Wednesday, 17 January 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 18,2024


Share:

SOMALI COMMUNICATION WORKERS UNION 'SOCOWU' CONDEMNS UNJUST ACTIONS AGAINST ITS MEMBERS


 Somali Communication Workers Union (SOCOWU) Condemns Harassment of Members by National Intelligence and Security Agency.

In a press release issued yesterday, the Somali Communication Workers Union (SOCOWU) expressed strong condemnation for the unjust actions faced by its dedicated members within Hormuud Telecom Somalia. The union alleges that the National Intelligence and Security Agency, tasked with safeguarding citizens, has been implicated in harassing SOCOWU members, causing unwarranted suffering.


SOCOWU urgently appeals to government officials, urging them to release the unlawfully detained workers promptly. The union emphasizes the need for justice, worker's rights, and creating an environment free from persecution for citizens contributing to the nation's progress.


The union further implores the President of the Republic of Somalia and the Prime Minister to intervene decisively against those responsible for the harassment. SOCOWU stresses the importance of holding those accountable responsible for their actions and ensuring justice prevails.


In closing, SOCOWU reaffirms its commitment to advocating for the rights and well-being of communication workers in Somalia, expressing hope that their plea for justice will be heard, and swift action taken to rectify this unfortunate situation.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 17,2024

 
Share:

Tuesday, 16 January 2024

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR

Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bw. Felix Makarius akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TBS katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar kwaajili ya kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

********************

USHIRIKIANO mzuri baina ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa kero za bidhaa ambazo hazina viwango kutoka Zanzibar kwenda Bara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Zanzibari kwa ajili ya kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Alisema shirika hilo limeshiriki maonesho hayo kwa ajili ya kuelimisha na kueleza umma mafanikio ambayo TBS limepata miaka 60 iliyopita, ambapo moja ya mafanikio makubwa ni ushirikiano baina yake na ZBS.

"Ilikuwa ni muhimu kuwa na ushirikiano huu kwa sababu biashara kati ya Visiwani (Zanzibar) na Bara ni kubwa sana na zinahusiana na bidhaa mbalimbali ambazo zinadhibitiwa viwango na TBS na ZBS, kwa hiyo mnaweza kuona umuhimu wa kuwa na ushirikiano huo," alisema Dkt. Ngenya.

Alisema ushirikiano huo umewezesha kupunguza bidhaa ambazo hazina ubora kwa kiasi kikubwa baina ya pande hizo mbili za Muungano.

Dkt. Ngenya alisisitiza kwamba bidhaa baina ya pande hizo mbili zimeongezeka ubora kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa upande wake mtaalam wa lishe na Kiongozi wa Jumuiya ya Wenye Viwanda Vidogo Tanzania (WAJATA) , Issa Njoka, alipongeza TBS kwa kuhudumia Watanzania na kuimarisha viwanda kea kuhakikisha vinazalishwa bidhaa bora ambazo zinalinda afya za watumiaji.

Njoka ambaye alitembelea banda la TBS kwenye maonesho hayo, alisema yeye kama mzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo kwa kufika kwenye banda la TBS alipata huduma na maelekezo ya kina kutoka kwa maofisa wa shirika hilo waliokuwa wanatoa elimu kwa wananchi.

"Lakini nimeweza kuelewa kuwa kila Mtazania na wazalishaji kwa ujumla wanatakiwa wafike TBS ili waelimishwe ni namna gani wanaweza kupata bidhaa bora ili pale unapokuwa unakula kitu lazima kiwe kimethibitishwa na TBS," alisema Njoka na kuongeza;

"Ni lazima Watanzani tuwe wazalendo tunapotaka kununua bidhaa, ni lazima kuangalia kama ina alama ya ubora ya TBS ili kuepuka kula bidhaa zenye madhara kiafya ambazo zinaweza kusababisha ukapoteza maisha."

Alisema kwenye vyakula zinapatikana sumukuvu na sumu mbalimbali, hivyo kila Mtanzania ajione ni sehemu ya TBS. "Natoa wito kwa kila Mtanzania kuitumia TBS ili kuweza kuboresha bidhaa zetu kupitia shirika hili,"alisema Njoka.

Njoka aliwataka wazalishaji kuhakikisha wanatengeneza bidhaa bora ili waheshimike, kwani wakiitumia TBS wanaenda kunyanyua taifa kuwa Taifa la viwanda na bidhaa bora.
Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bw. Felix Makarius akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TBS katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar kwaajili ya kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kaaya (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu katika Mkutano wa Wakuu wa Taasisi wakati wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar.
Share:

Video Mpya : INAGA MLYAMBELELE - NSO NI NSO

 

Share:

NAIBU WAZIRI DAVID KIHENZILE ATEMBELEA BANDA LA TCAA MAONESHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI


Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akizungumza na watumishi wa TCAA alipofika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mtumwa Khatib Ameir
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mtumwa Khatib Ameir katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid kuhusu Chuo hicho cha Usafiri wa Anga katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mtumwa Khatib Ameir katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mtumwa Khatib Ameir pamoja na watumishi wa TCAA katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger