na hadithi za kitamaduni zinazozunguka eneo hilo. Katika baadhi ya hadithi za watu wa eneo la Kondoa, kuna simulizi kwamba tembo alitumbukia kwenye chemchemi au kwenye eneo la maji na kwamba tukio hili lina umuhimu wa kihistoria au kitamaduni. Hizi ni baadhi ya mambo yanayohusiana na simulizi hiyo:

Kwa kifupi, chemchemi ya Kondoa Mjini ina umuhimu mkubwa katika nyanja mbalimbali, na inachangia kwa kiasi kikubwa katika maisha ya watu wa eneo hilo, uhifadhi wa mazingira, na urithi wa kiutamaduni.
Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika chemchemi ya ajabu ya maji iliyopo Kondoa Mjini Mkoani Dodoma 

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akijipiga picha za kumbukumbu kwenye  Chemchemi ya Kondoa
Waandishi wa habari wakipiga picha za kumbukumbu kwenye  Chemchemi ya Kondoa

Share:

NDOTO YA RAIS SAMIA NI KUWA NA MASHIRIKA YENYE UFANISI - BALOZI Dkt. KUSILUKA

 

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amesema kuwa ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha nchi inakuwa na mashirika yenye ufanisi mkubwa na wa viwango vya kimataifa.

Hivyo, amewataka Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa taasisi na Mashirika ya Umma kuhakikisha wanatekeleza kwa ukamilifu maagizo yaliyotolewa na Mhe. Rais Samia.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 30, 2024 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha viongozi hao kilichofanyika jijini humo tangu Agosti 27 hadi 30, 2024.

"Serikali itayachukua maazimio yote yaliyokubaliwa na nawaahidi yatafanyiwa kazi, tutawasaidia kuhakikisha yanatekelezeka ili kutimiza ndoto ya Mhe. Rais Samia juu ya taasisi na mashirika ya umma", amesema Balozi, Dkt. Kusiluka.

Amewataka viongozi wa taasisi na mashirika ya umma kujenga utamaduni wa kujifunza mbinu na mikakati mipya kutoka kwa mashirika yaliofanikiwa na kuitazama serikali kwa upana wake.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Mbaga Kida amesema kuwa wamewasilisha malengo na wanaamini watayasimamia malengo hayo ili kuweza kuhakikisha yale waliyojiwekea katika kusimamia na kuboresha utendaji kazi wa taasisi na mashirika ya umma yanaweza kufikiwa.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesoma jumla ya maazimio sita yaliyoazimiwa na viongozi hao ikiwemo, Ushiriki katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2050 na uandaaji wa mipango mkakati wa taasisi za umma; Utawala bora na mawasiliano ya umma pamoja na Usimamizi wa rasilimali watu, mafunzo na uendelezaji wa uongozi bora.

Maazimio mengini ni, Mikakati ya taasisi na mashirika ya umma kuwekeza nje ya Tanzania; Kuongeza uchangiaji na kupunguza utegemezi katika Mfuko Mkuu wa Taifa na kutekeleza kikamilifu maazimio yaliyotolewa kwenye kikao kilichopita ambayo hayajatekelezwa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba, Kamishna wa Bima Tanzania kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware amesema kuwa Wakuu wa Taasisi wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi na wanaahidi kuyatekeleza kwani wana hamu na mageuzi yanayotarajiwa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger