Saturday, 10 June 2023

JAMBO FM YAZINDULIWA RASMI...RC MNDEME AIPONGEZA KWA KAZI KUBWA YA KUHABARISHA UMMA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameipongeza Jambo FM inayorusha matangazo yake kutoka katika Manispaa ya Shinyanga kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhabarisha, kuelimisha na kurudisha umma kupitia masafa ya 92.7 MHz.


Mhe. Mndeme ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho cha Redio tukio ambalo lilitanguliwa na mazoezi ya Jogging kutoka SHY COM mpaka VETA na kurudi hadi eneo la NBC Mataa ambapo alishriki zoezi la kupanda miti eneo hilo ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa kituo sambamba na kutunza mazingira katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaahidi kuwapatia ushirikaino wakati wote.


"Nawapongeza sana Jambo FM na Jambo Food Products kwa ujumla kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa wananchi wa Mkoa huu wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla wake ya kuhabarisha umma, kuelimisha na kuburudisha huku Jambo Food Product mkizalisha ajira kwa wananchi pamoja na kukuza uchumi kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa, hongereni sana Jambo," alisema Mhe. Mndeme.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi alisema kuwa, Jambo FM wamekuwa wadau muhimu sana wakati wote katika utekelezaji wa kazi za habari kwa maeneo haya huku akiwataka kuendelea na utamaduni huu kwa maslahi mapana kwa wananchi.


Kwa upande wake Meneja wa Jambo FM Redio Ndg. Nickson George alimuambia mgeni rasmi kuwa, Jambo FM wamefurahi sana kwa kukubali kwake Mhe. Mndeme kuwa mgeni rasmi katika tukio hili la ufunguzi wa Redio na kwamba hii ni ishara tosha kwamba Serikali inafanya kazi na Jambo FM pamoja na Jambo Food Products huku akimuahidi kuendelea ushirikiano na Serikali wakati wote kwa weledi na kuzingatia maadil.


Jambo FM na Jambo Food Product leo wamefanya ufunguzi wa kituo cha Redio ambapo pamoja na mambo mengine pia wamefanya tamasha kubwa la burudani katika viwanja vya SHY COM tukio ambalo limejumuisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, ngoma za asili na michezo mbalimbali ijulikanayo kama SIKUKUU JAMUKAYA kauli mbiu "Tunakula Bata la Mafanikio".







NaShinyanga RS.
Share:

SERIKALI YAANIKA SABABU ZA KUICHAGUA KAMPUNI YA DP WORLD YA DUBAI KUENDESHA BANDARI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameeleza sababu za Serikali kuichagua kampuni ya DP World ya Dubai kuja kuendesha Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na uzoefu wa kampuni hiyo katika kazi.


Profesa Mbarawa amebainisha hayo leo Jumamosi Juni 7, 2023 wakati akitoa maelezo ya awali bungeni yakihusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.


Amesema kutokana na changamoto za bandari zilizopo na kwa kuzingatia dhima ya Serikali ya kuboresha sekta ya bandari nchini ili kuongeza ufanisi na mchango wake katika mapato ya nchi, ajira na kuchagiza sekta nyingine za kiuchumi; Serikali ilifanya uamuzi wa kutafuta wawekezaji wapya wanaoendana na dhima ya Serikali.

Chanzo - Mwananchi
Share:

MKE WANGU ALIYEFARIKI ANANISUMBUA SANA USIKU



Naitwa Juma kutoka kijiji cha Nyakimincha, Kisii nchini Kenya, nimekuwa na changamoto nyingi sana katika maisha yangu, ila kuna changamoto moja ndiyo hasa imekuwa ikininyima usingizi kila wakati.


Ni mwaka mmoja sasa tangu nilipompoteza mke wangu katika ajali mbaya ya barabarani, wakati narudi nyumbani kutoka kazini, nilipata mshtuko mkubwa sana mara baada ya kusikia mke wangu amefariki katika ajali hiyo.


Alikuwa nami kwa wakati wote, aliandaa chakula cha jioni na kisha tukaenda kulala kwenye chumba chetu, ila sasa hayupo, ilikuwa ni huzuni kubwa sana katika maisha yangu.


Hata hivyo, imekuja kuwa huzuni zaidi kwani baada ya maziko yake amekuwa akinitokea usiku na kuzungumza na mimi na asubuhi anakuwa haonekani.


Ninaogopa kumwambia mtu yeyote katika familia yangu kwa sababu ninaogopa kufungua kile ninachofikiria kuwa nafsi yangu ya pili bado inampenda sana mke wangu, na kweli nilimpenda hivyo bado ninampenda sana!.


Jumamosi iliyopita nilienda kanisa ambapo niliombewa na kwa bahati nzuri niliporudi nyumbani siku hiyo mke wangu hakuja, ila alikuja siku iliyofuata, nikawa na wazo jipya, nalo ni mimi kumtembelea mahali anapokaa!.


Nikawa na wasiwasi kama kuna mtu anaweza kuniambia nifanye nini juu ya jambo hilo, kanisa linaweza kunisaidia? Au kuna njia nyingine ya kuondokana na jambo hilo la kutisha maishani?.

Hata hivyo, kutokana na utafiti wangu nilibaina ni mganga wa jadi tu ndiye anayeweza kunisaidia kutoka katika changamoto hiyo, basi siku moja nilisoma katika gazeti moja na na kukutana na jina la African Doctors.


African Doctors wamekuwa wakiwasaidia watu kutoka kwenye changamoto mbalimbali ikiwemo kama yangu, niliwasiliana nao na mara moja wakanifanyia tiba na tangu wakati huo ukawa mwisho wa kutokewa na mzimu wa mke wangu!.


Wasiliana na wataalamu hawa wa mimea, wanaponya shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, kisonono, kaswende, TB, upungufu wa nguvu za kiume n.k.

Pia hutatua shida maishani kama matatizo ya kimahusiano, migogoro ya kifamilia, kuyumba kwa biashara, kukuwezesha kushinda kesi, kupandishwa cheo kazini, kukuondolea ndoto mbaya na hata kushinda bahati nasibu.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com


Share:

JINSI GGML INAVYOVUNJA UKIMYA JUU YA USAFI WA HEDHI

Afisa Uhusiano kutoka GGML, Ruth Mharagi akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya sekondari wasichana Nyankumbu, namna ya kutumia pedi pindi wawapo kwenye hedhi.
Na Mwandishi Wetu

Hedhi ni sehemu ya maisha ya kawaida na yenye afya, lakini kwa watu wengi wanaopata hedhi, ni chanzo cha aibu, hofu na ubaguzi.

 Ukosefu wa upatikanaji wa bidhaa za kutosha za hedhi safi na salama na elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana na hata wazazi, inaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya binti, elimu yake na hata maisha yake.

Kiujumla afya duni ya hedhi na usafi hudhoofisha haki za kimsingi ikiwa ni pamoja na haki ya kufanya kazi, kwenda shule kwa wanawake, wasichana na watu wanaopata hedhi hali hii inazidisha ukosefu wa usawa wa kijamii na kiuchumi.

Ni kwa sababu hiyo kwamba kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), inayothamini maendeleo endelevu kwa jamii, inachukua hatua kusaidia mipango ya hedhi safi na salama katika jamii inayozunguka migodi yake.

Akizungumzia jitihada za kampuni hiyo katika kujali na kuboresha mazingira ya upatikanaji wa pedi kwa wasichana, Makamu Rais wa AngloGold Ashanti-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo anasema GGML inaamini kwamba kwa kuboresha mazingira ya hedhi safi na salama, wanaweza pia kuwawezesha wanawake na wasichana, kupunguza unyanyapaa na ubaguzi, na kuchangia katika kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu.

“Ndio maana katika maadhimisho Siku ya Hedhi Safi na Salama Duniani, ambayo huadhimishwa tarehe 28 Mei kila mwaka, GGML tuliandaa mfululizo wa shughuli za kuongeza uelewa na kutatua changamoto zinazohusiana na usafi wa hedhi.

“Mojawapo ya matukio hayo ilikuwa ni ziara ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu, ambapo wadau mbalimbali walioungana na GGML walizungumza na mamia ya wanafunzi kuhusu suala hilo muhimu,” anasema.
Anasema GGML ilimwalika mhudumu wa afya kueleza vipengele vya kibaiolojia na kisaikolojia vya hedhi na usafi sahihi wa hedhi. GGML pia ilisambaza masanduku 72 ya pedi za usafi kwa wanafunzi na kuwaonyesha jinsi ya kuzitumia ipasavyo.

Tarehe 28 Mei, GGML iliandaa mkutano wa hadhara na Halmashauri ya Mji wa Geita kuadhimisha Siku ya Usafi wa Hedhi Duniani mkoani Geita. Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa, asasi za kiraia, vyombo vya habari na wanajamii.

Anaongeza kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kueneza ujumbe kwamba hedhi safi ni suala la haki za binadamu, si suala la afya tu, na kwamba kila anayepata hedhi anastahili heshima na utu.

“GGML inajivunia kuwa sehemu ya vuguvugu hili la kimataifa la kuvunja ukimya juu ya usafi wa hedhi na kuweka mazingira shirikishi zaidi na yenye msaada kwa watu wanaopata hedhi. Tunatumaini juhudi zetu zitawatia moyo wengine kujiunga nasi na kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya mamilioni ya wanawake na wasichana kote ulimwenguni,” anasema.

Akizungumzia jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na shule hiyo ya wasichana Nyankumbu, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Georgia Mugashe anasema suala la hedhi safi na salama ni kipaumbele ambacho kimewekewa mazingira salama katika kila eneo la shule hiyo.

Akianza na elimu, Mwalimu Mugashe anasema huwapa wanafunzi wa shule hiyo elimu kuhusu afya ya uzazi kila mara kwa mara na kuwafundisha namna ya kuchukua tahadhari.

“Kila mahali tumeweka pedi, mabwenini wao wanazo, kama wapo shule kuna chumba maalumu cha wasichana ambacho kimewekwa pedi na miundombinu yake.

“Nyingine zimeweka kwa daktari au nesi katika zahanati iliyopo karibu na shule hii… kwa hiyo hata kama mwanafunzi anaumwa tumbo akienda hospitali anapatiwa pedi bure kwa hiyo kila mazingira ya karibu anapewa huduma hii free,” anasema.

Anasema elimu hiyo kuhusu hedhi safi na salama inatolewa kwa ngazi zote ikianzia shuleni kwa wanafunzi kwa kushirikiana na halmashauri hata kwa wanafunzi wa shule nyingine lakini pia wanawashirikisha wazazi.

“Tunawaeleza wazazi kwamba sasa hivi suala la hedhi safi na salama ni kitu ambacho ni lazima kwa mtoto yeyote wa kike sio suala la kuficha hivyo tunazungumza nao ili nao watambue wajibu wao.

“Katika magroup ya whatsap mathalani wazazi wa wanafunzi wote wapo, hivyo tunawaeleza kabisa kwamba kila mwezi lazima atambue kuwa anatakikana kuwa na bajeti ya kumsitiri mtoto wa kike, anatakiwa kuwa na paketi moja ya pedi ambayo inauzwa Sh 1500 au 2000,” anasema.

Anasema mbali na njia hizo, pia hutumia vikao mbalimbali kuwaelekeza wazazi na watoto wa kike kuhusu umuhimu wa hedhi safi na salama ili kuzidi kuimarisha afya zao.

Pamoja na mambo mengine, Mwalimu Mkuu huyo anaishukuru Kampuni ya GGML kwa kuendeleza juhudi za kuwasaidia wanafunzi na jamii inayozunguka mgodi huo vifaa mbalimbali ikiwamo pedi ambazo zimeendelea kuwa mkombozi kwa watoto wa shule hiyo na hata kupunguza gharama za uendeshaji wa shule.

Katika maadhimisho ya siku ya hedhi duniani mwaka huu, ilikuwa na kauli mbiu ya kitaifa isemayo; “Hedhi ni tunu na Msingi wa Afya kwa wasichana na Wanawake, Tuiwezeshe,”.

Kauli mbiu hiyo ililenga kuendelea kuweka mkazo katika masuala ya hedhi iliyo salama kwa wasichana na wakina mama kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Share:

Friday, 9 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 10, 2023

 



















Share:

PROF. NOMBO AHIMIZA NACTVET KUSIMAMIA VYUO VYA MAFUNZO YA UFUNDI STADI


Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo tarehe 9 Juni 2023 ameitaka NACTVET kuongeza usimamizi wa vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kufikia ubora unaostahili.

Prof. Nombo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wamiliki wa vyuo binafsi vya Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayofanyika katika chuo cha Ualimu Morogoro.

Mafunzo hayo yamewaleta pamoja, wamiliki wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi Kanda za Kaskazini (Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara), Kanda ya Kati (Dodoma, Iringa, Singida) na Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Morogoro na Pwani). Malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wamiliki wa Vyuo na Wakuu wa Vyuo hivyo kutoa mafunzo yanayokidhi viwango vya sasa kwa mahitaji ya soko la ajira.

“NACTVET ihakikishe kuwa elimu na mafunzo ya ufundi stadi inatolewa kwa viwango na ubora unaohitajika na soko la ajira na hatimaye kuwa na wahitimu wenye ujuzi na umahiri”. Alisema Prof. Nombo.

Aliongeza kuwa, Serikali inathamini mchango wa vyuo katika kukuza ujuzi na umahiri na kuiagiza NACTVET itumie fursa hii kuendelea kukutana na wadau wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua kwa maendeleo ya nchi na uchumi endelevu.

Aidha, amevitaka vyuo kuandaa programu zenye tija na ubora unaokubalika kwani Serikali imewekeza katika miradi mbalimbali yenye kuhitaji wataalamu wenye ujuzi na umahiri katika kuendesha miradi hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la NACTVET, Prof. John Kondoro, alisema mafunzo haya yatawasaidia wamiliki na waendeshaji wa vyuo kufahamu sheria ,kanuni na taratibu za NACTVET katika kurekebu mafunzo ya ufundi stadi nchini pamoja na matarajio ya NACTVET kwa vyuo baada ya mafunzo haya.

Watumishi wa NACTVET wakiongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Adolf Rutayuga wameshiriki katika kutoa mafunzo hayo kulingana na idara pamoja na kurugenzi mbalimbali zilizo chini ya NACTVET. Miongoni mwao ni pamoja na Dkt. Alex Nkondola, Dkt. Amani Makota, Dkt, Jofrey Oleke na wakuu wa kanda husika - Dkt. Annastella Sigwejo (Mashariki), Dkt.Godfrey Komba (Kaskazini) na Bw. Ramadhani Samainda (Kati).
Share:

MUSUKUMA AKANA TUHUMA ZA KUHONGWA GARI



Na Dotto Kwilasa,DODOMA.

 

MBUNGE wa Geita vijijini Joseph Musukuma ameishauri Serikali kuona haja ya kuwa na utaratibu wa kuwapeleka Waandishi wa habari kushuhudia hali na mfumo wa miradi mbalimbali inayoanzishwa nchini ili kuwa na uhalisia wa hali ilivyo na kusaidia kupeleka taarifa sahihi kwa jamii zisizoweza kuzua taharuki.


Ameyasema hayo jijini hapa Leo June 9 aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uvumi ulioshika kasi hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa bandari hiyo imeuzwa na wengine wakisema imekodishwa kwa mkataba wa miaka100.


Amesema,"Kama serikali iliweza kutupeleka wabunge basi ione haja pia kuwapeleka waandishi zaidi ya 100 kushuhudia hali ilivyo mbaya bandarini,"amesema


Kuhusu kuhusishwa kwenye mpango wa kupewa gari na Kampuni ya Dubai ili mambo yaende Mbunge huyo amesema,"Mimi sijahongwa,Nina mali zangu na hata hiyo gari wanayosema nimehongwa nimenunua mwenyewe na vielelezo vipo,Mimi sio kama wao,"amefafanua.


Pia amewataka Watanzania kutoyumbwisha na maneno ya watu wasioitakia mema nchi bali waunge mkono jidihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uwekezaji mkubwa wa bandari ya Dar es salaam ambao utakuwa na tija kwa wafanyabiashara nadi na nje ya nchi.

 

"Mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, uwekezaji unaofanywa na serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia utasaidia sisi wafanyabiashara kutuondolea malalamiko ya kucheleweshewa kupata mizigo yetu kwenye bandarini"amesema Musukuma

 

Akieleza hali iliyopo sasa katika bandari kwenye upokeaji wa mizigo Mbunge huyo amesema hali ni mbaya mizigo inachukua muda mrefu na inasababisha wafanyabiashara wengi kuagiza mizigo kupitia bandari nyingine ikiwemo bandari ya Mombasa.

 

"Rais ni taasisi siyo mtu mmoja inawatu wengi sio kwamba wanavyozungumza mitandaoni hakuna tafiti zilizofanyika, Ikulu imefanya utafiti na sisi wabunge baadhi tulienda kuona na kuona ni kuamini, na sio wanaozungumza mitandaoni wanauwezo mkubwa sana sio kweli unaweza uakawa na uwezo mukubwa wa kuzungumza mitandaoni lakini hujui,"amesema 

 

Vile vile aliwataka watanzania kuunga mkono azimio hilo na kama kunamapunguvu yatasimama kwenye mkataba kwani kwa sasa kinachojadiliwani ni makubaliano ya nchi na nchi na hakuna aliyeuona mkataba huo.

 

"Nawahakikishia watanzania maneno yanayoandikwa kwenye mitandao sio ya kweli kwasababu hata Rais Samia atastaafu na yeye ataishi maisha kama ya kwetu si kweli kama ataenda kusaini mkataba ambao hauna maslahi kwa Taifa hili labda yeye kama iwe akistaafu anahama Tanzania lakini hapana tusikatishane tamaa,"amesisitiza 

 

Hata hivyo ameeleza watanzania wamekuwa na tabia ya kuzusha taarifa za uongo na kueleza kuwa  hakuna mkataba wa kimkakati ambao umewahi kufanyika kwenye awamu zote bila kuwa na kelele na kelele ambazo zinatengenezwa na watu wasiiitakia mema nchi .

 

"Hata kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Rais Magufuli, alipotaka kuanza ujenzi wa bwawa la kufua umeme Rufiji wapo waliopiga kelele lakini serikali haikukatishwa tamaa,wakati ule watu walipiga sana kelele kuliko hata hizi lakini Magufuli alijenga bwawa la Rifiji na hivisasa bwawa hilohilo watu wanaliombea kura wakati wa uchaguzi,"amesema.



Share:

DITOPILE AWAONYA WANASIASA WANAOHUBIRI UBAGUZI, CHUKI SAKATA LA BANDARI





Na Mwandishi Wetu


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewashukia wanasiasa wanaotaka kuwagawa Watanzania wanapojadili suala la makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari kadhaa nchini ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.

Ditopile amesema, miaka miwili ya utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan umeonesha mafanikio makubwa kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Mbunge huyo amesema hayo kipindi ambacho kuna mjadala unaendelea wa ushirikiano huo kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiujadili kwa misingi wa u-Tanzania Bara na Uzanzibar.

Kutokana na hilo, Ditopile ameibuka akisema,

"Natoa rai kwa wanasiasa wote nchini wanaojadili suala hili la bandari kuepuka kutumia maneno yenye kuibua hisia za ubaguzi, chuki na kuhatarisha amani na mshikamano wetu kama Taifa."

"Ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tumeshuhudia uzalendo wake, nia yake njema kwa Taifa hili na namna anapambana kwa maslahi ya nchi yetu, wanasiasa ni vyema kuweka siasa pembeni tukamuunga mkono Rais Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo."

"Wote ni mashahidi kazi kubwa na nzuri inafanyika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika uwazi wa mikataba na mashirikiano mbalimbali, tunaingia kama Taifa na yote inapitia bungeni kuonyesha nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema na kuongeza" alisema Ditopile na kuongeza 

"Tupuuze propaganda chafu, siasa za uongo, ubaguzi na fitina. Tusimame pamoja na Rais Samia katika kusimamia maslahi mapana ya nchi yetu. Natoa Rai kwa Watanzania kuwapuuza wanasiasa wanaohubiri siasa za kibaguzi na chuki."

Share:

GOD OF COINS SLOTI PENDWA DUNIANI

 

Bajeti ya kuhakikisha maokoto yako ya kila siku yanaongezeka huwa ni ngumu kidogo, kuna muda maokoto yanapotea lakini kama umejiunga na familia ya Meridianbet katika chimbo lake la Kasino ya mtandaoni, maokoto huwezi kuyakosa hata kidogo.


Meridianbet kasino ya mtandaoni ni moja ya chimbo la madini ya pesa kama ilivyo kwa mgodi wa Geita, Buzwagi kule Kahama, kila unapocheza kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti kama God of Coins inakuhakikishia unapata mtonyo kwa urahisi na zawadi kibao.

Sloti ya God of Coins inawalenga wapenzi kindakindaki wa historia ya kale, kasino ya mtandaoni hii inawasafirisha wachezaji wake hadi ulimwengu wa Misri ya kale kupitia picha zake za kuvutia na nyimbo zinazoendana na zama za enzi hizo.

Ikiwa na mpangilio maalum wa mistari ya 4x5, God of Coins Sloti ina ishara za alama 8 ikiwa ni pamoja na alama ya WILD. Katika mistari 20 ya malipo una uwezo wa kushinda mpaka mara 1000 ya dau lako katika kila mzunguko, mchezo huu unawafanya wachezaji kufurahia na kucheza kwa muda mrefu bila kuchoka. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet sasa!

Kwa kuzingatia teknolojia ya kasino ya mtandaoni duniani Meridianbet na Expanse studio wamehakikisha umakini mkubwa katika kila nyanja ya mchezo ikiwemo picha maridhawa, michoro, sauti na ufundi wa uchezaji wa sloti ya God of Coins.

Mashabiki wa historia ya kale na michezo ya zamani ya kasino ya mtandaoni, God of Coins ni chaguo sahihi kwao na mahali pekee kufurahia ladha halisi ya kasino ya mtandaoni, mizunguko ya bure na ofa mbalimbali ni Meridianbet. 


Share:

JINSI TABIA YA WIZI NILIVYOIKOMESHA

Kila kanisa lililosifiwa, kila mchungaji au mhubiri mpya aliyeibuka na kuwateka watu nilienda kwake kuombewa ili nifunguliwe lakini maombi yake yaligonga mwamba na kunirudia. Nimesafiri mpaka nje ya nchi kuwafuata manabii lakini bado sikuacha wizi.


Nilikuwa nimechoka kuiba nikataka kuishi maisha ya kawaida kama wanadamu wenzangu. Siku moja tulienda Mwananyamala kuiba kwenye duka la Mpemba. Tulipokuwa tunatoka, suruali ya mwenzangu ikanasa kwenye misumari ya ukuta, akashikwa na kuchomwa moto.


Kwa kuwa niliruka ukuta kabla yake, hakuna aliyenigundua kuwa nilikuwa mwenzake. Kuanzia siku hiyo rafiki yangu akawa ananijia ndotoni na kuniambia anaungua huko aliko. Akawa ananisisitizia niache wizi lakini hata nikiona majirani wameshau vijiko tu navipitia na kuvihamishia kwangu.


Mjomba wangu anayeishi Congo aliniambia kuwa alikuwa akiishi na daktari BAKONGWA na aliahidi kunisaidia kama ningekiri kuwa sikutaka tena wizi. Nikamhakikishia, akaniunganisha na daktari na baada ya kutumia dawa yake kwa wiki tu wizi ukaondoka bila kufukuzwa.

Sikuamini sana yale aliyosema kwa kuwa nilikwisha zunguka na kutembea kila kona ya huko aliko kiongozi bora wa ibada kwa kusali toba lakini tabia hii haikukoma kwangu.

Niliandikiwa nambari za whatsapp za daktari +243990627777 na tovuti zake pia https://bakongwadoctors.com kusudi nimtafute.Sikusita nikafaya hivyo kwani tabia ile ilikuwa imenichosha na ni sugu iliyodumu kwa muda wa miaka kumi namoja.

Daktari alinijibu na kunipa maelekezo ya tiba ambayo ingeniondoa mara moja kwenye tabia hizo huko akisisitiza kuwa awa ile ni ya masaa ishirini na nne, baada ya kutumia tu sikuwahi kujisikia vile nilivyokuwa mara zote nilipoona mali ya mtu imezagaa bila ulinzi .Asante sana daktaei kwa tiba nzuri nay a muda mfupi.

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 9,2023




















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger