Friday, 10 May 2024
Thursday, 9 May 2024
DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA OXFORD POLICY MANAGEMENT
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Wataalam kutoka Oxford Policy Management Ofisini kwake tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma. |
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy Management kuhusu Uwezekano wa matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence and Machine Learning) katika kufanya mapitio ya matumizi ya umma (Public Expenditure Review).
Kikao hicho kimefanyika tarehe 09 Mei 2024 ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi amesema pia lengo la kikao hicho ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD) nchini Tanzania.
Ikumbukwe Serikali ya Tanzania ilizindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali yam Mtoto (PJT-MMMAM) mwaka 2021 kama mpango mkuu wa kuzileta pamoja Wizara na wadau mbalimbali ili kuboresha Makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 8.
WANAFUNZI VYUO VIKUU WAFURAHIA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU
Rai hiyo imetolewa na mwanafunzi kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhimbili), Yuda Sale ambaye pia amepongeza uongezwaji wa wafanyakazi katika vyuo akisema unachangia kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake Alice Robert, mwanafunzi kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) amepongeza utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 akisema wana matarajio makubwa kuwa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 mageuzi makubwa katika sekta ya elimu yataenda kufanyika na kwamba wanafunzi watasoma katika mazingira bora zaidi.