Wednesday 7 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 8,2024

Share:

WAJIPANGA KUGAWA MBEGU CHOTARA ZA ALIZETI MSIMU UJAO KWA MFUMO WA RUZUKU

Alizeti aina ya Sunbloom mbegu chotara zitakazosambazwa Msimu ujao kwa bei ya ruzuku na Wakala wa Mbegu


Wakala wa Mbegu za Mazao wamejipanga kugawa mbegu chotara za alizeti kwa wakulima kwa mfumo wa ruzuku.

Tayari tani  zaidi ya 600 zipo na ziko kwenye mchakato wa kuziandaa ili ziingie sokoni. 

Kaimu meneja masoko wa Wakala wa mbegu za mazao,Edward Angolile Mbugi amesema mbegu hizo zimeagizwa kytoka nchini India na aina hii ya mbegu inaitwa SUN BLOOM. Itauzwa kwa shilingi 10,000 kwa kilo.

 Hivyo wananchi walichangamkie ili kupunguza pengo la upungufu wa mafuta ya kula.

Nao wadau wengine wa kilimo cha alizeti wamekuja na maonesho ya mbegu chotara na kuwataka wakulima wa mikoa ya Singida na Dodoma kwenda kujifunza kilimo bora'' na chenye tija cha alizeti kwenye maeneo ya mashamba darasa yaliyoandaliwa kwenye viwanja hivyo vya Nzuguni.

Afisa Ugani wa Halmashauri ya Singida  anahamasisha wakulima kutumia mbegu ya Aguara6 na SuperSun ambazo zimeonesha kufanya vizuri na kuwa na sifa tofauti ya kuwa na kichwa kikubwa na mbegu zilizojaza, nzito na zenye mafuta mengi.

Amewataka wakulima wa zao la Alizeti kufuata kanuni za kilimo bora'' na kuweka mbolea kwenye zao  hilo kwani wengine hawatumii mbolea kwenye kilimo cha alizeti matokeo yake wanavuna gunia moja kwa ekari.
Share:

HUYU NDIYO DR. MANGURUWE, MTANZANIA ANAYETUMIA MBINU ZA KISASA KUKUZA UFUGAJI NGURUWE


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Dr. Manguruwe wa Zamahero, Dodoma, ni jina la mfugaji wa nguruwe ambaye ameanzisha juhudi za kukuza ufugaji wa nguruwe nchini Tanzania katika mradi maarufu wa Dr. Manguruwe Project kupitia Kampuni ya DR MANGURUWE PLC!


Habari njema ni kwamba Mfugaji huyu maarufu wa Nguruwe na mmiliki wa Mradi wa Kijiji cha Nguruwe Project awali Mr Manguruwe Tambaye amejizolea umaarufu mkubwa Mitandaoni, ametunukiwa SHAHADA YA UDHAMIRI WA FALSAFA YA BIASHARA NA MAENDELEO YA JAMII( DOCTOR IN BUSINESS AND HUMANITY) ya Chuo kikuu cha AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY.
Ametukuniwa udaktari huo baada ya kuongoza vizuri biashara zake,kusaidia wengine na kuwa na Falsafa ya Kuamini na Kufanya kazi kwa Juhudi na Maarifa ili kufikia Malengo makubwa na kufundisha na kuhamasisha wengine kwa maendeleo ya nchi.

Digrii hiyo ya Udhamiri imetolewa na Professor Stephen Nzowa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo wawekezaji katika mradi wake, ndugu, jamaa na marafiki zake kutoka ndani na nje ya nchi.

Mr. Manguruwe kwa sasa Dr. Manguruwe ameeleza furaha yake baada ya kutunukiwa udaktari huo ambapo amemshukuru Mwenyezi Mungu na Mke wake Rose Simon Mnkondya kwa kuwa naye bega kwa bega ili kutimiza kazi zake vizuri na kuweza kutunukiwa Udaktari wa FALSAFA ya Biashara na Maendeleo ya Jamii.


UMAARUFU WA DR MANGURUWE UMETOKANA NA NINI?


Dkt. Manguruwe anafahamika kwa mchango wake mkubwa katika kilimo na ufugaji, akitumia ujuzi wake wa kitaalamu ili kuendeleza sekta hii.
Katika muktadha wa Zamahero, Dodoma, Dr. Manguruwe anajulikana kwa maarifa yake ya kiufundi na uzoefu wa ufugaji, akisaidia kuboresha mbinu za ufugaji na kuongeza tija katika shughuli zake.

Hivyo, jina lake limekuwa maarufu katika jamii kwa sababu ya juhudi zake na mafanikio aliyoonyesha katika sekta ya ufugaji.


Dr. Manguruwe anatumia mbinu mbalimbali za kisasa na za kitaalamu katika ufugaji wa nguruwe ili kuhakikisha uzalishaji bora na tija.


SIFA ZA PEKEE ZA DR MANGURUWE NI ZIPI HASA?

Sifa pekee za Dr. Manguruwe ni pamoja na kuwa na ujuzi mkubwa katika ufugaji wa nguruwe, akitumia mbinu za kisasa na za kitaalamu katika shughuli zake pamoja na kukuza sekta ya ufugaji kwa kutumia mbinu bora na kuleta maendeleo akijikita katika uwekezaji kwenye miundombinu ya kisasa kwa ajili ya ufugaji, kama vile mabanda na vifaa vya kisasa na amekuwa na mapenzi ya dhati kwa maendeleo ya jamii yake, akichangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Dr. Manguruwe ni mwekezaji mzuri nchini Tanzania kutokana na mchango wake katika sekta ya ufugaji na kilimo.
Dkt. Manguruwe ni mfugaji maarufu wa nguruwe nchini Tanzania, na anajulikana kwa kuwa na idadi kubwa ya nguruwe katika shughuli zake za ufugaji hivyo ameweza kuwa na mafanikio makubwa katika sekta hii.

Kwa hivyo, Simon Mkondya 'DR. MANGURUWE' anachukuliwa kuwa mmoja wa wafugaji wenye nguruwe wengi zaidi nchini Tanzania

Dr Manguruwe amechangia kwa kiasi kikubwa kukuza Sekta ya Ufugaji nchini Tanzania akitumia mbinu za kisasa katika ufugaji wa nguruwe zilizoleta matokeo bora na kuongeza tija.


Aidha amechangia Maendeleo ya Kiuchumi kwa kufanikisha kupatikana kwa ajira kwa watu wengi katika jamii yake.

Dr. Manguruwe anachangia pia kukuza uchumi wa taifa kwa uzalishaji wa chakula kwani Uzalishaji wa nguruwe hutoa nyama ya nguruwe ambayo ni chakula muhimu kwa watu na amefanikisha kupatikana kwa ajira za moja kwa moja wafanyakazi wanaohudumia kwenye mabanda ya nguruwe, wauzaji wa chakula cha nguruwe, na wengine walioko kwenye mchakato wa uzalishaji.


ANATUMIA MBINU GANI KUFUGA NGURUWE?

Baadhi ya mbinu anazotumia katika ufugaji wa nguruwe ni kama vile kudhibiti Magonjwa na Afya ya Nguruwe ambapo amekuwa na mpango wa kudhibiti magonjwa, kutoa chanjo za msingi, na kutibu magonjwa kwa wakati huku akidumisha usafi katika mabanda ya nguruwe ili kupunguza hatari ya maambukizi.


Lakini pia amekuwa akitoa Lishe Bora kwa nguruwe akiwapa chakula chenye virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji mzuri wa nguruwe.

Mbali na kuandaa mipango maalum ya chakula kulingana na umri, uzito, na hatua za ukuaji wa nguruwe, Pia Dr Manguruwe ametengeneza Majengo ya Kisasa akitumia mabanda yanayowekwa vizuri na yenye mazingira yanayofaa kwa afya ya nguruwe.

Hali kadhalika amekuwa na ushirikiano na wafugaji wenzake kwa ambapo amekuwa akitoa mafunzo na elimu kwa wafugaji wengine kuhusu mbinu bora za ufugaji wa nguruwe akitumia teknolojia mpya na kufanya utafiti ili kuboresha mbinu za ufugaji.


UMAARUFU WA KIJIJI CHA NGURUWE

Kijiji cha Nguruwe cha Dr. Manguruwe kinavutia wageni na watu mbalimbali kutokana na umaarufu wake katika ufugaji wa nguruwe. Wageni wanaotembelea kijiji hiki ni pamoja na Wafugaji na Wakulima, Wataalamu wa ufugaji, viongozi wa jamii na Serikali, wafanyabiashara na makundi mbalimbali ya watu wanaofika katika mradi huo hivyo kuchangia katika kukuza maarifa kuhusu ufugaji wa nguruwe na kusaidia kuboresha sekta ya kilimo na ufugaji katika eneo hilo na nchi kwa ujumla.

Idadi ya watu kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo watalii na wawekezaji wazawa na wa kigeni wenye dhamira ya kufanya uwekezaji katika kijiji cha Nguruwe imekuwa ikiongezeka siku hadi siku katika mradi huo uliopo kijiji cha Mayamaya wilayani Bahi Mkoani Dodoma ili kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa wa Nguruwe na kisha kuonyesha nia ya kuwekeza katika mradi huo uliochipuka kwa kasi hivi karibuni.


WASILIANA na DR Manguruwe Project Zamahero Dodoma +255 756 000 095
+255 769 300 200
Whatsapp +255 629 300 200
Share:

Tuesday 6 August 2024

NGAMIA 300 WAKAMATWA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA


Na Hadija Bagasha Tanga.

NGAMIA 300 wamekamatwa kwenye hifadhi ya msitu wa Mwakijembe uliopo mpakani mwa Tanzania na Kenya, wakichungwa kwa lengo la kupata malisho.

Ngamia hao wamekamatwa Julai 23 mwaka huu katika msitu huo wamebaki watatu baada ya wengine kutoroshwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa kimataifa uliopo eneo la mpakani Horohoro kwa ajili ya ukaguzi wa mnada huo na kueleza kuwa ngamia hao ambao wameingia mpakani hapo kutokea nchi jirani ya Kenya wapo chini ya ulinzi maalum hadi pale taratibu za kisheria zitakapokamilishwa ili kuruhusu ngamia hao kuchukuliwa na mmiliki kutoka Kenya kutokana na uharibifu uliofanywa na ngamia hao katika misitu ya TFS pamoja na misitu ya kijiji.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian alisema mfugaji aliyekamatwa akiwa na mifugo hiyo aliachiwa kutokana na ujirani mwema lakini mifugo hiyo alitakiwa ailipie Kwa Sheria ya TFS kutokana na ngamia hao kufanya uharibifu huo.
"Ngamia hawa wamekuwa wakiingizwa kupitia njia za panya kula malisho katika eneo letu na hao walikuwa 300 kwa ujirani mwema tumeendelea kuachia lakini sasa tumeona huwezi ukaingiza mifugo ama ukiwa mtanzania huruhusiwi kuingiza mifugo kwenye hifadhi ya misitu ya TFS na hata katika misitu ya kijiji baada ya kuwaona wako kwa siku 4 nzima jitihada za kuwaondoa zimeshindikana ilibidi sisi tuwashike mheshimiwa DC amefanya mawasiliano na wenzake wa Lungalunga tulimkamata mfugaji lakini tulimwachia kwa ajili ya ujirani mwema",alisema Batilda.

"Hawa mifugo tumeona kulingana na sheria zetu za kuingiza mifugo kwenye hifadhi ya misitu kuna faini ambayo hata mtanzania anatozwa ukiharibu uoto wa asili kuna faini yake yule mfugo tu kuingia ndani kuna faini yake mtu anayefuga kuingia ndani kuna faini yake na hivyo vyote lakini pamoja na gharama ya kuwalisha wale mifugo kuna gharama zake kwa hiyo Halmashauri imetengeneza gharama inayoingia kwenye gharama ya Halmashauri za Serikali tumempatia mfugaji aweze kuturejeshea gharama zile na kulipa faini zile za TFS ndio maana mnawaona hawa mifugo hapa, "alisema Batilda.

Aidha akizungumza mara baada ya kukagua mnada wa Kimataifa wa Horohoro Mkuu wa Mkoa Batilda ameagiza wataalamu wa sekta ya mifugo kupitia mpango wa utoaji vibali vya kusafirisha mifugo nje ya nchi ili kulinusuru soko jipya la kimataifa lililojengwa ambalo kwa sasa halitumiki ipasavyo kutokana na wafanyabiashara wengi kulikwepa na kutumia mpango wa vibali na kulikosesha Taifa mapato.

"Suala zima la dhana ya kuwepo kwa mnada huu wa kimataifa ni kuhakikisha kwamba mifugo yetu wawe Ng'ombe, Mbuzi, kondoo wanapigwa mnada hapa na sio eneo la kukatisha kibali cha kusafirisha mifugo nje ndio maana tukajenga na kilinge ili Ng'ombe akifika kwenye mizani apimwe aingie kwenye kilinge tumchague kwamba Ng'ombe huyu atauzwa kwa kiasi gani sasa ivi ananunuliwa kwenye soko la awali la pili akija hapa tunamkatia kibali cha kusafirisha nje sio madhumuni ya mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan", alisisitiza Batilda.


"Mheshimiwa Rais alikusudia soko hili litumike wafugaji wapate bei nzuri waende wakauze kule wapate fedha zao nzuri na sisi tumekubaliana na Halmashauri zetu tuchukue fursa hii vijana wetu waanze BBT mifugo na bahati nzuri tuna BBT mifugo kitaifa hapa Tanga wanakuja vijana kutoka Tanzania nzima tumemuomba Waziri tuweke vijana wetu 30 maadamu BBT mifugo ipo hapa Tanga vijana wetu hawatakuwa na gharama kwasababu wanaishi hapa hapa Tanga", aliongeza  Batilda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Gilbert Kalima ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote ya Mkuu wa Mkoa huku akimuomba aongeze msisitizo Wizarani ili suala la soko la mazao ambalo limetengewa eneo lipewe kipaumbele ili jamii iweze kulitumia na hatimaye kuimarisha uchumi wao.

Naye Mwenyekiti serikali ya Horohoro kijijini Jumapili Yohana amesema matarajio ya wananchi kwenye mnada huo ni kwamba mnada huo uwe ni soko la kimataifa wanyama wote ikiwemo mbuzi, kondoo, Ng'ombe wapelekwe mnadani hapo wananchi wajumuike kwa pamoja kufanya mnada na hatimaye serikali ipate mapato yake tofauti na ilivyo sasa.


Mnada wa mpakani Horohoro ulianza kufanya kazi Septemba 3 mwaka 2023 ambapo mpaka sasa jumla ya minada 49 imekwisha kufanyika ambapo katika kipindi cha miezi 11 jumla ya mifugo 7503 iliingia mnadani ikiwa Ng'ombe 6105 na mbuzi 1398 jumla ya Ng'ombe 4393 na Mbuzi na Kondoo 953 waliuzwa kati ya hao Ng'ombe 1556 Mbuzi na kondoo 263 waliuzwa nje ya nchi na kupata kiasi cha shilingi milioni 44.3 ziliingia kupitia Pos ya mnadani.




Share:

VIFARANGA VYA KUKU VYAPATA MUAROBAINI KATIKA UKUAJI

Mashine inayosaidia katika uleaji wa vifaranga vya kuku iliyobuniwa na Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Na Nora Damian

Wafugaji kuku wa kisasa na kienyeji sasa wataondokana na adha ya kupata hasara kutokana na vifo vya vifaranga baada ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kubuni teknolojia inayosaidia kulea vifaranga.

Teknolojia hiyo ambayo pia inatoa taarifa kwa mfugaji iwapo chakula au maji yameisha imebuniwa na mwanafunzi wa mwaka wa nne katika fani ya Uhandisi wa Mitambo, George Luambano.

Akizungumza Agosti 5,2024 kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Luambano ambaye pia ni mfugaji kuku amesema mashine hiyo inamsaidia mfugaji kulea vifaranga katika kipindi ambacho wanahitaji chanjo na matunzo mengine muhimu ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema.

“Mashine hii ni zao la vitu ninavyojihusisha navyo kwa sababu mimi ni mfugaji, baada ya kuona napata hasara na wafugaji wengine wanapata hasara wakati wa kufuga vifaranga, lilinijia wazo nitatue tatizo. Nimetengeneza mashine kuhakikisha kila mfugaji anaweza kukuza vifaranga na kupunguza vifo ili tupate vifaranga wengi na nyama nzuri.
“Mashine inasaidia kulisha kuku, kuwapa maji kwa muda maalumu, kuwapa joto na unyevunyevu. Inaweza kumsaidia mfugaji kutopoteza muda wa kuangalia kama maji au chakula kipo…chakula au maji yakipungua huwa inatoa taarifa mtu anakuja kuongeza,” amesema Luambano.

Amesema mashine hiyo inatumia taa za joto na hata likipungua zinaendelea kuwaka na ikifika linalohitajika kwa kuku (nyuzi 33) zitazimika huku pia kukiwa na feni inayoingiza hewa ndani.

Amesema kwenye maji kuna kifaa kinachopima kina cha maji na ikitokea kimepungua zaidi itatoa taarifa na mfugaji ataongeza.

“Matatizo ya ufugaji hayaishi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kiuchumi na mabadiliko ya teknolojia kwahiyo, tatizo linapotokea ni bora kulitatua mapema,” amesema.

Mwanafunzi huyo amesema tayari amepata maombi kutoka kwa wafugaji katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwatengenezea mashine hiyo ambayo inatatua tatizo ambalo kila mfugaji linamkuta.

Naye Ofisa Uhusiano Mkuu wa NIT, Tulizo Chusi, amesema wana kitengo cha kuendeleza bunifu ambacho kinalenga kuhakikisha bunifu zinazobuniwa na wanafunzi zinaifikia jamii.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa NIT, Tulizo Chusi, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema chuo kinafanya kazi ya kuendeleza bunifu za vijana hao na kuziingiza sokoni na tayari kuna ambazo zimesajiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kwenda kwa walaji.

“Tuna kitengo cha kuendeleza bunifu zinazobuniwa na wanafunzi na tuna wataalam mbalimbali kuhakikisha kwamba bunifu haziishii chuoni bali zinaifikia jamii,” amesema Chusi.

Ofisa huyo amesema dirisha la udahili bado liko wazi na kuwakaribisha wananchi waweze kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger