Tuesday, 10 January 2023

MGODI WA ALMASI MWADUI WAWAHAKIKISHIA WAATHIRIKA WA TOPE WOTE KULIPWA FIDIA

 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.


Na Marco Maduhu, KISHAPU

MGODI wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, umewatoa wasiwasi wananchi ambao ni waathirika wa kubomoka kwa bwawa la mgodi huo la kuhifadhia maji machafu, na kuharibu maeneo yao ikiwamo makazi kufunikwa na tope, kuwa hakuna ambaye hatolipwa fidia.
 
Meneja Mkuu wa Mgodi huo wa Almasi Mhandisi Ayoub Mwenda, amebainisha hayo leo Januari 10,2023 wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu, ambao ni waathirika wa tope la Mgodi, kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ng'wanholo.

Amesema Mgodi huo kwa sasa unasubiri watalaamu wamalize kufanya tathmini, ndipo waanze utaratibu wa kuwalipa fidia waathirika wote, na hakuna mtu ambaye hatalipwa fidia bali wote watapata haki zao kwa mujibu wa sheria.

"Malipo ya fidia yanategemea kukamilika kwa tathmini, hivyo nawaomba wananchi muwe na subira wakati zoezi la tathmini bado linaendelea, na hakuna ambaye hatolipwa fidia bali kila mtu atapata haki anayostahili," amesema Mwenda.

Aidha, amesema tangu tukio hilo la bwawa la mgodi kubomoka Novemba 7 mwaka 2022, licha ya kuendelea na taratibu za tathmini ili wananchi walipwe fidia, pia wameendelea kutoa huduma zote za kibinadamu kwa waathirika ikiwamo chakula, malazi na wanafunzi kuwapatia mahitaji yote ya shule.

Nao wananchi ambao ni waathirika wa tope la mgodi huo akiwemo Elias Mabele mkazi wa kijiji cha Nyenze, na Peter Bundala mkazi wa Ng'wangholo, wamesema tangu litokee janga hilo la bwawa kubomoka, hadi leo hakuna kinachoendelea juu ya kulipwa fidia zao.

Wamesema wamekuwa wakiona watu wanapishana kwenye maeneo yao wakija kuwahoji tangu mwezi Novemba mwaka 2022, lakini hadi sasa Mwezi Januari 2023 bado hawajajua hatima yao na hawana Makazi wala maeneo ya kulima, huku wakishukuru kupewa majibu juu ya hatma ya kulipwa fidia, na kuomba zoezi hilo lifanyika haraka ili wapate haki zao.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almas Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na NyenzeKata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almas Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na NyenzeKata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Bernard Mihayo akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na NyenzeKata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Mwananchi Maimuna Kasala akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Mwananchi Elias Mabele akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Ayoub Mwenda (kushoto) akiwa na Afisa Mahusiano wa Mgodi huo Bernard Mihayo kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.
Share:

NYOTA WA ZAMANI WA CHIPOLOPOLO AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA MBWA WAKE


Nyota wa zamani wa Chipolopolo ya Zambia, Philemon Mulala aliumwa na mbwa wake watatu nyumbani kwake Lichtenburg Afrika Kusini alipotoka nje kuchunguza kwanini mbwa hao walikuwa wanabweka sana baada ya umeme kukatika.

Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, alisema kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.

“Baada ya umeme kurudi , aliingia ndani ya nyumba hiyo akimtafuta mumewe lakini hakumpata, baada ya kuendelea na upekuzi, mwanamke huyo alimuona mumewe akiwa amelala nje kwenye bustani. Kisha akatoka nje kupeleleza kulikoni, na akagundua mume wake alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wao watatu.”

Mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni ‘Cross breed” ya Pitbul na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.

Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos.

Shirikisho la soka la Zambia (FAZ)limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Mulala likisema alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia cha mwaka 1984 kilichoshinda Kombe la East and Central Africa Challenge chini ya ukufunzi wake kanali Brightwell Banda.
Share:

Monday, 9 January 2023

MWANRI ATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

Balozi wa Pamba nchini Tanzania Agrey Mwanri akizungumza kwenye kikao.
Balozi wa Pamba nchini Tanzania Agrey Mwanri akizungumza kwenye kikao.

Kikao cha Pamba kikiendelea.

Na Sumai Salum, KISHAPU

Balozi wa Pamba nchini Tanzania msimu wa mwaka 2022-2023 Agrey Mwanri amewataka viongozi kusimamia wakulima wa zao la pamba kulima kwa kufuata sheria katika maeneo yao ili kuepuka kulima zao hilo kiholela.


Mwanri amesema hayo leo Januari 9, 2023  katika kikao kazi maalum cha kujengeana uwezo kilichowakutanisha watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji,maafsa ugani pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali ngazi ya halmashauri na wilaya katika ukumbi wa SHIRECU wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

“Wakati mwingine kutowajibika kwenu vizuri kunapelekea wakulima kulima kiholela, zao la pamba lipo kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kienyeji sheria No.2 ya mwaka 2001 na ile ya 2011 zilitungwa kanuni 10 moja wapo ya kanuni inamtaka kila mkulima kung’oa na kuchoma maotea yote ya msimu uliopita ili kuua wadudu waharibifu kuhamia kwenye msimu mpya,kupanda kwa mstari pamoja na kupulizia dawa ya kuua wadudu”,amesema Mwanri.

Ameongeza kuwa wilaya ya Kishapu na Maswa kata ya Itilima bado kuna uelewa mdogo juu ya kulima kilimo chenye tija jambo lililopelekea waanzishe kuwepo mkulima mwezeshaji ambaye atakuwa ni chambo kwa wakulima wengine,kutoa elimu ya kutosha huku akiwaasha viongozi wawe mfano katika zao hilo kwa kwa kufanya hivo kutainua na kuongeza pato la mtu mmoja na taifa ikilinganishwa na mwaka 2021-2022.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji na usambazaji viuadudu na vinyunyizi Bw Joseph Bukalasa alisema kamati hiyo yenye watu 10 kutoka taasisi mbalimbali za serikali imeundwa kwa maelekezo ya waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe yenye lengo la kudhibiti na kuzuia uchepushaji wa upotevu pamoja na udhibiti ubora baada ya kupokea kutoka kwa mdhabuni kwenda kwa mkulima.

Aidha Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Bw Shadrack Kengese alisema kuwa ukosefu wa uadilifu katika kazi unapelekea uzembe ndani ya baadhi ya vyama vya msingi na kusababisha washindwe kufikia malengo yaliyokusudiwa katika zao hilo la pamba.

“Kwa bahati mbaya mikataba haioneshi kama kiongozi wa AMCOS akikosea atawajibika vipi mdhamini wake japo tutafika tuendako, maafisa ugani tusimamie kanuni za kilimo kwenye maeneo yetu iwapo wakulima kila siku wanamwaga mbegu na wewe uko pale je unastahili kuwepo pale? Kila mtu akisimamia kazi yake vizuri tutakuwa tumemsaidia Mhe. Rais kufikia malengo yale ambayo ameksudia katika sekta ya kilimo. ndugu zangu yamkini nimesema kwa ukali lengo hapa ni kumtaka kila kiongozi kutimiza wajibu wake”,amesema Mwanri.

Afisa Uchunguzi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutokea jijini Mwanza Bw Protas Henry ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya usambazaji pembejeo alisema kuwa lengo la serikali ni kuinua zao la pamba na wataalamu wamethibitisha kwa mkulima atakayefanya vizuri na kuzingatia kanuni mavuno yataongezeka.

“Lengo la serikali msimu wa 2022-2023 ni kuzalisha tani 500,000 kutoka tani 17300 Kishapu inatakiwa kuzalisha jumla ya tani 50,000 na hili tutafanikiwa baada ya wakulima kulima mapema, kupalilia na viuadudu na vinyunyizi kufika kwa wakati kwa walengwa na sisi kama kamati tutasimamia vema kugawa na kusimamia mtiririko wa ugawaji kwanzia ngazi ya wilaya,amkosi hadi kwa mkulima ili uzalishaji uweze kuongezeka, kwa yeyote atakaeenda kinyume na sheria hatutasita kumchukulia hatua stahiki”,amesema.

Hata hivyo wilaya ya Kishapu msimu wa kilimo 2021/2022 haikufikia malengo ya kulima hekari 100,000 kutokana na upungufu wa mvua,upungufu wa vinyunyizi kwa wakulima hivyo kutokana na kampeini ya balozi wa pamba ya octoba 2022 wakulima wameendelea kupewa elimu ya kutosha kukabiliana na changamoto hizo huku wakikusudia ongezeko kubwa la wakulima wa pamba kwa msimu wa 2022/2023.
Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Bw Shadrack Kengese akizungumza kwenye kikao hicho
Share:

WATEMBEA ZAIDI YA KILOMITA 15 KUFUATA HUDUMA ZA AFYA ..."WAJAWAZITO WAJIFUNGULIA NJIANI"


Jengo la Zahanati ya Nyida Halmashauri ya Shinyanga ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi na halijaanza kutumika
Mkazi wa Kata ya Nyida akizungumza na mwandishi wa habari
Afisa mtendaji Kata ya Nyida Daudi Lazaro akizungumza na mwandishi wa habari
****
Na Mwamvita Issa - Shinyanga

Umbali wa huduma za afya maeneo ya vijijini bado ni changamoto kubwa licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma karibu lakini mahitaji ni makubwa ambayo yanahitaji nguvu ya wadau, wananchi na serikali kuweza kuwasaidia wananchi.


Kutokana na umbali wa huduma wananchi wamekuwa wakilazimika kutembea na wengine kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya zaidi ya kilomita 15,jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya akinamama wajawazito kujifungulia njiani na wagonjwa wengine kupoteza maisha.


Katika kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha serikali inapaswa kusogeza huduma karibu na wananchi hususani huduma za afya,kwa mujibu wa sera ya afya ya June mwaka 2007 ambayo inaeleza kila kijiji kuwa na zahanati na kila kata kuwa na kituo cha afya lakini utekelezaji wake bado haujafanikiwa kuweza kuondoa adha hiyo kwa wananchi.


Changamoto hizo za afya zinabainishwa na wakazi wa Vijiji vya Nduguti, Igembya na Nyida Halmashauri ya Shinyanga ambao wametoa kilio chao kwa serikali kuwatatulia changamoto ya kusafiri zaidi ya kilomita 15 kwenda zahanati ya Kijiji cha Nyashimbi kilichopo kijiji Kata ya Puni, kituo cha afya Tinde na Bugisi.


Wananchi wanasema kukosekana huduma za afya karibu inawalazimu kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 15 kufuata huduma za matibabu kata jirani ya Puni na maeneo mengine huku baadhi ya wajawazito wakijifungulia njiani na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.


Kufuatia changamoto hiyo,wananchi wa Kijiji cha Nyida wameamuwa kuchangia nguvu kazi kwa kuanzisha ujenzi wa jengo la zahanati ambalo liko hatua za mwisho kukamilika ambalo litasaidia kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma umbali mrefu.


“Tunapata tabu sana maana hakuna huduma za afya karibu tunapohitaji kupata matibabu tunasafiri umbali mrefu zaidi ya kilomita 15 na vijiji vingine vilivyopo karibu umbali ni wastani wa kilomita10,tunapata taabu sana tunaiomba serikali itusaidie kutusogezea huduma karibu”, anasema Devota David mkazi wa Kijiji cha Nyida.


Anasema kutoka Kijiji cha Nyashimbi hadi kituo cha kupata huduma ni umbali mrefu na kusababisha wakati mwingine wakinamama wajawazito wanazalia njiani hivyo kuhatarisha maisha ya mama na mtoto,pia wanapohitaji kupeleka watoto chanjo inakuwa changamoto na na wengine wanashindwa kupata huduma.


Anabainisha kuwa unaweza kupata mgonjwa usiku ama mama mjamzito anaumwa uchungu anatakiwa kwenda kujifungua sehemu ya kupata huduma ni mpaka Tinde, Bugisi na Nyashimbi na usafiri unaotumika ni pikipiki tunatozwa fedha nyingi tunaiomba serikali itusogezee huduma.


Katika kukabiliana na changamoto hiyo wananchi wamechangia nguvu kazi kwa kujenga jengo la zahanati ili kuondoa changamoto ya kufuata umbali mrefu huduma za matibabu ambapo Afisa mtendaji Kata ya Nyida Daudi Lazaro, anaeleza kuwa kilio kikubwa cha wananchi ni kupata huduma za afya karibu.


Afisa mtendaji anasema, akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano wanapata changamoto sana hususani kipindi cha masika mvua zikiwa zinanyesha wanashindwa kwenda kliniki na kupata huduma zingine za kitaalamu jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto.


Kufuatia hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nyida wameamuwa kuchangia nguvu zao kwa kujenga jingo la zahanati ambapo pia halmashauri iliongeza nguvu na liko hatua za mwisho kukamilisha ili changamoto hiyo wanaondokane nayo wananchi wa Kijiji cha Nyida lakini pia vijiji vingine vya Kata hii bado navyo havina zahanati.
Share:

MTOTO WA MIAKA SABA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUNYONGWA NA SHANGAZI YAKE


Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba mkazi wa mtaa wa Mission, Kata ya Pamba wilayani Nyamagana jijini Mwanza, amenusurika kifo baada ya kunyongwa na shangazi yake Elizabeth Bagwisa kwa madai kuwa alikuwa anacheza nyumba ya jirani ambapo shangazi yake huyo alimkataza.

Majirani wa mtaa huo wamesema mama huyo amekuwa na kawaida ya kumpiga mara kwa mara mtoto pindi anapokosea na kumsababishia majeraha kwenye mwili wake hadi hapo juzi alipoamua kumpiga vibaya na kumnyonga huku akiwa amefungulia redio kwa sauti ya juu ili asisikie mtu yoyote.

Hamisa Juma ni mtoto wa mama huyo anaeleza tukio lilivyokuwa wakati mdogo wake akinyongwa

"Alikuwa amesimama kwenye hii nyumba ya kwanza, alivyomuona amesimama akamuita na kuanza kumpiga Love na mwiko, mama ndiye alikuwa anampiga akampiga sana baadae nikamwambia Love kimbia uende nje akawa anampiga tu hadi baadae akamnyonga," ameeleza mtoto huyo

Musa Fereji mwenyekiti wa mtaa wa Mission anaeleza hatua alizochukua baada ya kupata taarifa za mtoto kunyongwa

"Nilipigiwa simu na wananchi kwamba kuna mama mmoja kwamba alikuwa ananyonga mtoto kweli hicho kitendo kilinishtua sana ikabidi niwatafute wajumbe wangu tukaenda tukamkuta huyo mama akiwa ndani tukamkamata na huyo mtoto kweli alikuwa anaonyesha dalili za kunyongwa maana alikuwa amekabwa shingoni na koromeo,"


CHANZO : EATV
Share:

WAZIRI MABULA AAGIZA HALMASHAURI KUTWAA MAKAZI NA MAPORI YASIYO ENDELEZWA MJINI  

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa mapema leo.Sehemu ya Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Makampuni yalioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa wakifuatilia jambo kwa makini kuhusu urasimishaji jijini Dar es Salaam.

************************

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameziagiza mamlaka za Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi nchini kuyatambua maeneo au viwanja ambavyo havijaendelezwa katika maeneo ya mijini yatambuliwe na kunyanganya milki zake ili zigawiwe kwa wengine wenye uwezo wa kuziendeleza.

Waziri Mabula amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.

Waziri Mabula akiongea mbele ya makampuni ya urasimishaji jijini Dar es Salaam alibainisha kuwa maeneo haya yasiyoendelezwa yanachafua taswira ya Miji lakini pia yanapoteza mapato ambayo kama yangeendelezwa yangekuwa na faida kiuchumi.

Aidha Waziri Mabula aliongeza kuwa baada ya Mamlaka hizo kuyatambua maeneo yanayoweka mapori mjini yawasilishe kwake ambaye pia atajiridhisha ili yaweze kutolea kibali cha kuyachukua baada ya kuchunguza na kujiridhisha kuwa yanastahili kutaifishwa.

Dkt. Mabula pamoja na agizo hilo pia amezikumbusha mamlaka husika kuhakikisha mipango ya uendelezaji miji ni lazima izingatie mipango kabambe iliyopo na si vinginevyo.

‘’Kama sehemu imepangwa kujengwa jengo la ghorofa kumi basi lisijengwe jengo la ghorofa ishirini na kama ni ghorofa mbili basi lijengwe la gorofa mbili, ramani kwa ajili mipango kabambe zishatoka hivyo uendelezaji makazi lizingatie hayo’’. Aliongeza Dkt. Mabula Waziri wa Ardhi.

Waziri Mabula katika hotupa yake kwa viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Makapuni hayo alisema Urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999 fungu la 56-60 na Sheria ya Mipangomiji Na.8 ya mwaka 2007 fungu la 23.



Waziri Mabula alibainisha kuwa msingi huu wa kisheria unatokana na Sera ya Taifa ya Ardhi 1995 ambayo inatambua makazi yasiyopangwa na kutamka kuwa yatapangwa na kuboreshwa kupitia mipango shirikishi, isipokuwa yale yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi.



Waziri aliongeza kuwa Sambamba na Sera ya Ardhi, Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 inaelekeza kuwa maeneo yaliyoendelezwa bila kupangwa yatarasimishwa kwa kushirikisha wananchi ili kuboresha makazi yao.

Waziri Mabula aliutaja Mkoa wa Dar es salaam kuwa ni moja ya mikoa muhimu katika mazoezi ya urasimishaji yanayoendelea nchini kote akiongeza kuwa kuna jumla ya Kampuni za Upangaji na Upimaji 86 zinatekeleza kazi za urasimishaji katika mitaa 272 ya halmashauri tano za Dar es salaam.

Aidha Waziri Mabula alisema takriban asilimia 24 ya kazi zote za urasimishaji nchini zinafanyika katika mkoa wa Dar es salaam na hadi sasa jumla ya viwanja 554,738 vimepangwa na kurasimishwa kupitia michoro 2,084 ya urasimishaji. Kati ya hivyo, viwanja 108,193 upimaji wake umekamilika na kuidhinishwa ambavyo ni sawa asilimia 20 ya vile vilivypangwa.

Waziri Mabula aliongeza kuwa asilimia 80 ya viwanja vilivyopangwa bado viko katika upimaji wa awali akiongeza kuwa jumla ya hati 25,083 zimeandaliwa ambazo ni sawa na asilimia 23.2 ya viwanja vyote vilivyopimwa.



Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi wakati akimkaribisha Waziri kufungua mkutano huo alisema kikao kazi hicho kipo kuwasilisha, kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu Mkakati ulioandaliwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili zoezi la urasimishaji katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Dkt. Kijazi alibainisha kuwa Kikao kazi hii inaanzia Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na ukubwa na wingi wa watu ambao ni takribani 8.5% na mchango wake katika uchumi wa nchi, ni 23.5% ya makazi yote yaliyorasimishwa nchini yako Dar es Salaam.

Dkt Kijazi ana matumaini kuwa Mamlaka za upangaji zitadhibiti ujenzi holela ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango kabambe utafuatwa akibainisha kuwa baada ya kikao hicho atakuja na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha ile asilimia 80 ya kazi ambazo hazijakamilika inakamilika.

Share:

AJALI YA COASTER YAUA WATU WATANO


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo.
**
Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana na gari la mizigo aina ya Mitsubishi Canter, katika eneo la Mwavi, Kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo, amesema basi hilo dogo la abiria lilikuwa likitoka Bagamoyo kuelekea mkoani Morogoro.

Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Januari 8 mwaka huu majira ya saa 1:40 asubuhi na kwamba chanzo cha ajali ni basi dogo aina ya Coaster lilikuwa linapita gari lingine bila tahadhari na kugongana na gari lingine kusababisha ajali hiyo.
Share:

IJUE SIRI KUBWA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA, HII NI NYOTA YAKO!


Ukweli ni kwamba kila mfanyabiashara ambaye unaona amefanikiwa, ana siri kuhusu mafanikio, kuna jambo la muhimu nyuma ya pazia katika yale mafanikio yake, na sio wote wapo tayari kuzungumzia hilo.

Nimekuja kuamini hilo baada ya kukutana na AfricanDoctors na kunieleza wafanyabiashara maarufu na wakubwa wengi wamepita kwao kutazamwa nyota zao kibiashara, na ndipo wakaenda kufanya kazi katika eneo la nyota zao na kufanikiwa.

Jina langu ni Philipo kutokea Nairobi nchini Kenya, Mimi ni Mfanyabiashara ambaye najishughulisha na usafirishaji wa mizigo kutokea bandari ya Mombasa kuja Nairobi.

Nashukuru sana kazi hii ambayo nimeifanya kwa miaka zaidi ya mitano sasa, imekuwa yenye faida sana kwenye maisha yangu na jamii yangu kwa ujumla, kipato kizuri napata sio haba, maisha yanasonga.

Hata hivyo, kabla ya kazi hii nilihangaika sana kwenye kazi nyingi na biashara mbalimbali bila mafanikio yoyote yale hadi kufikia hatua ya kukata tamaa na maisha naana nilikuwa naona kama ninapoteza tu muda wangu hapa duniani.

Katika pita pita zangu maeneo ya Mjini, ndipo nikakutana na tangazo la AfricanDoctors, nilivutiwa sana na huduma yao ya kutazama nyota ya mtu kibiashara ipo wapi, wanajua mtu akishatumbua nyota yake ni rahisi sana kufanikiwa kimaisha.

Niliwasiliana nao na kufikia uamuzi wa kusafiri hadi ofisini kwao, walinipokea vizuri sana, ndipo nikaketi nao chini na kuwaelewa kuwa nahitaji wanitazamie nyota yangu kibiashara ipo wapi maana nishafanya biashara nyingi bila mafanikio.

Basi walifanya kwa mujibu wa taratibu zao, baada ya muda walinieleza kuwa nyota yangu ya biashara ipo katika usafirishaji mizigo, bila kujaliwa mizigo kutokea wapi na kwenda wapi na ya aina gani.

Cha muhimu tu iwe ni biashara ya usafirishaji mizigo, ndipo nilianza kujipanga kwa ajili ya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kutafuta vibali vya mamlaka kufanya kazi hiyo.

Nashukuru sana tangu nianze kufanya kazi hiyo, nimepiga hatua kubwa sana kimaisha, kila mtu anashangaa imekuwaje nimeweza kufanikiwa kwa urahisi hivi, ila mimi najua siri ya mafanikio yangu ni AfricanDoctors.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba ya simu +254719153099.

Mwisho.
Share:

Sunday, 8 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 9,2023

Magazetini leo Jumatatu Januari 9, 2023











..

















Share:

MTOTO WA MIAKA 6 AMPIGA RISASI MWALIMU WAKE



Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 6 amempiga risasi na kumjeruhi mwalimu wake, katika jimbo la Virginia.

Mwanafunzi huyo mvulana, amekamatwa na polisi baada ya tukio hilo katika shule ya msingi ya Richneck.


Mkuu wa polisi Steve Drew amesema kwamba tukio hilo halikuwa la kimakosa na kwamba mwalimu, mwanamke mwenye umri wa miaka 30, amepata majeraha mabaya yanayotishia uhai wake.

Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Hakuna taarifa kamili kuhusu namna mtoto huyo alivyoapata bunduki.

Shughuli za masomo katika shule tukio lilitokea, zimesitishwa na hakuna masomo yataendelea Jumatatu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger