Monday, 27 March 2023

LEAT WATOA MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI JAMII NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI WA KATA NA MABARAZA YA KATA BUTIAMA

 

Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) wakitoa mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Butiama.

Na Marco Maduhu, BUTIAMA

TIMU ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo, Lawyers Environment Action Team (LEAT), wametoa mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Machi 27, 2023 ambayo yatakwenda muda wa siku tano hadi Machi 31 mwaka huu, kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa mazingira.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Hana Lupembe kutoka (LEAT), amesema viongozi hao wakipewa elimu hiyo ya mfumo wa ufuatilijai wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora itawasaidia katika utendaji wao kazi kwa wananchi na kufanya vyema katika usimamizi wa Rasilimali za nchi na kuzuia uharibifu wa mazingira katika uchimbaji madini.

“Mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii ni dhana Shirikishi inayohusisha watoa huduma na wapokea huduma kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, na mfumo huu ukifuatwa vizuri kutakuwa na uwajibikaji kwa viongozi, kutoa huduma bora, kuwa waadilifu na wawazi,”amesema Lupembe.

Aidha, ametaja hatua tano za mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii kuwa ni Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa utendaji, usimamizi wa uadilifu, na usimamizi wa uangalizi.

Naye Valeria Macha kutoka (LEAT) amesema licha ya kutoa mafunzo ua utunzaji wa mazingira pia wanawajengea uwezo wananchi na viongozi wanaoishi katika maeneo ya uchimbaji wa madini kujua haki zao za msingi pamoja na kurudisha uoto wa asili baada ya uchimbaji na kuhamia eneo jingine ili kuzia uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake Afisa usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira wilaya ya Butiama Karani Ruhumbika, amewataka viongozi hao kila mmoja katika eneo lake awe na wajibu wa kutunza mazingira pamoja na wananchi kufanya uchimbaji wa madini uwe salama bila ya kuathiri mazingira.

Nao baadhi ya Watendaji wa Kata Wilaya ya Butiama ambao wanatoka kwenye maeneo ya uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu, wamesema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya uongozi wao na kuongeza uwajibikaji katika majukumu yao pamoja na kusimamia vyema rasilimali za taifa na utunzaji wa mazingira.
Mkufunzi wa mafunzo Hana Lupembe kutoka (LEAT) akitoa mafunzo hayo kwa Watendaji wa Kata na viongozi wa Mabaraza ya Kata kutoka wilaya ya Butiama.
Mkufunzi wa mafunzo Hana Lupembe kutoka (LEAT) akitoa mafunzo hayo kwa Watendaji wa Kata na viongozi wa Mabaraza ya Kata kutoka wilaya ya Butiama.
Valeria Macha kutoka (LEAT) akitoa mafunzo kwa viongozi hao Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Valeria Macha kutoka (LEAT) akitoa mafunzo kwa viongozi hao Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Afisa usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira wilaya ya Butiama Karani Ruhumbika akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilayani Butiama mkoani Mara.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Share:

NAMNA YA KUSHINDA KIRAHISI KASINO YA MTANDAONI MERIDIANBET



 

 Jisajili Meridianbet na upate mizunguko 50 ya bure ya kasino ya mtandaoni! Bonyeza hapa kujisajili https://a.meridianbet.co.tz/c/RGCCr7

 

Hakuna aliyezaliwa bila bahati hata wewe una una bahati kubwa leo ya kushinda mkwanja mrefu Meridianbet Kasino ya Mtandaoni, ni sloti ya Foxpot inakuja na ofay a kushinda mara 1000 ya dau lako unapocheza.

Fahamu Kuhusu Sloti ya Foxpot

Unaweza ukawaza ni wapi hela zinakotoka kwa jinsi ambavyo zinatiririka, usiwaze hiyo ni sloti ya kijanja ya Foxpot inakuja na mnyama Mbweha kama zawadi wa Wild lakini pia kasino hii ya mtandaoni inakuja na Magurudumu 12 ya ushindi na kushinda ni rahisi sana.

 

Unasubiri nini? ingia mchezoni kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet sasa na ufurahie ushindi kwa kupitia http://www.meridianbet.co.tz

 

Jinsi ya Kucheza Sloti ya Foxpot

 

Ni rahisi sana! Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na kuchagua mchezo huu wa Foxpot ujishindie mamilioni!

 

Sloti hii ya Foxpot ina alama na machaguo mbalimbali. Ili ushinde, unatakiwa upate alama tatu zenye kufanana kwenye sloti hii yenye kolamu 5 na mstari mmoja wa malipo.

 

Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ina machaguo mbalimbali ambayo yanakupa fursa ya wewe mchezaji kuucheza mchezo huu kiurahisi. Kwa kubofya alama ya + na – ambazo zipo kwenye kitufe cha Bet, itakupa nafasi ya kuweka dau lako unalolitaka.

 

Kuna chaguo la Autoplay ambalo litakuwezesha wewe (mchezaji) kuzungusha mizunguko kiatomatiki. Alama za sloti hii ni ya matunda ambayo ni Cherry ambalo lina thamani ndogo, Zambarau ambalo litakurudishia mara 1.5 ya dau lako huku likufuatiwa na Ndimu ambalo litakulipa mara 2.5 ya dau uliloliwaka.

 

Endapo utapa alama 1, 2 au 3 za Lucky 7 basi utalipwa mara tatu ya dau uliloliweka huku alama moja ya Lucky 7 ikiwa ina uwezo wa kukulipa mara 10 ya dau lako, na alama 2 mbili za Lucky 7 zikitakurudishia mara 15 wakati alama 3, zitakurudishia mara 25 ya dau lako. Sio hivyo tu, kama ukipata alama ya Wild utarudishiwa mara 40 ya dau lako. Kumbuka, alama ya Wild inauwezo wa kubadilisha alama zozote kwenye mchezo huu na kukupatia ushindi isipokuwa alama ya bonasi. Unasubiri nini? Jiunge leo na Meridianbet na upate bonasi babkubwa, Odds za kubwa na Jackpoti kedekede kwa kutembelea tovuti yetu http://www.meridianbet.co.tz sasa!


Share:

WAZIRI JAFO PAMOJA NA NAIBU WAZIRI CHILO WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUPANDA MITI KITAIFA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Naibu Waziri Mhe. Khamis Hamza Khamis wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti kitaifa kwa hisani ya Benki ya NMB ikishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), uzinduzi uliofanyika katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma leo Machi 27, 2023 na Kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Share:

RC CHRISTINA MNDEME APOKEA MTAMBO WA KISASA WA KUCHIMBA VISIMA VIREFU VYA MAJI SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amepokea Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji ambao ni sehemu ya mitambo 25 ya kuchimba visima vya maji iliyonunuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji kwa Fedha za UVIKO – 19.

Mtambo huo wenye uwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300 umepokelewa leo Jumatatu Machi 27,2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza wakati wa kupokea mtambo huo wa kisasa wa kuchimbia visima virefu kwa niaba ya wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameagiza mtambo huo utunzwe na utumike kwa malengo yaliyokusudiwa.


“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua mtambo huu wa kuchimbia visima virefu vya maji. Mhe. Rais Samia amedhamiria kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama lakini pia kumtua mama ndoo kichwani….Nasi Shinyanga tunasema ‘Dkt. Samia Maji Safi na Salama Bombani, Maji nyumbani, Kazi Iendelee’”, amesema Mhe. Mndeme.


“RUWASA nendeni mkafanye kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na mhakikishe pia kabla ya kuanza kuchimba muwe mmefanya utafiti kuwa na uhakika kama kweli maji yapo”,ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.


Aidha amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji na miundombinu ya maji ili miradi ya maji inayojengwa idumu huku akibainisha kuwa serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.


Akitoa taarifa ya Mapokezi ya mtambo wa kisasa wa uchimbaji visima, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela amesema kwa kuanzia, uchimbaji visima virefu utaanza mara moja katika vijiji vinne ambavyo ni Itilima na Mwashinogela katika wilaya ya Kishapu na Ubagwe na Kinamapula katika Halmashauri ya Ushetu.


“Mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa kame kutokana na hali hiyo upatikanaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi imekuwa changamoto. Hata hivyo mkoa wetu ni mnufaika wa kwanza wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria ambao kwa sasa unahudumia mikoa ya Mwanza (Kwimba na Misungwi), Shinyanga, Tabora (Igunga, Tabora na Nzega) na Mji wa Shelui Mkoa wa Singida”,ameeleza Mhandisi Payovela.


Amefafanua kuwa ujenzi wa miradi ya maji kupitia Bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA), umeendelea ambapo hadi sasa jumla ya vijiji 89 vinapata maji na vijiji 50 ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kupitia bomba hilo upo katika hatua za utekelezaji na kwamba uunganishaji wa maji ya KASHWASA umeendelea kufanyika kwa vijiji vilivyo ndani ya umbali wa km 12 kutoka bomba kuu la KASHWASA.


“Kwa vijiji vilivyo mbali zaidi na mtandao wa KASHWASA, tumeendelea kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa visima virefu hivyo mtambo huu wa kisasa ulionunuliwa kwa fedha za UVIKO-19 wenye uwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300 utasaidia sana katika kufanikisha uchimbaji wa visima virefu kupitia RUWASA”,ameongeza.


Katika hatua nyingine amesema kupitia fedha za UVIKO – 19 , Mkoa wa Shinyanga ulitekeleza miradi ya maji,mradi mmoja kila Jimbo isipokuwa jimbo la Solwa imejengwa miradi miwili.


“Jumla ya fedha kiasi cha shilingi 3,061,459,641.73 zimetumika kutekeleza miradi 7. Miradi yote imekamilika na wananchi 26,902 wanapata huduma ya maji safi na salama”, amesema Mhandisi Payovela.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza leo Jumatatu Machi 27,2023 wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza leo Jumatatu Machi 27,2023 wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela akisoma taarifa kuhusu Mtambo wa Kisasa wa kuchimbia visima virefu
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela akisoma taarifa kuhusu Mtambo wa Kisasa wa kuchimbia visima virefu
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji 
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji 
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji 
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiendesha Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mtaalamu wa Mitambo kutoka RUWASA, Hamis Simwita akionesh namna ya kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akijaribishia kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akijaribishia kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akijaribishia kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger