Friday, 5 January 2024

TBS YAINGIA MAKUBALIANO NA JESHI LA POLISI KUKAGUA MAGARI YANAYOTUMIKA NCHINI

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji wakisaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Jeshi la Polisi ili kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kutekeleza azma ya kuendelea kulinda Maisha ya watanzania kwa kuhakikisha kuwa ukaguzi wa magari wakati yanapotumika hapa nchini unaofanyika kwa mujibu wa Sheria ya Trafiki (yaani Road Traffic Act, Cap 168), unafanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa ili kuthibitisha usalama wake.

"Kwa kuzingatia uwezo uliopo,TBS itatumia wataalam wake, viwango pamoja na mitambo ya kisasa katika kukagua na kupima magari yote yatakayoletwa na Jeshi la Polisi, Kitengo cha  Trafiki kwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Usalama Barabarani Sura 168 ambayo inalazimu kufanyika ukaguzi wa vyombo vya moto ili kuhakikisha vinakidhi matakwa ya vigezo vya usalama kwa lengo la kulinda usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara". Amesema 

Aidha amelihakikishia jeshi la polisi  kwamba TBS ni mshirika sahihi wa Jeshi la Polisi Tanzania, kwani ndiyo inayodhibiti ubora na usalama wa vyombo vya moto vinavyoingia nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji amesema kupitia makubaliano hayo wanatarajia usalama barabarani kuimarika zaidi kwa watumiaji wa barabara.

"Tukiwa na Vyombo vya Moto salama tutakuwa na watumiaji salama wa barabara, tutakuwa na barabara salama na pia shughuli za uokozi zinaweza kuimarishwa na mwisho tutakuwa na tumeimarisha uongozi katika usalama barabarani". Amesema 

Amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Maelekezo ya Tume ya Haki Jinai inayosisitiza kushirikiana na wadau mbalimbali katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kuzuia uhalifu barabarani.

Pamoja na hayo amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanatimiza wajibu wa kisheria wa kukagua vyombo vyao kama inavyoelekezwa katika sheria kwani jeshi la polisi litakuwa na muhari kwa watakaoshindwa kutii sheria bila shuruti.

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji wakionesha mikataba mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Makamishna wa Polisi wakifuatilia hafla ya utiaji saini Makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na Shirika la Viwango Tanzania katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wakurugenzi na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakifuatilia hafla ya utiaji saini Makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na TBS katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na Wakurugenzi na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Makamishna wa Polisi katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share:

PROF. NDALICHAKO ASISITIZA CMA KUJA NA MFUMO KIDIGITALI WA KURAHISISHA USULUHISHI NA UAMUZI




Na; Mwandishi Wetu - Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kuja na mfumo wa kidigitali ambao utarahisisha usuluhishi na utatuzi wa migogoro.

Prof. Ndalichako amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tathimini ya utendaji kazi wa tume hiyo na mafunzo kilichofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024 mkoani Morogoro.

Ameeleza kuwa, mfumo huo utasaidia kufanya utatuzi wenye haki na kwa wakati na pia kupunguza mrundikano wa kesi.

Kwa upande mwengine amewataka watumishi wa ofisi hiyo kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii na waledi ili kuimarisha uchumi wa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.

Pia, amewasisitiza kila mtumishi katika ofisi hiyo kushiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa yanalenga kuleta maendeleo na mahusiano mazuri katika utendaji kazi wao.

Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose Mlyambina amesema Tume inatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na mahakama ili kuweza kupunguza mlundikano wa mashauri, kwani Uchumi utakua kwa kasi na uwekezaji utaongezeka ukichochewa na huduma bora za utoaji haki hususani haki kazi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekerege Mpulla amesema kuwa CMA itahakikisha ina anzisha mfumo wa kidijitali ambao utawawezesha watumishi kufuatilia taarifa na kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.

Share:

Thursday, 4 January 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 05, 2024


Share:

SHUWASA YAANIKA MAFANIKIO KABAMBE MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA... YATANGAZA MIRADI MIPYA MIKUBWA KULETA MABADILIKO ZAIDI SHINYANGA

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 4,2024. Kushoto ni Afisa Mahusiano kwa Umma SHUWASA bi. Nsianel Gelard
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na SHUWASA kwa ajili ya taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA


Na Eunice Kanumba na Kadama Malunde - Shinyanga

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeeleza mafanikio makubwa iliyoyafikia ndani ya kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2022/2023 (Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan) ambayo ni pamoja na kupanua mtandao wa maji safi, kuongeza mapato yatokanayo na mauzo ya maji, kuongeza idadi ya wateja, kupunguza upotevu wa maji na ujenzi na utekelezaji wa miradi kabambe ya maji.


Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 4,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2022/2023 jumla ya shilingi 8,595,802,786 zilitumika katika ujenzi wa miradi na wanufaika wapatao 116,249 wanafaidika na miradi hii ambapo jumla ya miradi 10 imetekelezwa, miradi 7 imekamilika na miradi mitatu inaendelea kutekelezwa na inatarajiwa kukamilika ifikapo Mwezi Februari 2024.

Aidha amesema hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa sasa ni nzuri katika maeneo yote wanayoyahudumia kutokana na kwamba hivi sasa wanapata maji ya uhakika kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA).
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA.

Amesema SHUWASA ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga , kuanzia mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2022/2023 idadi ya wateja imeongezeka kutoka 24,580 mwezi Juni 2021 hadi kufikia 28,672 sawa na ongezeko la wateja 4,092 mwezi Juni 2023.

“Kwa sasa SHUWASA ina jumla ya wateja 30,135 na tunatarajia kuongeza wateja na kufikia 32,000 mwezi Juni 2024.
Tumeboresha mahusiano kwa wadau mbalimbali wa ndani na wa wadau wa nje”,ameeleza Mhandisi Katopola.


Kuhusu potevu wa Maji, SHUWASA
imefanikiwa kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 26 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi asilimia 20% kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Mwaka 2021/2022 tulifanikiwa kupata tuzo ya Mamlaka bora katika Mamlaka 26 za Mikoa katika Udhibiti wa upotevu wa maji kwa kuwa na upotevu wa asilimia 16%. Kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 hadi mwezi Desemba 2023, Mamlaka iko na upotevu wa maji asilimia 11%”,amefafanua Mhandisi Katopola.


WIZI WA MAJI

Mkurugenzi huyo wa SHUWASA amesema wamefanikiwa kukamata wezi wa maji wapatao 76 kati ya mwaka wa fedha 2021/2022 na mwaka wa fedha 2022/2023 na kuwakadiria adhabu inayofikia Tzs 29,161,858.


MAUZO YA MAJI

Katika Mwaka wa fedha 2020/2021, amesema mauzo ya maji yalikuwa shilingi 6,337,659,070.00, Mwaka wa fedha 2022/2023 mauzo ya maji yalikuwa 8, shilingi 789,159,353.00 sawa na ongezeko la shilingi 2, 451,500,283 ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.89%.


“Kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 hadi Desemba 2023 mauzo ya maji yalikuwa 5, 233,547,797. Matarajio yetu ya kuuza maji (Billing) yanayofikia kiasi cha shilingi 10,730,296,792”,ameongeza Mhandisi Katopola.


MAPATO YATOKANAYO NA MAUZO YA MAJI

Mhandisi Katopola amesema katika mwaka wa fedha 2020/2021 mapato yalikuwa Shilingi 6,713,002,426, na mwaka wa fedha 2022/2023 mapato yalikuwa shilingi 8,165,297,101 na kwamba SHUWASA inazidai taasisi mbalimbali kiasi cha shilingi 906,428,713.00 huku akibainisha kuwa ongezeko la mapato ni shilingi 1,452,294,674 sawa na asilimia 17.78%.


UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA


Mhandisi Katopola miradi mikubwa inatarajiwa kutekelezwa ikiwemo mradi wa IFF – OBA na mradi wa AFD ambapo jumla ya shilingi milioni 735, 464,939 zitatumika katika ujenzi wa mradi wa (IFF – OBA) wa kuchakata majitaka kufikia mita za ujazo 100 kwa siku.

Ameeleza kuwa kwa sasa SHUWASA ina uwezo wa kutibu majitaka kwa mita za ujazo 40 na mamlaka hiyo ipo katika hatua ya ununuzi wa gari la majitaka kama sehemu ya usimamizi wa mazingira.


Kuhusu Mradi wa AFD, amesema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ilisaini Mkataba wa fedha na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (French Development Agency - AFD) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa eneo linalohudumiwa na SHUWASA na kwamba mkataba huu wenye thamani ya EURO milioni 76 (Euro 75 ni mkopo wa riba nafuu toka Shirika la Maendeleo la Ufaransa na Euro milioni 1 zitatolewa na Serikali ya Tanzania) ulisainiwa mnamo tarehe 20.06.2022. Mkataba huu wa fedha unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Mei 2024 kufikia tamati mwezi Mei mwaka 2028.
“SHUWASA inaendelea na utekelezaji wa mradi huu ambao unahusisha, ujenzi wa Mtandao wa majisafi kwa kilomita 298,
 ukarabati wa mtandao chakavu wa majisafi kwa takribani kilomita 100 na ujenzi wa matangi mawili ya kuhifadhia majisafi yenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 1,500 eneo la Kolandoto na mita za ujazo 250 eneo la Didia”, ameeleza Mhandisi Katopola.


Kazi zingine zinazoendelea ni ujenzi wa mitambo minne ya kuchakata tope kinyesi eneo la Ihapa na Mwagala kwa Manispaa ya Shinyanga na Kituli na Iselamagazi - Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, ukarabati wa Mtambo wa kutibu maji Ning'hwa na tathmini ya Ufanisi na ukarabati wa bwawa la Ning'hwa na kuijengea uwezo SHUWASA ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la ofisi.

Mhandisi Katopola amesema tayari SHUWASA imeshatangaza zabuni mbili za kupata wahandisi washauri kwa eneo la Ujenzi na Usimamizi (Design & Supervision) pamoja na eneo la Usaidizi kwa Mamlaka (Technical Assistance) kwa usimamizi wa Mradi na zabuni moja ya kandarasi ya ujenzi (Construction of portable water infrastructure) ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Pia SHUWASA inaendelea na zoezi la kurasimisha maeneo mbalimbali ya mradi, ambapo maombi ya fedha za fidia kwa waathirika wa mradi yamewasilishwa Wizara ya Maji mnamo tarehe 24.10.2023 kwa hatua zaidi za utekelezaji.

Ameongeza kuwa kwa sasa SHUWASA inaendelea na maandalizi ya nyaraka mbalimbali za mradi ikiwa ni pamoja na maombi ya vibali mbalimbali kutoka kwa mfadhili na Taasisi nyingine za Serikali ili kuwezesha mikataba ya shughuli za ujenzi kusainiwa na utekelezaji kuanza.

“Imetazamiwa kuwa mkandarasi atakabidhiwa eneo la mradi na kuanza shughuli za ujenzi mwezi Machi, 2024. Mradi utahusiha ujenzi wa vyoo vya kisasa katika maeneo ya kijamii kama shule, vituo vya afya, stendi vipatavyo 36. Kuijengea uwezo SHUWASA ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la Ofisi”,ameongeza.


Share:

MBUNGE LUGANGIRA ATAKA MATUMIZI YA MITANDAO KATIKA UCHAGUZI YAINGIE KATIKA SHERIA




MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira ameshauri Mswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi uwe na Ibara inayoongelea masuala ya Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi ikiwemo (Akili Mnemba - AI).

Lugangira ametoa ushauri huo leo jijini Dar es Salaam wakati akichangia kwenye mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa unaoshirikisha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria za vyama vya siasa.

Alisema Novemba 2023, Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika (Association of African Election Authorities) ilipitisha Mwongozo wa Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi barani Afrika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe katika Jumuiya hiyo, hivyo itakuwa sio jambo jema kutunga Sheria ambayo inakinzana na maazimio hayo.

"Mswaada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijagusia kabisa suala la Matumizi katika Uchaguzi, jambo ambalo limeshathibika kuwa moja ya maeneo yenye changamoto kubwa katika chaguzi zetu," alisema

Alisema ni lazima kuangalia pia athari za teknolojia mpya kama akili mnemba “artificial intelligence” katika Uchaguzi kwa kuwa tayari dunia imekwenda huko.

"Napenda kushauri na kusisitiza Sheria hii ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi uhakikishe inaongezwa Ibara Mpya katika eneo hili la Matumizi ya Mitandao katika uchaguzi sababu Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika ambapo Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe, alisema.
Share:

MWENYEKITI SMAUJATA TANGA AHIMIZA UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KILA WILAYA






Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Tanga Hamis Ngota akizungumza wakati wa mkutano wake na wajumbe wa umoja huo uliofanyika Jijini Tanga








Oscar Assenga,TANGA

Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Tanga Hamis Ngota amehimiza umuhimu wa ushirikiano utakaokwenda sambamba na vitega uchumi kila wilaya ambavyo vitakuwa ni chachu ya kuweza kuukwamua Jumuiya hiyo.


Mbota aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na wajumbe wanaounda Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Tanga ambapo alisema hatua hiyo ni utekelezaji kwa vitendo maono ya viongozi wao wa Taifa.

Alisema viongozi wao umoja huo Taifa wameelekeza lazima kila mkoa uweze kuwa na kitega uchumi chake ambapo tayari kwa mkoa huo wameanza mchakato wa kufanikisha suala hilo.

“Viongozi wa Sumaujata Mkoa wa Tanga tujiathimini na tuhakikishe tunaunga mkono kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu Taifa kwamba kila shujaa awe na kadi ya bima ya afya na kitega uchumi chake“Alisema

Aidha alisema kuwa wanataka kuwa na mradi katika mkoa ambao utasimamiwa na wilaya ambao utasimama ili kuweza kuwa rahisi kutekeleza miradi yao.

“Lakini kikubwa naombeni ndugu zangu mnipe ushirikiano kwa maana tuna mipango mingi mizuri ya kuukwamua umoja wetu huu kwa mkoa wa Tanga na tayati tuna mpango kazi ambao utawasaidia wanataka kwenda wapi na wanataka kufanya nini”Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo aliwaomba ushirikiana ikiwemo kuhakikisha wanajitoa kwa nguvu zao kuhakikisha wanapata mafanikio makubwa kwani miradi itakapoanza kunahitajika usimamizi
 mzuri.

Akizungumzia suala kampeni ya kupinga ukatili wa Kijisnia na kusajili mashujaa Wazalendo ,Mwenyekiti huyo alisema kampeni hiyo ina umuhimu mkubwaa kwa jamii kutokana na kwamba elimu ambayo watakayokuwa wakiipata itawasaidia na kuwawezesha kupata uelewa wa namna ya kuepukana na hali hiyo.

"Kampeni hii ya kupinga ukatili wa kijinsia ni muhimu kwa jamii ya watanzania na sisi kupitia umoja wetu wa Smautaja tutahakikisha tunashiriki kikamilifu kwa kutoa elimu ambayo tunaamini itakuwa chachu ya kuweza kuondokana na vitendo hivyo kwenye jamii"Alisema 

Hata hivyo aliwaomba viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kukemea vitendo hivyo ili viweze kuondoka kwani Tanzania inawezekana bila kuwa na vitendo hivyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger