Wednesday, 1 February 2023

MA DC WAPYA WAAPISHWA SHINYANGA, RC NAWANDA AONYA WAKUU WA WILAYA KUGOMBANA NA WATUMISHI, ATOA MTIHANI WA KWANZA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (kulia) Dk. Yahaya Nawanda akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita mara baada ya kumaliza kumuapisha.
Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda, amewapa mtihani wakuu wa wilaya mkoani humo, hadi kufika siku ya Jumatatu wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wawe wamesharipoti shule.

Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, amebainisha hayo leo Februari 1, 2023 kwenye hafla ya kumuapisha Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita, ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.

Amesema mtihani wa kwanza ambao wanawapa wakuu wa wilaya wapya mkoani Shinyanga akiwamo na Mwenyeji Joseph Mkude wa Kishapu, kuwa wakafanye kazi ya kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shule, bila ya kujali wana sare za shule au hakuna wote waanze masomo.

“Hadi kufikia siku ya Jumatatu nataka wakuu wa wilaya wote wa Shinyanga mnipatie taarifa kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wapo shuleni na huu ndiyo utakuwa mtihani wenu wa kwanza,”amesema Nawanda.

“Kafanye hiyo kazi kwa kushirikiana na Maofisa Elimu, Wakuu wa Polisi wilaya, Maofisa Tarafa na Wakurugenzi na hakuna kiongozi yeyote kutoka nje ya Mkoa hadi watoto wote waripoti shule,”ameongeza.

Amesema Rais Samia ametoa fedha nyingi katika Sekta ya Elimu ikiwamo kuboresha miundombinu ili watoto wapate elimu na kutimiza ndoto zao, hivyo wao kama wasaidizi wake wanapaswa kusimamia watoto wote wanapata elimu na Taifa hapo baadae kuja kupata viongozi na wataalamu.

Amewataka pia wakuu hao wa wilaya wasiende kugombana na watumishi, bali waende wakafanye kazi kwa ushirikiano pamoja na kugusa maisha ya wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua ikiwamo na migogoro ya ardhi.

“Msiende kuwa watu wa maofisini kakagueni miradi ya maendeleo na kuisimamia, na mtende haki kwa wananchi ili kuhakikisha wilaya zenu pia zinakuwa salama,”amesema Nawanda.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya mkoani Shinyanga, wakafanye kazi kwa ushirikiano na watendaji wote wa Serikali pamoja na kushughulikia malalamiko ya wananchi na kutatua kero zilizopo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, ameshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Mkuu wa wilaya hiyo, huku akiahidi kuitumikia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi ambaye yeye hakuapishwa ikiwa amehamishwa kutoka wilaya ya Kwimba, alisema hatakuwa mtu wa Ofisi bali atakuwa wa kwenda site kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku akiomba ushirikiano kwa viongozi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Yahaya Nawanda akizungumza mara baada ya kumaliza kumuapisha Mkuu wa wilaya Mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya Mpya wa Kahama Mboni Mhita akizungumza mara baada ya kumaliza kuapishwa.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi ambaye amehamishiwa kazi kutoka wilaya ya Kwimba akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.
Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari 1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.
Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkuu wa wilaya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi, na Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi, kwenye uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkurungezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy.

Picha ya Pamoja ikipigwa mara baada ya zoezi la uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita kumalizika.

Share:

MAADHIMISHO WIKI YA SHERIA YAFUNGWA SHINYANGA....JAJI KILATI ATAKA USULUHISHI, "TUACHE KUTUNISHIANA MISULI MAHAKAMANI"

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Na  Halima Khoya  na Kadama Malunde - Shinyanga

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati amewataka Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea wawasaidie wateja wao kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani inaleta tija ili kuondokana na mrundikano wa mashauri, kupunguza chuki, kuokoa muda kutekeleza shughuli za maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi endelevu badala ya kuwaacha watunishiane misuli Mahakamani.

Jaji Kilati ametoa rai hiyo leo Jumatano Februari 1,2023 wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga yakiongozwa na Kauli Mbiu inayosema “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau”.

Jaji Kilati amesema Mawakili ni wadau wakubwa kwa kesi za madai na jinai hivyo ni vyema wakajitahidi kumaliza mashauri kwa njia ya usuluhishi kwa wateja wao kufanya mazungumzo ili kumaliza kesi na kuokoa rasilimali zao pamoja na kuondoa tofauti za migogoro katika mioyo yao.

Pia amewataka wananchi na viongozi wa kiutawala waonapata kesi nyingi za migogoro watatue migogoro kwa njia ya usuluhishi.

“Mawakili wa serikali na kujitegemea wasaidieni wananchi kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kuwasaidia kuokoa muda wakatekeleze shughuli za uchumi, kujenga undugu, kusaidia jamii inayowazunguka kwani migogoro inaleta uadui na chuki. Msiwaache watunishiane misuli mahakamani, tunataka mpoze hiyo misuli”,amesema Jaji Kilati.
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema faida za utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni pamoja na migogoro kumalizika mapema na haraka, ni njia rafiki kwa wadau wote kumaliza mgogoro, inaondoa tofauti za kimigogoro na chuki, tofauti na shauri kupelekwa mahakamani na Wadau wote kwenye shauri wanakuwa washindi kwa sababu wanakuwa wameafikiana kwa pamoja.

“Mahakama inatakiwa itoe haki bila kuchelewesha kwani ni wajibu wetu kikatiba . Utatuzi wa migogoro kwa Usuluhishi ni njia ambayo wadau wote kwenye shauri huwa ni washindi tofauti na kupelekana mahakamani ambako kila upande hutunisha misuli ili kuibuka mshindi”,amesema.

Ameeleza kuwa Migogoro katika jamii inasababisha mdororo wa uchumi na ili kuwa na uchumi endelevu ni vyema njia za usuluhishi zitakatumika kumaliza mashauri akisisitiza kuwa Mahakama inasisitiza usuluhishi iwe kipaumbele cha kutatua migogoro ili kuokoa muda na rasilimali.

“Japo bado mwitikio wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ni mdogo kutokana na wananchi kutotambua umuhimu wa kumaliza kesi kwa kuafikiana. Tusiendeleze migogoro kiasi cha kuathiri uchumi kwani wapo watu wanapenda kutunishiana misuli mahakamani na kesi zinachukua muda mrefu kukamilika, tunapoteza muda”, amesema Jaji Kilati.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akikagua Gwaride  kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.

Katika hatua nyingine amesema Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imefanikiwa kumaliza mashauri ya Mrundikano ambapo hivi sasa hakuna hata shauri moja la mrundikano na inaendelea kumaliza mashauri ya kawaida

“Tunahitaji nguvu za pamoja kumaliza kesi hizi za kawaida ambapo njia nzuri ya kumaliza migogoro ni usuluhishi”,ameongeza Jaji Kilati.
Muonekano wa mbele jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga

Kwa upande wake, Wakili wa serikali Mwandamizi Solomon Lwenge amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wote kwa kuendelea kuongoza vyema katika kuwaletea maendeleo wananchi na hali bora ya maisha.

Amesema pamoja na kuwapata waendesha usuluhishi, majadiliano, maridhiano na upatanishi 494 nje ya maafisa wapatanishi ambao ni waheshimiwa mahakimu majaji wengine waliopo kwa mujibu wa sheria bado idadi ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya nchi.

“Uhalisia uliopo ni kwamba ukiondoa migogoro yenye asili ya madai iliyopo kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba na mahakama za mwanzo yapo zaidi ya mashauri 15,000 ya madai ya aina mbalimbali ambayo hayajaisha katika mahakama za mahakimu na zile za juu yake”,amesema Lwenge.

“Hivyo kwa mazingira haya naamini wakati umewadia wa kuboresha tena sheria ya mwenendo wa madai sura ya 33 ili shauri la madai lipate sifa ya kusajiliwa mahakamani endapo kuna uthibitisho kwamba limepita hatua ya usuluhishi”,ameongeza Lwenge.

Amesema Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali zitaendelea kusimamia vyema kwa niaba ya serikali matakwa ya sheria ya kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Moses Chilla aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amesema serikali imeweka madawati ya kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi na mirathi kwa njia ya usuluhishi ili kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na upendo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea (TLS) Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, Shaban Mvungi amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini kwa kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara huku akiwahamasisha Mawakili wa kujitegemea na Serikali kuongeza kasi ya kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani migogoro inakwamisha maendeleo na kuongeza uadui katika jamii hivyo ni vyema migogoro ikatatuliwa nje ya mahakama.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Sheria akiwemo Simon Mboje na Rehema Chimiyu wamesema utatuzi wa migogoro kwa njia kutasaidia kuondokana na adha ya kesi kuchukua muda mrefu huku wakiwaomba baadhi ya mawakili wasio waaminifu kuacha udanganyifu na kuendekeza tamaa ya pesa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga

Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga, Seif Mwinshehe Kulita akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Warsha Silvester Ng'humbu akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Moses Chilla aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, Shaban Mvungi akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wakili wa serikali Mwandamizi Solomon Lwenge akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akikagua Gwaride wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Kwaya ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ikitoa burudani wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Wafanyakazi wa Mahakama wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yakiendelea
Wadau wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Msanii Chap Chap akitoa burudani kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakisoma shairi kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yakiendelea
MC Amos Events maarufu MC Mzungu Mweusi akisherehesha  Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Picha ya kumbukumbu kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria

Picha ya kumbukumbu kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

DHAMANA ZA ZABUNI NA UTEKELEZAJI WA MIKATABA

***************************

Na Zawadi Msalla- PPRA

Kuna msemo usemao mipango siyo matumizi, na sababu kubwa ya watu kusema maneno hayo ni kutokana na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza katikati ya mpango ulio uweka hivyo kupelekea mpango huo kutokutimia au kuchelewa kutimia.

Vihatarishi katika michakato ya ununuzi ni moja ya kikwazo kikubwa katika kufikia azma ya kupata huduma bora katika ununuzi. Vihatarishi vinavyojitokeza katika michakato ya ununuzi hupelekea Malengo ya taasisi nunuzi kuharibika au kuchelewa.

Moja ya kihatarishi kikubwa katika mchakato mzima wa ununuzi wa Umma ni matendo ya wazabuni kujitoa kwenye mchakato wa zabuni na kutotekeleza mkataba wa ununuzi. Hali hii hupelekea taasisi nunuzi kutofikia malengo yake ya kupata bidhaa, huduma na kazi za ujenzi kwa wakati, kwa ubora na kwa gharama nafuu.

Katika kukabiliana na kihatarishi hicho miongozo mbalimbali imewekwa ikiwemo utaratibu wa kudai dhamana za zabuni na utekelezaji wa mikataba ambapo taasisi nunuzi huweka utaratibu wa kudai wazabuni kuwasilisha dhamana za zabuni na utekelezaji wa mikataba..

Dhamana ni kitu cha thamani au tamko linalotoa hakikisho kwa mpokea dhamana kwa ajili ya utatekelezaji wa wajibu fulani kwa mujibu wa makubaliano ili kuepusha kutokea kwa mambo yasiyotakiwa.

Mhandisi. Amini Mcharo ni mkurugenzi wa Idara ya kujenga uwezo na huduma za ushauri kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma(PPRA) anasema Kudai dhamana ni moja ya njia inayotumiwa na taasisi nunuzi Ili kudhibiti hatari ya kutofikia malengo yao kutokana na matendo ya wazabuni.

“Taasisi nunuzi hudai dhamana kutoka kwa wazabuni ili kujihakikishia kuwa wazabuni hawatajitoa katika michakato ya zabuni kabla ya wakati unaoruhusiwa, watakubali marekebisho ya bei zao, watakubali tuzo za zabuni na kutekeleza mikataba ya ununuzi kwa uaminifu” Mhandisi Mcharo anaelezea.

Dhamana hudaiwa kwa wazabuni katika hatua ya mchakato wa zabuni na usimamizi wa mkataba; dhamana zinazodaiwa wakati wa mchakato wa zabuni huitwa dhamana za zabuni na zile zinazodaiwa wakati wa usimamizi wa mkataba huitwa dhamana za utekelezaji wa mkataba.

Akielezea lengo la kudai dhamana ya zabuni Mhandisi Mcharo anasema ni kuhakikisha kuwa mzabuni yoyote aliyeomba zabuni husika, hataondoa zabuni yake kabla ya tuzo ya zabuni kutolewa kwa mzabuni mshindi au kuisha muda wa uhai wa zabuni yake. Pia, atakubali marekebisho sahihi ya mahesabu ya bei yake kama yalivyofanywa na taasisi nunuzi na atakubali tuzo ya zabuni kama itatolewa kwake iwapo atakuwa ndiye mzabuni mshindi.

Dhamana za utekelezaji wa mkataba pia zimelenga kuhakikisha kuwa mzabuni mshindi atatekeleza wajibu wake wa kusambaza bidhaa, kutoa huduma au kufanya kazi za ujenzi kama ulivyoanishwa kwenye mkataba wa ununuzi.

Iwapo mzabuni hatotekeleza mambo ambayo alitoa hakikisho la kuyafanya kwa mujibu wa dhamana aliyoitoa basi huchukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa kushiriki michakato ya zabuni ya taasisi zote nchini au kutaifishwa kwa dhamana iliyowasilishwa.

Pia, akielezea kuhusu aina za dhamana zinazoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma mtaalamu wa ununuzi kutoka PPRA Bw. Frank Yesaya anasema dhamana hizo zimegawanyika katika makundi makubwa mawili, moja ni dhamana ambazo zipo katika mfumo wa kifedha na mbili dhamana ambazo zipo katika mfumo wa tamko.

Bw. Yesaya anaeleza kuwa dhamana za mfumo wa kifedha ni pamoja na dhamana zinazotolewa na benki na mashirika ya bima; wakati dhamana za mfumo wa tamko zinahusisha mzabuni kujaza tamko sanifu lililopo kwenye nyaraka za zabuni husika ili kutoa hakikisho kwa taasisi nunuzi.

“Ni muhimu taasisi nunuzi kuthibitisha uhalali wa dhamana za mfumo wa kifedha zinazowasilishwa na wazabuni kutoka benki au mashirika ya bima yanayotoa dhamana husika” Alisema Bw. Yesaya.

Aidha, akielezea endapo mzabuni ataenda kinyume na dhamana aliyoiweka mtaalam huyo wa masuala ya Ununuzi Bw. Yesaya anaeleza kuwa iwapo mzabuni atakwenda kinyume na dhamana ya mfumo wa kifedha taasisi nunuzi wanayohaki ya kuitaifisha dhamana husika, na kueleza Zaidi kuwa endapo mzabuni akienda kinyume na dhamana ya mfumo wa tamko, taasisi nunuzi wanayohaki ya kuomba mzabuni afungiwe na PPRA ili asishiriki katika michakato ya taasisi nunuzi zingine kwa kipindi kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili.

“Adhabu zinazotolewa kwa kukiuka masharti ya dhamana zimelenga kuhakikisha wazabuni wanakuwa makini katika utekelezaji wa zabuni zao”

Taasisi nunuzi wanaruhusiwa kuomba dhamana za mfumo wa kifedha iwapo thamani ya zabuni au mikataba ya ununuzi imefikia kiwango ambacho kinaruhusiwa kuomba dhamana za kifedha.

PPRA imetoa mwongozo wa dhamana unaotoa maelekezo kwa taasisi nunuzi kuhusu dhamana za zabuni na utekelezaji wa mikataba, kupitia mwongozo huo, imetambulishwa aina mpya ya dhamana ya utekelezaji wa mkataba ambayo ipo katika muundo wa tamko. Kwa kuanzia dhamana hii itadaiwa na taasisi nunuzi kwa mikataba ya ununuzi wa bidhaa, huduma na kazi za ujenzi isiyozidi fedha za kitanzania bilioni moja.

Wazabuni huingia gharama kupata dhamana za zabuni zilizo katika mfumo wa fedha, hivyo ni muhimu taasisi nunuzi kuomba dhamana hizo kwa zabuni ambazo zimefikia viwango vinavyoruhusiwa.

Taasisi nunuzi wanapoaihirisha michakato ya ununuzi huwaingiza wazabuni katika hasara ya kuendelea kukatwa marejesho ya dhamana za kifedha wakati michakato husika ilishafutwa.

Bila shaka wakati utafika dhamana za zabuni zilizo katika mfumo wa kifedha zitaweza kutolewa na benki na kuwasilishwa kwa taasisi nunuzi kupitia mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Share:

MKUU WA WILAYA MPYA KAHAMA MBONI MHITA AAPISHWA

Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari 1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.
Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.
Share:

TFS HAIJAZUIA VIBALI VYA KUKAMILISHA MIRADI YA KIMKAKATI YA KUPELEKA UMEME VIJIJINI- NAIBU WAZIRI MASANJA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kutochelewesha vibali vya kuruhusu umeme kupita kwenye hifadhi za misitu ili kuwahisha usambazaji wa umeme vijijini Bungeni jijini Dodoma leo.

***************************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) haijazuia vibali vya kukamilisha miradi ya kimkakati ya kupeleka umeme vijijini kwa kupitisha nguzo za umeme katika Hifadhi za Misitu nchini.

Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kutochelewesha vibali vya kuruhusu umeme kupita kwenye hifadhi za misitu ili kuwahisha usambazaji wa umeme vijijini.

“Sheria ya Misitu Sura ya 323 haijazuia upitishaji wa nguzo za umeme katika Hifadhi za Misitu hapa nchini” amesisitiza Mhe. Masanja.

Amefafanua kuwa Kifungu cha 26 cha Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002, kimeweka utaratibu kwa taasisi/mtu anayetaka kufanya shughuli mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Msitu na utaratibu huo unamtaka mtu huyo au taasisi kuwa na kibali kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kinachomruhusu kufanya shughuli husika.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali kupitia TFS kwa nyakati tofauti imekuwa ikizishirikisha Wizara za kisekta kukamilisha miradi ya kimkakati ya kupeleka umeme vijijini bila kuchelewa.

Katika hatua nyingine, akijibu swali Mbunge wa Mlimba, Mhe. Godwin Kunambi kuhusu utatuzi wa mgogoro kati ya wananchi na vijiji vya Utengule, Iduindembo, Upinde na Tanganyika na Kampuni ya Uwindaji ya Kilombero North’s Limited katika Jimbo la Mlimba amesema Serikali kupitia Kamati ya Mawaziri nane imeshalitembelea eneo lenye mgogoro kwa lengo la kufanya tathmini na kubaini maeneo halisi yanayostahili kuhifadhiwa kwa maslahi mapana ya Taifa na maeneo mengine wataachiwa wananchi ili waendelee kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger