Wednesday 24 July 2024

KAMATI YA SIASA CCM SHINYANGA MJINI YAVUTIWA NA MIRADI YA MAJI SHUWASA

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga mjini ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Mhe. Anord Makombe imeridhishwa na miradi mitano (5) iliyotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Julai 24,2024 baada ya kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi hiyo mitano yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe ameipongeza SHUWASA kwa kuimarisha huduma ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wakati na kushughulikia changamoto za wateja huku akiwahimiza kuendeleza ushirikiano huo.

“Mimi niwapongeze SHUWASA mnajitahidi sana lakini lipo eneo ambalo tumeona mmefanya vizuri japo halijafika kwa asilimia mia moja pamoja na ubora wa huduma za SHUWASA, mamlaka ya majisafi SHUWASA tumeona mtandao karibia kila eneo umefika lakini kwenye changamoto za kukatika kwa maji mnajitahidi kutoa taarifa mimi niwaombe tu muendelee kuongeza wateja kwa sababu tunapoongeza wateja na kipato kinaongezeka ili mamlaka iweze kustawi zaidi ya hapo tuendelee kuwa na ushirikiano tufanye kazi wote kama timu”,amesema Makombe.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko naye ameipongeza SHUWASA kwa kuyafikia maeneo yote ya Manispaa ya Shinyanga huku akiwasisitiza kuendelea kuzingatia suala la usafi katika maeneo ya miradi pamoja na kushughulikia kwa haraka changamoto pale zinapojitokeza kwa wananchi.

“Nawapongeza sana kwa sababu maeneo yote ya Manispaa yamefikiwa na maji kwahiyo vimebaki tu vile viunganishi kutoka hapa kwenda pale lakini kazi mnafanya vizuri na mnahitaji pongezi kubwa sana niendelee kuwatia moyo watumishi wa SHUWASA kazi wanazozifanya ni kubwa maana zinaonekana”,amesema Mhe. Masumbuko.

Wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini pamoja na mambo mengine wameridhishwa na miradi hiyo mitano ambayo wameitembelea huku wakiisisitiza mamlaka hiyo kuendeleza ushirikiano uliopo kwao na wateja wao.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya maji ambayo ilikuwa ni kero kwao huku wakiipongeza SHUWASA kwa kuendelea kuwashirikisha katika hatua mbalimbali kwa lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira.

Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya ameitaja miradi ambayo imetembelewa na kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mtandao wa bomba na vituo vya kuchotea maji kijiji cha Bugwandege ambapo amesema mradi huo tayari umekamilika na kwamba wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.

Amesema mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba kijiji cha Bugimbagu umekamilika kwa asilimia mia moja ambapo tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama, ujenzi wa mtandao wa bomba na kituo cha kuchotea maji kijiji cha Magwata mradi umekamilika pamoja na upanuzi wa mdandao wa bomba Ngelegani, Ndala na Butengwa tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.

Pia amesema mradi wa ujenzi wa mdandao wa bomba na kituo cha kuchotea maji kijiji cha Mwanubi umekamilika na wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama huku akiendelea kuwakumbusha wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kuduma. Viongozi na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakipata maelezo ya miradi kabla ya kuanza ukaguzi.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akifungua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemba ya Valve ya mtandao wa maji.
Mtahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akitoa ushauri.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akiandika ushauri unaotolewa na mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya na Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa wakiandika ushauri unaotolewa na mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemba ya Valve ya mtandao wa maji.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akielezea mradi huo katika kijiji cha Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwa amefungua maji.
Wananchi wakiendelea kuchota maji safi na salama katika kijiji cha Mwanubi.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Magwata Nhelegani Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe akiwasili katika Gati la maji kijiji cha Magwata manispaa ya Shinyanga.
Ukaguzi wa mradi ikiendelea.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akipata ufafanuzi katika Gati la maji Magwata Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akitoa maelezo ya mradi katika Gati la maji Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Nsianeli Gerald akiwa katika Gati la maji Bugimbagu kata ya Mwawaza.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bugimbagu wakisubiri maji.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea na ukaguzi wa miradi.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akizungumza.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza.
Kikao cha majumuisho kikiendelea baada ya kutembelea na kukagua miradi mitano.

Share:

WATUMISHI WANNE SHINYANGA DC WAKAMATWA TUHUMA ZA KUIIBIA MAPATO SERIKALI


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu 7 kwa tuhuma mbalimbali na uhalifu,wakiwamo watatu ambao wamekamatwa na vipande 20 vya madini ya dhahabu,pamoja na watumishi wanne wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma za kuiibia mapato serikali,kwa kutumia POS mashine ambayo haiingizi mapato serikalini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo julai 24,2024 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kufuatia misako,doria na operesheni ambayo wameifanya kwa kipindi cha kuanzia juni 26 hadi julai 26 mwaka huu.
Amesema kwa kipindi hicho wamewakamata watu watatu wakiwa na vifaa vya kutendea uhalifu,ambavyo ni gari moja Toyota Crown, vipande 20 vya dhahabu, brashi 26 za kusungulia madini hayo na mezani 3.

Amesema pia wanawashikilia watumishi 4 wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kutokana na kutumia POS Mashine ya ukusanyaji mapato,ambayo haiingizi mapato Serikalini na kuiibia Serikali.
“Polisi tunaendelea na upelelezi juu ya watuhumiwa hawa wote, ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria,”amesema Magomi.

Aidha,amesema katika msako huo pia wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi pamoja na madawa ya kulevya,zikiwamo pikipiki 14,bomba tatu za chuma, spana 22, redio tatu,simu tano, laptop moja, kinu kimoja cha mashine ya kusaga unga, Tv moja, Solar, betri, kaboni,na deki moja.

Vitu vingine walivyokamata ni mafuta ya dizeli lita 20, bati 10, Shock up nne za pikipiki, pombe ya moshi lita 176 na bangi kilogramu 65.

Amesema kwa makosa ya usalama barabarani, madereva wawili wamefungiwa leseni zao kwa kipindi cha miezi mitatu, kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendokasi zaidi ya kilomita 100 kwa saa, huku wakikamata makosa ya barabarani 3,943 magari makosa 2,752 pikipiki na bajaji makosa 1,191 ambapo wahusika walilipa faini.
Katika hatua nyingine ametaja jumla ya kesi 15 zimepata mafanikio, ambapo watuhumiwa mbalimbali wamefungwa jela, huku akibainisha kuwa jeshi hilo limetoa elimu na kufanya jumla ya mikutano 71 ya uelimishaji wananchi katika maeneo ya shule, nyumba za ibada na vyombo vya habari ili kusaidia kupunguza makosa ya uhalifu na ukatili.

Amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha usalama wa Mkoa unaendelea kuwa shwari, huku akitoa wito kwa madereva pamoja na wananchi kuendelea kutii sheria za nchi.
Share:

CHUO CHA VIWANDA VYA MISITU FITI CHAANZISHA KOZI YA BIASHARA YA HEWA KABONI

Na John  Bera - Kilimanjaro

CHUO cha Viwanda vya Misitu kimeanzisha kozi fupi ya biashara ya hewa kaboni  ambayo imelenga kuifanya nchi kunufaika na zao hilo jipya la misitu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (FITI), Dkt. Zakaria  Lupala amesema asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania ni hifadhi za misitu hivyo kuwa na fursa kubwa ya biashara ya hewa kaboni kwenye soko la kimataifa, lakini jamii haina ujuzi wa kunufaika na fursa ya biashara hiyo yenye mtazamo wa kuhifadhi mazingira.

Amesema pamoja na nchi kuwa na utajiri wa misitu, bado fursa ya biashara ya hewa ukaa haijatumika ipasavyo hatua ambayo imefanya Chuo hicho kuanzisha kozi fupi katika sekta hiyo.

“Chuo kimeamua kuongeza kozi ya zao lingine la mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu ambayo ni biashara ya hewa kaboni  kwani pamoja na utajiri wa misitu lakini watanzania hawana ujuzi"

“Hapa nchini tuna kiwango kikubwa cha hewa kaboni, na tuchopungukiwa ni ujuzi kuhusu biashara hiyo na ndio maana tukaanzisha kozi fupi ya biashara ya hewa kaboni. Tunataka kampuni ambazo zitakuwa na ujuzi wa kutengeneza wadadisi kwenye biashara ya hewa kaboni”,amesema.

Amesema chuo hicho kinawataalamu bobezi katika fani hiyo ambao watasaidia watanzania kutengeneza kampuni za uwakala (carbon blocker), uandishi wa mawazo ya biashara ya hewa kaboni, upimaji na namna ya kufanya majadiliano ya biashara katika soko la kimataifa.

“Ndani ya wanyamapori kwenye hifadhi zetu, pia tunaweza kufanya biashara huku tukiwa tunatunza hifadhi zetu, nje ya wanyamapori tutapata motisha ya hifadhi”.

Naye Afisa Misitu Mkuu kutoka Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Emmanuel Msoffe ametoa rai kwa watanzania kutumia fursa ya Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi kuwapeleka vijana wao kupata mafunzo ili waweze kupata ajira na kipato katika kuendeleza maisha yao ya kila siku.

“Tumefika chuoni hapa na tumeona fursa mbalimbali ambazo kama zikitumiwa vizuri zinaweza kusaidia kuleta ajira, kazi na kipato na fedha za kigeni. Tumeona vijana na ubunifu wao na teknolojia mbalimbali ambazo wanazitumia katika kuhakikisha kwamba wanajipatia ajira na kipato”,amesema.

Msoffe amesema Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 na Mkakati wa Utekelezaji wa 2021 hadi 2031 unaelekeza uhifadhi misitu endelevu ili ufaidishe vizazi vijavyo.

Amesema kutekeleza hilo, Wizara kupitia idara imekuwa ikitoa elimu kwa umma ili umma uweze kuelewa faida na fursa zilizopo katika uhifadhi na misitu na nyuki.
   

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger