Thursday, 20 October 2022
NHC KUZINDUA SERA YA UBIA ITAKAYO FUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI
![]() |
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara NHC, William Genya
Meneja habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya
Na Dotto Kwilasa, DODOMA
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linatarajia kuzindua sera ya ubia ya ushirikiano na sekta binafsi itakayowezesha utakelezaji wa miradi na uboreshaji wa majengo yenye hali mbaya yanayomilikiwa na shirika hilo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara NHC, William Genya amesema hayo Leo Jijini hapa wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kueleza kuwa ubia huo utawezesha uboreshaji majengo yenye hali mbaya ya NHC ya mitaa mbalimbali ikiwemo ya Kariakoo na Upanga.
Amesema hatua ya uzinduzi wa sera hiyo, itafanyika Novemba 14 mwaka huu huku ikitarajiwa kutoa fursa kwa NHC kuingia ubia na sekta ya binafsi kwa ajili kujenga miradi ya maendeleo katika viwanja inavyovimiliki na kuwa kisasa hali itakayo toa fursa ya familia nyingi kupata makazi na maeneo ya biashara.
“Sera imeboreshwa kwa kuongeza vitu vikubwa vinne ikiwemo kutumia ardhi kama mtaji, sera nyingine ni NHC inaweka ardhi na mbia anaweka fedha halafu wanatekeleza mradi kwa pamoja na hii ni kwa miradi mikubwa ya kuanzia sh.bilioni 50,"amesema.
Mkurugenzi huyo pia ametaja sera nyingine kuwa ni kujenga jengo kati ya shirika na wabia kisha kuuzwa na mapato kugawanywa na sera ya mwisho ni shirika kutoa ardhi kwa mkataba wa miaka 10 na mbia anajenga, baada mkataba kuisha jengo linakuwa mali ya shirika.
“Sera hii ina lenga kuwapa fursa wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini, ambapo itafungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ili kuunga mkono maono maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binfasi ambayo ni injini ya kuleta maendeleo ili iwekeze mitaji yao katika kujenga uchumi wa Taifa letu,” amesema
ameongeza kuwa uzinduzi huo una lengo la kuwaalika Watanzania kushiriki kwenye Sera hiyo iliyoanzishwa na shirika tangu mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika.
Katika hatua nyingine Genya amesema tangu kuanza kwa utaratibu huu jumla ya miradi 111 ilitekelezwa ikiwa na thamani ya sh.bilioni 300 ambapo katika miradi hiyo, miradi 81 yenye thamani ya sh.bilioni 240 imekamilika na kuanza kutumika na miradi 30 yenye thamani ya sh.bilioni 60 inaendelea kukamilishwa.
amefafanua kuwa miradi hiyo imechangia upatikanaji wa ajira, kuboresha mandhari ya miji, kuongeza mapato ya shirika, kuongeza wigo wa kodi za serikali, kuongeza maeneo kwa ajili ya biashara na makazi.
“Katika uzinduzi huo mkubwa tunakusudia kuwa na washiriki takribani 600 kutoka tasisi mbalimbali za serikali na binafsi, vyama na bodi za kitaalum pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi ambao wamealikwa,”amesema
Kwa upande wake Meneja habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya amesema uzinduzi wa sera hiyo utafanyika Novemba 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
ELIMU YA MSINGI KUISHIA DARASA LA SITA TANZANIA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.
Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
Via- EATV
Wednesday, 19 October 2022
BSL COLLEGE KAHAMA YATOA MISAADA SHULE 11 KAHAMA
BSL COLLEGE KAHAMA chini ya mkurugenzi Teacher Black leo tarehe 19/10/2022 wamekabidhi vitendea kazi katika shule 7 za msingi na 4 za sekondari katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga. Wametoa mifuko ya cement kg 250, Ngano kg 75, mipira, rangi, vipaza sauti, Reams na sukari.
ALIPO MAMA BSL TUPO.
@bslschools, www.bslschools.co.tz
0712583756
SERIKALI YAANDA MIONGOZO ITAKAYOSAIDIA UTEKELEZAJI WA UIMARISHAJI BORA WA ELIMU YA SEKONDARI KWA NJIA MBADALA
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge akitembelea mabanda ya wadau wa elimu leo Oktoba 19,2022 katika Kongamano la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salam (DUCE).
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salam (DUCE).
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salam (DUCE). 

*******************
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa miongozo mitano ambayo inasaidia katika utekelezaji wa kuimarisha ubora wa utolewaji wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP).
Mpango huo unatambua kisomo kama haki ya msingi kwa maendeleo ya mtu binafsi, kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Ameyasema hayo leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna wa Elimu nchini, Mwalimu Venancy Manori katika Kongamano la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salam (DUCE).
Amesema katika kipindi cha mwaka 2021, jumla ya wasichana 3,333 walijiunga na programu hiyo katika vituo 131 nchi nzima.
“Haya ni baadhi ya mambo yaliyofanywa na serikali, hivyo nawaasa wadau wote kutumia kongamano hili kujadili na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji katika progrmu za kimasomo yanayozingatia ubora, usawa na ujumuishi kwa makundi yote,” Amesema.
Amesema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UNESCO hivi karibuni, kiwango cha watu wazima wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu ni asilimia 77.89, hali ambayo imeelezwa si mbaya ingawa nchi imerudi nyuma ukilinganisha na miaka ya nyuma.
“Kupitia kongamano hili, watendaji mlitumie kuweka mikakati thabiti ya kuondoa changamoto ya kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu nchini, ni dhahiri Taifa lenye watu walioelimika ni rahisi kuleta maendeleo yatakayoweza kubadili maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” amesema.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akifungua kongamano hilo amesema lengo la maadhimisho hayo ya juma la Elimu ya Watu Wazima ni kujenga uelewa na kutambua changamoto mbalimbali, zinazoikabili tasnia hiyo kwa jamii na dunia kwa ujumla.
“Ni imani yangu tutaweza kubadilisha mitizamo juu ya mipango, uendeshaji, usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, ili kuendana na dira ya maendeleo ya mwaka 2025,” Amesema.
Amesema pia malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 hasa katika lengo namba nne, ambalo linalenga kuhakikisha vijana na watu wazima wote wanaume na wanawake wanafikia kiwango cha kujua kusoma, kuandika na kuhesababu ifikapo mwaka 2030.
MWANZA WAVUKA LENGO LA KITAIFA LA UTOAJI CHANJO YA UVIKO-19
Mkoa wa Mwanza umevuka lengo la kitaifa la utoaji chanjo kamili ya UVIKO-19 kwa wananchi ambalo ni asilimia 70 ifikapo mwezi Disemba mwaka 2022.
Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema hadi kufikia Oktoba 17, 2022 wananchi milioni 1.6 kati ya milioni 1.8 kwa mjibu wa Sensa ya mwaka 2012 wamepata chanjo kamili ya UVIKO-19 ikiwa ni sawa na asilimia 87 juu ya lengo la kitaifa.
Dkt. Rutachunzibwa aliyasema hayo Oktoba 18, 2022 wakati akifungua kikao cha tathimini ya chanjo ya UVIKO-19 na Uhuru wa Kupata Taarifa kilichoratibiwa na Chama cha Wanahabari Mkoa Mwanza (MPC) kwa ufadhili wa Shirika la Internews kupitia mradi wa Boresha Habari.
Alisema wakati zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO-19 linaanza nchini Agosti 03, 2021 kulikuwa na upotoshaji uliosababisha changamoto kwa wananchi kuwa tayari kupokea chanjo lakini waandishi wa habari walisaidia kuelimisha jamii.
Pia Dkt. Rutachunzibwa aliwaomba Waandishi wa Habari kuendelea kuhamasisha wananchi kuwa na desturi ya kupima afya hususani magonja yasiyoambukiza kama walivyosaidia kufanikisha utoaji wa chanjo ya UVIKO-19.
Aliwahimiza kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayoanza kitaifa katika uwanja wa Furahisha kuanzia Novemba 05-12, 2022 ambapo watapata huduma mbalimbali ikiwemo vipimo vya magonjwa hayo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko aliwakumbusha wanahabari kuendelea kuelimisha wananchi kuwa tayari kupata chanjo mbalimbali ikiwemo UVIKO-19 hatua itakayowaweka salama huku wakihakikisha wanaondoa ombwe la habari zisizo sahihi kwa wananchi hususani kuhusu chanjo ya UVIKO-19.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanahabari Tonny Alphonce akichangia mada kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja
SOMA>>> Habari zaidi hapa
TBS YASHIRIKI MAONESHO YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADILIAJI JENGO
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.**********************
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Maonesho hayo leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam, Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha amesema TBS limeshiriki kwenye Maonesho hayo ili kuwapatia elimu ya viwango wabunifu Majengo na Wakadiiliaji jengo ili majengo ambayo wanayabuni yawe bora na yenye viwango.
Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wabunifu majengo kuelewa na kufuata taratibu za viwango vya matumizi ya vifaa vya kupimia majengo ambayo wamekuwa wakiyabuni na kuondoa kasoro ambazo zingeweza kuleta athari kwenye majengo ambayo yatajengwa.
Aidha amesema ushiriki katika maadhimisho hayo ni mkuwa kwani wabunifu mbalimbali wa majengo wameweza kutembelea banda la TBS na kupewa elimu juu ya matumzi sahihi ya viwango.

















































