Wednesday, 5 April 2023

LEAT WAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI KWA JAMII NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI WA KATA NA MABARAZA YA KATA GEITA

 

Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.

Na Marco Maduhu, GEITA

TIMU ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo    Lawyers Environment Action Team (LEAT), wameendelea na utoaji wa mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora, kwa Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita, ili kuwakumbusha katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu katika kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa Mazingira.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa kuanzia Aprili 3 ambayo yatakwenda hadi Aprili 7 mwaka huu ambayo yanafanyika mjini Geita.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkufunzi Hana Lupembe kutoka (LEAT)amewataka viongozi hao kila mmoja anapaswa kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu.

“Mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii ni dhana Shirikishi inayohusisha watoa huduma na wapokea huduma kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, na mfumo huu ukifuatwa vizuri kutakuwa na uwajibikaji kwa viongozi, kutoa huduma bora, kuwa waadilifu na wawazi,”amesema Lupembe.

Kwa upande wake Mkufunzi Valeria Macha kutoka (LEAT) akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo, amewataka viongozi hao wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kuzifuata sheria za uadilifu kwa umma katika kuwahudumia wananchi na kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa Mazingira.
Hana Lupembe kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.
Hana Lupembe kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.
Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.
Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.
Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa katika mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea ya Mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya kata Geita.

Washiriki wakiwasilisha kazi za vikundi.
Uwasilishaji kazi za vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi za vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi za vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi za vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi za vikundi ukiendelea.
Share:

KAMPUNI ZA UCHIMBAJI MADINI ZATAKIWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA JAMII



Na Mwandishi wetu,TABORA.

SERIKALI imezielekeza kampuni za uchimbaji madini kuhakikisha wanaendelea kushiriki  katika shughuli za kijamii ili kujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka maeneo ya migodi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tabora Mhandisi, Abel Madaha  wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu fursa mbalimbali zitokanazo na sekta ya madini katika Mkoa huo.

Amesema Tume ya Madini imepewa jukumu la kusimamia  sheria ya madini katika kifungu cha 22 na kuhakikisha sekta hiyo inatoa mchango wake katika pato la Taifa.

“Tunatoa wito kwa kampuni zote za  uchimbaji kuhakikisha  zinashiriki katika shughuli za kijamii kwa kurudisha faida ya mapato wanayopata ili kujenga mahusiano mazuri na Wananchi  wanaozunguka migodi,” amesema Madaha

Mhandisi Madaha pia amesisitiza kampuni za uchimbaji wa madini kuhakikisha zinatoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania wazawa ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka miundombinu wezeshi katika sekta ya madini hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi utokanao na sekta hiyo na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa hadi kufikia asilimia 9,"anasema.

Kwa upande wake Mratibu wa Miradi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya TAUR Tanzania Limited, Edith Moses amesema katika kuhakikisha wanatekeleza sheria ya madini tayari wamejenga madarasa mawili na vyoo katika shule ya Msingi na Sekondari Nanga iliyopo Wilaya ya Igunga.

Naye Mwendesha mitambo wa Kampuni ya TAUR Tanzania amesema uwepo wa machimbo umesaidia kutoa ajira kwa vijana wengi ambapo sasa wanapata fedha ambazo zinawasaidia kuhudumia familia zao.

“Tunaishukuru Tume ya Madini kwa kusimamia sheria mbalimbali zilizowekwa katika maeneo ya machimbo ambapo sasa usalama unazingatiwa na vijana wengi wazawa wameajiriwa.
Share:

Tuesday, 4 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 5,2023















Share:

TSH MILIONI 5 ZA MERIDIANBET KASINO YA MTADAONI KUTOKA WIKI HII

 

Aprili ya Kishua unaambiwaje jisajili Meridianbet upate mizunguko 50 ya bure kucheza sloti ya kasino ya mtandaoni. Kujisajili bonyeza hapa: https://a.meridianbet.co.tz/c/0aIpIo

 

 

Promosheni Kabambe ya Endorphina

 

Ni kosa kubwa sana kwa kijana na mtu yeyote kukata tamaa katika Maisha haswa kwenye harakati za utafutaji wa riziki. Meridianbet Kasino ya mtandaoni inakupa nafasi nyingine ya kuusaka utajiri ni kupitia promosheni mpya ya Endorphina, ubashiri wa soka, bonasi kibao na michezo ya sloti kama Aviator, Poker na Roulette.

 

Kutoka Kasino ya Mtandaoni pekee ya Meridianbet kuanzia April 3 mpaka April 10 mwaka huu, kuna promosheni mpya na maalum kwako joka la kucheza sloti za michezo ya kasino ya mtandaoni. Cheza mchezo wowote uliochaguliwa wa Endorphina na ufurahie hali ya kusisimua itakayokupa mkwanja mrefu.

 

Sloti za Endorphina zilizopo ni kama Football 2022 yaani unacheza soka kama upo uwanjani vile au kwenye PS4, Chance machine 20, Book of Santa, Book stoker, Story of Xmass, 100 Zombies, The Vampires II, Book of Vlad, The Emirates II, Fisher King, Solar Eclipse ama kupatwa kwa jua na mingine mingi.

 

April ya kishua unaweza kuwa mshua kwa sababu, una nafasi ya kujishindia mgao wako wa zawadi kabambe ya TSH Milioni 5,000,000 kutoka kwenye droo ya zawadi yenye sloti rahisi kushinda.

 

Washindi wanapatikanaje?

 

Mwisho wa shindano, wachezaji wataorodheshwa kulingana na idadi ya mizunguko waliyocheza, na wachezaji 15 wa kwanza watajishindia zawadi kama ifuatavyo:

 

Nafasi ya 1: TSH 1,200,000

Nafasi ya 2: TSH 880,000

Nafasi ya 3: TSH 630,000

Nafasi ya 4: na 5: TSH 380,000 kila mmoja

Nafasi ya 6: mpaka 10: TSH 200,000 kila mmoja

Nafasi ya 11: mpaka 15: TSH 100,000 kila mmoja

 

Si utani, mawindo yameanza! Saka utajiri na Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet.

 


Share:

WIZARA YA ARDHI YAFUTURISHA WATUMISHI WAKE

Na Munir Shemweta, WANMM


Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewafuturisha watumishi wake waliopo Wizarani na ofisi ya Kmishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Naibu wake Geofrey Pinda waliwaongoza viongozi wa wizara hiyo kujumuika na watumishi katika futari iliyofanyika tarehe 3 April 2023 jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa futari hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaeleza watumishi kuwa, uamuzi wa kuandaliwa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara hususan kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa rezma.

‘’Uamuzi wa kuandaa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara yetu na ninaomba tuwe na umoja na kushirikiana katika kazi zetu’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Geofrey Pinda alishukuru uamuzi wa Wizara kukutanisha pamoja watumishi kuanzia ngazi ya chini hadi juu jambo alilolieleza kuwa ni nadra sana kutokea watumishi kukutana kwa wakati mmoja kuanzia kada ya chini hadi juu.

‘’Nishukuru uamuzi wa kuwakutanisha watumishi wa sekta ya ardhi pamoja maana ni nadra sana watumishi wa wizara kuanzia kada za chini hadi juu kukutana kwa mara moja’’ alisema Pinda

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga alihimiza watumishi wa sekta ya ardhi kuwa na umoja wakati wote wa utendaji kazi.

Aidha, aliwaeleza watumishi wa wizara ya ardhi kuwa, wizara hiyo kwa sasa iko kwenye juhudi za kuboresha mifumo yake ya ulipaji kodi ya pango la ardhi ambapo alieleza kuwa mfumo huo utakapokamilika wamiliki wa ardhi nchini watakuwa wakipata ujumbe utakaowawezesha kulipa kodi bila kufika ofisi za ardhi.


Hii ni mara ya kwanza kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuandaa futari ya pamoja ya watumishi wake tangu serikali ilipohamia rasmi mkoani Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 3 April 2023. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera na katikati ni Kaimu Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Isabela Chilumba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga akiwaongoza watumishi wa wizara ya ardhi kupata futari ya pamoja jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Sehemu ya watumishi wa wizara ya ardhi wakipata futari ya pamoja tarehe 3 April 2023.






Watumishi wa Wizara ya Ardhi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara hiyo jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Methew Nhonge akitoa neon la shukran wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Share:

AUAWA KWA KUPIGWA JIWE AKINYWA POMBE BAA MJINI SHINYANGA, MWINGINE AKIIBA MAHINDI SHAMBANI


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Watu wawili wamefariki Dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea katika Manispaa ya Shinyanga likiwemo la mwanaume kuuawa akiiba mahindi shambani na mwingine kupigwa jiwe akiwa Baa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu amewataja watu hao kuwa ni Tumaini Manyele Malima mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga na mwanaume mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40 ambaye hakufahamika jina na makazi yake.




Amesema Tumaini Malima amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mwawaza baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa jiwe katika sikio la kushoto na Yohana Daniel akiwa Bar ya Heinken mjini Shinyanga wakiendelea kunywa pombe kisha kuanza kupigana.

Kaimu Kamanda Nyandahu amesema tukio la pili ni kuhusu mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 – 40 ambaye hakufahamika jina wala makazi yake ameuawa kwa kushambuliwa baada kukamatwa na wananchi kwa tuhuma za kuiba Mahindi mabichi shambani katika kijiji cha Mwamalili kilichopo Manispaa ya Shinyanga usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2023.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi matukio ya uhalifu yanapotokea.
Share:

DITOPILE AGAWA FUTARI KONDOA, ASISITIZA KUIOMBEA NCHI NA KUMUOMBEA RAIS SAMIA



Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amegawa Futari kwa Wazee, Wajane na watu wasio jiweza Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma.


"Kwa imani yetu miezi yote ni bora lakini mwezi mtukufu wa Ramadhani ni bora zaidi, na pia tunaambiwa katika mwezi huu dua yoyote utakayoiomba mbingu ziko wazi na Mwenyezi Mungu ametukumbusha kupitia suratul Insan aya ya 8 tuwafuturishe kile tunachokipenda"

Ameongeza kuwa huu ni utaratibu ambao anautumia mwezi huu mzima kuzunguka Mkoa wa Dodoma kufanya zoezi hilo.


"Nimetumia mwezi huu wa Ramadhani kuzunguka Mkoa wote wa Dodoma kufuturisha, nimeanza pale Dodoma mjini kwa kufuturu na yatima na wajane zaidi ya 300 na kisha kuwapa sadaka, nimeshafuturisha wilaya za Bahi, Kongwa na leo nipo Kondoa. Pale Kongwa nilienda kijiji cha Mkoka pamoja na futari na nilienda kutembelea shule ya watoto wenye uhitaji maalum, ambako wapo watoto wadogo wenye ulemavu lakini walikuwa wamefunga"


Pia Mbunge Ditopile amewaomba kuendelea kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



"Sisi ni viongozi mmetuamini lakini juu yetu yupo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama Samia amepewa majukumu ya kutuongoza na Mwenyezi Mungu, hata majukumu yake ya kifamilia ameyasahau kidogo na muda mwingi anahangaika na wananchi wa Kondoa, Kasulu na kila mahali nchini leo, anawaza leo nipeleke mradi wa maji wapi, leo nipeleke mradi wa umeme wapi ni na dhamira yake njema ya kuwatumikia Watanzania wapo ambao hawaipendi, hasad haikosekani katika jambo lolote linaloambatana na neema, ili hasad isimkute ni jukumu letu sote kumuombea kwa Mwenyezi Mungu"




Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger