Wednesday, 12 October 2022

MTOTO ALIYELIMWA JEMBE KICHWANI AFARIKI DUNIA




Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) imeweka wazi hali iliyosababisha kifo cha mtoto aliyelazwa katika kituo hicho akiwa amedungwa jembe kichwani.


Hospitali hiyo, katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Oktoba 12, ilieleza kuwa ubongo wa mtoto huyo ulikuwa umevimba na ulionyesha dalili za uwezekano wa kuumia.


Kulingana na kituo cha rufaa, uchunguzi wa kimatibabu na vipimo vilibaini kuwa jembe ilipenya kwenye ubongo na kusababisha uvimbe wa ubongo wa mtoto huyo wa miaka miwili kutokana na kuvuja damu kwa ndani.


"Uchunguzi wa kliniki na uchunguzi juu ya mgonjwa, ikiwa ni pamoja na CT scans na vipimo vya damu, ulithibitisha jeraha la kupenya kwenye ubongo, uvimbe wa ubongo na kutokwa na damu inayoendelea na uwezekano wa maambukizi," inasomeka sehemu. ya taarifa.


Aidha, hospitali hiyo ilitetea uamuzi wake wa kuchelewesha upasuaji uliohitajika kuondoa kitu hicho kichwani.

Katika kukabiliana na suala hilo, kituo kiliamua kurekebisha tatizo la kuganda kwa damu kabla ya kuendelea na upasuaji kama ambavyo umma wangetarajia.

"Mchakato wa kurekebisha hitilafu zilizogunduliwa kwa kumpa bidhaa za damu na dawa, huku ufuatiliaji wa majibu ya mgonjwa ulianza mara moja," alisema George Ooko, Mwenyekiti, Usimamizi wa Bodi ya KNH.

Hatimaye, madaktari walifanikiwa kurejesha upungufu wa damu ya mgonjwa na hatimaye kufanya uamuzi wa kuanza mchakato wa upasuaji uliohitajika.


Hata hivyo, hospitali hiyo ilibaini kuwa hali ya mtoto huyo ilidhoofika akiwa ukumbini baada ya kupata matatizo.


Hatimaye, madaktari walifanikiwa kurejesha upungufu wa damu ya mgonjwa na hatimaye kufanya uamuzi wa kuanza mchakato wa upasuaji uliohitajika.


Hata hivyo, hospitali hiyo ilibaini kuwa hali ya mtoto huyo ilidhoofika akiwa ukumbini baada ya kupata matatizo.


“Mchakato wa kurekebisha kasoro zilizogunduliwa kwa kumpa bidhaa za damu na dawa, huku uchunguzi wa itikio la mgonjwa ulianza mara moja,” ripoti hiyo ilisema kwa sehemu.
Share:

MWALIMU WA ZAMU ATANDIKWA KOFI NA MWANAFUNZI WAKE HADI DAMU KUTOKA




Mwanafunzi wa darasa la 8 katika Shule ya Msingi ya Nkararo huko Transmara, Kaunti ya Narok, yuko mbioni baada ya kumpiga mwalimu wa zamu kofi alipotaka kuona kazi yake ya ziada.

Inasemekana mwalimu huyo anayefahamika kama Charles Miruka alitokwa na damu na kupoteza miwani yake.

Katibu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini (KNUT) Collins Oyuu alikashifu kisa hicho na kuwataka polisi kumtafuta na kumkamata mwanafunzi huyo.

Mwalimu huyo alikimbizwa hospitalini eneo hilo ambako alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku mwanafunzi huyo akitoroka na bado hajapatikana.

Katibu huyo wa KNUT alitoa wito wa kukamatwa mara moja kwa mshukiwa anayedaiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 18.

"Tunatoa wito kwa polisi kumkamata mara moja mtuhumiwa. Kwa nini mwalimu anapokosewa hakuna anayechukulia suala hilo kwa uzito? Tunaiomba serikali kuwapa ulinzi wa hali ya juu walimu wote nchini" alisema Bw. Korir.
Share:

MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA 9

Mwanamke aliyejifungua watoto tisa

MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 35 aliyefahamika kwa jina la Hajara Shu’aibu, amekuwa na kila sababu ya kutabasamu baaada ya kujaliwa kupata watoto 9 mapacha.


Mwanamke huyo anayeishi jimbo la Katsina nchini Nigeria alijifungua watoto hao Jumatano ya wiki iliyopita, Oktoba 5, 2022 na sasa ana jumla ya watoto 18. Hajara tayari alikuwa na alikuwa na watoto wengine tisa mapacha ambao aliwahi kujifungua miaka kadhaa iliyopita na wote wapo hai.


Mama huyu ambaye anaonekana kama mama aliyebarikiwa na zawadi ya watoto kwenye jamii yao, ameolewa na mkulima miaka 21 iliyopita.


“Nilijifungua nikiwa nyumbani, baadaye wakunga walinipeleka hospitalini na kuwekwa damu kisha kuniambia nipumzike. Watoto wangu wote waliozaliwa hapo awali wapo nyumbani. Watoto wangu wote nilijifungulia nyumbani bila upasuaji hata mmoja,” mama alisema.


Akizungumza kuhusu kujifungua kwake hivi majuzi, mama huyo alisema watoto hao wachanga walipelekwa katika Hospitali Kuu ya Funtua iliyoko karibu baada ya kujifungulia nyumbani.


Hata hivyo mama huyu alitoa wito kwa serikali na watu binafsi wenye moyo wa huruma kumsaidia kuwatunza watoto.
Share:

WAZIRI NDARICHAKO AMPONGEZA RC CHALAMILA KWA MAANDALIZI MAZURI YA KUELEKEA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, WIKI YA VIJANA

 



Katikati ni Profesa Joyce Ndarichako akizungumza na vyombo vya habari Mara baada ya kukagua maandalizi ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na wiki ya vijana.


Na Mbuke Shilagi Kagera.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi vijana ajira na ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila kwa maandalizi mazuri ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na wiki ya vijana ambayo Kitaifa inafanyika Mkoa wa Kagera Manispaa ya Bukoba.

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 11 Oktoba 2022, uwanja wa Kaitaba katika kukagua maandalizi ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge na wiki ya vijana Waziri Ndalichako amesema kuwa maandalizi ni mazuri kama alivyo kagua na kumpongeza Mkuu wa Mkoa pamoja na watumishi wake kwa maandalizi hayo.

Amesema kuwa kesho tarehe 12 Oktoba 2022 kutakuwa na uzinduzi rasmi wa wiki ya vijana katika viwanja vya Gymkana yaliyo anza tarehe 08 Octoba 2022 ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasim Majariwa.

Huku akiongeza kuwa tarehe 14 Oktoba 2022 sherehe zitaanzia katika Kanisa kuu la katholiki Manispaa ya Bukoba kwa ibada ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Kisha baada ya ibada mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan atakagua shughuli za vijana katika hitimisho la maadhimisho ya wiki ya vijana Kitaifa katika viwanja vya Gymkana.

Na kwamba baada ya hapo atakuwa uwanja wa Kaitaba katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru hivyo wananchi wote waweze  kujitokeza kwa wingi siku hiyo.


Share:

MO GREEN INTERNATIONAL YAJIPANGA KUHAKIKISHA INAINUA VIPAJI VYA MASUMBWI NCHINI

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Geen International Bw.Kessa Mwambeleko akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro.
Bondia Twaha Kiduku akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Dulla Mbabe akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Karim Mandonga akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Saidi Mbelwa akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mo Geen International Sports Promotion imeandaa pambano la ndondi mkoani Morogoro ikiwashirikisha mabondia nyota wenye historiia mbalimbali ndani na nje ya nchi, pambano ambalo litapigwa Novemba 25,2022.

Akizungumza leo Oktoba 12,2022 na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Geen International Bw.Kessa Mwambeleko amesema mabondia takribani sita wataweza kushiriki siku hiyo akiwemo Twaha Kiduku, Dulla Mbabe na kari Mandonga ambapo wote hao wamepewa muda wa kuelezea walivyojipanga na wote wapo tayari kwa pambano na kuwapa wananchi burudani.

"Bondia nyota Twaha Kiduku, ambaye ana historia kushinda mikanda mbalimbali, atapambana na Bondia Damian Bonell kutoka nchini Argentina ambaye pia ana historia ya kusisimua kwenye tasnia ya ngumi". Amesema

Amesema Pambano lingine katika siku hiyolitawahusisha mabondia Dulla Mbabe ambaye mashabiki wake walikuwa na kiu ya kumuona ulingoni kwa muda mrefu, akipambana na bondia Mkongo, Mbiya Kanku.

Aidha pambano lingine litamuhusisha bondia aliyejipatia umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni, Karim Mandonga atakayepambana na Bondia Said Mbelwa.

Nae Bondia Twaha Kiduku amewataka wapenzi ngumi waweze kushiriki kushuhudia burudani nzuri kutoka kwake na kuwahakikishia mashabiki ushindi dhidi ya mpinzani wake Muargentina Damian Bonell.

Pamoja na hayo ameupongeza uongozi wa kampuni ya Mo Geen International Sports Promotion kwa kuandaa pambano hilo ili mabondia wengine waweze kuonesha vipaji vyao katika tasnia ya ngumi na kuweza kupeperusha bendera ya taifa.

Kwa upande wake Karim Mandonga amesema atahakikisha anashinda pambano hilo na kumtambia mpinzani wake kuwa atampiga na kutoa burudani kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimshangilia.

Share:

CRDB KUTIKISA SHINYANGA TAMASHA LA MBIO BAISKELI KUMUENZI BABA WA TAIFA... "CRDB HATUNA JAMBO DOGO, TUKUTANE CCM KAMBARAGE"

Meneja wa Benki yaa CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB inatarajia kuadhimisha Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14,2022 kwa kufanya Tamasha la Mbio za Baiskeli litakaloambatana na hamasa ya uchangiaji damu salama kwa ajili ya wahitaji wa damu katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumatano Oktoba 12,2022, Meneja wa Benki yaa CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui amesema Mashindano ya Baiskeli yameandaliwa Benki ya CRDB kupitia tawi la Shinyanga.

“Tamasha la Mbio za Baiskeli litapambwa na mashindano ya mbio za baiskeli zenye washiriki 275 wakataogawanyika katika makundi matatu. Kundi la kwanza ni la Wabobevu wa baiskeli watakaokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,500,000/=”,amesema Pamui.

“Pia kuna kundi la Vijana watakaozunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60 ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi 500,000/=, kundi la tatu ni la wanawake ambao watazunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40 ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi 500,000/=”,ameeleza Pamui.

Amefafanua zaidi kuwa katika Tamasha la Mbio za Baiskeli, Benki ya CRDB inakusudia kutoa shilingi 6,450,000/= zawadi kwa washindi 40 kwa viwango mbalimbali.

“Katika tamasha hili pia kutakuwa na bonanza la mpira wa miguu kati ya CRDB Digital FC na SHUWASA, ngoma naa nyimbo kutoka kwa wasanii mbalimbali na sanaa nyingine nyingi zikishuhudiwa na wananchi wa mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani”,ameongeza Pamui.


“Tunakusudia kukusanya lita 500 za damu, kukutanisha watu zaidi ya 2000 wakiwemo wana michezo wa baiskeli 275. Tunategemea kuongeza mahusiano kati ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB na Jamii ya Shinyanga. Pia Benki ya CRDB itatoa elimu ya huduma za Benki kwa jamii”,amesema Pamui.
Meneja wa Benki yaa CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui

“Karibuni sana katika Tamasha la Mbio za Baiskeli CRDB Shinyanga. Baba wa taifa alikuwa mdau wa baiskeli na mashindano ya baiskeli yanapendwa sana na wananchi. Napenda kuwafahamisha kuwa CRDB hatuna jambo dogo, tukutane uwanja wa CCM Kambarage Oktoba 14,2022. Mwaka huu jambo letu ni kubwa sana",amesema Pamui.

Amesema Benki ya CRDB imejiwekea utamaduni wa kutoa msaada kwa jamii ili kupambana na changamoto zinazozuia maendeleo ya jamii ikiwa ni mkakati wake wa kuwekeza katika jamii husika na kwa sehemu kubwa ya mkakati huo unajikita sana katika kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu, afya na michezo.

Meneja wa Benki yaa CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Shinyanga

Share:

EWURA YAENDESHA SEMINA KWA MAFUNDI UMEME KANDA YA ZIWA...DC MBONEKO ATAKA UBORA WA HUDUMA 'UMEME USILETE MADHARA KWA WANANCHI'


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA. Kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina, kulia ni Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA, John Kitonga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendesha Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza) kwa lengo la kuwaongezea uelewa wa masuala ya kiudhibiti hususani katika ufungaji wa mifumo ya umeme na namna bora ya kufanya kazi zao ili kuhakikisha huduma zinakuwa salama, bora na zilizofanyika kwa viwango vinavyokubalika.

Semina hiyo ya siku mbili imeanza leo Jumatano Oktoba 12,2022 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga ikihudhuriwa pia na maafisa kutoka VETA, TEMESA na TANESCO.

Akifungua Semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema kazi zinazofanywa na wadau wa fani ya ufungaji mifumo ya umeme ni za muhimu sana katika ustawi wa uchumi wa nchi hivyo zinapaswa kufanywa kwa weledi wa hali ya juu ili kulinda usalama wa maisha ya watu na mali zao.

“Kwa sababu kazi za umeme zinaweza kuleta madhara ikiwa zitafanywa chini ya kiwango ama kufanywa na fundi asiye na utaalamu huo, inaelekezwa kufanywa na mwenye utaalamu na aliyethibitishwa na Mamlaka kwa kupewa Leseni. Hivyo haipaswi kutumia leseni ya mtu mwingine kufanya kazi za umeme nan i kosa linaloweza kuadhibiwa kisheria”,amesema Mboneko.


“TANESCO hakikisheni mnatumia mafundi umeme waliosajiliwa na wenye leseni ili kuondoa vishoka wanaoharibu kazi na kusababisha majanga ya moto kutokana ufungaji umeme mbovu. Hatutaki kuona mtu asiye na leseni na hajasajiliwa anafanya kazi ya kuunganisha umeme. Hawa Vishoka wanaharibu sifa za mafundi umeme wenye vigezo”,ameongeza.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA

Mkuu huyo wa wilaya amesema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kufikisha huduma ya umeme kwa wananchi ambao hauleti madhara kwa wananchi hivyo kuwataka wafundi umeme kuzingatia sheria za sekta ya umeme.

“Tunataka kuona umeme unaopelekwa kwa wananchi hauleti madhara kwa wananchi.Hatutakubali kuona wafundi wasiosajiwa na wasio na leseni wanafanya kazi ya kufunga umeme iwe majumbani, viwandani ama sehemu za biashara. Tunataka kuona ubora wa kazi ili kuondokana na lawama”,amesema Mboneko.

Kwa upande wake Meneja wa EWURA, George Mhina amesema EWURA imeamua kutoa semina kwa mafundi umeme kwa lengo la kuwaongezea uelewa wa masuala ya kiudhibiti hususani katika ufungaji wa mifumo ya umeme na kuwajengea uwezo wa namna bora ya kufanya kazi ili kuhakikisha huduma wanazotoa zinakuwa salama,bora na zilizofanyika kwa viwango vinavyokubalika ili kuepuka majanga ya moto.

Mhina ameeleza kuwa, mwaka 2008, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Umeme “Electricity Act” na kifungu namba 8 (h) cha sheria hiyo kinaelekeza kazi zote za ufungaji wa mifumo ya umeme (majumbani,viwandani ama sehemu za biashara) zifanywe na mtaalamu aliyeomba na kupewa leseni na mamlaka husika ambayo ni EWURA.

“Lengo kuu la kudhibiti huduma za ufungaji wa mifumo ya umeme ni kuhakikisha kazi hiyo inafanywa kitaalamu na wale tu wenye ujuzi na weledi katika fani ya umeme ili kumhakikishia mtumiaji wa huduma hizo usalama na ubora wa huduma”,amesema Mhina.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA leo Jumatano Oktoba 12,2022 Mjini Shinyanga. Kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina akizungumza kwenye Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA. Katikati ni ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA, John Kitonga. 
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina akizungumza kwenye Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA. Katikati ni ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA, John Kitonga. 
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina akizungumza kwenye Semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA. Katikati ni ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA, John Kitonga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimpatia Cheti na Leseni fundi umeme, Charles Jackson. Wa kwanza kushoto Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina wa pili kulia ni Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA, John Kitonga. 
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina akitoa elimu kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina akitoa elimu kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA

Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Maafisa kutoka TANESCO Shinyanga wakiwa kwenye semina kwa Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza  iliyoandaliwa na EWURA

Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na EWURA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na Mafundi Umeme mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na Mafundi Umeme mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na Mafundi Umeme mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na Mafundi Umeme mkoa wa Geita
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na Mafundi Umeme mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na maafisa kutoka taasisi mbalimbali mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko maafisa kutoka EWURA,TEMESA wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa EWURA.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

NAIBU WAZIRI MASANJA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA IPASAVYO MAENEO YA HIFADHI


************ 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia vyema maeneo ya hifadhi ili kuepusha migogoro baina ya shughuli za kibinadamu na hifadhi. 

Ameyasema hayo Oktoba 11, 2022 mkoani Rukwa wakati wa Ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya Ardhi katika vijiji 975 nchini. 

“Kila mtu akisimamia eneo lake vizuri hii migogoro itapungua sana ama kuisha lakini tukisubiri Serikali iseme au Kamati ya Mawaziri iseme, maeneo ya hifadhi yatakwisha” Mhe. Masanja amesisitiza. 

Amefafanua kuwa changamoto kubwa inayoipata Serikali kwenye uhifadhi ni muingiliano wa shughuli za kibinadamu na utunzaji wa maeneo ya hifadhi ambapo wananchi wanaanzisha vijiji katikati ya hifadhi. 

Mhe. Masanja amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Vijiji kuhakiki wahamiaji wanaoingia katika maeneo yao ili kujua sababu inayowafanya waanzishe vijiji katika hifadhi na pia watoe maelekezo ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi na kuwasimamia ili kuondokana na migogoro ya ardhi. 

“Ifike mahala wananchi wafahamu umuhimu wa uhifadhi na shughuli za kibinadamu” ameongeza. 

Amesema endapo hifadhi zitaendelea kuvamiwa changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi zitaendelea kujitokeza. 

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ameelekeza migogoro hiyo itatuliwe ambapo kwa sasa hifadhi zinaheshimika na wananchi wanaendelea na maisha yao ya kila siku. 

Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta itaendelea katika mkoa wa Katavi tarehe 12 Oktoba kabla ya kuelekea Kigoma Oktoba 13,2022.
Share:

Tuesday, 11 October 2022

WAUMINI WAPIGANA WAKIONDOLEWA MAPEPO KANISANI


Video iliyomnasa Pasta James Ng'ang'a akiyaondoa mapepo kutoka kwa waumini wake, imewasha mitandao ya kijamii huku wengi wakishangaa iwapo ni kweli au walikuwa wakiigiza.

Kwenye video fupi iliyosambazwa na katika Facebook na Channel 7 News, wanawake walianza kuanguka kwenye madhabahu baada ya Ng'ang'a kukemea kwa jina la Yesu Kristo.

Mtandao huu haujabainisha ni nini kilichokuwa kikiendelea ila kwa kukagua video hiyo, pasta huyo alionekana kuoyaondoa mapepo.

Waumini hao, wengi wakiwa ni wanawake walianza kufoka na kupagawa kwenye madhabahu, huku Ng'ang'a akiwashabikia.

Baadhi ya wanaume walijiunga kwenye sarakasi hizo na kuanza kupiga miereka, na kuzidi kufanya wengi kuchanganyikiwa hata ingawa hawakuumizana.

Matukio hayo yalionekana ni kama mchezo wa kuigiza, na dakika za mwisho Ng'ang'a aliwaambia walisifu jina la Yesu Kristo.

Wakenya watoa maoni kuhusu video hiyo.

Mohamed Hussein Saadad: "Nijuavyo, ukiamini umepona basi umepona tayari. Haihusiana kivyovyote na miujiza au pasta Nganga."

Mboya Denis: "Sasa vitimbi vya nini? Ninachoona na mchezo wa kuigiza huku kukiwa na waigizaji waliopewa mafunzo. Hongera pasta nganga."

Edson Bukenya: "Afrika imejaa vitimbi, ni Mungu aingilie kati!"

James Lukindo: "Hiyo ni drama ya miujiza kwenye makanisa pekee. Ikiwa ni kweli wanaponya na kukemea mapepo kwa nini wasiendee hospitalini ambako watu wengi wanateseka?"
Share:

APIGWA SHOTI AKIWAHUJUMU TANESCO 'ALIKUWA ANAPISHA SHOTI UMEME UKATIKE"


Kigodi Juma, aliyepigwa shoti ya umeme

Kigodi Juma (24), mkazi wa Kijiji cha Nkiniziwa kilichopo wilaya ya Nzega mkoani Tabora, amejeruhiwa vibaya katika maeneo ya mwili wake baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akikata nguzo ya umeme kwa kutumia shoka, majira ya usiku.


Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkiniziwa Hamisi Bundu, amesema kijana huyo alitenda tukio hilo usiku wa kuamkia Oktoba 10, 2022 ambapo majira hayo ya usiku walishtushwa na kukatika kwa huduma ya umeme.

Amesema kijana huyo kabla ya kuanza kukata nguzo hiyo alirusha waya uliokuwa umefungwa vipande vya miti kwa ajili ya kupigisha shoti ili umeme uweze kukatika ili apate urahisi wa kuangusha nguzo hiyo bila wasiwasi wa kujeruhiwa na umeme pasipo kujua kama umeme bado ulikuwa haujakatika.

Kijana huyo baada ya kupigwa shoti ya umeme alikimbizwa katika kituo cha afya Busondo na kwa sasa anaendelea na matibabu, huku Kaimu Mganga wa kituo hicho cha afya Juma Sosoma, akieleza licha ahueni aliyonayo kwa sasa ataandikiwa rufaa ya kwenda katika hospitali kubwa kwa ajili ya vipimo zaidi vya ndani ya mwili kutokana na kuumia vibaya katika maeneo ya miguu,shingo ,usoni na kwenye mikono.

CHANZO- EATV

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger