Sunday, 19 March 2023

SHEREHE YA SHY WOMEN’S DAY OUT YAFANA, MKURUGENZI SATURA AWATAKA WAENDELEZE UMOJA WAO

 

Wanawake wakiburudika Sherehe ya Shy Women's Day Out na mtoa mada Dokta Kumbuka.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SHEREHE ya wanawake Shy Women’s Day Out ambayo imeendeshwa na kikundi cha Wanawake Women For Change imefanyika kwa mara sita mfululizo, huku wakitaja mafaniko makubwa ambayo wameyapata wanakikundi, ikiwamo na kusaidia jamii ambayo inaishi katika mazingira magumu pamoja na kuiunga mkono Serikali katika sekta ya elimu, Afya na kuinua kiuchumi.

Sherehe hizo zimefanyika Jana katika ukumbi wa Mikutano wa Lyakale huku watoa mada akiwa ni Dokta Kumbuka, Anti Sadaka na Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Akisoma Risala ya kikundi hicho cha wanawake Women’s for Change Dk. Juliety Kabengula, amesema kikundi hicho kilanzishwa mwaka 2013 na sasa kina miaka 10 na kimekuwa kikifanya Matamasha ya kukutanisha Wanawake ndani ya miaka sita mfulululizo tangu mwaka 2016 hadi leo 2023.

Amesema kwenye kikundi chao ndani ya miaka hiyo 10 wameweza kuinuana kiuchumi, kusaidia Watoto na wazee ambao wanaishi katika mazingira magumu, ikiwamo kusomesha wanafunzi, kukarabati bweni katika shule ya kulea Watoto wenye ulemavu Buhangija, kununua Madawati katika shule ya Solwa na Lubaga.

Amesema mbali na kuchangia maendeleo katika Sekta ya Elimu pia wamenunua mashine kwa ajili ya kusaidia Watoto Njiti ambayo hivi karibuni wataikabidhi katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

“Women’s For Change tumekuwa tukiendesha Matamasha ya wanawake ndani ya miaka sita sasa mfululizo kwa lengo la kujengeana uwezo, kujitambua, kujikwamua kiuchumi, kukabiliana na vitendo vya ukatili, pamoja na kupambania haki zetu ikiwamo mirathi,”amesema Dk. Kabengula.

Aidha, amesema matarajio ya kikundi hicho ni kufanya uwekezaji mkubwa ili wapate kukua kiuchumi zaidi na kuendelea kuinuana wao kiuchumi pamoja na kusaidia jamii na kuungana na Serikali katika uchangiaji wa maendeleo mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amekipongeza kikundi hicho cha Wanawake Women For Change kwa kuandaa Sherehe hiyo ya wanawake, pamoja na kusaidia jamii na kushirikiana na Serikali katika mambo mbalimbali na kuwataka waendelee na umoja huo.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kikundi hicho katika kuhakikisha wanawainua wanawake wa Manispaa ya Shinyanga kiuchumi pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa akina mama na kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyabiashara zao ikiwamo ujenzi wa masoko.

“Wanawake ni Jeshi kubwa na leo mmethibitisha hilo na kuonyesha Vita mnaiweza na Jeshi hili likitumika vizuri litachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sisi Serikali tutaendelea kuwa unga mkono chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan,”amesema Satura.

Naye Mwezeshaji wa Mada ya kwanza Anti Sadaka, amewataka wanawake kujiamini, kusimama katika nafasi zao, kujipenda pamoja na kuchapa kazi kwa bidi na siyo kuwa tegemezi kwa waume zao.

Mwezeshaji Dk, Kumbuka amewataka wanawake waache pia kuishi maisha ya kuiga, pamoja na kupunguza marafiki wasiokuwa na faida (marafiki hewa) na kuacha kuchukiana bali wapendane na kushirikiana kuchapa kazi na kufanikiwa kimaendeleo.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akimlisha Keki Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake Women For Change Ansila Benedict.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akimlisha Keki Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's Day Out Faustina Kifambe.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Sherehe ya Shy Women's Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake Women For Change Ansila Benedict akizungumza kwenye Shere hiyo.
Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's Day Out Faustina Kifambe akizungunza kwenye sherehe hiyo.
Dk. Juliety Kabengula, akisoma Risala ya kikundi cha Wanawake Women's For Change kwenye sherehe hiyo ya Shy Women's Day Out.
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Sherehe hiyo ya Shy Women's Day Out.
Dokta Kumbuka akitoa Mada kwenye Sherehe ya Shy Women's Day Out.
MC Mama Sabuni mbali na kusherehesha pia alitoa ujumbe kwa wanawake kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ya Shy Women's Day Out ikiendelea.
Wanawake wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiingia ukumbini.
Awali watoa Mada wakiingia ukumbini wakiwa na Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's day Out Faustina Kifambe (kulia) (kushoto) ni Anti Sadaka na (katikati) Dokta Kumbuka.
Watoa Mada wakiwa ukumbini.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Msanii Christiani Belaa akitoa Burudani kwenye Sherehe hiyo ya Wanawake.
Christiani Bella akiendelea kutoa burudani.
Burudani zikiendelea kwenye sherehe hiyo.
Kikundi cha Wanawake Women's For Change wakiingia ukumbini.
Picha za pamoja zikipigwa na mtoa mada Dokta Kumbuka kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women's Day Out.
Picha ya pamoja ikipigwa kati ya kikundi cha Women For Change, Mgeni Rasmi pamoja na watoa Mada.
Picha ya pamoja ikipigwa na wanakikundi cha Women For Change na Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 19,2023



]]






















Share:

Saturday, 18 March 2023

VIJANA WANUFAIKA KWENYE KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KUPITIA MRADI WA OKP


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin J. Rwezimula ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali ya Uholanzi na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta ya elimu na kukuza ujuzi kwa vijana ili kuweza kuwapitia elimu itakayowawezesha kujiari.


Amesema hayo katika hafla ya kukamilika kwa mradi wa Orange Knowledge Programme (OKP) iliyofanyika katika ukumbi wa HORTI -Tengeru jijini Arusha Tarehe 17, Machi, 2023.


Dkt. Franklin amesema kupitia mradi huu vijana wamenufaika kwa kupata mafunzo na ujuzi katika kilimo cha matunda na mboga mboga (Horticulture), ujenzi wa miundombinu, na vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia kujikwamua na changamoto ya ajira.


Hivyo Wizara itahakikisha mafunzo na ujuzi uliopatikana unakuwa endelevu na kuhakikisha vyuo vyote vya Ufundi vinatoa elimu yenye ubora ili kusaidia vijana na taifa kwa kupata nguvu kazi yenye maujuzi unaohitajika ka soko la ajira.


Kwa upande wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Kaimu Katibu Mtendaji Dkt. Amani Makota amesema kuwa pamoja na manufaa mbalimbali ya mradi huo, walimu pia wameweza kupata mafunzo ambayo yamesaidia kuwajengea uwezo na ufanisi katika ufundishaji pamoja na uboreshwaji wa mitaala.


Mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya Uholanzi na kusimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mfunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Maastricht Uholanzi ulikua na lengo la kusaidia kuboresha kilimo cha matunda na mboga mboga nchini.


Vyuo vilivyonufaika na mradi huo ni pamoja na MATI Uyole - MBEYA, HORTI - Tengeru na Mahinya Institute of Sustainable Agriculture- Songea



Share:

TAASISI YA USTAWI WA JAMII WATOA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA NDANI 100 KUHUSU MALEZI YA WATOTO

Mkuu wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii (ISW), Dkt. Joyce Nyoni akifungua Mafunzo kwa mabinti wanyakazi wa ndani 100 leo Machi 18,2023 katika ukumbi  wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam

***************

Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) leo Machi 18 kimetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa malezi na makuzi ya watoto zaidi ya kwa wasichana 100 ambao wanyafanya kazi za ndani katika Mkoa wa Dar Es Salaam.

CHUO cha Ustawi wa jamii (ISW) kimefanikiwa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa malezi na makuzu ya watoto Wasichana wanaofanya kazi za ndani 100 katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kupunguza ama kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabiri wasicchana hao na nyumba ambazo wanafanyia kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 18,2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo hayo Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt. Joyce Nyoni amesema awali tulikuwa tunajaribu kuona muititikio wa wadada kuja katika mafunzo haya lakini maombi yaliyotufikia ni zaidi ya 200 hivyo watafanya mafunzo hayo zaidi siku zijazo.

“Leo tuna programu ya kuwajengea uwezo wadada wakazi katika malezi na makuzi ya mtoto tumeifanya hili tukiwa tunaelekea kuadhimisha siku ya ustawi wa Jamii Machi 21". Amesema

Dk Nyoni ameeleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na kelele nyingi na malalamiko kuhusu malezi na tabia za watoto kwahiyo wakaona kama mchango wao wawe na vipindi na wasaidizi hao ambao wanalea watoto nyumbani kwasababu wanakaa na watoto muda mrefu.

Amesema akinamama wengi wanaondoka asubuhi na kurudi jioni na mtoto anakaa na dada lakini dada hana uelewa kuhusu malezi na makuzi na ana mchango mkubwa katika kulea.

“Lakini tunatambua dada huyu kuna siku atakuwa mama ni muhimu kuelewa ni namna gani anapaswa kulea mtoto kutokana na mabadiliko tunamjenge uwezo wa kumuelewa mtoto na kuwa na msaada chanya katika maendeleo na makuzi ya mtoto,”amesisitiza.

Amebainisha kuwa baada ya kutoa tangazo hilo Watu wanaokaa na wadada wakazi wengi walisema wanakuja kuwahamasisha kupata haki zao ambapo dhana hiyo inamaanisha kuwa hawakai nao vizuri.

“Niwasihii sana hawa ni wale ambao tunawaachia watoto tukae nao vizuri hakuna binadamu ambaye hana mapungufu aelekezwe vizuri kwasababu ndio tunawaachia watoto jinsi unavyokaa naye vibaya anaweza kuhamishia kwa watoto wananafasi kubwa sana katika malezi na makuzi ya watoto,”ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa Wakati mwingine ukatili unatokea kwasababu dada hamuelewi mtoto kama dada atamuelewa anatajua namna yakumsaidia na mama pia anatakiwa kumsaidia dada awe katika mazingira ya kujiamini anavyomlea mtoto .

Mmoja wa wafanya kazi wa ndani kutoka Bunguruni alisema mafunzo haya yanawajenga uwezo kwani wanafundishwa vitu wanavyotakiwa kujua pia kama wazazi wa baadae .

“Mfano tumefundishwa kuhusu ukuaji wa mtoto kimwili,kiakili ,kiroho na kijamii mafunzo yanatujenga tujue je zile hatua na ukuaji anaopitia mtoto ni sawasawa na vile tumeeelekezwa kama kuna changamotu turipoti kwa mama.

Alieleza kuwa Changamoto wanazokutana nazo ni mahusiano ya mtoto na mama kwani muda mwingine mama anakuwa bize hapati muda wakuongea naye kuhusu mtoto anapitia changamoto gani, mama akirudi anakuwa bize na simu au anaenda chumbani kulala .

“Muda mwingine ukimwabia nataka kuongea na wewe anakwambia amechoka kesho na kesho ikifika umejisahau na ukitaka kumwambia yuko bize unakuwa na ugumu wa kumwabi na wakati mwingine hayupo makini na kile ambacho nataka kumwambia ,”alibainisha. Wahadhiri wa Chuo hicho wametoa pia mafunzo ya Jinsi ya kukabiliana na misongo ya mawazo, matumizi sahihi ya fedha na kuweka akiba, usafi na mawasiliano kwa Wadada hao.
Share:

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA AKABIDHI COMPUTER, PRINTER SHULE YA SEKONDARI OLD SHINYANGA





Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amekabidhi Kompyuta tano na Printer 1 katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji wa masomo ya TEHAMA.
Share:

ODDS KUBWA WIKIENDI YA MOTO MERIDIANBET

 

Meridianbet mabingwa wa kumwaga odds kubwa wikiendi hii, Ligi mbalimbali zinaendelea n EPL, Bundasliga, Ligue 1 na Serie A unaambiwaje kitaeleweka weka dau kubwa ushinde mkwanja mrefu.

 

Odds kubwa Wikiendi Hii

 

Unajiuliza ni mechi gani itakua na Odds kubwa pale Meridianbet, basi usiwaze leo nakusogezea mechi zotee za Ligi zote zenye machaguo kibao na odds nono kutoka kwa wakali wa michezo ya kubashiri mubashara na sloti za kasino ya mtandaoni kama Aviator, Poker na Roulette.

 

Chelsea moto umewaka saivi unaambiwa hachani tiketi yako hovyo atakuwa Stamford Bridge kukipiga na Everton, odds kubwa ni Everton 7.05 ashinde huku Chelsea mwenyeji ana 1.47 akishinda. Southampton atakipiga na Tottenham siku ya jumamosi 4.41 amepewa Soton ashinde na Spurs ana 1.81 akishinda.

 

Wikiendi ya kibabe jiunge na Meridianbet ubashiri mechi hii ina odds kubwa, moto utaenda mbali Zaidi mpaka Italia ni Inter Milan dhidi ya Juventus yeyote hapa anakupa matokeo mazuri, Torino vs Napoli, Lazio Rome vs AS Roma nani unampa wikiendi hii?

 

Meridianbet wakali wa odds kubwa na kasino ya mtandaoni yenye michezo pendwa ya sloti kama Aviator, Poker na Roulette wameongeza machaguo Zaidi 1000+ kwenye mechi hizi za Ligi ya Mabingwa. Bonyeza hapa kuona machaguo Zaidi na mchanganuo wa odds kubwa bashiri mubashara.

 

Vinara wa EPL Arsenal wameondoshwa kwenye michuano ya Uropa, nguvu na akili zao watahamishia kwenye EPL kwani msimu huu wameonesha kuutaka ubingwa, na kazi ni moja wataingia kukipiga na Crystal Palace. Manchester united atakuwa ugenini dhidi ya Brighton na Man City akiwasha Ethiad na West Ham mechi zote hizi zina odds kubwa na machaguo 1000+ Meridianbet mabingwa wa kutoa odds kubwa na kasino ya mtandaoni

 

Laliga moto wake utawaka pale Nou Camp ni El Classico Barcelona vs Real Madrid, mechi ya kwanza Barca alikufa mabao 3-1 je ataweza kulipa kisasi na kuendelea kuongoza msimamo wa Laliga? Meridianbet wanaikoleza mechi hii na odds kubwa 2.16 ya Barca vs 3.19 ya Madrid, sare ina 3.52

 

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

 

NB: Meridianbet imekuja na Jackport kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

 

#MERIDIANBET CHAGUA TUKUPE

 


Share:

IJUE DAWA INAYOWAFANYA WATOTO WAFAULU MASOMO YAO!

Share:

Friday, 17 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 18,2023















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger