Saturday, 11 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 11,2023























Share:

Friday, 10 March 2023

BRELA YATOA UFADHILI KWA WANAFUNZI 5 WANAOSOMA ‘MASTERS’ YA MILIKI UBUNIFU

 

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi watano ambao wanasoma Shahada ya Uzamili katika fani ya Miliki Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Akikabidhi hundi hizo za ufadhili leo Machi 10, 2023 Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amesema kuwa Wakala inafanya kila jitihada kuhakikisha watalaamu wanaongezeka na elimu ya Miliki Ubunifu inawafikia watu wengi zaidi.

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamefanikisha kuwepo kwa mafunzo hayo ya Miliki Bunifu ambayo kwa kiasi kikubwa yataongeza uelewa na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

“Ndugu Waandishi wa Habari tumetoa ufadhili huu kwa kuzingatia jinsia na makundi maalum na kwa awamu hii tumefadhili wanafunzi watano na kiasi cha Shilingi Milioni Kumi na Sita Laki Tano na Elfu Hamsini (16,550,000/=) Kimetolewa”, amesema Bw. Nyaisa.

Amewataja wanafunzi hao waliopata ufadhili kuwa ni pamoja na Bi. Grace Ezekiel Mwaikono kutoka Mahakama Kuu, Bw. Stanslaus Aidan Kigosi kutoka BRELA, Bw. Addo November Mwasongwe kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Eric Maximillian Mlasani kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Bi. Merciana Nehemiah Ntabaye kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Vilevile, ametaja lengo la ufadhili kwa wanafunzi hao kuwa ni kupanua wigo wa utaalamu katika nyanja ya Miliki Ubunifu kwakuwa eneo hilo muhimu halina wataalamu wengi hapa nchini, kuongeza ufahamu kuhusu Miliki Ubunifu kwa maendeleo chanya ya Taifa la Tanzania kutokana na umuhimu wake katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa ufadhili huo utahamasisha wanufaika kutambua faida zinazopatikana kutokana na elimu kuhusu Miliki Ubunifu na jinsi ya kuitumia katika kuendeleza na kukuza Ubunifu nchini, kuweka mkazo mahsusi katika muunganisho wa sheria na sera za Miliki Ubunifu katika muktadha wa mienendo iliyopo ya kiuchumi na kijamii inayopatikana barani Afrika.

Kwa upande wake Dkt. Sosthenes Materu, ambaye ni Amidi wa Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewashukuru BRELA kwa ufadhili huo sambamba na jitihada za Taasisi hiyo katika kuendeleza Miliki Ubunifu kwa ajili ya kuchochea maendeleo.

Mwailishi wa wanufaika wa ufadhili wa BRELA ambaye ametoka katika kundi la watu wenye mahitaji maalumu Bw. Erick Maximillian Mlasani, ameishukuru BRELA kwa ufadhili huo na kuahidi baada ya kuhitimu watakuwa miongoni mwa wataalamu watakaojitoa kwa jamii ili elimu ya Miliki Ubunifu ifike mbali zaidi.


Share:

PINDA ATAKA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KUONGEZA MADUHULI YA SERIKALI


Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiongea na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akiteta na jambo na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Makamishna Wasaidizi wa Ardhi Nchini wakifuatilia jambo leo Jijini Dodoma katika Kikao Kazi kilichowakutanisha pamoja ili kujadili namna bora ya ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la Ardhi.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara pamoja na Makamishna Wasaidizi wa Ardhi mara baada ya kufunga kikao kazi na viongozi hao Jijini Dodoma.

Na: Anthony Ishengoma- Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Bw. Makazi Geofrey Pinda amesema vipaumbele vya Wizara kwa sasa ni kuongeza kasi ya ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la Ardhi lakini kuboresha mawasiliano kati ya watendaji ardhi walioko katika Ngazi ya Halmashauri.

Naibu Waziri Pinda amesema kuna changamoto ya mawasiliano kati ya watendaji Sekta ya Ardhi walioko katika Halmashauri mbalimbali nchini kwani wengi wamekuwa wakiwajibika kwa mamlaka za Serikali za Mitaa badala ya Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa na kusahau kuwa mwajili wao ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri Pinda amesema kwa muda mfupi tu aliokaa Wizarani amegundua kuwa kuna changamoto hiyo kutokana na mamka za kupanga na kumilikisha ardhi kuwa katika Halmashauri husika wakati mwajili wa wataalam hao ni Wizara ya Ardhi jambo lilopelekea uwepo kwa changamoto hii.

Pinda amesema hayo mapema Jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Anthony Sanga pamoja na Makamishna Waasaidizi wa Miko na Waratibu Mikoa ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi hao kuwasilisha maoni ili sheria ya ardhi iweze kuboreshwa katika mapitio ya sheria yaliyoko kwenye mchakato.

Aidha Naibu Waziri Pinda amesema ipo haja ya kupitia muhundo upya wa watumishi hao ili ikiwezekana waweze kuwajibika kinidhamu kwa Kamishna Msaidizi wa Mikoa ili kuongeza uwajibikaji kiutendaji ili kusaidia Kamishna huyo kutekeleza kazi zake ipasavyo.

Suala lingine alilogusia kiongozi huyo nikuhimiza uwajibikaji wa pamoja wa watumishi walioko katika ofisi za mkoa bila kujali kada zao kwani wote kwa pamoja wanafanya kazi katika Sekta ya Ardhi hapa Nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga aliwambia watendaji hao kuwa kipaumbele chake ni kuongeza makusanyo ya kodi ya ardhi na kwamba yeye kila atakapita katika Ofisi za Ardhi Mkoa ataomba kupatiwa takwimu za makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Sanga ameongeza kuwa tayari timu ya wataalam wa Tehama na wengine wako kazini kutengeneza mfumo mpya na rafiki utakaowawezesha watanzania kulipa kodi ya ardhi kupitia miamala ya simu tofauti na sasa ambapo wananchi wanalazimika kupanga foleni katika Ofisi za Wizara Mikoani kwa ajili ya kulipa kodi.

Eng. Sanga amewataka waratibu wa Kodi Mikoani kote kuwa na takwimu sahihi za walipa kodi ikiwemo kuwatambua wote ikiwemo wale ambao hawajarasimisha ardhi yao ili waweze kuingiza katika mfumo wa walipa kodi kama ilivyo katika miamala ya Mamlaka za maji hapa Nchini.

Eng. Sanga amesema timu ya wataalam tayari iko kazini ikifanyia kazi mfumo wa ukusanyaji mapato ambao utakuwa ni wa aina moja nchi nzima tofauti na sasa ambapo mifumo ya ukusanyaji mapato inatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine suala ambalo amesema litaongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia Pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi anakutana na Makamishna wa Ardhi Nchini pamoja na Waratibu wa Kodi kutoka Ofisi za Wizara ya Ardhi walioko mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kupeana taarifa likini pia kukumbushana masuala muhimu ikiwemo yatakonayo na Mkutano wa awali uliowakutanisha mjini Morogoro hivi karibuni.
Share:

TUCTA: UWEKEZAJI KATIKA USALAMA NA AFYA UNALIPA


Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji wa OSHA, Bw. Joshua Matiko akiwasilisha mada juu ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi katika kikao cha Baraza Kuu la TUCTA unaofanyika Mkoani Morogoro.

Wajumbe wa Baraza Kuu la TUCTA wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji wa OSHA, Bw. Joshua Matiko inayohusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.


Mjumbe wa Baraza Kuu la TUCTA akimuuliza swali mwasilishaji mada kutoka OSHA ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji, Bw. Joshua Matiko wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Viongozi wa wafanyakazi wa TUCTA Mkoani Morogoro.


Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji wa OSHA, Bw. Joshua Matiko akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wajumbe wa Kikao cha Baraza Kuu la TUCTA

*********************

Na Mwandishi Wetu

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limetoa wito kwa maeneo ya kazi nchini kuzingatia taratibu zote za usalama na afya mahali pa kazi ili kulinda nguvukazi na mitaji iliyowekezwa jambo ambalo litapelekea tija kupatikana katika uzalishaji.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Hery Mkunda, wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la TUCTA unaofanyika Mkoani Morogoro (Machi 9 na 10, 2023) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo usalama na afya mahali pa kazi.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Mkunda amesema maeneo ya kazi yanapokuwa salama na wafanyakazi wake kuwa na afya njema ni dhahiri kwamba shughuli za uzalishaji zitafanyika kwa ufanisi mkubwa hivyo tija kuongezeka.

“Usalama na afya katika maeneo ya kazi ni jambo muhimu sana kwetu sisi wafanyakazi na waajiri pia. Hivyo basi, tunapokuwa na mazingira salama kazini morali ya kufanya kazi inakuwa juu na hivyo kupelekea kujituma zaidi katika uzalishaji jambo ambalo lina faida kwetu sisi kama wafanyakazi na kwa wawekezaji pia,” alisema Bw. Hery Mkunda na kuongeza:

“Kikao hiki ni cha Baraza Kuu la Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchi nzima kutoka Taasisi binafsi na za umma hivyo tumeona kuna umuhimu mkubwa sana kwa viongozi hawa kupata elimu ya usalama na afya mahali pa kazi kwasababu wao ni wawakilishi wa wafanyakazi wenzao katika mambo mbalimbali vikiwemo vikao vya maamuzi ya utekelezaji wa masuala mbali mbali likiwemo suala zima la usalama na afya mahali pa kazi.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bw. Joshua Matiko, ambaye aliwasilisha mada ya usalama na afya katika kikao hicho, amesema elimu hiyo kwa viongozi hao imetolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taasisi ya OSHA wa kuyafikia makundi mbalimbali ya watu.

Aidha, ameeleza kwamba uelewa waliojengewa viongozi hao katika mkutano huo utawawezesha viongozi hao kujenga hoja kwa waajiri nchini ili kuboresha mazingira ya ya kazi katika sekta mbali mbali za kiuchumi.

“Viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wanajukumu kubwa na muhimu la kutetea wafanyakazi wenzao katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la kuboresha mazingira ya kazi. Hivyo, ili waweze kutoa hoja zenye mashiko kwa waajiri wao ni lazima wawe na uelewa wa kutosha juu ya suala zima la usalama na afya. Matarajio yetu baada ya mafunzo hay ani kwamba watakaporudi katika maeneo yao ya kazi watafikisha elimu hii kwa wafanyakazi wenzao kupitia kamati za usalama na afya walizoziunda,” amesema Bw. Matiko.

Aidha, viongozi na wajumbe wa baraza hilo wameishukuru sana OSHA kwa kutoa elimu katika kikao hicho na kukikiri kuwa elimu hiyo imewaongezea hamasa ya kuzingatia masuala ya usalama na afya huku wakiahidi kufikisha elimu hiyo kwa wafanyakazi wenzao watakaporejea katika maeneo yao ya kazi.

“Kimsingi nimefurahishwa sana na hii mada ya OSHA kwasababu sisi kama wawakilishi wa wafanyakazi inatusaidia kusimamia misingi ya usalama na afya katika maeneo yetu ya kazi na pia itakuwa chachu katika kuwahamasisha wale tunao wasimamia na kuwaongoza kwenye vyama vyetu. Nawasihi viongozi wote waliohudhuria kikao hiki kupeleka elimu hii kwa wafanyakazi ili waweze kuwa na uelewa wa namna gani wataweza kujikinga dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi” alisema Mkamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Tanzania (TUGHE), Bi. Jane Madete.

Kwa upande wake Bw. Chrispin Ng’weng’we ambaye ni mjumbe wa Baraza hilo kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), amesema kuwa elimu hiyo imewajengea weledi wa kutambua haki zao

“Elimu hii imetutoa ukungu na kutujengea weledi juu ya mambo tuliyokuwa hatuyafahamu mfano baadhi ya wafanyakazi wanapata madhara wakiwa kazini lakini hawatambui haki zao hivyo basi sisi kama wawakilishi wa wafanyakazi tunalo jukumu la kuhakikisha elimu hii inawafikia wafanyakazi wenzetu,” alisema Bw. Chrispin Ng’weng’we.
Share:

VIDEO NA NYIMBO ZA HOVYO MARUFUKU KWENYE MABASI YA SHULE


Basi la shule

Wizara ya Elimu imepiga marufuku kuwekwa kwa miziki, nyimbo ama picha za video zinazokwenda kinyume na maadili, mila, desturi na tamaduni katika mabasi yanayotumika kusafirisha watoto kuwapeleka shule, badala yake ziwekwe nyimbo au video zenye kujenga maadili na uzalendo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa, na kusema kuwa wamiliki wote wa shule wenye kutoa huduma za usafiri kwa wanafunzi pia wahakikishe vitendo vya ukatili kwa wanafunzi wakiwa kwenye magari au mabasi vinakomeshwa.

Aidha Wizara ya Elimu pia imewataka wamiliki hao kuhakikisha kwamba magari au mabasi yao yanayotumika kusafirisha wanafunzi yanakuwa na vioo angavu na sio tinted.

Waraka huo umelenga kuboresha huduma za usafiri wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi wakati wa kurudi ama kwenda shuleni, kufuatia uwepo wa watoa huduma katika magari hayo kuwa na tabia za viashiria vya kuleta mmonyoko wa maadili, kuathiri ukuaji, ujifunzaji na kuhatarisha ustawi wa watoto kiujumla.

Ikumbukwe hivi karibu kupitia mitandao ya kijamii ilisambaa video fupi ikionesha watoto wadogo waliokuwa kwenye gari la shule wakiimba nyimbo ambazo hazileti afya nzuri katika ukuaji na ustawi wa maadili kwao.

CHANZO - EATV
Share:

AUABC : PAP PLAYS A PROMINENT ROLE IN COMBATING CORRUPTION



The African Union Advisory Board Against Corruption (AUABAC) says the noble role of the Pan-African Parliament (PAP) as it relates to the ongoing fight against corruption in Africa is vital.


“The importance of PAP as one of the major key stakeholders in the fight against corruption cannot be over-emphasised,” said Mrs. Charity Nchimunya, Executive Secretary at the Advisory Board on Corruption (AUABC) during a presentation to the PAP Committee on Audit and Public Accounts (CAPA) of the PAP.


“The importance of PAP as one of the major key stakeholders in the fight against corruption cannot be over-emphasized. PAP plays a pivotal role in the ongoing fight against corruption in the Continent. We must all bear in mind that the PAP represents all the people of Africa and pursues the objective of facilitating the effective implementation of the policies and objectives of the AU as well as promoting the principles of human rights and democracy in Africa.”

Titled “The Role of PAP in Promoting Transparency and Accountability and Fighting Corruption within the Continent”, the presentation transpired at the ongoing Sitting of the Permanent Committees, which are being held under the African Union Theme of the Year for 2023, “The Year of AFCFTA: Accelerating the Implementation of the African Continental Free Trade Area”.

Mrs. Nchimunya encouraged the African legislators to promote and strengthen the development of mechanisms to prevent, detect, punish, and eradicate corruption in both the Public and Private sectors.

“We always seek that as parliamentarians you promote, facilitate and regulate cooperation among the State Parties to prevent, detect, punish and eradicate corruption. You need to coordinate and harmonise policies and legislation between State Parties for purposes of prevention, detection punishment and eradication of corruption,” she added.

She further mentioned that for growth to be experienced in the continent, African legislators must as well promote socio-economic development by removing obstacles to development and foster transparency and accountability in the management of public affairs.

Mrs. Nchimunya also believes that for the fight against corruption to be won, PAP must lobby and involve the African citizenry.

“We need a collective effort to win this battle against corruption. PAP members must go out and encourage citizens’ confidence in the fight against corruption and try to protect whistle-blowers and informants. We need also to promote public awareness and education; create a conducive environment for participation of CSOs and Media, promotion of ethics,” she said calling for effective public management systems like auditing, accounting, hiring, procurement, customs and revenue etc.

Commenting on the presentation, CAPA Chairperson Hon. Miles Sampa from Zambia mentioned that corruption must be tackled at all levels and spheres.

“The challenge is not only about corrupt individuals, but those who assist them in keeping their loot. We have banks in Europe, America, the Middle East and Asia that are accomplices of corrupt African people. If we are to fight and win this war, we need to take this war to the people who work hand in hand with corrupt individuals. Let us destroy these havens where our looted monies and resources are kept. Then we will never have people who choose a corrupt path as they will not have anywhere to hide their loot,” added Hon. Sampa.

Hon. Ng’wasi Kamani from Tanzania encouraged the empowerment of the African Court if corruption is to be defeated.

“As a continent, we need to capacitate the African Court on Human and Peoples' Rights. We are not doing much to realise the role and importance of our court. Our continental court must be given more powers to act over mere talking. We also need other AU organs to be empowered to act decisively as opposed to their current advisory roles,” she emphasized.

-Ends-

Share:

SHOTI YA UMEME YAUA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA NYUMBA IKIUNGUA SHINYANGA


Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Old Shinyanga Rashid Mashaka miaka 14 amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala kuungua moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 10 majira ya saa 6 usiku katika kitongoji cha Senyenge kata ya Old Shinyanga baada ya shoti ya umeme kutokea katika nyumba hiyo kisha moto kuwaka na kuunguza vitu mbalimbali wakati kijana huyo akiwa amelala ndani.

Mama mzazi wa mtoto huyo Fatuma Rajab ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo amesema mvua zilizonyesha jana zilisababisha umeme kukatika na uliporejea majira hayo ndipo shoti hiyo ilipotokea kisha nyumba yake kushika moto.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Inspekta Stanley Luhwago amesema kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye mita ya nyumba hiyo.

Kijana huyo alikuwa akisoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Old Shinyanga.

Chanzo- AZAM TV
Share:

Thursday, 9 March 2023

KAMATI YA SIASA YA CCM IMESELA YATAKA WATOTO WALE CHAKULA SHULENI


Diwani wa kata ya Imesela Seth Msangwa akizungumza katika maadhimisho ya ziara ya kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) Imesela Wilaya ya Shinyanga.
Kamati ya siasa na uongozi wa shule wakiendelea na kikao cha kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi.

 Na Halima Khoya,Shinyanga.

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela  Halmashauri ya Shinyanga imeutaka uongozi wa Shule ya Msingi Mwamanyuda pamoja na kamati ya shule hiyo kuhakikisha watoto wanapata huduma ya chakula wakiwa shuleni ili kuongeza ufaulu kitaaluma.

Kamati hiyo imetoa agizo hilo katika kilele cha ziara ya Kamati ya chama Cha Mapinduzi iliyoanza Machi 7,2023 na kumalizika Machi 9 Mwaka huu kwa lengo la kutembelea taasisi mbalimbali na kukagua miradi iliyopo na kuangalia maendeleo na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Imesela,  Sebastiani Mwigulu  amesema ili kulijenga Taifa la baadae ni lazima kutoa elimu bora kwa watoto kwanzia shule ya msingi hadi sekondari sambamba na kupata lishe bora ili kuwa na  afya ya akili.

Hata hivyo Sebastian ameitaka kamati ya shule hiyo kuitisha kikao cha wazazi kwa ajili ya kuchangia fedha au nafaka kwa wanafunzi kupata chakula wakiwa shuleni hali itakayosaidia kuondokana na adha la utoro kwa wanafunzi.

Kwaaupande Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwamanyuda, Charles Mmasa amesema awali waliitisha kikao na wazazi kwa ajili ya kuchangia chakula shuleni lakini wazazi hao waliikataa hoja hiyo kwa kudai hali ngumu ya maisha huku akiiomba kamati ya chama kutumia nafasi zao kuwahamasisha wazazi kutoa mchango wa chakula kwa watoto.

Jumanne Bundala na Christina Salehe ni wanafunzi katika shule ya Mwamanyuda ambao wameeleza ugumu wanaokabiliana nao kwa kusoma kuanzia asubuhi hadi jioni bila kupata chakula hali inayowafanya wasielewe masomo yao na kupelekea kufeli kwenye masomo yao.

"Tunapata changamoto nyingi sana tuwapo shuleni tunashinda njaa, hatuelewi masomo, tunawaombaa wazazi mjitokeze kuchangia chakula,na Serikali itusaidie kupata chakula ili tusome vizuri na kufaulu"amesema Bundala.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Imesela, Seth Msangwa amesema kuwa ili kutatua suala la chakula shuleni ni lazima kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake kwa watakaoenda kinyume na makubaliano ya kuchangia chakula na kwamba wanawadumaza watoto kiakili kwa kukosa lishe bora.

"Suala la kupata chakula lipo ndani ya uwezo wetu,kile ambacho watoto walipaswa wale nyumbani ni sawaa sawa na kile ambacho watakula shuleni,iwe wakati wa njaa au hali ngumu basi kuchangia wazazi chakula inawezekana", amesema Msangwa.

Share:

Video Mpya : AMOS MALINGITA - EDINA

Share:

Video Mpya : NTEMI OMABALA - MAKUMBUSHO CENTER

Share:

BARRICK NORTH MARA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA MADINI


Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido (kulia) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko (kushoto) wakiwalisha keki viongozi wa Wanawake katika mgodi huo wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk. Melkiory Ngido,akishiriki kukata keki wakati wa hafla ya wanawake wa mgodi huo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido, akiongea na Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa North Mara wakati wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko,akiongea katika hafla hiyo.
Wanawake wa Barrick wakiandamana kuadhimisha siku ya wanawake duniani
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick North Mara, wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido( katikati) na Meneja Mkuu wa mgodi huo,Apolinary Lyambiko wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mgodini hapo.

***

Meneja Mkuu wa Barrick Tanzania, Dk. Melkiory Ngido ,amewataka Wanawake kijiamini na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini.


Akiongea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye mgodi wa Barrick North Mara, Dk. Ngido alisema Barrick, inayo programu maalumu ya kuwapa wanawake kipaumbele katika suala la ajira , kuwajengea uwezo wa shughuli za uchimbaji madini na kuwajengea mazingira bora zaidi ya kazi.


“Msijisikie kuwa second class (daraja la pili), onesha kuwa mnaweza na naamini uwezo mnao,” alisema Ngido katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Wafanyakazi Wanawake kutoka mgodi huo.


Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa mgodi huo,Bw.Apolinary Lyambiko, alisema anafurahishwa kuona idadi ya wafanyakazi wanawake katika mgodi huo imeongezeka uliganisha na miaka ya nyuma, na amewamiminia sifa kwamba wengi wao wanaonesha bidii na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kazini.


“Takwimu za mwaka jana 2022 na sasa zinaonesha kuna ongezeko la wafanyakazi wanawake katika mgodi wetu, na wengi wao wanafanya kazi nzuri. Hivyo tutaendelea kuwapa fursa, siyo tu kujishughulisha na uchimbaji, bali na kuwamotisha pia,” amesisitiza Lyambiko na kuwataka kuendelea kuonesha uwezo mkubwa kazini na kujenga tabia ya kujiamini.


Lyambiko, alisema pia mgodi utaendelea kutekeleza sera yake ya kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakuwa katika kiwango cha sifuri katika mgodi huo.


Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi wanawake wa mgodi huo walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili mada mbalimbali za maendeleo sambamba na kupata burudani na kufurahi pamoja.
Share:

DART WANAWAKE WAIPIGA JEKI HOSPITALI YA MBAGALA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Mwenyekiti wa Wanawake wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mwanamvua Stambuli akizungumza mara baada ya Kukabidhi msaada Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Ally Makori akizungumza mara baada ya Kukabidhiwa msaada kutoka DART ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.

Mwenyekiti wa Wanawake DART Mwanamvua Stambuli akikabidhi moja ya Msaada kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.

Baadhi ya picha mbalimbali ya Wanawake wa DART katika Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu walipokwenda kutoa msaada kwenye maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila machi 8 ya Kila Mwaka.

**************

Na Mwandishi Wetu

Wanawake wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Elimu ya Biashara (CBE) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vitu mbalimbali Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu kwa kuonyesha upendo kwa wananchi katika kujali afya zao.

Akizungumza wakati wa Kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Wanawake wa DART Mwanamvua Stambuli amesema kuwa msaada huo ni kutokana na kutambua umhimu wananchi wa Mbagala kwani siku za usoni watakuwa wateja wa kutumia huduma za usafiri wa mabasi yao.

Amesema wanawake wa DART wameguswa kipekee na kujitoa kwa wanawake wanaojifungulia hapo kupata msaada wa mahitaji mbalimbali.

Msaada wa DART unamegharimu shilingi milioni Nane kwa kununua mashuka 40 , Baiskeli ya kubebea waginojwa , Sabunj ya vipande, sabuni ya unga , Dawa ya Mswaki, pamoja na mashine mbalimbali

Aidha amesema katika msaada waliotoa utasaidia kutatua baadhi ya changamoto kwani kama wanawake wametambua ni mahitaji wanawake ikiwemo mashuka kwa ajili ya hospitali hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema licha ya kutoa msaada huo kwani itakuwa ndio mwendelezo kutokana na kutambua mahitaji ya hospitali hiyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Ally Makori ameshukuru msaada huo na kutaka baadhi ya Taasisi kuiga mfano mzuri kwa DART.

Amesema hospitali hiyo wanawake wanaojifungua katika hospitali hiyo kwa siku ni kati 30 hadi 40 hivyo msaada huo ni mkubwa kutokana na mahitaji ya wanawake hao.

Mmoja ya Mwanamke aliyejifungua katika Hospitali Asha Hamis amesema msaada huo kwao ni mkubwa kwani maadhimisho hayo yamegusa wanawake tulifika katika hospitali hiyo.

Share:

WAFANYAKAZI WANAWAKE GGML WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HALMASHAURI YA GEITA

Mmoja wa wafanyakazi wanawake wa GGML kutoka idara ya uchakataji dhahabu, Rehema Lusendamila (kushoto) akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa katika Kituo cha Afya Kasota (kulia). Katikati ni Lina Sitta - Makamu mwenyekiti wa kikundi cha wafanyakazi wa kike wanaofanya kazi katika kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML ladies).  Kikundi hicho kimegawa msaada wa vifaa tiba na mahitaji mbalimbali kwa kituo cha afya Kasota na hospitali ya Nzela Geita.


 
 KIKUNDI cha wafanyakazi wa kike wanaofanya kazi katika kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML ladies) wanaofanya kazi mjini Geita, wametoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kina mama wajawazito na wazazi wanaojifungua katika hospitali ya Nzela na kituo cha Afya Kasota zilizopo katika halmashauri ya Wilaya Geita.
 
Akizungumzia msaada huo uliotolewa jana Mjini Geita, Makamu mwenyekiti wa kikundi hicho, Lina Sitta alisema wanawake wanaofanya kazi GGML wameguswa na changamoto za uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya katika vijiji vinavyowazunguka.
 
“Tumeona kwa sasa tuanze na vijiji vya Kasota na Nzela ambavyo vipo karibu zaidi na mgodi wa GGML na tumekuwa tukiona changamoto ya akina mama kukosa sabuni,taulo za mama waliojifungua na nepi za watoto.Msaada huu tumeutoa maalum kuadhimisha siku ya wanawake duniani," alisema.
 
Mganga Msaidizi wa kituo cha afya Kasota, Stanley Victor amewashukuru GGML ladies kwa kutoa msaada huo lakini pia kwa GGML kusaidia ujenzi wa maabara, nyumba ya mtumishi na jengo la baba na mtoto kituoni hapo.
 
“Mmeitendea haki siku ya wanawake duniani mwaka huu.Wagonjwa wengi waliopo hapa wamefarijika sana kutokana na msaada huu,”alisema.
 
Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 9,2023



























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger