Sunday, 21 January 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 22,2024



 
Share:

DKT. NCHIMBI: KUKIMBILIA MAANDAMANO NI UOGA WA HOJA, KUKWEPA MAZUNGUMZO


-Asema CCM itaongeza kasi kusimamia Serikali kwa weledi, bila kiburi, wala kuwatukana watendaji

-Asisitiza Watanzania wanatambua CCM ndiyo Chama kiongozi, hakuna haja ya kutukana kusimamia Ilani ya Uchaguzi

-Awataka wanasiasa kutambua watapimwa kwa hoja, sio maandamano

Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewataka viongozi wa CCM kuongozea kasi ya kutimiza wajibu wa Kikatiba na kikanuni wa kuisimamia Serikali na watendaji wake wanapotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kwa weledi na heshima, bila kiburi wala kuwatukana.

Ndugu Nchimbi amesema kuwa katika kuisimamia Serikali inapotekeleza wajibu wake kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, wanaCCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuelezea mafanikio na kazi kubwa inayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Ndugu Nchimbi pia amesisitiza jinsi ambavyo milango ya CCM, ikiwa ni pamoja na kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama, iko wazi kwa ajili ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa na kuzungumza masuala mbalimbali kwa ajili ya maslahi ya taifa, huku akisema kuwa wanasiasa wanaohamasisha maandamano badala ya kujenga hoja katika majadiliano, ni waoga na wanakwepa mijadala.

Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi ameyasema Jumamosi, Januari 20, 2024 wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar Es Salaam, wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa CCM waliojitokeza kwa wingi Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar Es Salaam, kumlaki wakati wa mapokezi ya kumpongeza kwa kuteuliwa kushika dhamana hiyo ya Mtendaji Mkuu wa CCM.

“Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza ahadi zake na kuisimamia serikali. Ninawaahidi, kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama, tutaendelea kukiimarisha chama lakini pia kuhakikisha hatumuangushi Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Chama kwa imani yake aliyotupatia. Chama chetu kitaendelea kupata ushindi kwa sababu tumefanya kazi kubwa na zinazoeleweka.

“Tuendelee kufanya kazi usiku na mchana, kazi ya kutafuta ushindi wa chama chetu. Tufanye kazi kwa juhudi na umakini zaidi katika maeneo yaliyobakia. Wakati huo huo Chama chetu kisikwepe wajibu wa Kikatiba na Kikanuni kuisimamia Serikali, kwa weledi bila kutukana. Tuongoze kwa weledi, ili watendaji wa Serikali wafanye kazi vizuri na wajue kuwa tunawapenda na kuwaheshimu. Isipokuwa tu wote tuongeze kasi ya kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi,” amesema Ndugu Nchimbi.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa Watanzania kudumisha utaifa wao na kuenzi tunu za amani na utulivu kuwa ndiyo msingi wa maendeleo na alama kubwa ya Tanzania duniani, Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi amsema kuwa milango ya CCM na hususan kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, iko wazi wakati wowote utakapohitajika ushirikiano baina ya vyama vya siasa, kwa maslahi ya taifa.

“Tunavyo vyama vya siasa nchini, tuendelee kushirikiana navyo. Milango ya ofisi yangu iko wazi. Wote tuna nia moja. Tutaendelea kushirikiana nao. Lakini kushirikiana nao haimaanishi kupunguza kasi ya kutafuta ushindi, kuongeza wabunge bungeni na madiwani, Serikali za Mitaa na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa Rais mwakani.

“Vyama vya siasa, wanasiasa na wadau wote wa maendeleo dhamira ya mazungumzo ni muhimu ikaakisi kote. Kukimbia na kukwepa mazungumzo sio ujasiri. Huo ni uoga. Hoja hujengwa kwa mdomo sio kwa miguu. Tunataka tuwapime kwa hoja zao, sio kwa miguu yao kuandamana. Vyama vya siasa vijitofautishe na mashindano ya urembo ambako hupimwa kwa jinsi wanavyotembea. Tutumie ubongo kufikiria, sio miguu,” amesema Ndugu Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi pia alitumia hadhara hiyo pia kuwapatia pole wakazi wa Dar Es Salaam kutokana na athari za mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia siku ya mapokezi hayo, akimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Albert Chalamila kuhakikisha serikali mkoani humo inachukua juhudi za makusudi kuwasaidia wananchi kutokana na athari kubwa zilizosababishwa na mvua hiyo.

Amesisitiza kuwa katika utendaji kazi wake, daima amekuwa mtu anayependa vitendo zaidi, kuliko maneno, kwa sababu tija inayokusudiwa na kutumainiwa na wananchi, kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote, itapatikana kupitia vitendo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Abbas Mtevu amesema chama kinatarajia kushinda kwa kishindo mitaa yote 574 ya mkoa wa huo.

Halikadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Albert Chalamila amesema wanatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025, hivyo viongozi wanapoanza kampeni hawatapata tabu kujieleza kwa wananchi, kwa sababu kazi zinajieleza zenyewe, huku pia akiahidi kuwa hata miundombinu iliyoathirika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku, itafanyiwa kazi ndani ya saa 24 kurejesha hali vizuri.
Share:

MAKONDA AWATUMIA SALAMU WATUMISHI WAZEMBE TANGA

 













Na Oscar Assenga, TANGA

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Paul Makonda amewatumia salamu watumishi wa Serikali wazembe mkoani Tanga wasiowajibika kwamba hawatakubali kuwavumilia kwa sababu wao ndio wamekuwa chanzo cha kumchonganisha Rais na wananchi wake.

Alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa Hadhara kwenye viwanja vya Lamore Jijini Tanga mara akitokea wilayani Pangani akiwa kwenye ziara yake ya kichama mkoani hapa.

Alisema kwamba chama hicho hakiwezi kukubali kuwafumbia macho watumishi ambao wamekuwa wakishindwa kuwajibika huku wananchi wakiendelea kuteseka wakati wanapokwenda kupata huduma katika maeneo yao.

Makonda alisema moja kati ya maelekezo kumi aliopewa na Rais Samia baada ya kupendekezwa na hatimae kuteuliwa ni kuwa sauti ya wananchi wa hali ya chini na wasio na pesa vyeo wala elimu .

Alisema Serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo na wajibu wa chama ni kuhoji miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na iendane na thamani ya fedha zilizotengwa.

"Nina maelekezo kumi toka kwa Rais Samia,moja ni kuhakikisha je miradi inajengwa kwa wakati?kazi yangu na wenzangu kushughulika na wanaofanya ubadhilifu wa fedha hizo"Alisema Makonda.

Aidha alisema katika ziara yake ya siku mbili lengo la kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais 2025 ili kukidhi matakwa ya katiba ya Chama hicho ya kushinda chaguzi zote,kuunda dola na kuunda Serikali.

Alisema mbali na hilo pia katika ziara hiyo ameitumia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu yalikosekana kwa muda mrefu ambapo alitoa maelekezo mbalimbali kwa watumishi wa umma katika idara zilizolalamikiwa namna ya kumaliza kero za wananchi hao.

Makonda amekuwa na utaratibu wa kuwasimamisha watumishi wa Serikali toka idara zote mbele ya Mikutano yake ya hadhara moja wajibu maswali ya wananchi lakini pia wananchi wajionea wenyewe wanao wasababishia waichukie Serikali yao kwa kushindwa kuwahudumia.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutoa fedha nyingi mkoani Tanga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Rajabu alitumia fursa hiyo kumuomba Makonda miradi yote inayotekelezwa mkoani humo iwanufaishe wazawa ili kuondoa malalamiko ya wananchi kutokupata hizo za ajira na kushindwa kunufaika na miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati akitoa salamu za mkoa alisema mkoa uko salama na Serikali ina mahusiano mazuri na Chama na Wazee jambo ambalo limeufanya Mkoa huu kiendelea kuwa shwari na kutokuwa na matukio ya Uvunjifu wa amani.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 21, 2024

      
Share:

WANANCHI FUATILIENI TARATIBU NA MAELEKEZO YA SERIKALI KUKABILIANA NA MADHARA YATOKANAYO NA MVUA-DKT. YONAZI


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza na waandishi wa Habari amabao hawapo katika picha, katika eneo maarufu kwa jina la Daraja la Masai, lililopo katika barabara ya uhuru Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea.

Aliyesimama Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Baladya Eliakama, akizungumza kuhusiana na madhara ya mvua zinaoendelea kunyesha katika mkoa wa Mwanza kabla ya kuanza kwa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na Mvua hizo.

Kati picha (katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge n Uratibu Dkt. Jim Yonazi na wataalam kutoka Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, TARURA, TANROADS na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendela kunyesha, Mkoani Mwanza

Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakiwa katika kikao kabla kuanza kwa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge n Uratibu Dkt. Jim Yonazi ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendela kunyesha mkoani Mwanza.

Katika ni sehemu ya kingo za miundombinu ya Daraja unapopita mto Nyamilongo Wilayani Nyamagana lilivyoharibiwa na mvua zinazoendela kunyesha Mkoani Mwanza.




NA. MWANDISHI WETU – MWANZA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka wananchi kuzingatia na kufuata taratibu zinazotolewa na Serikali ili kuweza kukabiliana na madhara yatokananyo na mvua hasa za El nino kuweza kuokoa maisha na mali zao.

Ameyasema hayo Januari 20, 2024, Jijini Mwanza alipokuwa katika ziara ya kukagua hali ya Mafuriko katika Jiji la Mwanza ambapo mvua la El nino zinazoendelea zimeleta athari mbalimbali na kuharibu miundombinu pamoja na mali za watu.

Dkt. Yonazi amesema ni muhimu sana wananchi kuwa wazalendo na kufuata maelekezo ya serikali kwa sababu suala zima la uokoaji ni gharama.

“Suala hili ni gharama kwa Serikali lakini pia inaweza kugharimu maisha hivyo ni muhimu sana pale ambapo tumeelekezwa na Serikali kufuata taratibu tuweze kufuata taratibu.” Alisisitiza.

Katibu Mkuu Dkt. Yonazi amebainisha kuwa kwa wananchi ambao wameelekezwa kuhama katika maeneo hatarishi waweze kuhama ili waweze kulinda maisha yao, mali zao na maisha ya jamii kwa ujumla na ametoa wito kwa wananchi kote nchini kufuata taratibu, miongozo na maelekezo halali ya Serikali na ndiyo namna ya kujilinda dhidi ya mafuriko na majanga.

Amewataka pia wananchi kushiriki katika miradi mikubwa akitolea mfano mradi wa ujenzi wa kingo za mto Nyamilongo unaopita katika wilaya ya Nyamagana ili maji yake yasiende katika makazi ya watu na kuharibu mali nyingine na kufahamu kwamba ushiriki wao utaleta faida katika maana ya kutunza mali zao, mali za asili na kuhakikisha kwamba maisha yanaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine,Dkt. Yonazi amewaasa watumishi wa umma kufuata utaratibu hasa katika kusimamia suala zima la ujenzi holela, kwani unapofanyika ujenzi holela ni rahisi sana kupata madhara.

“Ili kuweza kuwa na makazi bora kwa wananchi wetu ni vizuri kuhakikisha maisha hayahatarishwi na mafuriko na hata yanapotokea mafuriko inakuwa rahisi kuokoa.” Amesema Dkt. Yonazi

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema, mvua hizi za El nino kwa baadhi ya maeneo katika mkoa wa Mwanza zimeleta uharibifu wa baadhi ya miundombinu kama vile madaraja na Barabara.

Aidha amepongeza Wakala wa Barabara vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Mwanza kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba miundombinu hiyo inarejea katika hali yake ya kawaida.

Sambamba na hilo aliongelea suala la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo, ambapo alisema ulianzia katika Wilaya ya Magu na kufika katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana ambapo Serikali ya mkoa kwa kiasi kikubwa imechukua hatua, tahadhari pamoja na Kudhibiti.
Share:

Friday, 19 January 2024

KOCHA TAIFA STARS AKUTANA NA RUNGU CAF, KUZIKOSA MECHI AFCON

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche Amefungiwa Mechi nane na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kufuatia kauli zake alizozitoa kuwa Morocco ina ushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Kufuatia adhabu hiyo, Kamati ya Utendaji ya TFF pia imemsimamisha kocha huyo na kumteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha akisaidiana na Juma Mgunda.

Kocha Amrouche amefungiwa ikiwa ni siku moja imesalia Stars kushuka dimbani dhidi ya Zambia kesho Januari 20,2024.

Share:

TANZANIA, INDIA MEZA MOJA USHIRIKIANO SEKTA YA USAFIRI WA ANGA

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (katikati kushoto) amefanya kikao maalum na Waziri wa Usafiri wa Anga wa India Mheshimiwa Jyotiraditya M. Scindia (wapili kulia)kuhusu maeneo ya Ushirikiano baina ya Tanzania na India.
Share:

Ngoma Mpya : BHUDAGALA - BHANA BHANE

 

Share:

KWELI NIMEAMINI UKIZAA NA MWANAMKE HUWEZI KUACHANA NAYE

Jina langu ni Banda kutokea Mbeya nchini Tanzania, nilikuwa na mwanamke hadi tukazaa nae watoto wawili hapo katikati kukawa na mambo mengi yaliyotufanya hadi tukatengana.

Ila cha kusikitisha mimi niliamua kuoa kabisa mwanamke mwingine, watu wapenda chuki walimwendea na kumwambia wampe hadi nauli aje na watoto akaniharibie ili nisifunge ndoa.

Kilichotokea yule mwanamke akawaambia acha aoe tu mimi bado ni mke wake pia, hivyo akawa amewakata mdomo, akaendelea na maisha yake na mimi nikawa nimeendelea na yangu.

Baada ya kuoa nikawachukua watoto nikawa naishi nao tukaendelea tu kuwasiliana kwa sababu ya watoto, si unajua tena mkiwa wazazi, kuna muda ataka kuongea na watoto au watoto watataka kuongea na mama yao.

Kuna wakati akawa anataka tukutane kimwili mimi nikakataa ila mwisho wa siku tukakutana tena, baada ya tukio lile tumekuwa tunatamaniana sana hadi napoteza hamu ya kufanya na mke wangu.

Nashindwa kujua sababu gani inakuwa hivyo, ila kuna siku nilishika simu yake nikakuta anachati na rafiki yake WhatsApp na kumueleza kuwa amefanikiwa kulirejesha penzi letu kwa msaada wa Kiwanga Doctors.

Ilibidi niinge mtandaoni (google) na kumtafuta huyo Kiwanga Doctors, nilifanikiwa.

Huyu Kiwanga Doctors anamrejesha mpenzi ambaye umeachana naye hata kama ni kwa muda, sikuwa na shida na hilo kwa sababu sasa tunapendana sana kuliko ilivyokuwa hapo awali na huyu ni mzazi mwenzangu.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger