Sunday, 12 March 2023

Picha : MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI RICHARD MAKORE ALIYEFARIKI KWENYE AJALI YA BASI LA SHERATON YAFANYIKA SERENGETI


Mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Richard Makore aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Nipashe Kanda ya Ziwa yamefanyika nyumbani kwake Kijiji cha Remong'orori Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ijumaa Machi 10, 2023.


Makore aliyezaliwa mwaka 1978 alifariki Jumanne Machi 07, 2023 katika ajali ya basi la Sheraton iliyotokea katika eneo la Kasamwa mkoani Geita likitokea jijini Mwanza na kusababisha jumla ya vifo 10 na majeruhi kadhaa.


Mauti yalimkuta Makore akiwa safarini akielekea kwenye majukumu ya kikazi mkoani Geita.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG


Share:

Video Mpya : SENGI MILEMBE - UTAMADUNI

Share:

NAPOL WASHIRIKI MKUTANO WA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU MWAKITOLYO WA USOMAJI MAPATO NA MATUMIZI



Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 wilayani Shinyanga wa kusoma mapato na matumizi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIWANDA cha Uchenjuaji dhahabu (NAPOL ELUTION PLANT) wameshiriki Mkutano wa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 wilayani Shinyanga, wa kusoma mapato na matumizi.

Mkutano huo umefanyika jana kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mwakitolyo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Shinyanga, na wadau wa maendeleo.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 Mathew Tune, amesema wameitisha Mkutano huo wa kusoma mapato na matumizi kwa wachimbaji kupitia umoja wao wa Vitalu, ili kutekeleza Sera ya ukweli na uwazi na kuondoa migogoro isiyo na tija ya madai ya fedha kuliwa.

“Kutosoma Mapato na matumizi hua ni chanzo cha kutengeneza Migogoro, hivyo sisi wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 tumeamua mambo hadharani ili kuwepo na uwazi na kuondoa maneno ya kusema hela zinaliwa na viongozi,”amesema Mathew.

“Nawaomba wachimbaji wenzangu wa madini ya dhahabu tuendelee na ushirikiano ili tufikie malengo yetu na matarajio yetu hadi kufikia mwaka 2025 tunataka tuwe wachimbaji wa Kati,”ameongeza Mathew.

Naye Meneja wa Vitalu Leonard Waziri, akisoma taarifa ya uzalishaji madini kwa mwaka (2022) kupitia Vitalu vitano, amesema kwa kipindi hicho wamezalisha dhahabu gram 18,507.8 sawa na thamani ya fedha Sh.bilioni 2.3.

Amesema kupitia uzalishaji huo wa dhahabu wameweza kulipa mapato ya Serikali kuu Sh. Milioni 165 na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sh.milioni 7.7, huku wakichangia pia Shughuli za kijamii kwa kujenga Kituo cha Polisi, vyumba vya Madarasa kwa shule za Msingi na Sekondari na Madawati, Ofisi ya Mwenyekiti wa kijiji, Soko la Madini na kuboresha miundombinu ya uchimbaji.

Mhasibu wa umoja huo wa Vitalu Mwakitolyo Namba 5 Janeth Ngangula, akisoma taarifa ya fedha amesema kulingana na matumizi waliyoyafanya mpaka sasa kwenye Akaunti wamebakiwa na kiasi cha fedha Sh.milioni 213, na mikakati ya mwaka huu (2023) katika uchangiaji shughuli za kijamii wamepanga kununua gari la wagonjwa (Ambulance).

Aidha, Mdau wa Madini kutoka Kiwanda cha Uchenjuaji wa Madini ya dhahabu NAPOL ELUTION PLANT Meneja wa Kiwanda hicho Shaibu Juma, amepongeza viongozi wa wachimbaji Mwakitolyo namba 5 kwa kusoma mapato na matumizi na kuweka mambo yao kwa uwazi na kutoa wito kwa migodi mingine iinge utaratibu huo ambao utaondoa migogoro isiyo na tija na kusonga mbele kimaendeleo na kuongeza kasi ya uzalishaji dhahabu.

“Sisi NAPOL tupo pamoja na wachimbaji wa madini ya dhahabu na tutaendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji madini zinaendelea vizuri na kuongeza uzalishaji wa dhahabu, na Serikali itanufaika pia kwa kupata mapato,”amesema Shaibu.

Mgeni Rasmi kwenye Mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, naye amewapongeza viongozi kwa maamuzi waliyoyachukua kusoma mapato na matumizi huku akitoa wito kwa viongozi wote wilayani humo kuanza ngazi ya vitongoji wajenge utaratibu wa kusomea wananchi wao mapato na matumizi kama walivyofanya Mwakitolyo namba 5.

Katika Mkutano huo uliendana sambamba na utoaji wa zawadi mbalimbali vikiwamo vyeti vya pongezi kwa Vitalu ambavyo vilifanya vizuri katika uzalishaji wa madini ya dhahabu, utoaji wa Tshet kutoka NAPOL na makabidhiano ya Tuzo kutoka Hollysmile.

Meneja wa Kiwanda cha kuchenjua Dhahabu (NAPOL ELUTION PLANT) Shaibu Juma kilichopo Kahama Mtaa wa Nyasubi akizungumza kwenye Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wa usomaji mapato na matumizi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza kwenye Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wa usomaji mapato na matumizi.

Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 Mathew Tune akizungumza kwenye mkutano wao wa usomaji wa mapato na matumizi.
Meneja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 Leonard Waziri akisoma taarifa ya uzalishaji madini.

Mhasibu wa Vitalu Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 Janeth Ngangula akisoma taarifa ya mapato na matumizi.
Mdau wa maendeleo Arnold Bweichum kutoka Kampuni ya Hollysmile ya utoaji wa Tuzo Mdau Shupavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wadau wa madini kutoka kiwanda cha uchenjuaji wa dhahabu NAPOL Elution Plant wakiwa kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu mwakitolyo wa usomaji wa mapato na matumizi
Wadau wa madini wakiwa kwenye Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wa usomaji mapato na matumizi.

Wadau wa madini wakiwa kwenye Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wa usomaji mapato na matumizi.
Viongozi wa umoja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomea wachimbaji mapato na matumizi.
Viongozi wa umoja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomea wachimbaji mapato na matumizi.
Viongozi wa umoja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomea wachimbaji mapato na matumizi.

Viongozi wa umoja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomea wachimbaji mapato na matumizi.

Meneja wa Kiwanda cha uchenjuaji dhahabu (NAPOL Elution Plant) Shaibu Juma (kulia) akitoa zawadi za T-Shet kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba Tano kwenye mkutano huo,(kushoto) ni Mwenyekiti wa wachimbaji Mathew Tune.

Mwenyekiti wa wachimbaji wa dhahabu Mwakitolyo namba 5 Mathew Tune akionyesha T-Sheti kutoka Kiwanda cha uchenjuaji madini ya dhahabu (NAPOL Elution Plant).

Mdau wa Maendeleo kutoka Kampuni ya Hollysmile Arnold Bweichum Mdau shupavu (kulia) akikabidhi Tuzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 kutokana na kuwa na mchango mkubwa Serikalini wa ulipaji mapato na kuzalisha madini kwa wingi, (kushoto) ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Mathew Tune.

Mdau wa Maendeleo kutoka Kampuni ya Hollysmile Arnold Bweichum Mdau shupavu (kushoto) akikabidhi Tuzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 kutokana na kuwa na mchango mkubwa Serikalini wa ulipaji mapato na kuzalisha madini kwa wingi, (kulia) ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Mathew Tune.

Tuzo ambayo wamekabidhiwa wachimbaji hao wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela (kulia) akikabidhi vyeti vya pongezi wa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Zoezi la utoaji vyeti vya Pongezi likiendelea kwa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Zoezi la utoaji vyeti vya Pongezi likiendelea kwa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Share:

Saturday, 11 March 2023

RAIS SAMIA AMPANDISHA CHEO KAMANDA JUMANNE MULIRO




Muliro Jumanne Muliro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura imesema Muliro
amepandishwa cheo hicho kuanzia February 20, 2023.
Share:

BUNGE LA AFRIKA LASHIRIKI MKUTANO WA 146 WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI 'IPU'

Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira akishiriki Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (Inter-Parliamentary Union - IPU) ulioanza leo Jumamosi Machi 11 hadi Machi 15,2023 Manama, Bahrain.

 *****
The President of the Pan-African Parliament (PAP), H.E. Chief Fortune Charumbira is leading a delegation to the 146th Assembly of the Inter-Parliamentary Union (IPU) and its related meetings which kick off today till 15 March 2023 in Manama, Bahrain.

All IPU statutory bodies, including the Governing Council, Standing Committees, Committees on the Human Rights of Parliamentarians and on Middle East Questions, as well as the Forum of Women Parliamentarians and the Forum of Young MPs, are expected to convene during this Assembly. The General Debate will focus on the overall theme of Promoting peaceful coexistence and inclusive societies: Fighting intolerance - and provide a platform for delegates to deliberate, exchange views and galvanize parliamentary action in this area.

The PAP is taking part in the IPU Assembly for the second time as an Associate Member of the international parliamentary body. This follows the continental Parliament’s active first participation in the 145th Assembly held in Kigali, Rwanda where the President of the legislative arm of the African Union addressed world parliamentarians on gender equality.

Leading up to the opening of the 146th IPU Assembly in Manama, the President of the PAP took part in the traditional preparatory engagements including meetings of the Southern African Development Community (SADC) and the Africa groups on 10 March 2023. These consultations covered several items including the report of the executive committee, emergency items to be included in the agenda of the Assembly and the security situation in Eastern DRC.

Intervening on the occasion of these meetings, the President of the PAP, H.E. Chief Charumbira reiterated the Continental Parliament’s commitment to working closely with all stakeholders to ensure alignment and consensus on African positions.

“Our role as Africa’s Parliament is to facilitate cooperation among Regional Economic Communities and their Parliamentary fora. We’re also called upon to cooperate with National and Regional Parliaments and similar bodies within and outside Africa. Our participation in these global gatherings is therefore to ensure that Africa speaks with one voice,” said Chief Charumbira.

On the issue of Palestine, the President of the PAP sought to reaffirm the African Union (AU)'s unwavering support for the Palestinian cause.

“ The 36th African Union Summit of Heads of State and Government held in February 2023 in Addis Ababa was unequivocal about the issue of Palestine. Africa is fully behind the cause and this is the position we must all adopt during this IPU Assembly,” said H.E. Chief Charumbira.

Finally, the 147th IPU Assembly expected to hold in Luanda, Angola received an overwhelming support from the Africa group.

Share:

SIMBA SC YAONESHA UMWAMBA MTIBWA SUGAR, YAICHAPA 3-0



KLABU ya Simba sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu baada ya kuichakaza timu ya Mtibwa Sugar kwa mabao 3-0, katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Manungu mkoani Morogoro.



Katika mchezo huo tumeshuhudia Jean Baleke akifunga mabao hayo yote matatu Hat Trick na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi huo mnono kwenye mechi hiyo.
Share:

TGNP YAWASILISHA RASIMU YA SERA YA JINSIA CHAUMMA

Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam. Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KUTOKANA na Changamoto ya Ushiriki wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kwenye siasa hasa kwenye nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya vyama vya siasa TGNP iliona ni muhimu mkubwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuviwezesha vyama kutengeneza sera ya jinsia, na moja ya Chama ambacho kilinufaika kwa mara ya kwanza ni Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Ameyasema hayo leo Machi 11,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho ili baadae kiweze kupeleka rasmi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Akiwasilisha rasimu hiyo Bw.Temba amesema rasmi ya Sera ya Jinisia kwa CHAUMMA inakwenda kusaidia kukua kwa dhana ya demokraisia ya Kijamii kwa sababu wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu watapata fursa sawa ndani na nje ya chama hicho hasa katika masuala ya maamuzi.

Amesema katika mikakati ya sera hiyo, inaenda kuboresha dhana ya “Ubwabwa wa maharagwe” ili kuwa na Jamii yenye ustawi kwa kuboresha huduma za jamii hasa afya, ustawi, elimu na maji safi na salama.

"Wakati nawasilisha rasmi hii, CHAUMMA wametoa mapendekezo machache ya kuboresha lakini wameipenda kwani inaonesha na kutafsiri vizuri falsa yao ya Ubwawa na Maharage mashuleni". Amesema

Pamoja na hayo Bw.Temba amesema kuwa katika misingi ya Chama hicho, katika Katiba yake (2015), na Kanuni za uendeshaji toleo la 2012, kimebainisha misingi ya itikadi yake kuwa binadamu wote sawa, binadamu wanastahili kuwa huru na kulinda utu wao bila kukandamizwa na mtu yeyote kwa misingi rangi, kabila na jinsia.

Ameeleza kuwa dhumuni ya hii sera ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na maamuzi ili kuweza kuonesha ujuzi wao katika uongozi licha ya baadhi ya jamii kuamini wanawake hawawezi katika uongozi na kufanya maamuzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe amesema wamependezwa na uwasilishwaji wa rasimu ya sera ya Jinsia ya Chama hicho hivyo basi watahakikisha sera hiyo inatekelezwa ndani ya chama na wataanza kutafuta rasilimali fedha kwaajili ya kutekeleza sera hiyo.

Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim Rungwe akipendekez jambo mara baada ya Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) kuwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja na Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama hicho kutoka kwa Mwezeshaji wa TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share:

Video : LUKUBHA LUGOSHA - NYABHULUGUTU

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger