Friday, 14 October 2022

RFB YAPOKEA WASILISHO LA MFUMO WA UANDAAJI GHARAMA ZA UJENZI WA BARABARA

Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Alois Matei, akizungumza na wadau kutoka Taasisi za Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), katika kikao cha wasilisho la mfumo wa uandaaji gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara, kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Eng. Rashid Kalimbaga Meneja Msaidizi kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara na Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi Dkt. Samson Mturi.

Mhandisi Moses Laurence kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), akiwasilisha pendekezo la mfumo wa uandaaji gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara, katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila pamoja na Mkurugenzi wa Barabara Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Eng. Alois Matei.

Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi Dkt. Samson Mturi, akizungumza na wadau kutoka Taasisi za Sekta ya Ujenzi katika kikao cha wasilisho la mfumo wa uandaaji gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara, kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Eng. Alois Matei.


Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Arch. Edwin Nnunduma, akizungumza jambo katika kikao cha wasilisho la mfumo wa uandaaji gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara, kilichofanyika jijini Dodoma. Walioketi mbele ni Meneja Msaidizi John Aswile na Meneja Msaidizi Godlove Stephen wote kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara

Baadhi ya washiriki wa kikao cha wasilisho la mfumo wa uandaaji gharama za matengenezo na ujenzi wa barabara, kilichofanyika jijini Dodoma, wakifuatilia kwa makini kikao hicho.

Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabra

*************************

Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), imepokea wasilisho la kwanza la mfumo wa kuandaa gharama za kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara uliotengenezwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ujenzi, Mhandisi Alois Matei ambae ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, amesema kuwa kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika kukadiria gharama za kazi za barabara hapa nchini, ambapo changamoto hizo zimekuwa zikiathiri uandaaji wa mipango na bajeti kwa upande wa Wakala za Barabara kwani mara nyingi bajeti za kazi za barabara hutofautiana sana na gharama halisi.

“Uhitaji na umuhimu wa kuwa na mfumo kama huu umekuwepo kwa muda mrefu kwa lengo la kutatua changamoto za wakala wa barabara, wakandarasi na hata wataalamu washauri katika kukadiria gharama za miradi ya barabara. Ni kwa msingi huu Wizara iliielekeza Bodi ya Mfuko wa Barabara kuratibu na kugharamia uundaji wa mfumo huu”…

“Hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Bodi kwa kufanikisha uundwaji wa mfumo huu kwa mafanikio makubwa na kwa wakati. Vilevile, naupongeza uongozi wa Baraza la Taifa la Ujenzi pamoja na wataalam wake, kwa kazi nzuri iliyotuwezesha kuwa na mfumo huu”, amesema Mhandisi Matei.

Kwa upande wake mwakilishi wa Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Mhandisi Rashid Kalimbaga amesema kuwa Baraza la Taifa la Ujenzi, lilipewa kazi ya kutengeneza mfumo huo tangu mwaka 2020 na sasa wanawasilisha kwa mara ya kwanza pendekezo la mfumo huo kabla ya kuanza kutumika.

“Mfumo huu utakapokamilika utasaidia sana kwenye michakato ya manunuzi ya kazi za barabara. Hii ni kwa sababu wakala wa barabara watakuwa na makadirio mazuri ya gharama za miradi husika na hivyo itakuwa rahisi kubaini mkandarasi anayetoa ofa ya chini zaidi ambayo haiakisi gharama halisi kwa kazi husika”, amesema Mhandisi Kalimbaga.

Akijibu maswali ya wadau wa mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Dkt. Samson Mturi amewatoa wasiwasi wadau hao kuhusu gharama za awali zilizomo kwenye mfumo huo, kwakuwa zoezi zima la uandaaji limehusisha wataalamu wa barabara, wakadiriaji majenzi, wakandarasi pamoja na wazabuni wa vifaa vya ujenzi.

Nao washiriki wa kikao hicho kwa nyakati mbalimbali, wamepata fursa ya kuuliza maswali kuhusu mfumo huo, pamoja na kutoa michango mbalimbali yenye lengo la kuboresha zaidi mfumo huo mpya wa uandaaji gharama za matengenezo pamoja na ujenzi wa barabara mpya.

Kikao cha kwanza cha wasilisho la mfumo wa kuandaa gharama za kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara kimefanyika kwa siku moja jijini Dodoma huku kikihusisha wadau wa mfumo huo kutoka taasisi mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Imetolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB).
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 14,2022

















Share:

Thursday, 13 October 2022

MWENGE WA UHURU ZAZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MIRADI MANISPAA YA BUKOBA


Na Mbuke Shilagi Kagera.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma amezindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera mara baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa leo Oktoba 13, 2022 katika maeneo ya uwanja wa shule ya msingi Ibura iliyopo Manispaa ya Bukoba ukitokea Wilaya ya Muleba na kukimbizwa kilometa 27.7 katika Halimashauri ya Manispaa ya Bukoba.


Mbio za Mwenge wa Uhuru zimezindua miradi miwili (2) imeweka jiwe la msingi miradi miwili (2) na kutembelea mradi mmoja (1) ambapo miradi hiyo ni vyumba vya madarasa, mradi wa kikundi cha vijana cha utengenezaji wa thamani, mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Kashai na mradi wa ujenzi wa ujenzi wa tank na upanuzi wa mtandao wa maji ambapo miradi hiyo yote imegharimu kiasi cha zaidi ya bilion nne.


Ikiwa ni kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao Kitaifa utazimwa Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba, Mwenge wa Uhuru utalala katika uwanja wa Mayunga uliopo mtaa wa Uswahilini Kata Bilele Manispaa ya Bukoba na kuzimwa kesho tarehe 14 Octoba 2022 katika uwanja wa Kaitaba na mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma pamoja na viongozi mbalimbali akikagua mradi wa ujenzi wa daraja Kyabtembe Manispaa ya Bukoba
Kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akizindua daraja Kyabtembe Manispaa ya Bukoba na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Moses Machali
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mh. Kemilembe Rwota akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Moses Machali katika uwanja wa shule ya msingi Ibura iliyopo Manispaa ya Bukoba
Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Moses Machali akishika Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Mayunga uliopo mtaa wa Uswahilini Kata Bilele Manispaa ya Bukoba
Wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya kashai Manispaa ya Bukoba
Emmanuel Chacha mkimbiza Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Kagera akiongoza maandamano ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kuelekea katika uwanja wa Mayunga uliopo mtaa wa Uswahilini Kata Bilele Manispaa ya Bukoba ambapo utakesha
Wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Gerarumaakifungua maji kwa ishara ya kumtua mama ndoo kichwani
Katikati ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Rwamishenye
Pichani ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa tank na upanuzi wa mtandao wa maji Bugashani Manispaa ya Bukoba
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Moses Machali na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma wakimtua mama ndoo katika mradi wa ujenzi wa tanki na upanuzi wa mtandao wa maji Manispaa ya Bukoba
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Moses Machali na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Rwamishenye akizindua kilabu ya mapambano dhidi ya rushwa
Wa pili kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa tank na upanuzi wa mtandao wa maji Manispaa ya Bukoba
Pichani ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akikata utepe ili kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Rwamishenye
Share:

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA ULINZI NA UFUATILIAJI MIENENDO YA WANYAMAPORI


Serikali Kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kutumia teknolojia ya kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika maeneo ya hifadhi kwa kuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kutambua mienendo ya wanyamapori mbalimbali wakiwemo wale walio hatarini kutoweka na wanaosababisha migogoro kwenye jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokua akizindua zoezi la Kuvisha Mikanda yenye Redio za Mawasiliano kwa wanyamapori linalofanywa na Watalaam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania ( TAWIRI) lililofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo jumla ya makundi 53 ya wanyamapori yanatarajiwa kifungwa mikanda hiyo nchi nzima.

"Katika kufuatilia mienendo ya wanyamapori waliohatarini kutoweka, teknolojia hii husaidia kutambua uwepo wao, mienendo na mtawanyiko katika mifumo ikolojia yao. Utambuzi huu husaidia katika kuimarisha nyanda za malisho na ulinzi." amesema Balozi Dkt . Chana

Amesema kwa upande wa wanyamapori waharibifu, teknolojia hiyo husaidia kutambua makundi na mienendo yao na kutoa taarifa mapema kuhusu uwepo wa makundi hayo nje ya hifadhi na kichukua hatua kabla ya hayajasababisha madhara.

"Taarifa hizi husaidia katika kupanga mbinu muafaka za kukabiliana na wanyamapori hao. " amesisitiza Balozi Dkt. Chana

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa zoezi hilo alilolizindulia limelenga kuimarisha uhifadhi na utalii kusini mwa Tanzania hususan katika Hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha na Mikumi akifafanua kuwa litasaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza migogoro baina ya jamii zinazozunguka hifadhi. "Jumla ya makundi ya wanyamapori 53 yatafungwa mikanda hii yenye redio za mawasiliano katika hifadhi hizi tatu." amesisitiza Balozi Dkt. Chana

Sambamba na hayo, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameongeza kuwa wanyamapori watakaofungwa mikanda hiyo ni pamoja na makundi ya tembo, simba, chui, duma, mbwa mwitu na twiga.

Aidha, taarifa na takwimu hizo zitasaidia kuandaa ramani za mitawanyiko ya wanyamapori katika misimu na nyakati mbalimbali ambazo zitasaidia kufungua njia mpya za utalii “tourism circuits” pamoja na kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi hizo.

Naye Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Tekinolojia hiyo itasaidia kuwalinda Wanyamapori na Hifadhi zetu hapa nchini. Pia, itasaidia kufuatilia mienendo ya Wanyamapori hai na kuweza kuwaona kidijitali pindi wanapotaka kuleta madhara.

"Kwa kutumia tekinolojia hii tunaweza kuwaona kidijitali wanapotembea na hasa wanapokaribia maeneo hatarishi ya kuleta madhara kwa wananchi"
Share:

OSHA, IDARA YA USALAMA NA AFYA ZNZ KUSHIRIKIANA KATIKA KULINDA NGUVU KAZI NCHINI.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji – Zanzibar, Dkt, Islam Seif Salim akizungumza na viongozi wa Menejimeniti ya OSHA Pamoja na baadhi ya Watendaji waandamizi kutoka Idara ya Usalama na Afya Zanzibar wa Idara ya Usalama na afya mahali pa kazi alioambatana nao katika ziara ya kutembelea Ofisi za OSHA kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda akitoa neno la ukaribisho kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji – Zanzibar, Dkt, Islam Seif Salim pamoja na Watendaji waandamizi kutoka Idara ya Usalama na Afya Zanzibar Idara ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi alioambatana nao katika ziara ya kutembelea Ofisi za OSHA Dar es salaam.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji – Zanzibar, Dkt, Islam Seif Salim (aliyekaa mbele), Watendaji waandamizi kutoka Idara ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Zanzibar pamoja na Viongozi wa Menejimenti ya OSHA wakibadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo usimamizi wa usalama na afya katika maeneo ya kazi.


Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na afya Mahali pa Kazi Zanzibar, Dkt. Ali Said Nyanga akifuatilia mada mbalimbali zilizowalishwa na Wakaguzi wa usalama na afya wa OSHA wakati wa kikao kifupi cha kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali.


Meneja wa Usalama wa OSHA, Mhandisi Robert Mashinji (kulia) akiwasilisha mada mbele ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Dkt, Islam Seif Salim (hayupo pichani) Pamoja na Watumishi wengine wa OSHA na Idara ya Usalama na Afya Zanzibar.


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji – Zanzibar, Dkt, Islam Seif Salim mara baada ya ziara ya Watendaji waandamizi kutoka Idara ya Usalama na Afya Zanzibar kutembelea katika Ofisi za OSHA Jijini Dar es salaam.

*********************

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar , Dkt Islam Seif Salimu ameipongeza OSHA kwa hatua kubwa inazoendelea kufanya za kulinda nguvu kazi kwa kuhakikisha inaweka mifumo Madhubuti ya usalama na afya katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini.

Dkt, Seif amesema hayo jijini Dar es salaam baada ya Watendaji waandamizi kutoka Idara ya Usalama na Afya Zanzibar kufanya Ziara Ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali Kazi (OSHA) kwa lengo la kujifunza namna taasisi hio inavyosimamia sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi

“Kimsingi OSHA imepiga hatua kubwa sana katika usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo niwapongeze sana kwa kuweka mifumo madhubuti katika usimamizi wa masuala mbalimbali ya usalama na afya kazini hivyo tumeona kuna haja kubwa ya kuja katika taasisi hii kujifunza na kushirikiana nao katika masuala mbalimbali ikiwemo kutengeneza mkakati wa pamoja wa kuhakikisha maeneo yetu ya kazi yanakuwa salama” alisema Dkt, Islam Seif Salim

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi.Khadija Mwenda amesema kuwa taasisi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na Idara ya Usalama na Afya ya Zanzibar ili kujenga ustawi wa wafanyakazi wote nchini.

“Tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Wazanzibar katika mambo mbalimbali kiwemo usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi, ziara hii imejikita zaidi katika kujifunza namna tulivyofanikiwa kutoka katika kitengo ndani ya idara ya kazi mpaka kujitengemea kama wakala na tunaamini kuwa itawapa chachu ya kufanya mapinduzi juu ya uboreshaji wa masuala ya usalama na afya katika maeneo ya kazi” alisema Mtendaji Mkuu, Bi Khadija Mwenda akiongeza kuwa.

“Tumeshuhudia Zanzibar ikikua kiuchumi kwa haraka sana na shughuli nyingi za kiuchumi zinapofanyika zinakuja na vihatarishi ambavyo vinahitaji mbinu mbadala ya kukabiliana navyo na ndio maana wamekuja kujifunza ni namna gani sisi tumeweza kufanya usimamizi lakini zaidi tutakuwa na ushirikiano mzuri katika usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili kujenga ustawi wa wafanyakazi wote Nchini”

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya OSH Zanzibar, Dkt. Ali Said Nyanga amesema kuwa kupitia ziara hii itawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wakikumbana nazo wakati wakitoa huduma vilevile itawasaidia kulinda nguvu kazi kwa kuhakikisha mazingira yote ya kazi yanakuwa salama.

“Tumekuwa tukikumbana na changamoto mbalimbali katika utoaji huduma na changamoto hizo zimepatiwa majibu mahali hapa pia tumeshuhudia ongezeko kubwa sana la uwekezaji nchini ambao utahitaji sana huduma zetu hivyo nilazima tuhakikishe nguvu kazi hizi zinalindwa ipasavyo iliziweze kuzalisha mara dufu” alisema Mkurungezi wa Idara ya Usalama na Afya kazini, Dkt. Ali Said Nyanga.

Idara ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi nchini Zanzibar ni idara iliyo chini ya Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji yenye jukumu la Kusiamia masuala ya usalama na afya katika maeneo ya kazi Tanzania Visiwani (Zanzibar).
Share:

DKT.KIKWETE KUSHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI NA MICHEZO LA WATOTO BAGAMOYO

Mratibu wa Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, Bi.Akanashe Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani. Mratibu wa Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, Bi.Akanashe Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Africaree, Bi. Angela Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha la utamaduni na Michezo la Watoto litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani.

********************

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, litakalofanyika Oktoba 16,2022, katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13,2022 Bagamoyo mkoani Pwani, Mratibu wa Tamasha hilo, Bi.Akanashe Mwanga amesema Tamasha hilo linatarajia kushirikisha watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 15, ambao wataonyesha fani mbalimbali.

Amesema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa kwani lengo ni kuendeleza vipaji vya watoto mjini hapa ili kuhakikisha wanafikia malengo yao waliojiwekea.

"Tumeandaa tamasha la watoto kuanzia umri wa miaka mitano hadi 15 litahusisha watoto 80 wa fani mbalimbali ambapo tunarajia mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu, Dkt Kikwete na ushiriki ni bure kabisa". Amesema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Africaree, Bi. Angela Ngowi, amesema tamasha hilo litakua la aina yake kwani litashirikisha sanaa mbalimbali na michezo.

Alitaja baadhi ya sanaa zitakazoonyeshwa na watoto hao kuwa ni ufinyanzi, ngoma, kuchora, muziki, kuruka kamba, rede na michezo mbalimbali ambayo imekuwa na faida ikichezwa na watoto.

"Tunatarajia tamasha litakuwa la aina yake kutokana na maandalizi tuliyoyafanya, tunatambua vipaji vya vijana wanaotoka familia za kawaida, hivyo tumeamua kuwaendeleza kutokana na vipaji vyao," Amesema

Aliongeza pia katika tamasha hilo wataendesha harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za kujengea shule ya vipaji itakayokuwa na uwezo wa kuchukua watoto wengi zaidi kutoka Bagamoyo na Tanzania nzima.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger