Wednesday, 21 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 222023










































Share:

SIKU YA MABAHARIA DUNIANI "SEAFARERS DAY' KUADHIMISHWA JIJINI MWANZA

 

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye ofisi za TASAC zilizopo Jijini mwanza, kuhusu maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 22 Juni,2023 na kufikia kilele tarehe 25 Juni,2023 kwenye Viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela,Jijini Mwanza
Baadhi ya Wanahabari na wafanyakazi wa TASAC na Wizara – Sekta ya Uchukuzi wakifatilia mada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali (hayupo pichani) wakati wa kikao kuhusu maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 22 Juni,2023 na Mgeni rasmi Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Mkame ambapo yatafikia kilele tarehe 25 Juni,2023 kwenye Viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela,Jijini Mwanza


Na Mwandishi wetu Mwanza 

Maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yenye kauli mbiu ya “Miaka 50 ya MARPOL, Uwajibikaji wetu unaendelea” yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho tarehe 22 juni,2023 kwenye Viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza ambapo mgeni rsmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi na uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe.Suleiman Masoud Makame


Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za Tasac jijini mwanza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Nelson Mlali amesema siku ya Mabaharia Duniani huazimishwa wiki ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka Duniani kote na Nchi wanachama wa Shirika la Bahari Duniani(IMO) ambapo Tanzania ni Nchi mwanachama na kwa mwaka huu 2023 maadhimisho haya yatafanyika Kitaifa Jijini MWANZA


Bw. Mlali amesema Maadhimisho haya yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo maonesho ya Taasisi zinazojihusisha na masuala ya usafiri kwa njia ya maji,warsha ya wadau itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, kufanya usafi katika mialo, kutoa elimu kwa wadau na Wanafunzi wa Vyuo, na zoezi la majaribio ya uokoaji inapotokea dharura majini


“Maonesho haya yatahusisha wadau wote wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Maji ambapo watapata fursa ya kutangaza shughuli na majukumu yanayotekelezwa na taasisi zao,kutoa elimu ya uhamasishaji katika shule,vyuo,mialo pamoja na masoko ya samaki yaliyopo jijini mwanza” amesisitiza Mlali


Aidha Bw. Mlali amesema katika siku ya kilele cha maadhimisho tarehe 25 Juni,2023 kunatarajiwa kuwa na mbio za hisani (SeaFarers Marathon) zitakazoanzia katika mwalo wa kirumba kupitia barabara ya isamilo,samaki kutokea nyamagana,kamanga feri na kumalizikia katika mwalo wa kirumba ambapo utafanyika usafi wa mazingira na kugawa Medali kwa washiriki wote na baadae kuelekea katika viwanja vya furahisha kwa ajili ya kufunga maadhimisho


“Natoa rai kwa wananchi wote kutoka sehemu mbalimbali za Viunga vya Jiji la Mwanza na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi na kutembelea katika viwanja vya maonesho ili kupata elimu ya usafiri majini na kujiandikisha kwa wingi kwenye mbio za hisani kwani hakuna gharama za uandikishaji na kutatolewa tshirt na medali kwa washiriki wote” ameongeza Mlari


Maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayoanza tarehe 22 mpaka 25 Juni, 2023 yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta Uchukuzi kwa Tanzania Bara kupitia Shirika la uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) na Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Zanzibar(ZMA), Pamoja na wadau mbalimbali wa Uchukuzi kwa njia ya maji Nchini.

Share:

WATUMISHI WA KANDA YA KUSINI MTWARA WATAKIWA KUWA WAADILIFU




Kamisha wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyekaa katikati kushoto kwake ni Katibu Msaidizi Kanda ya Kati kusini Bw Philoteus Manula na kulia kwake ni Afisa Tawala Bw Steven Jarka wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Sekretarieti Kanda ya Kusini Mtwara ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Mtwara tarehe 21 Juni 2023.


Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi katika akiwa katika ziara yake kutembelea ofisi ya Kanda ya kusini Mtwara ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma tar 21 Juni 2023

Na.Mwandishi Wetu Watumishi wa Kanda ya Kusini Mtwara, wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa Uadilifu, umakini na weledi wa kiwango cha juu.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi katika ziara yake ya kutembelea Kanda hiyo tar 21 June 2023.

Aisha, Jaji Mwangesi katika hotuba yake ameongeza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza rasmi tar 16 June na kuhitimishwa tar 23 June 2023.

Mhe, Kamishna alifafanua kuwa , lengo kubwa la ziara yake katika maadhimisho haya ni kuwakumbusha watumishi wa Umma na viongozi kwa ujumla kuhusu wajibu wao, na maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kuhusu changamoto zilizopo katika kanda hiyo, Mh Mwangesi alifafanua kuwa kuhusu uhaba wa watumishi na upungufu wa magari suala hilo linafanyiwa kazi na mchakato unaendelea.

Mh Mwangesi amewataka watumishi wa Kanda ya Kusini Mtwara kutunza jengo la Maadili ambalo ni zuri na kubwa ili liweze kudumu kwa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya uboreshaji wa mazingira ya kafanyia kazi.

Aliongeza kuwa Sekretarieti iko katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa Online Decrelation Syterm (ODS) ambao utasaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na pia kuwawezesha viongozi kutuma matamko yao kwa njia ya Mtandao kwa uhakika na urahisi zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Ziara hii ya Mh Kamisha wa Maadili katika kanda ya kusini Mtwara ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa iliyoanza rasmi tarehe 16 juni na kuhitimishwa tar 23 junior, 2023.
Share:

TBS YAKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU ZENYE THAMANI YA ZAIDI MILIONI 25 KANDA YA MAGHARIBI


BIDHAA za mafuta ya breki ya dot 3, nguo za ndani za mitumba na nyaya za umeme ambazo zimepigwa marufuku nchini zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 25 zimekamatwa kupitia operesheni maalum iliyoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Magharibi.

Operesheni hii maalum imefanyika katika Mikoa ya Rukwa na Kigoma, ambapo wakaguzi wa shirika hilo walibaini uwepo wa bidhaa hizo zilizopigwa marufuku kutumika nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa operesheni hiyo, Afisa wa TBS, Elisha Meshack, alisema operesheni hiyo ya ukaguzi imeenda sambamba na utoaji elimu kwa wenye maduka yanayouza bidhaa hizo ili waweze kuzingatia matakwa ya viwango na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

“Operesheni hii ambayo imemalizika katika mikoa ya Rukwa na ni endelevu na lengo ni kuhakikisha soko la Tanzania linakua na bidhaa bora na salama kwa matumizi ya wananchi na mazingira” alisema Meshack.

Alitaja madhara ambayo mtu anaweza kuyapata kwa kuvaa nguo vya ndani za mitumba zilizopigwa marufuku kuwa ni magonjwa ya ngozi pamoja na yale yanayoshambulia sehemu za siri.

Kwa madhara ya kutumia nyaya zilizopigwa marufuku, Meshack alisema ni kuunguliwa na vitu na hata kuweza kusababisha vifo.

Kuhusu madhara ya matumizi ya mafuta y breki aina ya dot 3, Meshack alisema yanawez kusababisha breki zikafeli na kusababisha ajali ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa mali na hata vifo.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS, Deborah Haule alisema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kukamata bidhaa zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni ishirini na tano katika operesheni hiyo na kusisitiza kuwa operesheni hiyo ni endelevu.

“Operesheni hii ni endelevu na tutaendelea na ukaguzi wa bidhaa hafifu sokoni mpaka pale tukapojiridhisha kuwa Tanzania yetu ni salama na wafanyabiashara wanasimamia ubora wa bidhaa katika maeneo yote,” alisema Haule.

Haule alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kufuata matakwa ya viwango wanaponunua na kutengeneza bidhaa ili kujiepusha na hasara wanazoweza kupata pale bidhaa zao zitakapogundulika kuwa zina ubora hafifu na vile vile aliwasisitiza kuwasiliana na ofisi za TBS pale wanapoona wana mashaka na bidhaa yoyote.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wameomba elimu hiyo izidi kutolewa na kudhibiti wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza bidhaa ambazo zilipigwa marufuku.

Mmoja wa wafanyabiashara wa mkoani Kigoma, Ibrahim Ramadhani, alipongeza kazi nzuri inayofanywa na TBS na kushauri utaratibu huo uendelee ili soko la Tanzania liwe na bidha zinazokidhi matakwa ya ubora.


Share:

Picha : TCRA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA...."MSITUMIE VISHOKA KUANZISHA VYOMBO VYA HABARI"


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta iliyofanyika leo Jumatano Juni 21,2023 katika Ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga.

Mhandisi Mihayo amesema lengo kuu la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha waandishi wa habari  wanatambua majukumu ya TCRA na kuzijua sheria na taratibu ili wafanye kazi vizuri pamoja kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. 

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha wadau wa mawasiliano wanaotaka kuanzisha vyombo vya habari mfano Redio kuepuka kutumia vishoka ili kupata huduma badala yake wawasiliane na TCRA ili kusaidia kupata huduma.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta




Share:

Tuesday, 20 June 2023

WAFANYABIASHARA MAARUFU 'JAMBO - JAMUKAYA' GILITU WANG'AKA SAKATA LA BANDARI

Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya amesema wafanyabiashara nchini ndiyo waathirika wakubwa wa Bandari ya Dar es salaam kutokana mizigo yao kuchukua muda mrefu mpaka siku 16 akisisitiza kuwa anatamani kama mkataba wa uwekezaji katika Bandari wangeruhusiwa kuusaini wangekuwa tayari wameshausaini.

Jambo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 20,2023 wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.


“Sisi wafanyabiashara tunaijua bandari kuliko mtu yeyote yule. Mngeturuhusu sisi tungeenda kuusaini huo Mkataba mara moja. Huu siyo mkataba wa kwanza katika Bandari, huu ni mkataba uliofanyiwa marekebisho baada ya wawekezaji waliopita”,
 amesema.

“Wafanyabiashara tunauhitaji huu mkataba huu kuliko kitu chochote….Nawashangaa hao wanaoshangaa mkataba wa uwekezaji. Mimi ningeomba nyinyi serikali muangalie hao wanaopinga ni akina nani. Wafanyabiashara tunataka makontena yetu yawe yanatoka haraka bandarini, tuyachukue haraka. Tunatumia gharama kubwa kucheleweshewa mizigo yetu bandarini. Hizi gharama sasa zinatosha”,amesema Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Jambo Food Products.

“Sisi wafanyabiashara msihusishe na wanasiasa, wanasiasa hawana mizigo bandarini, Sisi wenye mizigo tunataka uwekezaji katika bandari, kwani mizigo yetu inachukua mpaka siku 16”,ameongeza Jambo/Jamukaya.

Kwa upande wake mfanyabiashara maarufu Gilitu Makula amesema amefuatilia na kubaini kuwa wengi wanaopinga uwekezaji katika bandari hawajawahi hata kuwa na kontena bandarini.


“Usumbufu uliopo bandarini ni mkubwa sana. Mkataba huu utasaidia sana mizigo itoke haraka. Hakuna mtu anayetaka kuuza nchi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ni mzalendo. Hawa wanaopinga ni kutafuta umaarufu tu wa kisiasa”,ameongeza Gilitu.
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Soma pia



Share:

WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA HAZINA WAHIMIZWA WELEDI KAZINI


Na Mwandishi Maalumu

WATUMISHI katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) wamehimizwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuhakikisha kila mmoja anatoa mchango wake katika kuleta tija kwa Ofisi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Hazina, Lightness Mauki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dar es Salaam.

Mauki alisema wajibu na weledi huo unatokana na ukweli kuwa ofisi hiyo ndiyo yenye jukumu la kusimamia uwekezaji mkubwa wa serikali wenye thamani ya Sh trilioni 70 kwenye taasisi, mashirika ya umma na kampuni ambazo serikali ina hisa.

Katika kuadhimisha wiki hiyo, viongozi na watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wameungana katika kuhudumia wateja na wadau wa ofisi kwa kutenga eneo maalumu katika makao makuu ya ofisi, Mtaa wa Mirambo, Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu inayosema; “Kufanikiwa kwa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika Kunahitaji Usimamizi wa Utumishi wa Umma Wenye Mtazamo wa Kikanda” yanayotarajiwa kufikia tamati Ijumaa wiki hii, Mauki aliwataka watumishi hao kushughulikia malalamiko ya wadau na wateja wanaofuata huduma katika Ofisi ya Msajili wa Hazina na kutunza kumbukumbu ya namna wateja wa ndani na wa nje wanavyohudumiwa huku wakihakikisha kuwa wanatatua changamoto zao.

Aidha, Mauki alisema katika maadhimisho hayo, ofisi imejikita katika maeneo matatu ambayo ni viongozi wa Idara na Vitengo kufanya vikao na watumishi wanaowasimamia ili kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuiwezesha ofisi kufikia malengo yake kwa ufanisi mkubwa.

Alisema katika kuhitimisha maadhimisho hayo Juni 23, 2023 watumishi wote watatembelea Kituo cha Wazee cha Nunge kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam kwa lengo la kufanya shughuli za kijamii na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wazee hao.

Kutokana na umuhimu wa wiki ya utumishi wa umma, Mauki aliwasisitiza watumishi kutoa huduma sawa kwa wateja na wadau wote wa ndani na nje ya ofisi.

“Ninawakaribisha wateja na wadau wote wa ofisi kufika katika Ofisi yetu ya Msajili wa Hazina kuja kupata huduma wanazohitaji kutoka kwetu. Karibuni sana,” alisema.

Maadhimisho haya yanayofanyika kati ya Juni 16 na 23 ya kila mwaka, ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afirika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonesho ya kazi mbalimbali na kongamano kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma. Kwa Tanzania, yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger