Monday, 10 April 2023

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE WA YANGA KWA IHEFU


Na Alex Sonna

SIMBA SC wameendelea kuitafuta Yanga SC katika mbio za Ubingwa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Ihefu mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Highland Estates jijini Mbeya .

Mabao ya Simba yamefungwa na Mshambuliaji hatari Jean Baleke dakika ya 83 na 87 na kuvunja mwiko wa Ihefu wa kuendelea kuzifunga timu kubwa katika uwanja wao ambapo Yanga na Azam zote zilipata kichapo huku Singida Big stars ikiambulia sare.

Kwa Matokeo hayo Simba SC imefikisha Pointi 60 ikiwa imecheza mechi 25 huku Yanga SC bado anaongoza Ligi akiwa na Pointi 65 akiwa amecheza mechi 24.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Yanga SC itakuwa kibaruani kucheza na Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera mchezo utakaopigwa uwanja wa Chamazi Complex Azam majira ya saa moja usiku.
Share:

JK APONGEZA KASI YA UKUAJI NBC,AHAMASISHA UTOAJI WA MIKOPO ZAIDI


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kulia) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Edward Mpogolo (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo . Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipata chakula kwenye hafla hiyo.
Hafla hiyo iliambatana na Dua maalum kutoka kwa viongozi wa dini.

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amepongeza kasi ya ukuaji wa benki ya Taifa ya Biashara (NBC) huku akiihamasisha benki hiyo iendelee kutoa mikopo zaidi ili kuchochea ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara na kilimo.


Akizungumza kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dkt Kikwete pamoja na kuipongeza benki hiyo kuwa karibu na wateja wake, alionyesha kuridhishwa na uimara wa taasisi za fedha nchini kwasasa huku akitolea mfano benki hiyo ya NBC inayomiliki mali (Assets) zenye thamani ya TZS 1.52 trilioni na amana (Deposits) zenye thamani ya TZS 1.96 trilioni.

“Mnapoandaa matukio kama haya mnaongeza imani kwa wateja wenu kwa kuwa mnathibitisha namna mlivyo nao pamoja. Hata hivyo nafarijika pia kuona mnaendelea kufanya vizuri kiutendaji kwa maana idadi ya matawi yenu inaongezeka sambamba na idadi ya mawakala wenu ambao kwasasa wamefika 9,430 nchini nzima. Mmeendelea kubuni huduma zinazowagusa wananchi wa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wakulima hongereni sana,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Dkt Kikwete uimara wa taasisi za fedha nchini kwasasa utasaidia zaidi ukuaji wa uchumi kwa kuwa wawekezaji kwenye sekta ya biashara na kilimo wanategemea zaidi taasisi hizo ili kufanikisha uendeshaji wa miradi yao.

“Hakuna uchumi bila uwekezaji kama ambavyo pia hakuna uwekezaji bila mikopo ya uhakika kutoka taasisi za kifedha. Nawasihi sana benki ya NBC na taasisi nyingine za kifedha muendelee kuwa karibu na wawekezaji kwa faida ya ukuaji wenu kama wakopeshaji, pia na kwa faida ya wawekezaji wenyewe, jamii pamoja na serikali kwa ujumla,’’ alisisitiza.

Awali akizungumzia hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi, alisema ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa miaka 9 sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

“Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo.” Alisema Sabi.

Zaidi alibainisha kuwa benki hiyo ina huduma maalum inayojikita katika kutoa huduma kwa wateja wake wa imani ya Kiislam, yaani Islamic Banking inayopatikana kwenye matawi yote ya benki hiyo ikiendeshwa katika misingi ya dini hiyo ikiwa na huduma mbalimbali ikiwemo akaunti ya La Riba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Amosi Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Edward Mpogolo aliipongeza benki hiyo kwa mchango wake katika kuinua uchumi wa mkoa huo kwa kuwa karibu zaidi na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara pamoja na program zake mbalimbali za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

“Kama mkoa tunafurahishwa zaidi kuona kwamba taasisi za fedha zinaheshimu imani za kidini za wateja wao sambamba na kuwa karibu zaidi na viongozi wa dini. Matunda na hatua hii ni pamoja na amani ambayo ndio msingi wa ustawi wa biashara na uchumi,’’ alisema Mpogolo.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Share:

KARIBU PEACEFUL K HOTEL SHINYANGA MJINI....HUDUMA BORA KABISA!


Karibu Peaceful K Hotel kwa huduma bora za Chakula & Vinywaji, Malazi,Ukumbi wa mikutano, vikao, sherehe n.k. Pia WiFi Bure!

Peaceful K Hotel ipo Mjini ShinyangaNdembezi ya Balina karibu na soko la Milunda

Wasiliana nasi 0699389570 au 0756730303






Share:

MWENYEKITI AUAWA BAADA YA KUNASWA NA MKE WA MTU MADAI WAKIELEKEA GESTI KUPAKUA ASALI

 

Na Daniel Limbe,Chato


WAKATI waumini wa dini ya kikristo duniani kote wakiendelea kusherehekea Sikukuu ya Pasaka,  wilayani Chato mkoa wa Geita kumetokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabazengi, kata ya Muungano,Robert Msodock, baada ya kukutwa akiwa na mke wa mtu.

Imedaiwa kuwa chanzo Marehemu kuuawa ni wivu wa mapenzi, baada ya John Mbonge kumfumania akiwa na mke wake jana kwa kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakielekea nyumba ya kulala wageni kwenye kijiji cha Itale Branchi (Kahumo).

Habari zinasema kuwa marehemu amekuwa akifanya uzinifu na mke wa mtu tangu mwaka 2018 na kwamba kabla ya umauti huo tayari alikuwa ameshafumaniwa mara mbili.

Imedaiwa kuwa pamoja na fumanizi hizo,alikuwa akilipa faini ya fedha ikiwa ni adhabu ya kushiriki tendo la ndoa na mke wa mtu.

Katibu wa ulinzi wa Jadi, (Sungusungu) kijiji cha Itale Stoo, Enos Joseph,anakiri kuwa marehemu amekuwa akifumaniwa mara kwa mara na kwamba fumanizi lililosababisha kifo chake ni la awamu ya tatu.

"Ni kweli marehemu ameshafumaniwa mara mbili na hili tukio ni la tatu, baada ya kupewa taarifa za kuwa amefumaniwa jana, mimi na viongozi wenzangu wa sungusungu tulikwenda eneo la tukio kwaajili ya kumkamata, tulipofika pale tulimkuta amelala chini akiwa hai lakini hali yake ilikuwa mbaya sana,nilimuuliza kama ananijua akajibu ndiyo wewe ni Eno.

"Baada ya kunitaja jina nilimuuliza imekuwaje? akaniambia kutongoza wake za watu ndiyo imenifanya kuwa hivi, nikamuuliza tena simu yako iko wapi akasema John ndiyo kaichukua baada ya kunikatakata na mapanga, baada ya maneno hayo hakuongea tena tukamchukua na kumkimbiza hospitali ya wilaya ya Chato kwa matibabu"amesema Joseph.

Amesema wakiwa hospitalini hapo muuguzi aliyewapokea alimpima mgonjwa wao kisha kuwajulisha kuwa ameshafariki dunia baadae akapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Mwenyekiti wa kijiji cha Itale Stoo, Njingo Lubinza, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku akidai limetokea akiwa safarini.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, ACP Safia Jongoamekiri kuwepo kwa tukio la mwenyekiti huyo kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kukutwa akiwa amesimama na mke wa mtu, huku akidai hajapewa taarifa za kifo cha majeruhi huyo.


"Nilipewa taarifa za mwenyekiti huyo kujeruhiwa vibaya upande wa paja la kulia,mkono na kichwani kutokana na wivu wa mapenzi na kwamba hali yake ilikuwa mbaya, taarifa za kuwa ameshafariki hizo nilikuwa bado sijatumiwa", amesema Jongo.

 Hata hivyo amesema kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alikimbia baada ya kutenda kosa hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.

Share:

RAIS SAMIA APONGEZWA KUCHUKUA HATUA RIPOTI YA CAG

Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan amemwagiwa sifa na wananchi na viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kushughulikia uzembe na ubadhirifu wa pesa za umma uliobainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu Jumapili, Rais Samia alivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli la Tanzania (TRC) na kutengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandishi John Nzulule.


Aidha, Rais Samia amemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wote wa wizara pamoja na Watendaji Wakuu wa taasisi za serikali kusoma ripoti zote za CAG za mwaka wa fedha 2021/22 zilizotolewa hadharani Aprili 6 mwaka huu, kujibu na kuzifanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa.


"Watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria," imeeleza sehemu ya taarifa ya Ikulu.


Hatua hizo za Rais Samia zimeibua shangwe za wananchi nchini Tanzania na hata kuwagusa wananchi wa nchi za jirani za Kenya na Uganda ambao wametoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.


"Natamani huyu Mama (Rais Samia) angekuwa Rais wetu, Kenya tungekuwa sawa sana," alisema raia wa Kenya, Jibril Ndiema, kupitia Twitter.


Wananchi kadhaa wa Uganda na Kenya walitoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii wameweka bayana shauku yao ya kuwa na Rais kama Samia ambaye anachukua hatua za hadharaka na madhubuti dhidi ya tuhuma za ufisadi serikalini.


"Ikulu ya Kenya tunawaomba tafadhali mchukue hatua kama hizi za (Rais Samia) kwa Shirika la Ndege la Kenya," alisema Donald Omoro, raia wa Kenya, kupitia akaunti yake ya Twitter ya @DonaldKOmoro1.


Naye Farhiya Abass, mfanyabiashara anayeishi Mombassa, Kenya, alisema kupitia akaunti yake ya Twitter @farhiyaabass kuwa:"Mama Suluhu hana mchezo kabisa."


John Luke Tambiti, Mkurugenzi Mtendaji, wa taasisi isiyo ya kiserikali ya INUA Initiative Uganda, naye alitoa sifa kwa Rais Samia kuonesha uongozi mahiri kwa kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma waliohusika na uzembe na ubadhirifu kwenye ripoti ya CAG.


"Kwa Uganda, kwetu hii ni ndoto tu (kupata Rais anayechukua hatua dhidi ya ufisadi). Huku kwetu wezi ndiyo kwanza wanazawadiwa nafasi kubwa zaidi," alisema kupitia akaunti yake ya Twitter ya @LukeTambiti.


Hapa nyumbani, wananchi wa sehemu mbalimbali nchini nao wameonesha hisia zao za kuvutiwa na hatua za Rais Samia kuagiza ripoti ya CAG ifanyiwe kazi kikamilifu na makatibu wakuu na watendaji wengine wa serikali.


"Kwa kweli Rais Samia amejibu kilio chetu wananchi cha kutaka kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya watumishi wa umma wachache wanaofuja pesa za umma. Tungependa tuone wabadhirifu wote wanafukuzwa kazi na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma dhidi yao," alisema Francis Mwenegoha, mwanafunzi wa chuo anayeishi Morogoro.


Naye Shomari Msabaha, fundi ujenzi wa Dar es Salaam, amemtaka Rais Samia kutorudi nyuma katika mapambano dhidi ya ufisadi.


"Sisi wananchi wa Dar es Salaam tunaunga mkono juhudi za Rais Samia kupambana na ufisadi na tunamtaka asonge mbele, tuko naye bega kwa bega kwenye vita hii," alisema.


Asha Bakari, Mama Lishe wa mkoa wa Mwanza, alimuomba Rais Samia awadhibiti maafisa wa Manispaa na Halmashauri za miji na wilaya ambao wanafanya ubadhirifu kwenye pesa za kuwakopesha vikundi vya kina mama.


"Serikali kila mwaka inatoa pesa kwa ajili ya kutukopesha sisi kina mama wa hali ya chini kupitia vikundi vyetu, lakini pesa hizi zimekuwa zinaliwa na maafisa wa umma wasio waaminifu na hazifiki kwetu. Tunamuomba Rais Samia akomeshe huu ubadhirifu," aliongeza.

Share:

ABIRIA AFARIKI AKISUBIRI NDEGE UWANJANI

Polisi wanachunguza kifo cha abiria mmoja ambaye mwili wake ulipatikana eneo la kusubiri ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa akielea Mombasa usiku wa Jumamosi - Aprili 8,2023 na alikuwa amemaliza taratibu zote yarau kuabiri lakini akakosa kuelekea kwa ndege inavyohitajika. 

Wahudumu wa shirika la ndege la Jambojet waliita jina lake mara kadhaa wakimuomba kuabiri lakini hilo halikufua dafu, maafisa hao wamesema. 

Mwanaume huyo alikuwa ameketi kwenye moja ya viti katika eneo la kusubiri na aliaga dunia akiwa ameshika begi lake mkononi, kwa mujibu wa ripoti ya polisi.

Baada ya kubainika kuwa alikuwa hasongi katika kiti hicho, wahudumu wa afya wa ndege hiyo waliitwa kumhudumia na kubaini kuwa alikuwa ameaga dunia. 

Polisi wangali kubaini chanzo cha kifo hicho lakini walitaariu familia ya mwendazake huku uchunguzi ukiendelea.

 Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti unakotarajiwa kufanyiwa upasuaji na kupiga jeki uchunguzi wa polisi.

Via Tuko News
Share:

Sunday, 9 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 10, 2023































Share:

RAIS SAMIA AVUNJA BODI YA SHIRIKA LA RELI TANZANIA 'TRC', AMLA KICHWA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI





Share:

CAG AFICHUA SERIKALI YA MAGUFULI ILIVYOLISABABISHIA TAIFA HASARA YA SH 1.7 TRILIONI MRADI WA SGR


👉Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

 👉Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa 
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara 
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia 
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa 
kodi.
Share:

TANZANIA IS SAFE FOR TOURISTS





Share:

KAMA RIPOTI YA CAG NI NZURI, RAIS NI MZURI



Na Mwandishi Wetu

MJADALA wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) unaoendelea baada ya kuwasilishwa kwake bungeni Dodoma wiki hii, umeacha nje jambo moja – nafasi na umuhimu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye jambo hilo.

Ni rahisi kuelewa kwa nini macho na masikio ya wengi yataelekezwa kwenye taarifa kuhusu kinachoonekana kama matumizi mabaya na upotevu mkubwa wa mali ya umma yaliyomo kwenye ripoti hiyo. Mara nyingi taarifa ya CAG huumiza na kukera wengi. 

Wakati akipokea taarifa hiyo ya CAG wiki mbili zilizopita, Rais Samia hakutofautiana na wengi na – kwa kuonyesha namna alivyokerwa na yaliyomo, alitumia lugha kali ambayo Watanzania hawajazoea kumsikia akizungumza hadharani.

Lakini huo ni upande mmoja wa shilingi. Upande wa pili wa shilingi ni kwamba kama Rais Samia angetaka kuficha madudu yaliyomo serikalini kwake, angeweza kufanya hivyo kama ilivyo kwa viongozi wengine wa Kiafrika na duniani wasiopenda dhana ya uwajibikaji ndani ya serikali zao.

Katika dunia ya sasa, desturi kwa viongozi wakubwa wa dunia ni kuingia madarakani kihalali na kuanza kupambana na vyombo na taasisi zinazoweza kubana mamlaka ya watawala au kuibua uozo uliomo serikalini na kwenye maisha ya watawala.

Njia wanazotumia viongozi wengi ni kuviondolea uhalali vyombo na watu waliojitolea kupambana na uozo, kuvipunguzia bajeti ili visitimize majukumu yake na wakati mwingine kuvifuta kabisa.

Mdhibiti Mkuu kwenye Siasa za Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni taasisi ambayo iko kikatiba. Hata hivyo, katika miaka walau 40 ya kwanza ya Uhuru, nafasi ya CAG (ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa NAOT), haikuwa na umaarufu wala ushawishi ilionao sasa.CAG wa kwanza Mzalendo, Mohamed Aboud, alidumu kwenye nafasi hiyo kuanzia mwaka 1969 hadi 1996. Alifuatiwa na Thomas Kiama aliyeanza mwaka 1996 hadi alipostaafu mwaka 2005.Ofisi hiyo ilianza kubadilika mwaka 2005 wakati alipoingia Ludovick Utouh. 

Ukizungumza na Watanzania wengi, utadhani kwamba Utouh ndiye alikuwa CAG wa kwanza hapa nchini. Hata hivyo, Utouh alikuwa vile alivyokuwa kwa sababu moja tu; Jakaya Kikwete.Rais Kikwete ndiye aliyeibadili ofisi ya NAOT kisheria na kimajukumu kufanya inachofanya sasa. 

Aliongeza bajeti kubwa iliyofanya ofisi hiyo kuongeza idadi ya wafanyakazi na utaalamu kiasi kwamba kufikia mwishoni mwa utawala wake, ofisi hiyo ilipewa kazi ya kukagua vitabu vya hesabu vya Umoja wa Mataifa (UN).

Isingewezekana kwa CAG Utouh kufanya yote aliyofanya bila Kikwete.

Kama Rais huyo wa nne wa Tanzania asingetaka, NAOT ingeweza tu kuendelea na shughuli zake kama ilivyozoea au kama ilivyo kwenye nchi nyingi za kiafrika ambako haina meno.

Kama kulikuwa na migogoro yoyote baina ya Utouh na Serikali ya Kikwete hatukuwahi kuisikia.

Tulichokuwa tunasikia ni kuwa bajeti ya CAG ilikuwa inaongezeka kila mwaka na majukumu ya kikaguzi kuongezeka ndani na nje ya nchi.

Alipoingia madarakani hayati Rais John Magufuli, kulikuwa na migongano ya wazi baina yake na Profesa Mussa Assad aliyechukua nafasi ya Utouh baada ya kustaafu kwake. 

Miaka mitatu tu baada ya kuingia madarakani, bajeti ya CAG ilikatwa kutoka shilingi bilioni 69.1 mpaka shilingi bilioni 61.4. 

Mafunzo zaidi kwa watumishi wa ofisi hiyo yakaanza kuadimika na mawanda ya ukaguzi yakapunguzwa. 

Hali ikawa mbaya kiasi kwamba ikafikia wakati Bunge likakataa kufanya kazi naye – pengine kwa maelekezo ya Mkuu wa Nchi na mwishowe Assad akaondolewa kwenye wadhifa huo kinyume cha taratibu. 

Kama kuna funzo moja la kudumu kwenye historia ya Tanzania ni kwamba uimara na uhuru wa CAG kwenye kutimiza majukumu yake unaendana moja kwa moja na Rais aliye madarakani. Kama Rais anataka ripoti ya CAG iwe imara na thabiti, ripoti ya CAG itakuwa imara na yenye weledi.

Rais Samia na CAG

Wakati Rais Samia anaingia madarakani mwaka 2021, nchi ilikuwa inapita katika kipindi kigumu kiuchumi kutokana na athari za ugonjwa wa Uviko-19 uliosababisha kuyumba kwa uchumi wa dunia.

Pamoja na hayo, miongoni mwa hatua za awali alizochukua – katika mazingira hayo magumu, ilikuwa ni kuongeza bajeti ya ofisi ya CAG kutoka shilingi bilioni 80 alizokuta hadi bilioni 80.9. 

Zaidi ya hapo, tangu siku yake ya kwanza madarakani, Rais amekuwa akitoa ujumbe wa mara kwa mara wa kutaka taasisi za uwajibikaji na zile za utoaji haki kutimiza majukumu yao waliyopewa kikatiba.

Kwa kufanya hivyo, alikuwa anamtia moyo CAG Charles Kicheere, kuwa anachotakiwa kufanya ni kutimiza wajibu wake. 

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takribani miaka minne iliyopita, CAG aliruhusiwa kufanya ukaguzi katika maeneo kama ya manunuzi ya ndege za serikali ambayo yalikuwa ‘kaa la moto’ kuyajadili wakati wa zama za mtangulizi wake.

Kwa sababu ya kuwepo kwa uhuru wa kutosha wa wanasiasa, wanaharakati, wabunge na waandishi wa habari, ina maana ripoti ya CAG ya safari hii itakuwa na mwangwi mkubwa pengine kuliko ilivyokuwa miaka michache nyuma.

Lakini Watanzania sasa wanajua kwamba haya yote ni matunda ya utawala wa Rais Samia. 

Kama angeamua kufuata nyayo za mtangulizi wake, tungesikia na kujadili yale tu ambayo watawala wangetaka tuyasikie na kuyajadili. 

Kama tunasikia vitendo vya ubadhirifu na ufisadi, maana yake ni kwamba Rais Samia anataka kujua wapi panapovuja ili hatua zichukuliwe. 

Hata hivyo, ni hatari sana kumlazimisha Rais aanze kuchukua hatua tu kwa sababu amekerwa na alichokisoma na kuambiwa.

Ili tusirudi tulikotoka na kumfanya Rais abaki kuvipa nguvu vyombo vyake, ni muhimu mchakato na taratibu za kihasibu na kisheria kufuatwa ili kwamba kama mtu atakutwa na hatia, aadhibiwe baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchunguzi.

Wale wote wanaotaka Rais achukue hatua za papo kwa papo sasa hivi bila ya uchunguzi wa makini kwa sababu ya ripoti hii, hawaitakii mema nchi yetu.

Tunataka Rais ambaye anachukua hatua kwa kufuata katiba, sheria, kanuni na utaratibu (due process) baada ya uchunguzi kukamilika na hakuna anayeonewa. 

Wafanyakazi wa NAOT ni wanadamu na hivyo wanaweza kukosea hapa na pale.

Kama tunataka Rais wetu apate kile anachokitaka kutoka kwenye ripoti hizi na sisi wananchi tuendelee kuwa salama kwa sababu ya kuwa na Mkuu wa Nchi anayependa kufuatwa kwa taratibu zote, ni muhimu kuacha michakato iende mpaka mwisho.

Lakini katika yote, tusisahau jambo moja katika mijadala yetu, kwamba kama tumefurahi kuwa ripoti ya CAG imeshiba taarifa na inatoa picha halisi ya mahali tulipo kwenye uwajibikaji wa mali ya umma, tujue kwamba kuna mkono wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hilo. 

Historia inatuonesha kuwa asili ya ripoti ya CAG ni kufichua madudu. Kwa vile watumishi wa umma ni wanadamu, jambo hilo halitabadilika. Kitakachobadilika ni Rais.

Kwa sababu hiyo, ni muhimu kutambua bahati tuliyonayo sasa ya kuwa na Rais anayetaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali atimize majukumu yake,.

Mwisho
Share:

Video Mpya : NELEMI MBASANDO ACHA KUNIZOEA

Share:

Ngoma Mpyaaa!! BHUDAGALA - GEREJI

 

Share:

Saturday, 8 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 9,2023

















Share:

AJIUA CHUMBANI AKIACHA MKEKA WA MADENI ANAYODAIWA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwanaume aitwaye Ally Hamis (48) amejiua kwa kujinyonga ndani ya nyumba yake katika kijiji cha Itwangi Wilaya ya Shinyanga huku akiacha ujumbe kuhusu madeni anayodaiwa ndugu zake wayalipe.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limebainika kutokea leo Jumamois Aprili 8,2023 majira ya asubuhi baada ya familia kumkuta Ally Hamis amejinyonga ndani ya nyumba yake.


Mwenyekiti wa kijiji cha Itwangi Kisendi Lubinza amesema Ally ameacha ujumbe kwa kuorodhesha madeni anayodaiwa na kuwaomba ndugu zake kulipa madeni hayo likiwemo deni la baskeli yake aliyokuwa anadaiwa sh 40,000/= , baba yake mdogo alipwe laki tatu na mwingine alipwe debe moja la mahindi.


"Kwenye wosia wake pia ameandika kwamba ‘nimeamua kujiua mimi mwenyewe asishikiliwe mtu yoyote nimeamua kwa moyo wangu, nimeamua kumfuata Mama yangu aliyetangulia mbele za haki miaka mingi iliyopita", ameeleza Mwenyekiti huyo wa kijiji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


“Ni kweli mtu huyo alijinyonga na akaacha ujumbe kuwa ana madeni kwa hiyo askari wameshaenda wakakagua eneo la tukio walikuwa na daktari mwili umefanyiwa uchunguzi na walikabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishu”, amesema Kamanda Magomi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger