Thursday, 15 December 2022

Picha : SAMIA DAY YATIKISA SHINYANGA!! KATAMBI ATINGISHA... 'ASANTE MAMA TUMEKUELEWA KAZI IENDELEE'


Makada wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakicheza muziki wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Maadhimisho ya Siku Maalumu ya Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopewa jina la ‘SAMIA DAY’ ikiongozwa na Kauli Mbiu ‘Asante Mama Tumekuelewa na Kazi Iendelee’ iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi yamefanyika mkoani Shinyanga.


Samia Day iliyolenga kumshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya ndani ya Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha miaka miwili tangu awe Rais wa Tanzania imefanyika leo Alhamisi Desemba 15,2022 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa.


Akizungumza katika Maadhimisho hayo,Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu amesema Mkoa wa Shinyanga una kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kwa mambo mbalimbali ya maendeleo aliyofanya katika sekta zote ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu.


“Asante Mama Samia Suluhu Hassan, Shinyanga Tumekuelewa na Kazi Iendelee”, amesema Katambi.


“Hiki siyo kipindi cha kufanya majungu, mmetutuma kufanya kazi siyo kuleta umbea, mimi hasira yangu ni kuleta maendeleo…Wakati wa kupigana vijembe umeisha, kazi iliyobaki ni kuleta maendeleo. Ni wakati wa ujenzi wa Shinyanga yetu,tutaendelea kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mzunguko wa fedha mkoani Shinyanga”,ameongeza Katambi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema Rais Samia amefanya mambo makubwa ndani ya miaka miwili ambayo hayajawahi kufanyika yangu nchi ipate Uhuru.


Rais Samia kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake amefanya mambo ambayo alipaswa kuyafanya kwa kipindi cha miaka mitano, Shinyanga tunamshukuru na tunampongeza sana”,amesema Mabala.
Makada wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakicheza muziki wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makada wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakicheza muziki wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Makada wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakicheza muziki wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Makada wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakicheza muziki wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Kada wa CCM, Toffee Uptown akiwa ameshikilia picha ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Kada wa CCM, Toffee Uptown akiwa ameshikilia picha ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Kada wa CCM akiwa ameshikilia bango wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.


Kada wa CCM akiwa ameshikilia bango wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Samia Day leo Mjini Shinyanga.










Wakazi wa Shinyanga wakiwa kwenye maadhumisho ya Samia Day.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

MCHUNGAJI AKUTWA AMEFARIKI...ALIFUNGA SIKU 30 AKATARAJIA KUFUFUKA DESEMBA 8



Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja halmashauri ya mji Geita amekutwa amefariki ndani kwake akiwa kwenye mfungo wa siku 30 akitarajia kufufuka Desemba 8

Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya pamoja na marehemu ambaye alikuwa mchungaji wao anasema marehemu aliwaaminisha kuwa ifikapo Desemba 8 atafufuka lakini kufikia siku hiyo akawa amefariki na mwili wake kuharibika

"Ameingia ndani amelala kwenda tarehe 3 kumwangalia tukakuta mwenzetu amebadilika sasa tukajiuliza ndio haya aliyoyasema kwamba anabadilishiwa mwili kwenda kufanya huduma, lakini cha ajabu tangu tarehe 2 hiyo alivyofariki usiku tukiwa kwenye maombi anakuja anakushika begani anakushika mkono mtu yeyote akiwa amelala usiku anamwambia amka muendelee kuomba, tukaendelea kuomba tukajua Labda ni kawaida alivyokuwa amedai lakini siku tunaona zinazidi kwenda", alisema John

"Tulikuwa tumefunga tangu tarehe 28 mwezi wa 11 ilivyofika tarehe 2, kwenye chumba chake cha maombi kumcheki alikuwa mzima, tarehe 3 kwenda kumwangalia Ile hali ilitutisha tukakuta ameanguka kitandani yupo kifua wazi yupo kwenye bukta ikabidi tumkusanye miguu tumuoshe vizuri tukamfunika mdomo macho vizuri tukamlaza vizuri alafu tukaenda kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa kwa ajili ya taratibu zinazofuata", alisema Zuberi.

Via: EATV
Share:

NDEJEMBI AKEMEA TABIA YA WIZI KWA WATUMISHI INAYOKINZANA NA DHAMIRA YA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala (hawapo pichani), akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika Halmashauri hiyo ya Jiji.

Sehemu ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Jiji la Ilala wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (aliyekaa meza kuu katikati), alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo ya Jiji.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika wilaya hiyo.


Afisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Bi. Charangwa Makwiro akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi mara baada ya kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika wilaya hiyo.


Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala, Bi. Subira Mwakibete akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo ya Jiji.

**********************

Na. Veronica E. Mwafisi-Ilala

Tarehe 15 Disemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa umma nchini kujihusisha na vitendo vya wizi ambavyo vinakwenda kinyume na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora.

Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ndejembi amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana maono makubwa ya kuujenga utumishi wa umma wenye uadilifu, hivyo amewataka watumishi wa umma nchini kutokumuangusha badala yake wafanye kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa katika kulitumikia taifa.

“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua wazi kututhamini watumishi wa umma kwa kuboresha maslahi na stahili zetu hivyo, hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuunga mkono kwa vitendo dhamira yake ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma kutafakari madhara ya wizi na kutathmini mienendo yao ili kutokuwa ni sehemu ya kukwamisha dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha huduma kwa wananchi na kuliletea taifa maendeleo katika sekta zote muhimu kama vile afya, kilimo, uvuvi, biashara, uwekezaji na miundombinu.

Sanjari na hilo, Mhe, Ndejembi amewataka Waajiri na Maafisa Utumishi Serikalini kuwasimamia vema watumishi wanaowaongoza badala ya kusubiria mpaka viongozi wa juu wa kitaifa kufika katika maeneo yao ya kazi kukemea uovu pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.

Akizungumzia matumizi ya fedha za umma, Mhe. Ndejembi amesema kuwa fedha za umma zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali kwani kinyume na hilo ni ukosefu wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Mhe Ndejembi ameeleza bayana kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita haitomvumilia mtumishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma kwa kujihusisha na vitendo vya wizi katika eneo lake la kazi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameendelea na ziara ya kikazi Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Share:

SELEMAN MPEPE WA NANYUMBU ABONGEKA NA BIKOSPORTS

Mkazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara, Selemani Mpepe, aliyenyoosha mikono juu, akiwa na marafiki zake baada ya kufanikiwa kukabidhiwa fedha zake Sh Milioni 4 alizoshinda kama sehemu ya bonasi Bonge kutoka kwenye mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani wa Bikosports.
Mkazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara, Selemani Mpepe, akiwa na furaha kubwa baada ya kufanikiwa kukabidhiwa fedha zake Sh Milioni 4 alizoshinda kama sehemu ya bonasi Bonge kutoka kwenye mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani wa Bikosports.

MKAZI wa Nanyumbu mkoani Mtwara, Selemani Mpepe, ameibuka na bonasi bonge ya kiasi cha Sh Milioni 4 kutoka kwenye mchezo wa kubashiri matokeo wa bikosports unaoendelea kumwaga manoti kwa Watanzania wanaotumia bikosports kuweka mikeka yao.

Akizungumza katika makabidhiano ya zawadi hiyo ya fedha, Mpepe amesema zawadi hiyo aliyoipata kama bonasi imefungulia njia nzuri katika maisha yake sanjari na kupunguza makali.

Amesema amekuwa akitumia mchezo wa Bikosports kama njia ya kutafuta njia ya kutimiza malengo yake, akiamini kuwa ni sehemu nzuri inayoweza kumpatia ufumbuzi wa maisha yake.

“Katika mkeka wangu niliweka mechi nane na kuingiza kiasi cha 40,000 kama mtaji wangu, jambo ambalo lilinipatia kiasi cha fedha ambacho kitasogeza mbele gurudumu la maisha yangu.

“Nitatumia kiasi cha pesa katika biashara zangu ndogo ndogo ambazo siku zote nimekuwa nikizifanya kwa lengo la kunipatia mwangaza mzuri zaidi,” amesema.

Mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ni rahisi kucheza na kushinda ambapo namba ya Kampuni ni 101010, huku ukitoa fursa ya kucheza live mtandaoni kwa www.bikosports.co.tz bila kusahau wanaobeti njia ya kwa kupiga *149*89# wakitumia pia 101010 kama namba ya kampuni ya Bikosports.
Share:

Wednesday, 14 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 15,2022











Share:

UZALENDO NI TUNU KWA TAIFA: KATIBU MKUU MMUYA



Na Mwandishi wetu- Mara

Wasomi na vijana wamekumbushwa umuhimu wa kuwa wazalendo, kujenga ,kuiendeleza na kuilinda Nchi na watu wake kwaajili ya maslahi ya Maendeleo ya Taifa.


Akizungumza katika sherehe ya Mahafali ya 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Wialaya ya Musoma Mkoani Mara Katibu Mkuu Mteule Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Bwa. Kaspar  Mmuya amesema mustakabali wa Maendeleo ya Taifa lolote Duniani unategemea mchango wa Taasisi za mafunzo katika kuandaa wataalam wenye weledi ambao ndio chachu ya kuleta mageuzi ya kifikra na maendeleo Jumuishi na endelevu kwa Jamii.


"Wizara inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Chuo hiki katika kuandaa wataalam wa fani ya maendeleo ya jamii ambao ndiyo injini ya kutafuta suluhisho la changamoto za maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia, kiutamaduni, kisiasa na kimazingira kwa kutumia rasilimali zinazoizunguka jamii, hivyo mafunzo yanayotolewa hapa sharti yaakisi mipango ya nchi na vipaumbele vya jamii ili kuleta matokeo chanya ya maendeleo" Amesema Katibu Mkuu huyo.


Pia  Bwa. Mmuya amekipongeza Chuo hicho kwa kuanzisha programu ya uanagenzi ambayo imesisitizwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambapo hadi kufikia sasa baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya uanagenzi wamepata ajira katika taasisi na makampuni mbalimbali Nchini.


Aidha Mmuya ametoa rai kwa Chuo kuhakikisha kinafanya utafiti kwa lengo la kuishauri serikali kuhusu changamoto zinazohitaji mabadiliko ya kisera ,kimkakati au kisheria.


"Kwa upande mwingine tafiti zinaweza kuwa na msaada mkubwa katika kubuni na kuboresha zana na mbinu shirikishi za kuhamasisha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini shughuli au miradi ya maendeleo, hivyo jitahidini sana kutekeleza jukumu hilo kwa kiwango kikubwa",ameeleza.

Share:

MWAMALA WAFUNGUKA…”TUKIACHANA NA MME WANGU SASA HIVI TUNAGAWANA MALI PASU KWA PASU, HANYANYASWI MTU HAPA”


Afisa Mtendaji kata ya Mwamala Halmashauri ya Shinyanga, Suzana Kayange

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia inayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kupenya kwenye maeneo mbalimbali wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ambapo sasa wananchi wameanza kuuzika mfumo dume kwa kuhakikisha wanawake wanamiliki mali na kugawana mali pindi wanapotengana na waume zao.

Haya yanajidhihirisha katika kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambako Malunde 1 blog imetembelea eneo hilo na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo ambao wanasema sasa mambo yamebadilika jamii imeanza kuachana na mfumo dume unaomfanya mwanamke aonekane si lolote.

“Sasa hivi hakuna kufukuza mwanamke, mkiachana mnagawana pasu kwa pasu, hakuna kunyanyasa mwanamke”,anasema Masesa Masele.

“Sasa tuna elimu ikitokea tumeachana na mme wangu lazima tugawane mali, kila mtu anachukua nguvu zake”,anaongeza Esther Thomas.

Naye Mboje Malale anasema kidogo kidogo jamii imeanza kubadilika kutokana na kelele za kupinga ukatili wa kijinsia.

“Inapotokea mwanamke na mwanaume wakaachana, lazima kuna aliyeanzisha mgogoro hivyo lazima anayeanzisha mgogoro lazima wagawane”,amesema Mzee Malale.

Afisa Mtendaji kata ya Mwamala Halmashauri ya Shinyanga, Suzana Kayange amesema licha ya wananchi kuwa na elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia lakini bado kuna mfumo dume, mfano mwanamke na mwanaume wanalima pamoja lakini wakati wa mavuno mali zinaonekana ni za mwanaume tu, Mwanamke anaonekana wa kuja tu.

“Matukio ya ukatili wa kijinsia yamepungua kwa kiasi kikubwa, kesi zimepungua sana, wanawake hawanyanyaswi mfano kupigwa kama zamani, wanaume wanaogopa kuchukuliwa hatua endapo watabainika kunyanyasa wake zao kwani wananchi wameshajua mahali pa kuripoti matukio ya ukatili, wajane pia sasa wanapata haki zao”,amesema Suzana.
Share:

Breaking News : MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023

 

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023, WAMETANGAZWA.

OR-TAMISEMI NA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger