Thursday, 23 March 2023

ATE YAZINDUA AWAMU YA 9 YA PROGRAMU YA MWANAMKE KIONGOZI

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE - Bi. Suzanne Ndomba akizungumza wakati akizindua Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE - Bi. Suzanne Ndomba akizungumza na wadau mbalimbali mara baada ya kuzindua Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************

NA MWANDISHI WETU

JUMLA ya Wanawake 73 wamejiunga na kuanza Mafunzo ya Programu ya Mwanamke Kiongozi ya awamu ya 9 yaliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Chuo cha Hisami na Kudhaminiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika la Waajiri .

Akizungumza katika hafla uzinduzi wa Programu hiyo leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE - Bi. Suzanne Ndomba amesema progrramu hiyo ilianza mwaka 2016 na kuzinduliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu na tokea kuanzishwa kwake wamekuwa kimeendelea kufanya programu hiyo.

"Mwaka 2016 ambapo programu hii imeanza, imekuwa ikiendelea kukua ambapo kwa week iliyopita tulifanya mkutano wa mwaka wa mwanamke kiongozi ambapo wahitimu wa programu hiyo wa awamu ya nane waliweza kuhitimu masomo yao wanawake 65". Amesema Bi.Suzanne.

Kwa upande wake Mkurugenzi Rasilimali Watu- CRDB , Bw.Godfrey Rutasigwa amesema kwa ushirikiano ambao wameufanya ATE na programu ya mwanamke kiongozi inamanufaa makubwa na wanawake ambao wanashiriki kwenye programu hiyo wengi wao wameonekana kuongeza utendaji kazi wao na kupata nafasi za juu zaidi za uongozi.

"CRDB Bank inaamini katika nguvu ya wanawake na katika kufanya hivyo tumekua tukiwekeza kila mwaka kwenye kuendeleza wanawake ambao ni wafanyakazi wetu ili waweze kukua na kushika nyadhfa kubwa mbalimbali za kiuongozi". Amesema Bw.Rutasigwa.

Aidha amewashauri washiriki wote ambao wametoka kweye Benki ya CRDB wachukulie uzito suala hilo, wajifunze kwa bidii na kuhakikisha wanaweza kufanya vipindi vyote na kazi zote ambazo wamepewa na kuyachukua mafunzo hayo kwenda kuyaweka kwenye vitendo ili kuweza kuonyesha yale manufaa biashara yao kwa wafanyakazi wengine lakini pia wateja wanaowahudumia.

Naye Makamu wa Rais GGM- Bw. Saimon Shayo alisema lengo la kuwaleta wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ni kuwajengea uwezo ili waweze kuchukua nafasi za uongozi.

"Kwa desturi Duniani kote wanawake ni wachache kwenye sekta ya madini lakini kwenye uongozi pia ni wachache hivyo tunafuraha ya kwamba katika wale walioshiriki miaka ya nyuma tayari wamepata nafasi ya uongozi kwenye kampuni". Amesema Bw.Shayo. Mkurugenzi Mtendaji wa ATE - Bi. Suzanne Ndomba akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Rasilimali Watu- CRDB , Bw.Godfrey Rutasigwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais GGM- Bw. Saimon Shayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam
Share:

MISAADA ILIYOTOLEWA NA SERIKALI YA TANZANIA KWA WAHANGA WA KIMBUNGA FREDDY YAVUKA MPAKA KUELEKEA MALAWI






Na Mwandishi wetu,OWM.


MKURUGENZI Msaidizi  anayeshughulikia Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Nchini Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na madawa mbalimbali ambayo yatasaidia wahanga wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.

Luteni Kanali Masalamado amesema hayo wakati Msafara wa magari ya jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre Nchini Malawi tarehe 22/03/2023.

“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” amesema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi Mhe. Roderick Mateauma ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo kati ya nchi hizo mbili.

 

  

Share:

BODI YA PAMBA TANZANIA YAANIKA MAFANIKIO MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA, VIONGOZI AMCOS WANASWA WIZI WA VIUADUDU, VINYUNYIZI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimbe ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi TCB akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Afisa Kilimo Mwandamizi TCB, Renatus Luneja akifuatiwa na Mkaguzi wa Viuatilifu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Richard Danstan. Kulia ni  Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Kusimamia Usambazaji wa Viuadudu na Vinyunyizi vya zao la pamba, Bw. Protas Henry.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Bodi ya Pamba Tanzania (Tanzania Cotton Board – TCB) imeeleza matokeo chanya ya mikakati ya kuongeza zao la Pamba katika kipindi cha miaka Miwili ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan huku ikiweka nguvu zaidi katika kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kusimamia usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi vya zao la pamba kuanzia kwenye maghala hadi kwa wakulima.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi Machi 23,2023, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimbe ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi TCB, amesema Bodi ya Pamba Tanzania inajivunia mafanikio makubwa ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kikao hicho cha Bodi ya Pamba na Waandishi wa Habari Mjini Shinyanga kililenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Bodi ya Pamba Tanzania ndani ya kipindi cha miaka miwili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na utekelezaji wa shughuli za kamati ya kusimamia usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi vya zao la pamba kuanzia kwenye maghala hadi kwa wakulima ambayo iliundwa kutokana na agizo la Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe.


“Kwa kipindi hiki cha miaka miwili ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambacho ametumikia wananchi vizuri na sisi tumefanya kwa juhudi kumuunga mkono na kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanafanikiwa kama adhma ya serikali inavyotaka kwamba kuwe na maendeleo kwa wananchi/wakulima wenyewe na taifa kwa ujumla”, ameeleza Shimbe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimbe ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi TCB.

“Katika msimu huu wa kilimo 2022/2023 tuliagiza viuadudu chupa 11,839,225 zenye thamani ya shilingi Bilioni 51 ambapo lengo la kuagiza viuadudu hivyo ni kusambaza kwa wakulima kwa ajili ya kukabiliana na visumbufu vya zao la pamba. Hadi kufikia leo tumekwisha sambaza zaidi ya viuadudu chupa milioni 8”,amesema Shimbe.

Katika hatua nyingine amesema Msimu huu 2022/2023 zao la pamba linaenda vizuri sana na wanatarajia kupata mavuno ya pamba zaidi ya tani 500,000 (Kilo Milioni 500) huku akiongeza kuwa wanatarajia kuwa na ongezeko la pamba katika msimu 2023/2024 ambapo matarajio ni tani 700,000 kwa sababu hali ya hewa ni nzuri na bahati nzuri viuadudu vimepelekwa kwa wakulima.


“Lakini pia huwezi kupeleka viuadudu bila kuwa na vinyunyizi, tumenunua vinyunyizi 42,584 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 4 na vyote tumevisambaza kwa wakulima na bahati nzuri vinafanya vizuri kwenye maeneo ya wakulima”,ameongeza Shimbe.
“Kabla ya vyote hivyo tumekwisha sambaza mbegu za kupanda za pamba ambazo zimeondolewa nyuzi kwa wakulima zaidi ya tani 22,000 kwa msimu huu 2022/2023. Bodi ya Pamba Tanzania imefanya hayo na inaendelea kusambaza viuadudu kwa wakulima”,amefafanua Shimbe.

Aidha amewataka wakulima kutambua kuwa bado viuadudu vipo na vinaendelea kusambazwa hivyo waendelee kujitokeza kwa wingi kunyunyizia mashamba yao ili wadudu wanaojitokeza wakiwemo funza, Chawa Jani, Vidukali na Vithrip (Thrips) waliopo kwenye mashamba waweze kuangamizwa ili kuhakikisha zao la pamba linaenda vizuri.


“Pamba inalimwa katika mikoa 17, Halmashauri 60 na halmashauri 56. Kwa sasa nchi nzima viuadudu vipo vinasambazwa na wananchi wakae mkao wa kuhakikisha mashamba yao yamekaa sawa kwa ajili ya kukabiliana na wadudu”,amesisitiza Shimbe.
James Shimbe

Katika hatua nyingine amesema TCB imenunua ndege 20 zisizo na rubani zenye thamani ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya kunyunyizia viuadudu kwenye mashamba makubwa ya wananchi.

“Hali kadhalika Msimu huu tumejipanga vizuri kufikisha elimu kwa wananchi kilimo cha pamba, Balozi wa pamba nchini Aggrey Mwanri pia anaendelea kutoa elimu kwa wakulima. Tunawaomba wakulima wazingatie matumizi sahihi ya viuadudu lakini muda sahihi wa kunyunyizia”,amesema.

Ameongeza kuwa TCB pia imegawa baiskeli 2500 kwa wakulima wawezeshaji na pikipiki 250 kwa maafisa ugani ngazi ya kata katika halmashauri 13 ili kufikisha elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha pamba.
Richard Danstan akizungumza na waandishi wa habari

Kwa upande wake, Mkaguzi wa Viuatilifu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Richard Danstan amesema viuadudu vinatolewa bure kwa wakulima na kwamba wanaendelea kufanya misako kwenye magulio na minada ili kuwabaini na kuwachukulia sheria wanaouza viuatilifu sambamba na kuhamasisha kuepuka kuweka viududu juani ili visipoteze ubora.
Renatus Luneja akizungumza na waandishi wa habari

Afisa Kilimo Mwandamizi Bodi ya Pamba Tanzania, Renatus Luneja amesema TCB inataka pembejeo zilindwe na ziwafikie walengwa huku akiwataka wakulima kufika katika AMCOS ili kuchukua pembejeo za kilimo badala ya kulalamika kuwa pembejeo zinachelewa kufika.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kusimamia Usambazaji wa Viuadudu na Vinyunyizi vya zao la pamba inayoundwa na wajumbe 10, Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati hiyo, Bw. Protas Henry amesema lengo la kamati hiyo ni kuhakikisha viududu na vinyunyizi vinawafikia wakulima.

“Kamati hii ina jukumu la kujiridhisha ubora na kiasi cha viuadudu kabla ya kusambazwa kwa wakulima, kuhakiki maelezo ya matumizi yaliyopo katika vifungashio kama yanaendana na yale yaliyoidhinishwa na mamlaka husika na kusimamia ugawaji wa viuadudu na vinyunyizi kwenye Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS),kufuatilia ufanisi wa viuadudu kwenye mashamba na kutoa ushauri wa kitaalamu”,ameeleza Henry.

Amesema kamati hiyo inaendelea kutekeleza majukumu yake tangu mwezi Desemba 2022 hadi sasa ambapo imekwisha fanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye AMCOS zinazohusika moja kwa moja na ugawaji viuadudu na vinyunyizi na kukutana na viongozi mbalimbali.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Kusimamia Usambazaji wa Viuadudu na Vinyunyizi vya zao la pamba, Bw. Protas Henry akitoa taarifa kuhusu shughuli za kamati hiyo.

“Miongoni mwa changamoto tulizobaini ni pamoja na viongozi wa kisiasa kama vile madiwani na wenyeviti wa vijiji/vitongoji kuingilia ugawaji wa viuadudu na vinyunyizi badala ya viongozi wa AMCOS, maafisa ugani na watendaji wa vijiji, baadhi ya viongozi wa AMCOS kutozingatia utaratibu wa ugawaji wa viuadudu na vinyunyizi na kujihusisha wizi wa pembejeo”, ameeleza Henry.


“Changamoto nyingine ni taarifa kwenye fomu za kugawia viuadudu na vinyunyizi kutojazwa kwa maksudi kwa nia ya kutengeneza mianya ya wizi wa pembejeo husika,baadhi ya viongozi wa AMCOS kughushi taarifa za kwenye fomu za kugawia viuadudu na baadhi ya wakulima kutoa taarifa zisizo sahihi za ukubwa wa mashamba yao ya pamba ukilinganisha na uhalisia”,amesema Henry.
Protas Henry akizungumza na waandishi wa habari

Kutokana na baadhi ya viongozi wa AMCOS kadhaa kuhusika katika tuhuma za wizi na kughushi taarifa za wakulima/viuadudu, Henry amesema jumla ya majalada 12 yamefunguliwa katika vituo vya Polisi, TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi katika wilaya za Bunda,Chato,Busega, Magu na Nyang’hwale na kamati hiyo imeokoa upotevu wa viuadudu vyenye thamani ya shilingi 34,370,000/=.


“Jumla ya kesi 6 zimefunguliwa mahakamani dhidi ya viongozi wa AMCOS kuhusu tuhuma za kupatikana na mali za serikali, wizi na kughushi katika wilaya ya Bunda, Chato, Igunga na Nyang’hwale lakini pia kesi moja imehukumiwa mahakamani ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya shilingi 1,000,000/= katika wilaya ya Chato”,ameongeza Henry ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya kusimamia usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi.


Henry amewakumbusha viongozi wa AMCOS na watendaji wengine waliopewa dhamana ya kusambaza na kugawa viuadudu na vinyunyizi kwa wakulima kutimiza wajibu wao kulingana na taratibu na sheria na kujiepusha na vitendo vya wizi, kughushi na rushwa kwa ajili ya kujipatia faida binafsi na kuwa tayari kuwafichua wote wanaohujumu usambazaji viuadudu na vinyunyizi ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Kusimamia Usambazaji wa Viuadudu na Vinyunyizi vya zao la pamba, Bw. Protas Henry akitoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo leo Alhamisi Machi 23,2023.

Picha na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog


Share:

WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA MPANGO SHIRIKISHI KUKABILIANA NA KIPINDUPIND

 
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akizindua Mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia kipindupindu jijini Dodoma.


Na 1Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog DODOMA 

SERIKALI kupitia Ofisi ya Wa Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu imezindua mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu 2023/2027 huku ikitangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo kuanzia Februari 19 hadi Machi 15 mwaka 2023  imepokea taarifa ya wagonjwa 60 Kutoka mikoa 4 ya Tanzania Bara.

Akiongea kwenye uzinduzi wa Mpango Shirikishi wa Taifa wa  Kuzuia na Kukabiliana na Kipindupindu , Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene ametumia nafasi hiyo kuitaka Wizara ya afya kuongeza nguvu ya ufuatiliaji ili kuhakikisha wagonjwa na tetesi zote zinatolewa taarifa kushughulikiwa mapema kwenye vituo vya afya  kabla ugonjwa haujasambaa .

Waziri Simbachawene ameitaja mikoa hiyo yenye wagonjwa wa kipindupindu kuwa ni pamoja na Ruvuma mgonjwa 1, Kigoma 7, Katavi 34 na Rukwa18.

"Hivi karibuni baadhi ya mikoa kama Katavi, Kigoma, Ruvuma, Manyara na Rukwa imekuwa ikipata milipuko ya Kipindupindu katika baadhi ya Halmashauri zake,ni hatari na aibu,ugonjwa huu unachukuliwa kama umaskini kutokana na namna unavyoanza,"amesema 

Amesema kuwa ugonjwa wa kipindupindu kama yalivyo magonjwa mengine ya mlipuko, unasambaa kwa kasi na wakati mwingine kuvuka hata mipaka ya nchi.

" Taarifa kutoka shirika la Afya Dunia inaeleza kuwa na mlipuko mkubwa wa Kipindupindu nchini Malawi ambapo hadi kufikia tarehe 15 Machi 2023 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 53,925 na vifo 1,658 vilivyotolewa taarifa"amesema na kuongeza;

Hii inatupa tahadhari ya mlipuko huo pia kuvuka mipaka na kuingia nchini kwetu hususani pale tusipo imarisha afua mbalimbali za kujikinga na kipindupindu kwa jamii zetu hususani kwa Mikoa inayopakana na nchi hiyo" amesisitiza 

Pamoja na hayo amesema  tetesi za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu pia zipo kwa nchi nyingine zinazo pakana na Tanzania ikiwemo Msumbiji, DRC Congo, Zambia na Kenya .

"Ni mategemeo yangu kuwa Mikoa hii na Nchi nzima kwa ujumla imejiandaa vyema kuhakikisha kuwa ugonjwa huo kwanza unazuiwa lakini pia unakabiliwa pale utakapokuwa umevuka mipaka na kuingia kwetu,"amesema 

Simbachawene pia ametoa wito kwa ngazi zote za utekelezaji kuhakikisha kuwa shughuli zote zilizopangwa kwenye mpango huo zinatekelezwa kwa wakati na weledi mkubwa ili matokeo yake yaweze kuwa chanya katika kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huo hatari, hususan kwenye maeneo yenye kupata milipuko ya Kipindupindu mara kwa mara. 

"Natumia nafasi hii kuwaomba wadau wote wa maendeleo kuendelea kufanya kazi na serikali katika kutekeleza mpango huu ili kuhakikisha ugonjwa huo unazuia kabisa au kuhakikisha madhara yake yanapunguzwa kabisa,ushirikiano wenu unahitajika katika kutekeleza shughuli zote zinazohusiana na kipindupindu,"amesisitiza .
 
Wakati huo huo amezitaka Ofisi za tawala za Mikoa na Halmashauli zote kushirikiana na mamlaka za maji mijini na vijijini (RUWASA) kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo yao inaimarika.

 Vilevile amezitaka mamlaka za maji kupitia jumuiya za watumia maji kutibu maji kabla ya kuyasambaza, kuchukua sampuli za maji kila mara kutoka katika vyanzo tofauti na kuyapima katika maabara za mikoa za ubora wa maji, kuhimiza wananchi kujenga vyoo bora na kuvitumia na kuviweka katika hali ya usafi.

"Ofisi za Serikali za Mikoa na Halmashauri zote ziendelee kutoa elimu kwa wananchi kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kuoga, kufua, kutupa takataka ovyo na kadhalika ,Ushirikiano wa kisekta unahitajika katika kutekeleza shughuli zote zinazohusiana na kipindupindu,"amesema

Naye mwakilishi mkazi wa Shirika lisilo la kiserikali la SAVE THE CHILDREN  amesema juhudi za pamoja bado zinahitajika Katika mapambano ya magonjwa ya mlipuko na kwamba shirika hilo litaendelea kupambana na magonjwa  hayo kuhakikisha watoto wanakuwa salama na jamii kwa ujumla.

Amesema katika kukabiliana  na kipindupindu shirika hilo linafanya juhudi kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watoa huduma ngazi ya Jamii na ufuatiliaji wa kanuni za afya kwa Jamii ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kanuni Bora za afya.

"Tumekuwa tukishirikiana na Ofisi za baadhi ya waganga wakuu kuelimisha wananchi kuepuka kutupa takataka ovyo na  kuwahimiza kula vyakula vya moto na Usafi wa mazingira Kwa ujumla lengo letu kuhakikisha wananchi wanaacha tabia ya kutiririsha maji ya vyoo kwenye mifereji ya wazi na tabia nyingine hatarishi,"amesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge na Uratibu  Jim Yonaz amrsema mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya Sasa na baadae ili kutokomeza kabisa kipindupindu .

"Suala la kuzuia na kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ni mtambuka hivyo Wizara za Serikali, Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kishirikiana Kwa ukaribu,na sisi kama Serikali tutaendelea kutoa elimu Kwa jamii namna ya kuuepuka ugonjwa huu,"amesema 



Share:

EACOP INAHESHIMU HAKI NA UTU WA JAMII ZINAZOGUSWA NA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA


Meneja Mkuu wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika ya Mashariki ( EACOP) Wendy Brown akipeana mkono na kiongozi wa kimila wa kabila la Wataturu Gesuda Masanja wakati wa zoezi la kusaini makubaliano na EACOP ili bomba la mafuta kuchepuka makaburi yao ya asili ili kuheshimu mila na tamaduni zao. 

Jamii ya Wataturu wa kijiji cha Mwamayoka wilayani Igunga mkoani Tabora wakiwa katika sherehe ya kusaini makubaliano na mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP) ya kuchepusha makaburi yao ya asili ili kuendelea kulinda mila na tamaduni zao. 

****************** 

Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP Ltd) kwa kuheshimu mila na desturi za watu walioguswa na mradi (PAPs) imesaini mkataba wa kusimamia haki na kuheshimu tamaduni za Wazawa (FPIC) na jamii ya Wataturu wanaoishi katika kijiji cha Mwamayoka katika Wilaya ya Igunga, Tanzania kwa ajili ya kuchepusha njia ili kuyalinda makaburi yao ya kimila 

Awali Wataturu hao walikuwa na wasiwasi wa kuathiriwa kwa makaburi yao yaliyopo eneo la Bung’enda na maeneo yao mengine kadhaa ya kuabudia endapo mradi ungeanza ujenzi. 

Akizungumza wakati wa sherehe ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa EACOP Tanzania Wendy Brown amesema baada ya majadiliano na jamii na viongozi wa kimila, EACOP ilifanya mapitio ya kiufundi na kukubali kupitisha bomba hilo katika njia mpya ili kutokuwa na athari yoyote katika maeneo yao muhimu ya mila na kiutamaduni. 

Bi. Wendy Brown amesema, EACOP inaheshimu haki na mila za makundi yote ya kikabila yanayoguswa na mradi. 

Hivyo, amesema EACOP itaendelea kushirikiana na jamii zote zilizoguswa na mradi pamoja na viongozi wao wa kimila ili kuhakikisha kuwa maoni yao yamezingatiwa wakati wote wa kupanga na kutekeleza mradi. 

Mkataba huu wa FPIC ni wa pili kusainiwa na EACOP baada ya kusaini mkataba kama huo hapo awali na jamii ya Akie inayoishi Kanda ya Kaskazini. 

Amesema kusainiwa kwa mikataba hii ni kielelezo tosha kuwa mradi wa EACOP unashirikisha makundi yanayoguswa katika ngazi zote za utekelezaji wake na kuheshimu mila, tamaduni na haki za jamii husika. 

Ameongeza mradi wa EACOP unatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, jamii na utunzaji wa mazingira. 

Gesuda Masanja, ambaye ni chifu wa jumuiya ya Wataturu alipongeza hatua ya EACOP kwa kuzingatia mila zao, akisema kuwa mradi huo utasaidia kwa maendeleo ya jamii yake. 

Akizungumza awali, Martha Bayo, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Igunga, pia alipongeza hatua ya EACOP na kuitaka jamii ya Wataturu kuwa walinzi wa bomba hilo la mafuta ghafi litakapokamilika. 

Lucas Bugota, ambaye ni Diwani wa Kata ya Igunga pia ameusifu mradi wa EACOP kwa hatua hiyo, akisema jamii ya Wataturu wameweka historia katika kulinda mila na tamaduni zao. 

Nailejileji Tipap kutoka Jukwaa la Wafugaji lisilokuwa la Kiserikali (Pingos) alisema hatua ya kampuni ya EACOP kusaini mkataba wa FPIC inalinda maslahi ya jamii ya Wataturu hao. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo (DAS) Godlove Kawiche aliihakikishia kampuni ya EACOP juu ya dhamira ya serikali ya kutekeleza mradi wa bomba hilo la mafuta ghafi. 

Pia aliipongeza timu ya wataalam wa EACOP kwa kushirikisha jamii zilizoathiriwa katika mchakato mzima wa ujenzi wa bomba hilo
Share:

BARRICK YAKABIDHI GARI LA WAGONJWA 'AMBULANCE' KITUO CHA AFYA BUGARAMA


Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakikata utepe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick imechangia gari maalumu la kubebea wagonjwa 'Ambulance' katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo kata ya Bugarama Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.


Gari hilo limekabidhiwa leo Jumatano Machi 22,2023 na
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.


Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya gari hilo iliyofanyika katika Kituo cha Afya Bugarama, Bristow amesema Barrick inathamini suala la usalama na afya katika jamii ndiyo maana imeamua kutoa gari hilo kama sehemu ya mchango wao katika kuboresha huduma za afya kwa jamii inayozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala.


"Gari hili tumelitoa kama sehemu ya mchango wetu kwa jamii ni nje ya Fedha za mfuko wa uwajibikaji kwa jamii,tunaamini litasaidia katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Tutahakikisha tunaendelea kushirikiana na  jamii inayozunguka migodi yetu", amesema Bristow.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ameishukuru Kampuni ya Barrick kwa namna inavyojitahidi kutekeleza miradi  mingi inayogusa wananchi huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Wawekezaji ili kuwaletea maendeleo wananchi.


"Tunawashukuru Barrick kwa kutekeleza ahadi ya kuleta Ambulance katika kituo hiki cha Afya Bugarama. Gari hili litasaidia kutatua changamoto zilizopo...Nasi tunaahidi kutunza na kutumia gari hili kwa malengo yaliyokusudiwa. Ambulance hii itaongeza nguvu katika utoaji wa huduma za afya", amesema Mhita.

"Barrick wamekuwa wadau wakubwa katika wilaya ya Kahama, wana miradi mingi inayogusa wananchi na hii inatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali na Kampuni ya Barrick", ameongeza.


Nao Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leonard Mabula na Diwani wa Kata ya Bugarama, Mhe. Prisca Msoma wameishukuru Barrick kwa kutekeleza kwa wakati ombi la Ambulance ili kutatua changamoto ya huduma za matibabu katika kituo hicho cha afya kinachohudumia jamii ya Bugarama na maeneo ya jirani ikiwemo Geita.


Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Bugarama Dkt. Silas Kayanda na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha wamesema walitoa ombi la kupatiwa Ambulance kutoka Barrick mnamo Januari 25,2023 huku wakieleza kuwa kupatikana kwa gari hilo kutapunguza changamoto ya usafiri kwa wagonjwa katika kituo hicho cha afya.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakikata utepe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakikata utepe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita funguo ya gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakishikana mkono wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakishikana mkono wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Muonekano wa gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Muonekano wa gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leonard Mabula akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Diwani wa Kata ya Bugarama Mhe. Prisca Msoma akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Bugarama Dkt. Silas Kayanda akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.

Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo katika Halmashauri ya Msalala.
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Awali Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto).
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakipiga picha na viongozi mbalimbali wa Kampuni ya Barrick na Serikali
Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Bristow na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakipiga picha na wadau mbalimbali.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger