Wednesday 14 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 15, 2024

Share:

MISA TAN YALAANI WAANDISHI WA HABARI KUKAMATWA MBEYA

 

Share:

Tuesday 13 August 2024

MGODI WA GGM WAANZA KUTUMIA UMEME WA GRIDI BADALA YA MAFUTA

📌 Dkt. Biteko azindua kituo cha kupoza umeme cha GGM (MW 34)

📌 Asema kitaongeza mapato ya mgodi kwa Serikali

📌 Aipongeza GGM kuzipa kipaumbele kampuni za kizawa

📌 TANESCO kuingiza mapato ya sh.Bilioni 2 hadi 3 kwa mwezi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua kituo cha kupokea na kupoza umeme katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) chenye uwezo wa megawati 34 ambacho sasa kinawezesha GGML kuanza kutumia umeme wa gridi kwa matumizi yake badala ya mafuta na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

Baada ya kuzindua kituo hicho tarehe 13 Agosti 2024 wilayani Geita mkoani Geita,  Dkt.Biteko amesema ujenzi wa kituo hicho ni alama halisi ya umoja na ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Sekta Binafsi kwani mradi huo umehusisha ujenzi wa laini ya umeme ya kV 33 ambayo imejengwa na TANESCO kwa gharama ya shilingi bilioni 8.04 huku  GGML ikijenga kituo cha kupoza umeme kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 24.

Amesema GGM  ilikuwa inatumia shilingi bilioni 130 kwa mwezi kama gharama za uendeshaji  na kwenye umeme wa mafuta ilikuwa inatumia shilingi bilioni 13.4 kila mwezi na kuathiri mapato yake kwa Serikali, hivyo kuanza kazi kwa kituo hicho kunapunguza gharama za uendeshaji kwa mgodi na kupelekea Serikali kuongeza mapato yake, kuongeza ajira na pia GGM kuweza kutanua shughuli zake.

Dkt.Biteko ameipongeza kampuni hiyo kwa kuanza kutumia umeme wa gridi ambao unapunguza  gharama za uendeshaji ambapo ametoa angalizo kuwa, kupungua kwa gharama hizo  kuguse pia watumishi kwa kuboresha maslahi yao.

Ameeleza kuwa, umeme mwingi unaozalishwa kwa sasa unatoa uhakika wa kwenda kwa wananchi na walaji wakubwa kama GGM na kuweka mkazo kuwa, hayo ni matokeo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuijali sekta binafsi.

Vilevile, ameipongeza GGM kwa kuzipa kipaumbele kampuni za kizawa katika kutoa huduma kwenye mgodi huo na kusisitiza kuwa huo ndio msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kuhakikisha kampuni za ndani zinapewa kipaumbele kwenye miradi mbalimbali.

Dkt. Biteko amewaagiza Watendaji wa Wizara ya Nishati, TANESCO na Taasisi nyingine za Serikali kujali sekta binafsi kutokana na manufaa yake ikiwemo kuwa walipakodi wakubwa na kuongeza ajira nchini.

Pia, amewashukuru  watangulizi wake katika Sekta ya Nishati, Dkt. Medard Kalemani na January Makamba ambao katika kipindi chao wakihudumu kama Mawaziri wa Nishati waliusimamia mradi huo ipasavyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema hali ya umeme nchini kwa ujumla ni nzuri huku uzalishaji ukikidhi mahitaji na ziada kidogo.

Kuhusu usambazaji umeme mkoani Geita amesema kuwa Mkoa una Vijiji 486 na kati ya hivyo vijiji 483 vina umeme sawa na asilimia 99.38.

Ameongeza kuwa, kazi ya kupeleka umeme vitongojini  mkoani Geita inaendelea ambapo kati ya vitongoji 2,197, vitongoji takriban 1000  tayari vina umeme.

Ameongeza kuwa,  Mkoa wa Geita umetengewa Shilingi  bilioni 8.5 kwa ajili ya kupeleka umeme maeneo ya migodi na viwanda na utekelezaji umefikia asilimia 41.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella  amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ambayo yamepelekea wawekezaji kufanya kazi na kuletea nchi faida akitolea mfano kuwa,  katika kipindi cha miaka mitatu GGM imezalisha tani 51 za dhahabu ambayo ni mafanikio makubwa yanayochangia ukuaji wa pato la Taifa.

Amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha umeme kufika pia kwenye migodi  ya Wachimbaji wadogo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu wachimbaji wadogo 19 wamepelekewa umeme kwenye migodi yao na kuwezesha uzalishaji wa kilo za dhahabu takriban 11,000.

Wabunge mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wamempongeza Rais Samia pamoja na uongozi wa Wizara ya Nishati kwa kutekeleza mradi huo ambao una umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi  na mgodi wenyewe.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha.Abubakari Issa amesema  kuzinduliwa kwa kituo hicho  kutaiwezesha GGML kuanza kutumia umeme wa gridi kwenye matumizi yake pamoja na kuongeza mapato ya TANESCO ambapo inategemewa yataongezeka kwa kiasi cha shilingi bilioni 2 hadi 3 kwa mwezi. 

Makamu wa Rais wa kampuni ya Anglo Gold Ashanti-Tanzania anayeshughulikia Miradi Endelevu, Simon  Shayo  ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na miundombinu madhubuti ya umeme inayowawezesha kufanya biashara kwa ufanisi.

Amesema mradi huo ni muhimu kwa GGM kwani unawawezesha kupata umeme wa gridi na kupunguza matumizi ya umeme wa mafuta ambapo gharama zitapungua kwa asilimia 92. 

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ni Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge, Wabunge kutoka Mkoa wa Geita, Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na GGM.
Share:

AMSHA AMSHA ZA MSIMU MPYA NA BETWAY.


Dar es Salaam, Tanzania - 8 Agosti, 2024

Ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu mweingine wa burudani katika ligi kubwa duniani, Kampuni ya ubashiri Betway iko pamoja na wateja kuwaba burudani na huduma bora za kubashiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko Betway Tanzania Calvin Mhina amesema walishiriki vyema kuwa sehemu ya burudani kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mitanange ya ngao ya jamii katika viunga vya uwanja wa Taifa pamoja na Betway Arena ya kisasa iliyoko Mbezi Beach Dar es salam.

Amesema wateja waliojitokeza walipata wasaa wa kushiriki michezo mbali mbali na kujishindia zawadi za papo hapo toka Betway.

Aidha amesema pamoja na kutoa elimu ya kubashiri kistaarabu pia ilikuwa ni wasaa wa kueleza wateja huduma mpya na bora zitakazowawezesha kufurahia kubashiri na kushinda zaidi.

"Msimu huu tunawaletea promosheni ya Pata Zaidi na Betway ikiwa imesheheni ofa lukuki. Promosheni hii inakuruhusu kuchagua Offer Uipendayo, yani hatukuoangii ofa wewe ndio unachagua ipi inakufaa kila wiki Wateja wanatakiwa kutembelea kurasa yetu ya promosheni katika tovuti www.betway .co.tz na kuchagua kushiriki ili wasipitwe na of hizi na nyingine nyingi msimu". Amesema

Share:

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA, PSSSF NA WCF WAINGIA UBIA KUMILIKI KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE

 

Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu, akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kumiliki kiwanda hicho iliyofanyika katika Ofisi ya PSSSF, Msajili wa Hazina iliyofanyika Agosti 9,2024 Jijini Dodoma.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu, akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo Jijini Dodoma. - wakwanza kushotokwake, ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul -Razaq Badru, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), wameingia ubia wa kumiliki Kiwanda Cha Chai cha Mponde kwaajili ya kuongeza tija katika uzalishaji, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika zao la Chai.

Katika ubia huo Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa niaba Serikali inamiliki hisa ya asilimia 16, huku PSSSF na WCF wanamiliki asilimia 42 kila mmoja jambo ambalo litaongeza kasi ya utendaji katika ushindani wa soko na kuifanya Taifa kupata gawio kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

Akizungumza jijini Dodoma Agosti 9, 2024 katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kumiliki kiwanda hicho iliyofanyika katika Ofisi ya PSSSF, Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu, amesema kuwa uwekezaji huo unakwenda kuongezeka thamani ya kiwanda kutoka shilingi milioni 790 zilizopo na kufikia bilioni 4.8.

Bw. Mchechu amesema wanatarajia kuwekeza shilingi bilioni nne ambapo mpaka sasa tayari uwekezaji katika kiwanda hicho umefika bilioni 2.5.

“Kiwanda hiki kinakwenda kufufua uchumi kwa wakazi wa Korogwe na wakulima wa zao la chai watapata fursa ya kupata soko la uhakika wa kuuza mazao yao" amesema Bw. Mchechu.

Bw. Mchechu ameongeza kuwa kupitia uwekezaji huo, Serikali inakwenda kunufaika na ulipaji wa kodi, huku akisisitiza umuhimu wa Menejimenti kuongeza ufanisi katika utendaji ili waweze kuleta gawio kama ilivyo kwa taasisi nyengine.

“Nawashukuru sana PSSSF, WCF kwa kukubali wito wa kwenda kufanya uwekezaji katika sekta ya kilimo cha chai, ukiangalia tuna ardhi nzuri ambayo tunaweza kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali nchini” amesema Mchechu.

aidha, amesema kuwa Tanzania kuna ardhi kubwa na yenye rutuba ambayo inakubali kilimo cha chai hasa Mikoa ya Iringa na Mbeya, huku akieleza kuwa kulikosekana wawekezaji wa viwanda katika zao la chai ambalo linalimwa kwa muda mrefu na kuleta tija.

"PSSSF na WCF wanapoonekana katika uwekezaji sekta ya kilimo itawavutia wadau wengine na kufanya vizuri sekta hii, kwani kwa muda mrefu wakulima walishindwa kulima zao la chai kutokana na kukosa soko la uhakika" amesema Mchechu.

Mchechu amebainisha kuwa Tanzania inazalisha kiwango kidogo cha chai na kufanya mauzo kuwa dola milioni 50 kwa mwaka, tofauti na nchi jirani ya Kenya ambao wanauza zaidi ya dola Bilioni moja.

“Tupo chini katika mauzo kwa sababu tuna mwamko mdogo wa kufanya uwekezaji katika zao la chai, lakini leo tunashukuru tunawapa nafasi kiwanda hiki, menejimenti, bodi kuanza kukimbia katika utekelezaji wa majukumu yao” amesema Mchechu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema kuwa uwekezaji huo unakwenda kuibua uchumi wa wananchi katika mkoa husika, kwani wakulima wengi wa eneo wanakwenda kuuza zao la chai katika kiwanda hicho.

"Ni busara imetumika kutumia fedha za Mifuko kuleta hapa kwa ajili ya kufanya uwekezaji na kuleta faida kwa kiwanda na Wananchi" amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul -Razaq Badru amesema kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya mipango yao kutimiza jukumu linalotarajiwa na Serikali kuwekeza katika maeneo yenye mchango kwa wananchi na wanachama wao.

"Tumefarijika kuwekeza katika sekta ya kilimo sehemu ambayo inatoa mchango mkubwa kwa Taifa, tutaendelea kushiriki katika maeneo mengine na kuleta tija kwa wananchi" amesema.

Meneja Mkuu wa Kiwanda Cha Chai cha Mponde Bw. Muhoja Manane, akizungumza alipokuwa akitoa taarifa fupi ya uzalishaji wa Kiwanda hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma, akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul -Razaq Badru, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Agosti 9,2024 Jijini Dodoma.

PICHA; ZOEZI LA UTIAJI SAINI, NA MAKABIDHIANO.

PICHA MBALIMBALI ZA WADAU NA WATUMISHI


Share:

AZAKI ZAIOMBA SERIKALI KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM

Meneja Programu wa FCS Bi. Nasim Losai akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 Jijini Dar es salaam

Na; Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM


Asasi za Kiraia nchini kupitia Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), imeiomba Serikali iangazie katika kuhakikisha makundi maalum yanawezeshwa kufikia miundombinu ya kidigitali ili waweze kushiriki katika michakato ya maendeleo na kujiimarisha kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Meneja Programu wa FCS Bi. Nasim Losai katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 Jijini Dar es salaam.


Bi. Losai amesema kuwa mkutano huo umejikita katika kuangazia ushiriki wa watu wenye ulemavu katika maendeleo, uchumi na kijamii, huku ukiangazia matumizi ya takwimu za sensa katika kuboresha mipango ya halmashauri za wilaya na ngazi za kata.


Aidha, ameeleza kuwa Serikali imekuwa Sikivu katika kuhakikisha makundi maalum yanafikiwa na kuwezeshwa katika shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato, nakwamba FCS wamekuwa wakIisadia serikali katika kuunga mkono juhudi hizo kutokana na zoefu wao wa zaidi ya miaka 20 ya kufanya kazi na jamii.


"FCS tuna zaidi ya miak 20 tumekuwa tukisaidia serikali hasa katika shughuli za jamii na kutetea watu wenye ulemavu na michakato ya kiserikali, hasa kwenye majengo mengi mioundombinu imebadilika na kazi kubwa imefanywa na FCS pamoja na makundi haya" amsema Bi. Losai.


Kwa upande wake Mshauri wakitalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania Peter charlse, amesema mkutano huo umejumuisha watu mwenye ulemavu zaidi ya 600 kutoka ndani ya Jiji la Dar es salaam wakiwepo madiwani 60 wa viti maalimu na wale wakuteuliwa.


Amesema kuwa malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali na kuangazia zaidi eneo la uchumi na kuona fursa zipi walemavu wameweza kushirikishwa na ambazo wanaziweza.


"Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu bado ni mdogo ndio maana tumewaalika madiwani ili kuangalia changamoto zilizopo na kuwajengea ili kuyaingiza katika mipango yao ya maendeleo kupitia Mabaraza yao ndani ya halmashauri" amesema.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania Hamadi Abdallah komboza, amesema changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni masuala ya ajira, huku akimuomba kamshina wa kazi na vyama vyenye ulemavu kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi ambazo zinapaswa kuajiri watu wenye ulemavu lakini bado hazijatekeleza nakwamba msukumo zaidi unahitajika.


Katibu Mkuu Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania, Jonas Lubalo ameishukuru taasis ya Ikupa Trust Fund kwa kuendelea kuchangia na kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mshauri wakitaalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania, Peter Charles Mwita akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano huo Jijini Dar es Salaam.
Share:

Monday 12 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 13,2024

Share:

Wimbo Mpya : NG'WANA PAULO - MARAFIKI FEKI

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger