Tuesday, 7 May 2024

SERIKALI YAIPA TANROADS BIL 6.5 KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL-NINO MKOANI RUKWA


Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepeleka kiasi cha shilingi bilioni 6.5 kwa ajili ya matengenezo ya dharura ya kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharika kutokana na mvua kubwa za El-nino zilizonyesha kwa wingi Mkoani Rukwa.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kukubali kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho kimewezesha kurejesha miundombinu iliyoharibiwa.

Mhandisi Mwanga amesema hayo tarehe 6 Mei 2024 baada ya kutembelea na kukagua miundombinu iliyoharibika ikiwa ni pamoja na Daraja la Solola lililopo barabara ya Ilemba – Kaoze ambapo barabara unganishi ilisombwa na maji na hivyo kufanya upana na kina cha mto kuongezeka.

Pia amempongeza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta na Viongozi wengine wa Wizara, TANROADS na Serikali kwa maelekezo, usimamizi wa karibu na msukumo wa pamoja kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa haraka.

Amesema kwa ujumla maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hizo zilizonyesha Mkoani humo kuanzia mwezi Disemba 2023 hadi Aprili 2024 ni Barabara ya kutoka Kasansa – Muze hadi Kiliamatundu ambako jumla ya madaraja takribani 18 yalipata athari kati ya hayo madaraja 6 ndio yaliyoharibika zaidi.

“Tangu tumepata athari ya mvua hizi tumekuwa tukifanya matengenezo endelevu ya kuhakikisha kwamba kila kunapotokea athari barabara inafunguka na magari yanapita, tumeendelea kufanya hivyo na mpaka sasa Serikali imeshatuletea shilingi bilioni 6.5 kwa ajili ya kufanya marekebisho na kufungua njia pale ambapo inapojifunga’’ amekaririwa Mhandisi Mgeni na kuongeza kuwa

“Kuanzia wiki ya tatu ya mwezi Aprili - 2024, Mvua imepungua kwa hiyo tumeanza kufanya maboresho ya muda wa kati, tunarudishia madaraja ambayo yamebomoka na mpaka sasa hivi zile barabara unganishi ambazo madaraja hayakusombwa na maji tumeshazirudishia na barabara zinapitika vizuri’’

Mhandisi Mgeni ametoa wito kwa watumiaji wa barabara hasa wakati huu wa mvua kuwa na subra na kuongeza umakini pale ambapo wanaona maji yamepita juu ya barabara au daraja ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Naye Msimamizi wa Kitendo cha Matengenezo TANROADS Mkoa wa Rukwa Mhandisi Galasiano Tovagonze amesema kutokana na athari hizo wamefanikiwa kufanya manunuzi ya Wakandarasi 7 ambao wanafanya kazi ya matengenezo ya muda wa kati.

Ameongeza kuwa Wakandarasi wawili wapo katika barabara ya kutoka Kasansa – Muze, Mkandarasi mmoja yupo kipande cha Muze – Mtowisa na Wakandarasi wanne wapo kipande cha Mtowisa -Ilemba, wote wanafanya kazi ya kurejesha miundombinu iliyoharibika.

Share:

Monday, 6 May 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 7, 2024

Share:

Video Mpya : RAMANI YA DUNIA - MAVUNO

 

Share:

Video Mpya : BHUDAGALA - MOTO

Hii hapa kazi mpya ya Bhudagala Mwanamalonja inaitwa MOTO!
Share:

ATCL YAINGIA MAKUBALIANO KUPELEKA MARUBANI KUFUNDISHA NA KUSIMAMIA NDEGE MPYA NCHINI NIGERIA



Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imeingia makubaliano ya kupeleka marubani wake kufundisha na kusimamia ndege mpya za Airbus A220 za Kampuni ya Ndege ya Ibom iliyopo nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mha. Ladislaus Matindi, amethibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo ambapo amesema ATCL imetoa marubani wake waandamizi wawili ambao watakuwa na jukumu la kuwafundisha kwa vitendo marubani na walimu wa marubani wa Ibom Air kwa muda wa miezi sita.

"Marubani wa ATCL watakuwa na jukumu la kufundisha na kusimamia mafunzo kwa vitendo hadi watakapojiridhisha kuwa marubani wanafunzi na walimu wao wamefikia viwango vinavyotakiwa kurusha ndege hizo", alisema Mha. Matindi.

Aidha, Kampuni ya Ibom Air itailipa ATCL gharama za mafunzo hayo kwa mujibu wa mkataba kwa kipindi chote cha makubaliano.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya ATCL kuonesha uzoefu wa muda mrefu wa kumiliki ndege za Airbus A220-300 na pia kuridhishwa na kiwango cha umahiri wa marubani wa Air Tanzania.

Mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo kwa marubani wa Ibom Air watakaorusha ndege za Airbus A220, ambazo ATCL ina uzoefu wa miaka mingi wa kumiliki ukilinganisha na Ibom Air ambao ndio wanaanza kutumia ndege za aina hiyo.

ATCL ina zaidi ya marubani 100 na inamiliki ndege aina ya Boeing B787-8, B737 MAX 9, B767-300F, Airbus A220-300 pamoja na Dehaviland Q400 na Q300.
Marubani waandamizi wa Kampuni ya Ndege Tanzania Kept. Sajjad Moloo na Kept. Arif Jinnah (kulia na kushoto) wakiwa ndani ya ndege kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na marubani wa ndege ya Ibom, nchini Nigeria
Marubani waandamizi wa Kampuni ya Ndege Tanzania Kept. Sajjad Moloo na
Kept. Arif Jinnah (kulia na kushoto) wakiwa ndani ya ndege kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na marubani wa ndege ya Ibom, nchini Nigeria
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 6, 2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger