Sunday, 6 November 2022

RAIS WA PAP CHIFU CHARUMBIRA ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KANISA LA ZCC RAYTON PRETORIA, APONGEZA VIONGOZI WA DINI KUHAMASISHA AMANI NA UMOJA


Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira ameshiriki Ibada ya Jumapili leo Novemba 6, 2022 katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.

Akihutubia maelfu ya waumini wa Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) kwenye Ibada iliyoongozwa na Askofu Dkt. Nehemiah Mutendi, Mhe Chifu Fortune Charumbira amewapongeza viongozi wa dini kwa jukumu muhimu wanalofanya katika kukuza umoja duniani kote huku akibainisha kuwa Bunge la Afrika linatambua jukumu muhimu ambalo kanisa linachukua katika kushughulikia migogoro katika kutafuta amani na maendeleo duniani.


“ZCC imedhihirisha kuwa ni kanisa la dunia nzima, si la nchi flani, kwenye Ibada hii kuna watu kutoka nchi mbalimbali kwenye mkusanyiko huu wa kanisa. Askofu Nehemiah Mutendi ana mikutano mikubwa katika mabara yote. Bunge la Afrika linaamini kuwa ili kuwa amani na utatuzi wa migogoro lazima tumtangulize mbele Mwenyezi Mungu. Ulimwengu wa kiroho hufundisha watu kuwa waaminifu na kupiga vita ufisadi. Kadiri watu wanavyojiunga na kanisa ndivyo matatizo mengi kama vile migogoro na njaa yanavyotatuliwa", amesema Chifu Charumbira.
Askofu wa Kanisa la ZCC Dkt. Nehemiah Mutendi akimkaribisha Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kulia) katika kanisa la ZCC.
Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kushoto) akiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kushoto) akiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.


Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira akizungumza katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.


Waumini wakiwa katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.

Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe. Chifu Fortune Charumbira (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wa dini katika Kanisa la Zion Christian Church (ZCC) lililopo Mbungo 2 Rayton, Pretoria nchini Afrika Kusini.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WATU 19 WAFARIKI AJALI YA NDEGE KUANGUKA ZIWA VICTORIA TANZANIA



Watu 19 wakiwemo abiria na wahudumu wamefariki dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Ndege la Precision Air iliyotokea asubuhi ya leo Jumapili Novemba 6, 2022 katika  Ziwa Victoria Mkoani Kagera.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza vifo hivyo leo jioni baada ya kuwasili kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi kutokana na ndege hiyo kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mkoa wa Kagera na kutumbukia Ziwa Victoria ambalo lipo karibu na uwanja huo.

Ndege hiyo ilikuwa na watu 43, kati yao 39 wakiwa abiria, marubani wawili na wahudumu wawili ambapo tayari 28 wameokolewa.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Issessanda Kaniki alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu watatu kabla ya Majaliwa kufika na kutangaza idadi ya waliokufa kuwa ni 19.

 Ndege hiyo ya Precision Air ATR 42 SH PWF ambayo ilikuwa na watu 43 ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.
Share:

Breaking News : NDEGE YA PRECISION AIR YAANGUKA ZIWA VICTORIA







Habari zilizotufikia hivi punde ni Ndege ya Kampuni la Ndege la Precision Air imeanguka katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba wakati ikijaribu kutua kwenye uwanja huo asubuhi hii leo Jumapili Novemba 6,2022.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na wanaendelea na juhudi za uokozi.
Share:

BSL YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JIJINI DODOMA







Mkurugenzi wa The BSL Investment Company Limited na BSL SCHOOLS amekabidhi ufadhili wa vifaa mbalimbali mbele ya afisa elimu msingi na sekondari jiji la DODOMA.

 Shule 10 zimenufaika 9 za msingi na 1 ya sekondari. Ametoa lita 120 za rangi, cement kg 500, mipira ya miguu 2, vitabu 117 na vifaa vinginevyo vya kielimu.

Share:

Saturday, 5 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 6,2022








Share:

BENKI YA CRDB YAZINDUA MFUMO WA KUPOKEA MAONI YA WATEJA KWA NJIA YA SMS KANDA YA MAGHARIBI

Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB wakifurahia pamoja wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS shortcode) kupitia namba 15089 
**
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS shortcode) kupitia namba 15089 ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa kuboresha zaidi huduma zake za Kibenki.

Mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya SMS umezinduliwa leo Jumamosi Novemba 5,2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ukihudhuriwa pia na wateja  na Mameneja wa matawi ya Benki ya CRDB yapatayo 26 katika Kanda ya Magharibi inayoundwa na mikoa ya Shinyanga , Tabora , Kigoma , Geita na wilaya ya Segerema na Buchosa.

Mfumo huo ni rahisi sana kwani wateja wake hawatahitaji kutumia intaneti katika simu ya kiganjani ikiwa ni huduma mpya na ya kwanza kutumiwa na Benki ya CRDB hapa nchini pamoja na Afrika na Mashariki na kati na Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza kutumia kupokea maoni ya wateja kwa kutumia SMS ya kawaida (Normal SMS) kwa namba 15089.

Akizindua mfumo huo, Mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga ameipongeza benki ya CRDB kwa kwenda na kasi ya dunia katika mifumo ya matumizi ya kidigitali sasa kupitia njia hiyo wateja watatoa maoni yao popote pale na kwa simu za kawaida .


"Njia hii mpya tuliyozindua leo ya kutuma ujumbe mfupi wa (SMS) ni rafiki na rahisi kwani mteja hataihitaji kuwa na gharama ya kutumia intaneti kwenye simu yake wala simu janja na anaweza kutumia mtandao wowote",amesema Kiswaga.

"Nitoe wito kwa benki ya CRDB ni mzidi kuongeza juhudi katika kutoa huduma bora ili muendelee kuwa mfano wa mafanikio kwa taasisi za wazalendo na ninawahakikishia Serikali ipo nanyi bega kwa bega hivyo kwa pamoja tufanye kazi ya kuijenga nchi yetu" amesema Kiswaga.

Akieleza mfumo huo Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Jumanne Wagana amesema kwa Afrika Benki ya CRDB itakuwa ya kwanza kutumia mfumo huo ambapo mteja atatuma SMSkwa kutumia simu yoyote na bila intaneti.


Naye Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa benki ya CRDB , Yolanda Uriyo amesema matumizi ya mfumo yanalenga kuboresha mifumo ya huduma kwa wateja ya utoaji wa maoni .

Uriyo amesema awali mteja akitaka kutoa maoni ilikuwa kwanza lazima uwe na simu janja yenye kutumia intaneti kwa sasa wateja wanapotaka kutoa maoni, watatoa maoni yao kupitia njia ya SMS kwa simu za kawaida na kwa gharama nafuu.


Amesema benki ya CRDB tayari imezindua mfumo huo, Visiwani Zanzibar kwa mikoa yote ya Pwani lengo ni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja ambao sasa anayetoa maoni atatuma akiwa popote pale hata nyumbani.

Kwa upande wao wateja wa benki hiyo waliokuwa wamehudhuria uzinduzi wa mfumo huo wameipongeza benki ya CRDB kwa kuendelea kuwajali wateja wake na sasa watatoa maoni kwa SMS.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida (NORMAL SMS) kupitia namba 15089 uliofanyika katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama leo Novemba 5,2022
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Jumanne Wagana akitoa ufafanuzi mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida (SMS shortcode) kupitia namba 15089 
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Benki ya Yolanda Uriyo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida kupitia namba 15089 
Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB wakifurahia pamoja
a

Picha na Patrick Mabula - Kahama
Share:

MISA-TAN YAHITIMISHA MAFUNZO YA KUANDIKA HABARI ZA UHURU WA KUJIELEZA KWA WANAHABARI


Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za uhuru wa kujieleza.

Na Marco Maduhu, SINGIDA

MAFUNZO ya kuandika habari za uhuru wa kujieleza kwa Wanahabari wapatao 40 kutoka Mikoa ya Tabora, Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Singida yamehitimishwa Rasmi.

Mafunzo hayo yalianza kutolewa Novemba 3, mwaka huu yamehitimishwa leo Novemba 5 ambayo yalikuwa yakiratibiwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (Misa-Tan)kwa ufadhili wa Ubalozi wa Kanada nchini Tanzania.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Marko Gideon, amesema Wanahabari wanapaswa kutumia Kalamu zao vyema katika kuandika habari za uhuru wa kujieleza katika Nyanja mbalimbali na kupaza sauti za wananchi.

Amesema unapokosekana uhuru wa kujieleza, Utawala wa kisheria hautakuwepo, uwajibikaji kwa viongozi, hakutakuwa na usawa wa kisheria, hakuna uwazi, uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki, wala kudhibiti matumizi mabaya ya viongozi, " amesema Gideon.

Naye Andrew Marawiti kutoka Misa-Tan, amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuona Wanahabari wakiandika habari nyingi zinazohusu uhuru wa kujieleza.

Nao baadhi ya Wanahabari walioshiriki mafunzo hayo, wamesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi na weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa kuandika habari za uhuru wa kujieleza pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia kwa vyanzo vyao vya habari.

Mwezeshaji Marko Gideoni akitoa mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa Wanahabari.

Mwanahabari Amini Nyaungo kutoka Radio Standard FM mkoani Singida akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Mwanahabari Jeniva kutoka Radio Faraja mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Wanahabari wakiendelea na mafunzo.

Wanahabari wakiendelea na mafunzo.

Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.

Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.

Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo katika kazi za makundi.

Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo katika kazi za makundi.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya mafunzo kumalizika
Share:

NDALICHAKO: WEKENI PROGRAMU ZA KUWALINDA WAFANYAKAZI DHIDI YA MAGONJWA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akizungumza na watumishi na waajiri kutoka maeneo mbali mbali jijini Dar es salaam waliojitokeza kushiriki michezo katika bonanza la waajiri (Waajiri Health Bonanza) lililoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) nakufanyika katika viwanja vya Leaders Club.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako (wapili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkaguzi wa Afya wa OSHA, Dkt. Zakayo Mmbaga, kuhusu huduma mbali mbali za afya zinazotolewa na OSHA kwenye bonanza la michezo katika viwanja vya Leaders Club. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akizungumza kuhusu umuhimu wa waajiri na watumishi kuzingatia masuala ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi katika bonanza la Waajiri Health Bonanza lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club.


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, akifuatilia mchezo wa mpira wa pete kati ya OSHA dhidi ya TUICO iliyomalizika kwa OSHA kuibuka na ushindi wa mabao 11 kwa 5. Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu Kitengo cha Sheria wa OSHA, Bi. Netiwe Mhando na kulia kwake ni Meneja Rasilimali Watu na Utawala Bi.Thandie Mfikwa.


Timu ya mpira wa miguu ya OSHA (wenye jezi za kijani) ikicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Access Bank katika bonanza la waajiri lililofanyika katika viwanja vya Leader Club na mchezo huo ulimalizika kwa timu ya OSHA kupata ushindi kwa mikwaju ya penati 3 kwa 2.


Timu ya mpira wa pete ya OSHA (wenye jezi za kijani) wakicheza mchezo wao dhidi ya timu ya TUICO na mchezo huo ulimalizika kwa timu ya OSHA kuibuka na ushindi wa goili 11 kwa 5.

Na Mwandishi Wetu

Waajiri nchini wametakiwa kuwa na programu endelevu za mazoezi kwenye maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi dhidi magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni yamekuwa chanzo kikubwa cha vifo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, alipokuwa akizungumza na mamia ya waajiri na wafanyakazi walioshiriki katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Bonanza hilo lilowashirikisha waajiri zaidi ya 100 limefanyika katika viwanja vya Leadres Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo timu za waajiri zilishindana katika michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mbio fupi, kuvuta Kamba, kufukuza kuku na kukimbia kwenye magunia.

Aidha, Waziri Ndalichako amewakumbusha waajiri kuweka mifumo madhubuti ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuwakinga wafanyakazi na vihatarishi vya magonjwa na ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu au kuwasababishia ulemavu.

“Ninawapongeza sana waajiri wote ambao wameitikia wito wa ATE na kujitokeza kwenye bonanza hili kwa wingi kwani mwitikio umekuwa mkubwa sana hivyo nawasisitiza kwamba programu kama hizi kuwa endelevu,” amesema Waziri Ndalichako, nakuongeza:

“Kwa upande wa OSHA ninawashukuru kwa kuona umuhimu wa kuwahamasisha masuala ya mazoezi kwasababu natambua kwamba wameshiriki kwa kufadhili bonanza hili ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa na ningependa kuona kwamba linakuwa endelevu.”

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba, amesema lengo la kuandaa bonanza hilo ni kuwahamasisha waajiri kuona umuhimu wa kuwekeza katika afya za wafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini.

“Tunashukuru waajiri kwa kuitikia wito wetu wa kushiriki kwenye bonanza hili kwani mwitikio umekuwa mzuri. Jumla ya waajiri 129 wameshiriki pamoja na kwamba bonanza hili tumelifanya kwa mara ya kwanza. Hivyo, tunawakumbusha waajiri kuwekeza katika afya za wafanyakazi kupitia programu za mazoezi kwenye maeneo yao ya kazi,” amesema Bi. Ndomba.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema Taasisi yake imefadhili bonanza hilo baada ya kubaini ongezeko kubwa la wafanyakazi wanaopata magonjwa yasiyoambukizwa katika sehemu za kazi.

“Katika shughuli zetu za ukaguzi pamoja na uchunguzi wa afya za wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi tumebaini kwamba wafanyakazi wengi wanapata magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, presha na uzito uliokithiri kutokana na mtindo wa maisha. Hivyo, tumeshiriki katika bonanza ili kuwahasisha waajiri kuchukua hatua za kudhibiti ongezeko la magonjwa hayo kwenye maeneo yao ya kazi kupitia michezo.”

Aidha, Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA, amesema michezo ina mchango mkubwa katika kuondoa kihatarishi cha kisaikolojia kwenye maeneo ya kazi ambacho ni chanzo kikubwa cha ajali na hivyo ni vema waajiri wakawekeza katika programu endelevu za michezo kama namna mojawapo ya kupunguza ajali mahali pa kazi.

Share:

MWANAUME ALIYEJIFANYA 'HOUSE GIRL' AKAMATWA AKIJARIBU KUMDHULUMU KIMAPENZI MTOTO WA KIUME WA BOSI WAKE

Mwanaume aliyejifanya mwanamke nchini Zambia ili kuajiriwa kama mjakazi 'House Girl' amekamatwa kwa kujaribu kumdhulumu kimapenzi mvulana wa miaka 19.

Christopher Mukutindwa, 29, ambaye anatoka Mtendere alijaribu kujilazimisha kwa mpwa wa mwajiri wake baada ya kufanya kazi nyumbani kwao kwa miezi mitano.


Mwebantu aliripoti Mukutindwa alimvuta mwathiriwa wake chumbani kwake na kujaribu kujilazimisha kwake lakini alizidiwa nguvu na kijana huyo ambaye alikimbia kuokoa maisha yake na kuripoti kisa hicho kwa polisi. 

“Ukweli kwa ufupi Mukutindwa alimuita mwathiriwa chumbani kwake, akavua kitenge alichokuwa amevaa ili afanye mapenzi naye.

 Hapo ndipo mwathiriwa alipogundua kuwa mjakazi huyo alikuwa ni mwanaume na kuanza kumenyana naye akafanikiwa kumzidi nguvu,” alisema msemaji wa Polisi Rae Hamoonga mnamo Alhamisi, Novemba 3, 2022.
Share:

DINGI AVAMIA SHULE KULALAMIKA KWANINI WANAFUNZI WENGINE WANAMCHUKIA BINTI YAKE



Msichana moja mchanga amemtia babake wasiwasi baada ya kurejea kutoka shuleni kila siku akilia.

Msichana huyo alilalamika kuwa amekuwa akikumbana na matatizo shuleni kwani wanafunzi wenzake hawampendi na kila mara wanamtoroka.

Kulingana na Dexterouz11 kwenye Twitter, baba huyo aliamua kukabiliana suala hilo kwa kutembelea shule hiyo ambapo alizungumza na wanafunzi wenzake waliothibitisha ripoti za bintiye. 

Wanafunzi wenzake walifichua kwamba walikuwa wakimtenga msichana huyo mdogo kwa sababu alikuwa mkaidi na mwalimu wao aliwaagiza waepukane naye.

"Huyu jamaa aliniambia kuhusu mtoto wake anayerudi nyumbani kila mara kulalamika kuwa kila mtu anamchukia shuleni. Alimfuata shuleni ili kujua tatizo na wanafunzi wakasema hawaongei naye kwa sababu mwalimu wao aliwaambia wamuepuke." 

Walipokabiliwa, mwalimu huyo alisema kuwa binti wa jamaa huyo alikuwa mkaidi na hiyo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na kiburi chake.

Mwalimu ambaye aliwaagiza wenzake kumuepuka alisema ilikuwa njia bora ya kumrekebisha. Maelezo yanaonyesha kuwa baba huyo aliyekasirika alizua tafrani hivi kwamba shule ilimfukuza kazi mwalimu huyo muda mfupi baadaye.
Share:

RC MJEMA ATAKA WAMILIKI WA MIGODI NA MAKAMPUNI SHINYANGA KUTOA MIKATABA YA AJIRA KWA WAFANYAKAZI KUEPUKA MIGOGORO

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger