Tuesday, 20 June 2023

Tazama Picha : MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKIZUNGUMZA NA WAWEKEZAJI NA WAMILIKI WA VIWANDA SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuelezea fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani Shinyanga sambamba na kutoa 
maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji  na uboreshaji  kazi wa Bandari Tanzania.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Khatibu Mgeja akizungumza kwenye mkutano wa Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Juni 20,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 


Share:

WAWEKEZAJI VIWANDA WAASWA KUZINGATIA SHERIA NA MIONGOZO YA KAZI

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo kilifanyika kikao kifupi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea viwanda Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamiii, Mhe.Fatma Hassan Toufiq( wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa OSHA, Dkt. Jerome Materu (wakwanza kushoto) alipokuwa akijibu hoja inayohusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi iliyoibuliwa na wawekezaji wa kiwanda cha Fides Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamiii, Mhe.Fatma Hassan Toufiq pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakipata maelekezo kwa muwakilishi wa kiwanda cha kutengeneza transfoma cha TANALEC Limited kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zao.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akishona nguo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika kiwanda cha A to Z Mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamiii, Mhe.Fatma Hassan Toufiq (watano kushoto) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kiwanda cha kuzalisha maua cha Fides Tanzania aliyekuwa akieleza kuhusu hatua za kiusalama wanazotumia kumlinda mafanyakazi katika mnyororo mzima wa uzalishaji maua.


***********************

Wawekezaji wa sekta ya viwanda wametakiwa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali ya kazi nchini ikiwemo kuboresha mifumo ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi ili kuwalinda wafanyakazi dhidi ya athari wanazoweza kuzipata wakiwa kazini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maenedeleo ya Jamii ya kutembelea viwanda Mkoani Arusha akiambatana na kamati hiyo ili kujionea utekelezaji wa sheria na miongozi mbalimbali ya kazi ikiwemo Sheria Na.5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003.

“Kwanza kabisa tunapenda wawekezaji waje nchini kwa wingi na wanapowekeza basi waendeshe shughuli zao zote kwa kuzingatia sheria mbalimbali za nchi ikiwemo sheria na miongozo mbalimbali ya kazi, huwa tunafurahi sana tunapoona wawekezaji wanatengeneza ajira kwa vijana wetu lakini pia wakiendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria za nchi “ alisema Prof. Joyce Ndalichako.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Manendeleo ya Jamii, Mhe. Riziki Saidi Lulida amewataka wawekezaji hao kuhakikisha wanaweka miundo mbinu rafiki katika maeneo mbalimbali ya viwanda vyao kwa watu wenye ulemavu.

“Tunazo sheria za nchi zinazoelekeza viwanda kujenga miundo mbinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, kwa mfano mimi leo nimeshindwa kuingia ndani katika baadhi ya viwanda tulivyotembelea kutokataka na ulemavu wangu wa miguu kwasababu maeneo mengi yana ngazi, naamini kuna wafanyabishara wengi wenye ulemavu ambao pengine wanatamani kuingia katika maeneo ya viwanda na wakashindwa kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki kwao hivyo wito wangu kwa wawekezaji wote nchini katika sekta hii ya viwanda waboreshe miundommbinu ili kuwapa fursa wenye ulemavu” alisema Makamu Mwenyekiti, Bi. Riziki Saidi.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Jang’ombe, Mhe. Ali Hassan King ameishauri taasisi ya OSHA kuendelea kuimairisha mifumo ya usimamizi wa usalama na afya katika ameneo ya kazi nchini huku akiahidi kuwa wataendelea kuishauri serikali juu ya uimarishaji wa mifumo ya usalama na afya katika viwanda.

“Kupitia ziara hii tumepata mengi ya kujifunza na kuishauri serikali na katika maeneo yote tuliyotembelea kwa kiasi kikubwa tumeridhishwa na hali ya utekelezaji wa sheria na miongozo ya usalama na afya na kuna mambo mbalimbali tumehoji katika viwanda hivi na tumewaelekeza kutoa majibu kwa kuandikia taarifa nasisi tutaiandikia ripoti ili kuiwasilisha bungeni kwa lengo la kuishauri serikali” alisema Mhe. Ally Hassan

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi wa OSHA, Dkt. Jerome Materu amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa wawekezaji wote kuzingatia taratibu na miongozo yote ya usalama na afya kwasababu huongeza tija na kupunguza gharama za uendeshaji wa maeneo yao ya kazi.

“Unapowekeza katika masuala ya usalama na afya mahali pa kazi kuna mahusiano makubwa kati ya upunguzaji wa gharama na uendeshaji wa eneo la kazi hivyo tunaishukuru sana Kamati hii ya Bunge kwasababu na wao wamekuwa ni jicho la tatu katika kuangalia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na wametupatia ushauri ambao tutautumia katika kuboresha usimamizi wa mifumo ya usalama na afya katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini “ alisema Dkt. Jerome Materu

Aidha wawakilishi wa viwanda vilivyotembelewa wameishukuru kamati hiyo kubainisha kuwa ziara hiyo imewapa funzo kubwa huku wakiahidi kuendelea kuboresha zaidi mifumo ya usimamizi ya usalama na afya mahali pa kazi.

Katika Ziara hiyo Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendelea ya Jamii imetembelea viwanda vitatu Mkoani Arusha ambavyo ni: Kiwanda cha kuzalisha Transifoma cha TANELEC Limited, Kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo cha A to Z Textiles Mills Ltd pamoja na kiwanda cha maua cha Fides Tanzania.
Share:

MBUNGE MTATURU APAZA SAUTI YA WAFUGAJI BUNGENI



MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jijini Dodoma katika swali la msingi alilouliza kwa niaba ya Mbunge wa Kondoa Mjini Ally Makoa aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga majosho katika Kata za Kolo,Kingale na Bolisa.

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha afya ya mifugo kupitia majosho wanayojenga nchini.

Pamoja na pongezo hizo ameihoji serikali ni lini itajenga josho katika Kata ya Siuyu iliyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida ili kuweza kutoa huduma ya mifugo katika Kata hiyo.

Mtaturu ameuliza swali hilo Bungeni Jijini Dodoma Juni 20,2023,wakati akiuliza swali la nyongeza katika swali la msingi alilouliza kwa niaba ya Mbunge wa Kondoa Mjini Ally Makoa aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga majosho katika Kata za Kolo,Kingale na Bolisa.

“Kwa sababu majosho haya yanalenga katika kuboresha afya ya mifugo na mwisho wa siku tunapata kitoweo kizuri,nini mkakati wa serikali wa kuhakikisha kwamba ujenzi ule unasimamiwa vizuri na majosho yanakamilika kwa muda uliopangwa,

“Kwenye Jimbo la Singida Mashariki katika Kata ya Siuyu tulikuwa na josho ambalo sasa hivi limeingiliwa na eneo la kanisa la RC, na tuliomba lihamishwe liende eneo lingine kwa sababu linakosa sifa ya kutumika pale,tumeshatenga eneo katika kijiji cha Siuyu na tuliomba muda mrefu zaidi ya miaka mitatu,Je ni lini serikali itajega josho kwa ajili ya kutoa huduma ya mifugo katika kata ya Siuyu,”?amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde amemuondoa hofu mbunge na kusema Wizara hiyo chini ya Waziri wake Abdallah Ulega na walio chini yake wameahidi kutekeleza yote waliyoyapanga katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.

“Yale ambayo hayajakiamilika tutahakikisha katika mwaka wa fedha unaokuja yanakamilika kwa wakati,kwa sababu hili ndio lengo letu na ndio lengo la Mh Rais Samia Suluhu Hassan,

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa josho katika Kata ya Siuyu,Silinde amesema amelipokea na kuliwekea kipaumbele.

“Mh Mbunge amezungumzia josho katika Kata ya Siuyu,nimwambie tu nimelipokea,nitaangalia katika orodha niliyonayo kama tumeliweka ,na kama halipo tutaona namna gani tunatafuta fedha ili tuliweke katika moja ya kipaumbele chetu,”amesema.

Share:

KUTANA NA NYANI MDOGO ANAYEISHI KIFAHARI SASA GUMZO MTANDAONI


Nyani mdogo na mrembo ambaye anaishi maisha ya kifahari ambayo wengi wangependelea, ndiye anayegonga vichwa vya habari mtandaoni.

Maarufu kama Mojo, mnyama huyo kutoka Marekani anajivunia wafuasi milioni 8.5 ambao huvutiwa na maisha yake ya kifahari.

Kwenye video zake zinazovutia kwenye TikTok, Mojo anaonekana akipata kikao cha kujipamba kwa utulivu, akionyesha nguo nzuri, na akifurahia chakula kizuri pamoja na vitafunio vyake vinavyopendwa kama pilipili tamu.

Wafuasi wake pia wanashiriki katika safari zake za barabarani, wachezaji wenzake ndani na nje ya nyumba, na kuendelea kuuliza kilichotokea tangu video ya mwisho waliyoangalia.

"Kuwa na nyani kama kipenzi ni gharama kubwa sana, anatumia nepi nne kwa siku na pakiti moja inagharimu KSh 6000. Atatumia nepi kwa maisha yake yote," alisema mmiliki wake." "Pia anahitaji unga wa lishe ambao ulikuwa KSh 5000 na tangu azidi kuzihitaji, sasa nampa biskuti za sokwe, matunda, na mboga. Gharama ya haya yote ni KSh 8500 kwa wiki. Pia wanatoka nje na kula nyasi kwa virutubisho vyao," alisema.
Share:

WAHUNI WAVAMIA KWA PASTA NA KUIBA MAHINDI


Mchungaji anayeishi Sachangwan katika eneo la Molo nchini Kenya anahesabu hasara baada ya wezi kuvamia nyumbani kwake na kuiba mali kadhaa.

Mtu huyo wa Mungu, Joel Tanui, alisema wezi waliondoka na mifuko mitano ya mahindi, blanketi saba, na matandiko.

Kwenye tukio hilo, Tanui alisema wahalifu hao kwanza walivunja ghala na kuiba mifuko ya mahindi yaliyokaushwa, kulingana na ripoti ya Citizen TV. 

Kisha waliingia kimyakimya katika shamba la mahindi lililoko karibu, ambapo waligawanya nyara hizo katika mifuko midogo kabla ya kuzibeba.

Wakazi wa eneo hilo walilalamika juu ya ongezeko la matukio ya wizi, hasa unaozingatia nyumba.

 Walisema wanalazimika kufunga biashara zao mapema kwa hofu ya kushambuliwa. Inasemekana wezi wanawalenga kuku, mbuzi, na bidhaa nyingine za nyumbani.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 20 2023

  



















Share:

Monday, 19 June 2023

HALMASHAURI YA MULEBA IMEENDELEA KUPATA HATI SAFI MIAKA 5 MFULULIZO



 Katibu Tawala mkoa wa Kagera Toba Ngunvila 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Justus Magongo
Madiwani wakiwa ukumbini.

Na Mwandishi wetu - MALUNDE 1 BLOG

Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera imeagizwa kuongeza ufanisi katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na kuibua vyanzo vipya vya mapato jambo ambalo litasaidia halmashauri hiyo kuendelea kupata hati safi.


Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala mkoa wa Kagera Toba Ngunvila wakati akisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG) akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera katika kikao maalum cha kujadili taarifa hiyo ambapo halmashauri ya wilaya ya Muleba imepata hati safi katika kipindi cha miaka 5 mfululizo.
.

Bwana Ngunvila amesema kuwa agizo hilo la serikali linatakiwa kuendelea kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 na kuhakikisha juhudi za makusudi zinafanyika ili mapato yote ya halmashauri yakusanywe kwa njia ya kielektroniki na sio vinginevyo ambapo madiwani wanatakiwa kusimamia swala hilo .


Kikao hicho ni mwendelezo wa utekelezaji wa Agizo la Mhe.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akipokea taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2021/2022 ambapo alielekeza kila Taasisi ifanyie kazi taarifa hizo na kuhakikisha hoja husika zinafungwa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Justus Magongo amesema kuwa katika mafanikio ya halmashauri hiyo kupata hati safi ni kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya watumishi wa halmashauri hiyo na madiwani wa kata 43 ambapo ameaidi kuwa halmashauri hiyo itaendelea kufanya vizuri hasa kwa kusimamia mapato kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo.


Aidha ameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Muleba kwa ushirikiano wanaowapatia ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa halmashauri hiyo kuendelea kufanya vizuri.

Share:

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA WELEDI


Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.


Washiriki wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.

Washiriki wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omar Ramadhan Mapuri akisalimia wakati wa mkutano huo wa mafunzo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza.
Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Mh. Ruth Mkisi akiwaongoza wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri.

Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata wakila kiapo cha kujitoa unachama wa vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza jana jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata wakila kiapo cha kujitoa unachama wa vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza jana jijini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
******************Na Mwandishi Maalum, Tanga.
Wasimamizi wa Uchaguzi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata leo tarehe 19 Juni, 2023 jijini Tanga.


Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.


“Jambo muhimu mnalotakiwa kuzingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, mnapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo,” amesema Jaji Mbarouk.

Amewaasa washiriki hao wa mafunzo kuhakikisha kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yao wanao katika uendeshaji wa uchaguzi, wahakikishe wanazingatia maelekezo watakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

“Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa, hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na kupunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi,” amesema Jaji Mbarouk.

Amewataka watendaji hao wa uchaguzi kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yao kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa ili kurahisisha utendaji wa kazi.

Jaji Mbarouk amewaelekeza wasimamizi hao wa uchaguzi kuhakikisha kuwa watendaji wa vituo vya kupigia kura ni watu wenye weledi na uwezo mkubwa na kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha vituo kufunguliwa saa 1:00 asubuhi siku ya kupiga kura.

Kata zilizotarajiwa kufanya uchaguzi mdogo ni pamoja na Ngoywa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kalola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Sindeni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Potwe iliyopo Halmashauri Manispaa ya Muheza, Kwashemshi iliyopo Halamshauri ya Wilaya ya Korogwe, Bosha iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Mahege iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Bunamhala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Nyingine ni, Njoro na Kalemawe zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mnavira iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kinyika iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Magubike iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Mbede iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger